WhatsApp imeweka mfumo wa "Disappearing Messages" kwa chatting mpya

WhatsApp imeweka mfumo wa "Disappearing Messages" kwa chatting mpya

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Wiki hii WhatsApp inaweka uwezo wa kuchagua mfumo wa Disappearing Messages katika chats zote mpya. Disappearing Messages ni option ya kuamua chats zifutike baada ya masaa 24, Siku 7 au Siku 90.

Mfumo mpya unaofanana na mfumo wa Snapchat, utawezesha watumiaji kuweka option ya Disappering Messages katika chats zote mpya. Mwanzo ilikuwa unaweka option hii kwa mtu mmoja mmoja.

Meta imesema sababu ya kuweka hivyo ni kuwapa watu uhuru wa kuepuka ku-save messages nyingi hasa wale ambao wanapata messages nyingi za watu wapya na hakuna umuhimu wa kutunza chats. Bado ni option, mtu anaweza kuamua kuzima au kuweka option hii.

Kwa watumiaji wa Android na iOS, feature hii itakwepo katika WhatsApp Settings > Account > Privacy > Default Message Timer. Hakikisha ume-update WhatsApp yako katika App Store au Google Playstore.
 
Zitafutika kwangu tuu au hata kwa yule niliechat nae?
zinafutika kwako ukitaka kufuta na kwa mwingine baada ya kutuma ujumbe ukiufuta basi na message za unae chati nae zinafutika.
 
Ila hiyo ili ifanye kazi, lazima yule unayechat naye pia awe ame update WhatsApp. Shida kubwa ni kwamba watanzania wengi hatuna utaratibu wa ku update apps, wengine hata hawajui ku update ndo nini.
 
Back
Top Bottom