Whatsssssss!!!!!!!!!????

Nakuwa na amani kama ndo sadaka niliyonayo... Naamni Mungu anaangilia utayari wa moyo kumtolea na sio kiwango kikubwa nitoacho
Nakuaminia jembe[emoji1] [emoji1] [emoji23] [emoji23]
Kanisani unaenda lakini?
 
CHIZI ALIOZWA MKE, HARUSI YA KUFANA MASHAALLAH...
SHAMRASHAMRA KAMA KAWAIDA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI.
HARUSI IKAISHA WATU WAKAFUMKANA KWENDA MAKWAO....
CHIZI AKAINGIA CHUMBANI MWAKE AKAKUTA BI HARUSI KAKAA KITANDANI....!!!
AKASEMA KWA HAMAKI, NILIJUA TU HII SHAMRA SHAMRA YOTE PATASAHAULIWA MTU HAPA[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
MKALIMANI AZUA KIZAA ZAA KANISANI
MCHUNGAJI: We need to thank GOD for Goals that we set in our hands.
MKALIMANI: Tunamshukuru mungu kwa magoli yote ya mikono.
HIVI SASA KANISANI HAKUNA VITI[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Umerudi zako nyumbani ukakuta panya 6;
Panya wa kwanza anakula Biblia na Msaafu.
Wa pili anakula cheti cha degree,
Wa tatu anakula hati ya nyumba,
Wa nne anakula viza ya kusafiria .
Wa tano anakula cheti cha ndoa na
Wa sita anakula cheki ya million 20.
Utaanza kumuua panya yupi?[emoji23] [emoji23]
 
Mwanafunzi wa darasa la pili alimuuliza mwalimu wake hivi:-
Mwanafunzi:- Ukichanganya OMO na FOMA zitatoa povu?
Mwalimu kwa hasira:- Swali gani hilo la kipuuzi...!! lazima zitatoa povu sababu zote ni sabuni.
Mwanafunzi:- Sasa wewe ndiye una majibu ya kipuuzi...!! zitatoaje povu wakati haujaweka maji[emoji12]
 
Akaunti Benki Ina Elfu 4,
Mfukoni Una Jero,
Kwenye Simu Umekopa.....
Halafu Unaimba "Chop Ma Money"[emoji1] [emoji117] Badili Uimbe Tenda Miujiza[emoji13] [emoji13]
 
*WATOTO WA SIKU HIZI HAWAJUI KABISA ENZI ZETU UNAWEZA KUCHAPWA KWA SABABU ZIFUATAZO:*
1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa hukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa.
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa.
27. Ukitembea na mtu mzima, akajikwaa ukamcheka, utachapwa.
28. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa.
29. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa.
30. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa.
31. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa.
32. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa.
33. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa.
=> Na mengine uyajuayo wewee
Ndio maana watoto wa zamani tuna heshima hata wakati wa kupokea meseji napiga magoti[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wazungu bhana wameona watu tumefulia hatuna hela ya kununua vipodozi wameamua kutuwekea make up kwenye simu tunapiga picha kawaida halafu ndio tunajipodoa kwenye simu,hadi ma wigi ya kila aina yapo[emoji13] [emoji13]
 
Hii ndio Bongo
Ilikuwa Ijumaa mida ya saa 10 jioni, mzee mmoja aliingia na kibinti kizuri kwenye yard ya magari mapya.
MZEE: Chagua gari unalotaka mpenzi....kabinti kakazunguka yard yote mwisho kakachagua Verrosa metallic .
BINTI: Mi naitaka hii...
MZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima upate gari uloichagua mwenyewe.
Mzee akatoa kitabu cha cheki na kuandika palepale na kumpa mwenye yard.
MUUZAJI: Sasa Mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa Account yako ina pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee
MZEE: Hakuna tatizo (akampa namba).
Haya twende zetu sweetie Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lako... Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.
MUUZAJI: We Mzee kavu sana, akaunti yako haina hata senti tano.
MZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Mzee hapendagi ujinga.
 
