Fuata historia, safari za Kikwete na kukutana na Museveni kule New York ndio zilitumika kumbadilisha Museveni mawazo na kuwaza safu ya Tanzania
TANZANIA : Museveni and Kikwete discuss the pipeline in New York
Mtaukataa huo ukweli lakini rais wenu huyo wa awamu ya nne pamoja na mapungufu yake ya kutopigana na ufisadi ipasavyo, lakini aliiweka Tanzania kwenye ramani ipasavyo. Yeye kidogo alikua ameanza kuileta Tanzania kwenye level yetu, na kikubwa uhusiano baina yetu haukua wa ugomvi ugomvi kama mnavyojitutumua siku hizi.
Leo hii hamna jipya zaidi ya visasi na mikwara na uchokozi usiokua na tija, mnaibua ugomvi kila uchao na makelele mengi ila mwisho wa siku ukuaji wa uchumi haujafikia level aliyokua amewafikisha Kikwete ya 7.3%.
Alichukua uongozi GDP yenu ikiwa 16b USD akatoka ikiwa 48.2b USD.
Vitu vingi mnazindua leo, alivianzisha Kikwete, masterplan zote zake, hata reli mnazotutambia kila siku kazifanyia planning zote, kama unajua kudadavua uchumi kitaalam nenda kasome mlivyokua kwenye MDG kabla yake na wakati anaachia uongozi, pia kabla yake tegemezi lenu la ufadhili kwenye bajeti ilikua 42%, aliondoka kama imepungua hadi 8%
Ugomvi wa Kenya na serikali ya Kikwete ulikua ukiibuka mara kwa mara, lakini ulikua unazimwa in a very diplomatic and statesmanship way, sio kuropokeana.