Whatsssssss!!!!!!!!!????

itakua alimchoka hadi kero [emoji12] [emoji12]

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Mwalimu Wa Stadi Za Kazi Aliingia Darasani Akawaambia Kila Mwanafunzi Amchore Tembo,
Kila Mwanafunzi Akawa Bize Kuchora
Kisha Mwalimu Akawa Anapita Kukagua Akafika Kwa Zuzu,
Mwalimu: Eeeh Si Nilisema Mchore Tembo Mbona Wewe Umeweka Nukta?
Zuzu: Na Mimi Nimemchora Ila Yuko Kwa Mbaaaali.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Zuzu Alikuwa Anaandika Barua Mara Akatokea Rafiki Yake Akamuuliza:
Rafiki: Iyo Barua Unamwandikia Nani?
Zuzu: Najiandikia Mwenyewe.
( Jamaa Akacheka Sana Halafu Akamwambia)
Jamaa: Kwahiyo Barua Yenyewe Inahusu Nini?
Zuzu: We Vipi Nitakuambiaje Wakati Haijanifikia.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mfugaji Alitembelewa Na Mwandishi Wa Habari Kwakua Hawapendi Waandishi Akaamua Kumpa Majibu Ya Kumchosha.
Mwandishi: Unawalisha Chakula Gani?
Mfugaji: Ng'ombe Yupi Mweupe Au Mwekundu?
Mwandishi: Mweupe.
Mfugaji: Namlisha Nyasi Na Viguta Vya Mahindi.
Mwandishi: Na Mwekundu.
Mfugaji: Vile Vile Namlisha Nyasi Na Viguta Vya Mahindi.
Mwandishi: Ahaa Sawa Sehemu Ya Kulala Ni Wapi?
Mfugaji: Yupi Mweupe Au Mwekundu?
Mwandishi: Mweupeee!
Mfugaji: Mweupe Bomani Kulee.
Mwandishi: Na Mwekundu?
Mfugaji: Vile Vile Ninamlaza Na Mwenzie.
Mwandishi: Hii Sehemu Yote Majumba Mengi Na Wakienda Kulisha Unafanyaje?
Mfugaji: Yupi Mweupe Au Mwekundu?
Mwandishi: Wooote (Kwa Hasira)
Mfugaji: Mweupe Ninamfunga Kamba Na Kumzungusha Malishoni Na Kumrudisha.
Mwandishi: Na Mwekundu?
Mfugaji: Ninamfunga Kamba Na Kumzungusha Kama Mwenzie.
Mwandish: Kwanini Kila Mara Nikikuuliza Huduma Za Ng'ombe Unaniuliza Mweupe Au Mwekundu Halafu Kazi Zao Wote Sawa?
Mfugaji: Kwasababu Mweupe Ni Wangu.
Mwandishi: Na Mwekundu?
Mfugaji: Ni Wangu Vile Vile.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi Unaikumbuka Hii Misemo Ya Utotoni???
1. Dogoro => Godoro
2. Sempeli => Penseli
3. Gloo => Droo
4. Kipombe => Kikombe
5. Shamoo => Shikamoo
6. Pichisi => Chipsi[emoji12][emoji23][emoji23]
 
Mtoto: Mama Mi Nashangaa Sana.
Mama: Unashangaa Nini?
Mtoto: Mbona Uyu Jirani Anatoa Msaada Kwetu Mkubwa Hivi Inakuwaje?
Mama: Yani We Jua Kila Kitu Ningekua Namtegemea Baba Yako Hata Wewe Usingezaliwa.[emoji12][emoji13][emoji13][emoji13]
 
Kuna Jamaa Na Mke Wake Waliangaika Sana Kutafuta Mtoto Walienda Kwa Waganga, Mahospitali Na Wataalamu Mbalimbali Lakini Ikashindikana,
Ndipo Kuna Mtu Akawashauri Waende Kwa Padri,
Walipofika Kwa Padri Na Kumuelezea Akawaambia Wana Bahati Sana Maana Kesho Kutwa Anaenda Kwa Papa Na Atauwasha Mshumaa Wa Baraka Na Watapata Mtoto,
Na Padri Akasafiri Akakaa Miaka 4 Akiwa Masomoni Na Baadaye Akarudi Na Yule Jamaa Aliposikia Padri Amerudi Akafanya Haraka Akaenda Na Padri Alipomuona Akafurahi Na Kumuuliza Kuhusu Familia Yake,
Jamaa Akajibu " Hilo Ndo Lililonileta Yani Mwaka Ule Wa Kwanza Ulipoonda Mke Wangu Akajifungua Mapacha 2 Na Mwaka Uliofuata Mapacha 3 Na Mwaka Uliokuja Mapacha 4 Na Mwaka Huu Ni Mjamzito Tafadhali Padri Kazime Mshumaa. "[emoji120]
 
