Jamaa uko idle sana. Ukizeeka utaregret yale masaa yote uliyoyapoteza kwenye internet wakati Wakenya na Watanzania wajanja humu jf wanaingia humu dakika tano tu kila siku kisha wanasepa wanaenda kusoma au kufanya kazi. Wananunua mashamba, magari, wanafanya biashara na kadhalika. Wewe uko hapa tu unapost kuhusu Kenya na maisha inakupita. Wanasema "Time" is a precious resource, once it leaves it never comes back. Tumia muda wako vizuri ndugu yangu, siku za usoni usije ukawa mzee wa miaka sabini umekaa hapo ubungo flyover na kibakuli unaomba mapeni kutoka kwa akina Kadoda11, Motochini na Ichoboy ambao watakuwa wachoyo wanakunyima pesa. Tafuta pesa saa hii wakati una nguvu. Wachana na Kenya, wengine wetu ni Wakenya lakini hatuko Kenya saa hii bali tuko kwenye nchi za wenyewe tukitafuta pesa kwa ajili ya siku za usoni. Mimi sina fikra za Kenya sana japo mimi ni Mkenya halisi, basi mbona wewe ufikirie Kenya usiku na mchana?