Whatsssssss!!!!!!!!!????

Kumbe si kinyonga tu anayebadilika kulingana na mazingira.
Kumbe hata binadamu pia hubadilika!
Nitakupa mifano
maana wewe kwa ubishi sikuwezi;
Mtu akiwa kwenye
Basi unaitwa Abiria,
Mtu akiwa stendi ni Msafiri,
Akiwa darasani Mwanafunzi,
Akiwa Garage ni Fundi,
Akiwa Shamba Mkulima,
Akiwa Kanisani Muumini,
Akiwa gerezani mfungwa,
Akiwa hospitali mgonjwa,
Akiwa kwenye jeneza marehemu.
Sasa kuna kitu kinaniumiza sana kichwa:
Je!, mtu akiwa chooni anaitwaje?[emoji12] [emoji13]
 
Kuna mahadhimisho ya smartphone jumamosi ijayo
Techno-Mtakutana viwanja vya Jangwani
Huawei - Viwanja vya Mnazi mmoja
Nokia-Viwanja vya Biafraa
Samsung - Ukumbi wa Diamond Jubilee
Blackberry -Viwanja vya leaders club
HTC-Viwanja vya Karimjee
Sony-Serena Hotel
LG-Golden Tulip
Iphone - Kilimanjaro Hotel....
Je wewe utakuwa wapi?najua wengi mtakutana jangwani[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
And when a student fails an exam, his father says:-

In the UK:- "U can still do better darling"

In the US:- "Yes you can, I know you can".

In Tz:- "Hivi kumbe niliuza Ngo'mbe na nikapeleka Ng'ombe mwingine shule ee!?"[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wazee wa kichaga bwana ni noma:-
Mzee mmoja alikuwa kila siku usiku anapita mbele ya Bank anasimama na gari lake, kisha anapiga honi, akitoka askari mlinzi, anaondoka.
Hilo jambo likamkera sana askari mlinzi, akamvizia alipokuja tena akamkamata...!
Akamuuliza:- Kwa nini kila siku unakuja unapiga honi kisha unakimbia?
Mzee akasema:- Haki ya mungu babaangu, Nina pesa zangu katika account hapa Bank naogopa usilale usingizi, ndio maana kila siku usiku napita kukuangalia kama umelala[emoji23] [emoji23]
 
Mwaka jana mwishoni nilimpa rafiki yangu namba ya mpenzi wangu amjaribishe kama atamkubalia maana mpenzi wangu alikuwa ananiambiaga hawezi nisaliti na hakuna kama mimi.
SASA Jumamosi hii NI HARUSI YAO!![emoji15]
 
Nimetumiwa sms na bodi ya mikopo kuwa nadaiwa .wamenipa siku 30 nijisalimishe.
Nimewambia mbona sijasoma chuo kikuu wananambia mbona kila siku najiunga vifurushi vya chuo[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
KIFO SI MCHEZO! Familia ilivamiwa na majambazi,yakapanga kuwaua wote ila kabla ya kuwaua yaliamua kuwauliza majina yao kwanza.
Jambazi:wee unaitwa nani?
Mke:naitwa Elizabeth.
Jambazi:umesalimika mana jina lako ni km la mamangu...
Jambazi:eeh! na wewe je?
Mume:naitwa John ila kazin wananiita Elizabeth[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mchooni, Msalani, mnyaji, mkata kimba au mkimba kimba! [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa 1 alikuwa amelala na mke wake, katikati ya usiku mke akaweweseka "wewe amka uondoke mume wangu anakuja". Mume ghafla akakurupuka akabeba nguo zake na kurukia dirishani, duh! Kufika mbali akakumbuka "aaah !Kumbe leo nimelala nyumbani kwangu!"
Je kati yao nani ni msaliti wa mwenziwe?[emoji12][emoji13][emoji13]
 
Unajua tangu tufiwe na bro wetu Remmy Ongala, nikikuona wewe roho inaniuma sana sana!
Ama kweli duniani wawili wawili[emoji12]
 
HUYU MLOKOLE HAFAI: Alikwenda kwa wakwe akalishwa viazi, si akala kiazi cha moto akaona aibu kukitema akaamua kukimeza, mara chozi likaanza kumtoka..
Akaulizwa vipi mbona unalia?
Akajibu, nakumbuka mateso ya Bwana Yesu pale msalabani kwa ajili yetu[emoji1][emoji1]
 
Boss Aliacha Zipu Ya Suruali Yake Waz. Sasa Secretary wake Akamshtua Na Kumwambia:
Boss Umesahau Kuifunga Garage iko Wazi.
Boss: Duh! Sorry Umeiona Benz Yangu?
Secretary: Hapana Ila Nimekiona Kibajaji Kidogo Chenye Tairi 2 Zenye Pancha![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
VP tatizo lako la kingereza limeisha ama bado? Unakumbuka siku ile ulipoenda hoteli ya kitalii na ukahitaji kula kuku lakini hujui anaitwaje ila ulipoona mayai kisha ukamwambia mhudumu:
You waiter you see that?
Waiter; yes,
Ukamwambia I need their mother.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mzee wa miaka 60 alimwambia mkewe, leo nataka tukumbukie enzi zetu kutongozana, mke akajibu sawa, inabidi unisubiri mwembeni saa 1 usiku nitapita, mzee akafika saa 1 alikaa hadi saa 5 usiku, aliporudi nyumbani akamuuliza mkewe kwa hasira; sasa tumepanga nin halafu haujatokea ? Mke; leo mama alinikataza nisitoke nyumbani usiku nijisomee ! Babu hoii.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
WIVU MBAYA!!!!
JAMAA ALIUGUA KANSA KWENYE INI IKASAMBAA MPAKA HALI IKAWA SIO, IKASHINDIKANA MATIBABU AKASUBIRI KUFA TU,
SIKU MOJA MWANAE AKAMUULIZA:-
MTOTO: HIVI BABA KWANINI WATU WAKIJA KUKUSALIMIA UNAWAAMBIA UNA UKIMWI, WAKATI NI KANSA!?
BABA: WE HUJUI TU, WAPUUZI SANA HAWA, USIPOWAAMBIA HIVYO NIKIFA WATANIIBIA MKE WANGU[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ebu chemsha bongo,Umeipenda Nguo Dukan Bei 10,000/= HUNA PESA. Ukakopa kwa Dada Yako 5000/= na kwa Kaka Yako 5000/= Ukenda Kununua Ukalilia Bei..
Ukanunua kwa 9,700/= Ukarudishiwa 300/= Ukapunguza Deni Ukampa 100/= Kaka na 100/= Dada, Ukabakiwa na 100 ilinde Mfuko. Hivyo Una Deni kwa Kaka 4900/= na kwa Dada 4900/= Ukijumlisha ni 9800/=, Ukiongeza ile 100/= ya Kwako Inakuwa 9,900/= JE 100/= Imekwenda Wapi?[emoji12]
 
Mwalimu wa Kiswahili:
Je!, Kama una Chocoleti 12!
1. Anitha ukampa 5
2. Betha ukampa 3 na
3. Judy 4.
Utabakiwa na nini!?
Mwanafunzi: Wachumba wa3 wapya[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Baba yake Mary anawatoto watano:-
1. Nana
2. Nene
3. Nini
4. Nono
Jina la mtoto wa tano ni nani!?[emoji12]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…