Jamaa Mmoja Alikuwa Anapiga Chabo Dirishani Huku Wanandoa Wanaendelea Na Mambo Yao,
Na Kuna Jamaa Alikuwa Anapita Anaendesha Baskeli Ghafla Tairi Likatoa Mlio Wa Pancha Na Wanandoa Waliposikia Ndani Wakaacha Kufanya Yao,
Yule Jamaa Wa Chabo Huku Akiwa Amenogewa Akaropoka " JAMANI ENDELEENI HIYO PANCHA TU." [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wagogo Flani Walienda Kumtembelea Mwenzao Mjini
Walipofika Akawanunulia Soda Na Baada Ya Kunywa Mmoja Akaficha Kisoda,
Na Walipokuwa Njiani Wanarudi Mmoja Akamwambia Mwenzake "Hivi Unajua Nimeficha Mbegu Tuliyokunywa." [emoji12][emoji13][emoji13]
 
JAMAA: Unajua Mi Nataka Kuwa Pilot.
DEMU: We Hiyo Acha Tu.
JAMAA: Kwanini?
DEMU: Umeshindwa Kurusha Vocha Ndo Utarusha Ndege.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bakari Ni House Boy Kwenye Nyumba Flani Na Mara Nyingi Anakunywa Wine Ya Bosi Na Kuichanganya Maji Bosi Alimgundua
Baba: Bakari.
Bakari: Naam Baba.
Baba: Kwanini Unaiba Wine Yangu?
Kimya.
Baba: We Bakari?
Bakari: Naaam.
Baba: Kwanini Unaiba Wine Yangu?
Kimya.
Akaamua Kumfata Jikoni,
Baba: We Mbona Nikikuita Unaitika Halafu Nikikuuliza Unakuwa Kimya?
Bakari: Yani Baba Huku Jikoni Sijui Kuna Nini Yani Unasikia Jina Tu Kama Unabisha Nenda,
(yule Baba Akaenda)
Bakari: Baba.
Baba: Naam Bakari.
Bakari: Kila Siku Saa Sita Unaenda Kufanya Nini Kwenye Chumba Cha Housegirl.
(Kimya)
Bakari: We Baba?
Baba: Naam.
Bakari: Uwa Unaenda Kufanya Nini Kwenye Chumba Cha Housegirl?
(Kimya, Na Akatoka)
Baba: Kweli Ulivyosema Yani Unasikia Jina Tu.
Mara Akatokea Mama Akawauliza Walikuwa Wanabishana Nini.
Bakari: Yani Ukiwa Jikoni Unasikia Jina Tu Kama Unabisha Nenda (Akaenda)
Bakari: Mama.
Mama: Abee.
Bakari: Iyo Mimba Ya Baba Au Yangu?
Kimya.
Bakari: Iyo Mimba Ya Nani?
(Kimya, Akatoka)
Mama: Kweli Ukiwa Humu Unasikia Jina Tu[emoji12][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Baba Flani Alimtuma Mwanae Vocha Ya 1,000 ,
Dogo Akaenda Akarudi Baba Akamuuliza,
Baba " Mbona Hujaleta Vocha?"
Dogo " Za 1000 Zimeisha Zimebaki Za 500"
Baba " We Kweli Unanipotezea Ada Zangu Tu Sasa Si Ungeleta Za 500 Mbili.
Siku Nyingine Akamtuma Akanunue Gazeti La Tarehe 10, Dogo Akaenda Akarudi Na Magazeti Mawili,
Baba " Mbona Umenunua Mawili?"
Dogo " La Tarehe 10 Nimekosa Nimenunua Ya Tarehe 5 Mawili." [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa Akiwa Kuzimu Akaomba Ampigie Simu Mkewe,
Akapewa Apige, Alipomaliza Kuongea Akauliza " Gharama Za Kupiga Ni Sh.Ngapi?"
Akajibiwa "Kuzimu Kwenda Kuzimu Ni Free." [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa: Dada Mambo?
Mdada: Powa.
Jamaa: Samahani, Hivi Upo JF?
Mdada: Hapana.
Jamaa: Twitter?
Mdada: Sipo.
Jamaa: Whatsap?
Mdada: Sipo.
Jamaa: Instagram?
Mdada: Sipo.
Jamaa: Eeeeh Sasa Uko Wapi?
Mdada: Niko M-pesa.[emoji12][emoji13][emoji13]
 
MDADA: pm yako sijaiona
JAMAA: msaada kila nikituma pm zinafeli
MODS : zihamishe shule[emoji12][emoji13][emoji13]
 
Jamaa Flani Mchaga Alidumbukia Kisimani, Mkewe Akaja Na Kamba Kumtoa,
JAMAA: Iyo Kamba Umenunua Wapi?
MKE: Duka La Hapo Nyuma
JAMAA: Sh.Ngapi?
MKE: 1,000.
JAMAA: Arrrrghh Iyo Rudisha Ebu Nenda Pale Kwa Massawe Anauza 500 Fanya Haraka Nazama."
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Denti Flani Baada Ya Kushindwa Kujibu Maswali Akaandika Hivi Kwenye Karatasi Ya Majibu
////////////////
" KWANGUA UTAONA MAJIBU"
[emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa Mmoja Alienda Kuomba Kazi Ya Ulinzi,
Bosi Akawa Anamhoji,
Bosi " Kazi Ya Ulinzi Unaiweza? "
Jamaa " Ndiyo Naiweza."
Bosi " Una Elimu Gani? "
Jamaa " Nimesoma Mpaka Form 4."
Bosi " Unajua Kuongea Kingereza? "
Jamaa " Eeeeh Kwani Hao Majambazi Wanaokuja Kuiba Ni Wazungu.."[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…