Mdada alienda super-market kununua
kuku, bahati mbaya kwenye friji
kulikuwa na kuku mmoja tu.
Muuzaji akamtoa akamuweka kwenye
mzani, akaonekana ana kilo moja na robo.
Mdada akamuuliza muuzaji, ’Huna mkubwa zaidi?’
Muuzaji akamchukua yule kuku na
kujifanya kamrudisha kwenye friji, halafu
akamtoa tena kwenye friji na kumrudisha kwenye mzani, safari hii akagandamiza mzani kwa gumba, kuku akaonekana ana kilo mbili.
Mdada akasema "Duh afadhali huyu
mkubwa kidogo, naomba unifungie
nawachukua wote wawili"[emoji13] [emoji13]