JINSI YA KURUDISHA UPYA NGUO YAKO ILIYOCHAKAA!!
'Watu wengi wanakosa raha hasa pale nguo zao wanazozipenda zinapopauka ama kuchakaa.
Zifuatazo ni hatua za kufata ili nguo iliyochakaa ama kupauka kurudia upya wake;
1. Chemsha maji kwenye sifuria kubwa mpaka yachemke (100°C)
2. Tumbukiza nguo yako ndani ya hayo maji,subiri nusu saa afu uitoe kwenye sufuria
3. Weka mafuta ya kula,weka kitunguu na nyanya kisha kologa weka nguo yako humo kwenye mchuzi af tia chumvi kidogo na uonje he he he unadhani unaunga nyama hapo hebu ona unavofatilia kwa makini,acha ujinga wewe kwani umeambiwa nyengine madukani zimeisha!![emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Baada ya kufunga ndoa siku ya pili wakapelekana kwa hakimu...
Hakimu akawauliza nini tena?
MKE AKASEMA:
Mi nilifikiri iko hivi
==========>
Ama hivi
=======>
Kumbe iko hivi
==>
Bora talaka tu...
MUME NAE AKASEMA:
Nami nilifikiri iko hivi
( )
Ama hivi
( ___ )
Kumbe iko hivi
(______)
Bora nimpe talaka.
Sipendagi Ujinga mimi[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Mirembe Mental Hospital.
DAKTARI :- Unajisikiaje?
CHIZI:-Kila siku naota nyani wanacheza mpira wa miguu.
DAKTARI :- Nitakupa dawa leo hautaota tena.
CHIZI:-Hiyo dawa nipe kesho sababu leo wanacheza fainali, na nilibet[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nimepita Hapa Central Police Station Nikaona Signboard Inasema:
"MAN WANTED FOR ROBBERY..."
Nimeingia Ndani Kuapply For The Job,
Waneniweka Kwa Room Flani Hapa tupo kama 10, vidirisha vidogoooo!!,
but I Think Ni Interview Room[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Polisi ametusimamisha tukiwa na taxi akamuuliza dereva:- Mbona number za mbele hazifanani na za nyuma?
Dereva wetu akamjibu:- Wewe kwani uso wako unafanana na makalio yako?
Tumecheka hadi sasa bado hatujaachiliwa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
TANGAZOOO!!!
TANGAZOOO!!!
TANGAZOOO!!!
MUWE MAKINI
Mabibi na Mabwana
Waume na wake,
Wadogo na Wakubwa,
Vijana na Mabinti,
Wenye mimba na wasio Nazo,
wanaonyonyesha na wanaonyonya,Wachungaji na Mashehee,
Wachawi na Wanga,
Wezi na majambazi
Nadhani mnaona kabisa sina hata lakusema juu yenu, ninyi mashahidi[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Umbali kutoka DAR kwenda ARUSHA ..
ni sawa sawa na umbali kutoka ARUSHA kwenda DAR.
Lakini Umbali kutoka IJUMAA mpaka JUMATATU ni mfupi kuliko umbali wa kutoka JUMATATU mpaka IJUMAA[emoji12]
 
Leo nimeingia Supermarket pale Kibo Complex Tegeta,..Basi nikachukua Mkate Mkubwa na Maji,
Ajabu tangu nachagua bidhaa kwenye Shelf kuna Mzee mmoja alikuwa ananifuata nyuma mpaka nikaogopa,
nikaenda kaunta kwa Cashier bado ananifuata nyuma!,
Nikarudi kwenye Shelf kuchukua Soda bado Mzee yupo! Duh!
MZEE : Sory kijana kama nimekutisha, unafanana sana na Mwanangu aliyefariki juzi na kuzikwa Makaburi ya Kinondoni,
MIMI: kwa hiyo mzee unataka kusema nini?
MZEE : bahati mbaya Mwanangu amefariki bila hata kusema bai, naomba unisaidie kitu kimoja, wakati naondoka nikikupa Mgongo walau useme BAI BABA! Ili nijisikie kama niliagwa na Marehemu Mwanangu jamani!, nisaidie (akatokwa machozi)
MIMI: hilo tu? Usijali Mzee!.
Kisha Mzee yule akachukua bidhaa zake mafurushi kibao mpaka pale kaunta akahesabiwa vitu vyake akabeba na kunipa Mgongo ili nitimize alichoomba.
MIMI : Bai baba!
MZEE: Bai Mwanangu Mpenzi, asante!!
Mzee yule alipoondoka nikaenda Kwa Cashier na kupigiwa hesabu
CASHIER : Kaka Unadaiwa Tsh 238,500/=
MIMI : kivipi? Yaani Mkate, Maji na Soda pesa yote hiyo? Acha Wizi wewe dada!!
CASHIER: wewe unadaiwa sh 8500 na Baba yako amesema unamlipia bili yake sh 230,000/=
Ngachoka kabisa!...By the way bado nipo hapa napiga Misamba na madekio!...leo nipo night shift, Korido ya juu kule TRA nitadeki kwa Ulimi![emoji23] [emoji23]
 
John : Mpenzi, kweli nakuhitaji naomba uwe wangu.
Kademu: Lol, samahani Nina boyfriend wangu.
John : Kweli ila Hata miamba ya Goli ina makipa lakini mastraika wanafunga.
Kademu : Haha,upo kama beki Sasa Katika hili.
John : Sergio Ramos ni beki lakini ana magoli mawili Katika Fainali za Ligi ya Mabingwa.
Kademu : Vyovyote, Boyfriend wangu ni mrefu na ni tajiri.
John : Sikia,Manuel Neüer ana Futi 6.4 Ila Messi bado anamfunga kwa kuchop.
Kademu : Sawa ila unajua Messi ni tajiri kuliko Neüer ?
Nina uhakika na hilo.
John : ni Kweli Lakini Messi Sio mrefu kama Neüer kwahiyo Hapo ni 1-1.
Kademu: Hujawahi Kukata tamaa wewe?
John : Chile wamecheza Mpira kwa miaka 99 bila kushinda Copa America,Lakini Wamekomaa na Wamelipata.
Kademu : Uelewa wako Wa soka Unaweza kukupatia nafasi sehemu.
John : Kabisa na Next destination ni kwenye Moyo wako.
Kademu : Jamani, Af Unajua nitakublock Sasa hivi
John : Mwaka 2006, Petr Cech alijaribu kumblock Stephen Hunt ili asifunge,Baadae Aliishia kuumia na nasfi yake.
Kademu: We ni Genius, NIPITIE SAIZ,NIPO FREE.
John : NAKUFATA[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…