WhatsApp yafanya Maboresho Yaja na Features Mpya

WhatsApp yafanya Maboresho Yaja na Features Mpya

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Mtandao wa WhatsApp ambao ni mali ya kampuni ya facebook, Yaja na Features Mpya katika mtandao huo.
Mabadiliko na maboresho yalifanywa na mtandao huo tarehe 28/09/2021 hivyo ilikuwa lazima kwa kila mtumiaji wa mtandao huo kuupdate ili kupata maboresho yaliyo fanywa.

Maboresho hayo yaliyo fanywa ni;
1- Mabadiliko kwenye kasi ya kucheza sauti (Audio) zilizo tumwa.
Hivyo mteja anaweza kuongeza kasi ya sauti kuchezwa hapa sauti itakuwa na kasi ya kawaida ikiwa na alama ×1 lakini pia kasi zingine ni ×1.5 hii itakimbiza kidogo yaani kasi ya kucheza sauti itaongeza, pia kasi ya mwisho ni ×2 hii itaongeza Zaidi kasi. Option hizo zote zipo mbele ya Kicheza sauti hivyo unaweza bonyeza.

2- maboresho mengine ni kuruhusu ujumbe picha na video kutumwa mara moja na kujifuta.
Hapa itamuruhusu mtumaji ujumbe aweka mipangilio kwenye ujumbe pindi mpokeaji atakapo pokea ujumbe na kuusoma Hato wezi kuihifadhi bali utajifuta kiautomatiki.
Hivyo msomaji akisha usoma ujumbe huo utajifuta Papo kwa papo.
Lakini WhatsApp ameweka maelezo kuwa mpokeaji anaweza kupiga picha ujumbe huo Kabula haujajifuta, hivyo kuwa makini.

3- Pia imefanya maboresho mengine madogo madogo kama vile kubadili muonekano wa ndani pamoja na rangi.

Mtandao huo utaendelea kufanya maboresho zaidi.
 
Mbona mabadiliko haya ni ya muda sasa.....
Hapana hawakuwa na option ya kuongeza kasi ya kucheza sauti yaani ×1 kasi ya sauti ya kawaida ×1.5 unaongeza kasi pamoja na ×2 .
Pia kutuma ujumbe na kujifuta automatiki hawakuwa nayo.
 
Hii ni mbaya sana.

Kuna mwanamke wangu alinitumia video tamu ya Utupu.

Bahati mbaya sana niliiangalia mara moja tu pasipokutulia.. Kumbe kai-set on view once.

Kuja kutulia, naona ipo 'opened'. Video hakuna. Nilisikitika sana.
 
Ndio mkuu hii ipo kiusalama na kuficha ushahidi kwahiyo ukitumiwa iliyo setiwa hivi ni mara moja tu inapotea.
Labda dawa uwe na screen recorder ukiwa unaangalia huku ikijirekodi.
 
Mbona aya mabadiriko yana muda sana au unazungumzia mabadiriko gani.?.
hawakuwa na option ya kuongeza kasi ya kucheza sauti yaani ×1 kasi ya sauti ya kawaida ×1.5 unaongeza kasi pamoja na ×2 .
Pia kutuma ujumbe na kujifuta automatiki hawakuwa nayo.
 
hawakuwa na option ya kuongeza kasi ya kucheza sauti yaani ×1 kasi ya sauti ya kawaida ×1.5 unaongeza kasi pamoja na ×2 .
Pia kutuma ujumbe na kujifuta automatiki hawakuwa nayo.

Option ya kasi ya sauti haina umuhimu wowote 😃
 
Back
Top Bottom