Whatsssssss!!!!!!!!!????

Unamtumia baba yako meseji ukiwa shule "
Baba naomba unitumie 100,000 ya pckt mny'"anakuuliza pckt mny ndo nini? Unamjibu ni kifupi cha pocket Money halafu anakutumia 10,000/=, unamuuliza hiyo hela ni ya nini? Anakwambia ni kifupi cha 100,000.
Baba Hapendi Ujinga Kabisa[emoji23][emoji23]
 
BABA: kwanini umefeli?
MTOTO: sina akili
BABA: sasa leo nitakupiga fimbo hadi upate akili
MTOTO: Kama fimbo zingeleta akili, basi punda angekuwa profesa
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Mhindi aliambiwa amalizie methali za
Kiswahili
1.Nyani haoni:
[emoji117]Valisa miwani
2.Debe tupu:
[emoji117]Weka unga
3.Asiyesikia la mkuu:
[emoji117]Peleka yeye polisi
4.Bandu bandu?
[emoji117]Baba yake Somji iko Bombay
5.Simba mwenda pole:
[emoji117]Huyo naogopa yanga
banah.
6.Chovya chovya:
[emoji117]Mwisho yake tapata mimba
7.Maskini akipata:
[emoji117]Itaacha iba jumbani
8.Penye kuku wengi:
[emoji117]Chinja bili au tatu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa 1 alikua anafundishwa kuswali akaambiwa na shehe kwamba baada ya Tahiyatu toa salaam.
Jamaa alipomaliza tu tahiyatu akaanza kwa sauti. Namsalimu kaka Juma wa Tandale,
Saidi wa kigamboni,
Mamdogo zaina wa ilala,
Mwisho kabisa ni Haji wa mbagala.
Shehe: mtihani mkubwa huu[emoji120]
 
Jamaa kaenda dukani siku ya
kwanza ikawa hivi
JAMAA: za saa hizi kaka nimekuja kununua chakula cha mbwa
MUUZAJI: mbwa wako yupo wapi??
JAMAA: yupo nyumbani
MUUZAJI: samahani kaka huwa hatuuzi chakula cha mbwa mpaka tumuone mbwa mwenyewe.
Zikapita siku mbili jamaa akaenda dukani tena
JAMAA: za saa hizi kaka nimekuja kununua chakula cha paka
MUUZAJI: paka wako yupo wapi??
JAMAA: yupo nyumbani
MUUZAJI: samahani hatuuzi chakula cha paka mpka tumuone paka mwenyewe
zikapita siku 3 jamaa akaenda dukani na mfuko
JAMAA: kaka ingiza mkono ndani ya mfuko huu
MUUZAJI: kuna nini kwani?
JAMAA: we ingiza tu kaka
muuzaji kuingiza kutoa akashika kinyesi
JAMAA: hicho ni kinyesi changu nimekuja uniuzie toilet pepa maana najua ningekuja ungesema hamuuzi toilet pepa bila kuona, nimeamua kukwepa usumbufu [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23]
 
HAKIMU: Una chochote cha kujitetea
MTUHUMIWA: ndio
HAKIMU: jitetee
MTUHUMIWA: "Aliyeniibia Mimi Mali, kaibiwa na aliyekuibia Wewe siku nilipo muibia Mimi. Je Mali Iko kwa nani?
HAKIMU: kuanzia sasa upo huru [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mmasai alipewa kipaza sauti msibani ili aseme japo machache mambo yakawa hivi
" Musiba oyee , jenesa safii? mwenye wifu akufe kama hii mutu hapa kwenye jenesa ,
kwansa kabisa napenda kushukuru hii marehemu hapa sababu ina upendo , nafanya sisi nakutana leo , nakula wali musuri, nakunywa bia na maji ile nauswa kwa duka. Naomba kesho ikufe ingine tubaki hapa tukule, tukunywe mpaka siku ya munada.
Musiba oyeee[emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtalii amekodi boti anazunguka nalo kwenye mto zambezi kuangalia mandhari, akamuuliza kijana anayeongoza boti,
MTALII: do you know biology, psychology and anthropology?
KIJANA: no
MTALII: what the hell do you know under the sun? You are useless, and you will die with your illiteracy!”
baada ya muda boti ikaanza kuzama,
KIJANA: do you know kuogeleaology and kusepaology from mambaology?
MTALII: no
KIJANA: you will kufalogy and mambalogy will eat you because of your bad-mdomology [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtanzania na mzungu walipanda ndege bahati nzuri walikaa pamoja na mambo yalikuwa hivi;
MZUNGU: watanzania siku zote ni wajinga sana
MTZ: kwa nini?
MZUNGU: tuulizane maswali ukishindwa kujibu utatoa sh 500 na mm nikishindwa nitatoa sh 100,000 ok?
MTZ: ok, anza wewe
MZUNGU: ni nchi gani ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya dunia?
MTZ akatoa sh 500 kuashiria kwamba hajui
MTZ: ni kitu gani kikiwa angani kina miguu minne kikitua kina miguu mitatu?
MZUNGU akatoa sh 100,000 kuashiria kwamba
hajui ila akaomba aambiwe ni nini hicho?
MTZ akatoa sh 500 kuashiria na yeye pia hajui.[emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Walikutana madaktari 3 wa China, Ujerumani, Tanzania kuelezea mafanikio walioyafikia katika nchi zao. DK wa UJERUMANI: kwetu alizaliwa mtoto hana miguu tukamwekea ya bandia sasa ni mwanariadha na ana medali 3 za dhahabu DAKTARI wa CHINA: sisi kwetu alizaliwa mtoto hana mikono tukamwekea ya bandia sasa ni mcheza kareti maarufu sana duniani
DAKTARI wa TANZANIA: akacheka kwa dharau akasema hamjatufikia sisi kwetu alizaliwa mtoto Bagamoyo hana kichwa tukamwekea dafu [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa kaambiwa na demu wake
Happy birthday baby
Jamaa kajibu: happy birthday too

Kizungu witooo
 
10 hrs mkuu Supermarket hujaweka vichekesho vipya? Jitahidi please utupie vingine. Wengine ndo imegeuka relaxation yetu and we are hooked. Hope you are OK!
 
Sio kwa kutesa mbavu zangu hivi.
Mungu anakuona
 
10 hrs mkuu Supermarket hujaweka vichekesho vipya? Jitahidi please utupie vingine. Wengine ndo imegeuka relaxation yetu and we are hooked. Hope you are OK!
Poa mkuu nipe dkk 3 tu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Usisahau: target yangu vitimie vichekesho 1,000 ( 1k replies) ndo nitaomba likizo.
-nina wiki sasa sijaingia jukwaa la MMU, SIASA wala celebrities.
 
 
Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku wakaamshwa na mtu akipiga hodi mlangoni kwao. Wakabishana nani akafungue hatimae mume akiwa usingizini kaenda na kufungua mlango. Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
MUME: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia
MLEVI: Okay nisukume basi. [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…