Cute Wife
Platinum Member
- Nov 17, 2023
- 3,054
- 8,449
Wakuu,
Watanzania tulipokea barua ya Nchimbi kujiuzulu kupitia mitandao ya kijamii, hakutoa Press au kusikia akihojiwa sehemu, na baadaye Rais Samia akasema amepokea barua yake ya kujiuzulu, kamati ya CCM ikasema imemvua uanachama na kwamba hawamtambui tena na Makamu wa Rais mteule akatajwa!
Pia soma
~ https://www.jamiiforums.com/threads/makamu-wa-rais-dkt-emmanuel-nchimbi-ajiuzulu.2466077/
~ https://www.jamiiforums.com/threads...s-wa-jamhuri-ya-muungano-wa-tanzania.2466316/
Siku chache kabla, mpaka kutangazwa kwa taarifa hiyo Nchimbi hajaonekana wala kusikia chochote kutoka kwake. Kule nyuma wanasema kama Nchimbi angekuwa nje ya nchi tungepata neno, walau hata yeye mwenyewe kutangaza kwa video kujiuzulu kwake au hata kuthibitisha kuwa taarifa zilizotolewa ni za kweli. Maana baada ya tu ya barua ile kuonekana kwenye kurasa yake ya mtandao wa kijamii watu walikuwa wanajiuliza kama ni kweli au lah, barua yenyewe ilionekana ya mchongo.
Sauti za kwenye korido zinasema Nchimbi yupo humuhumu ndani, ila amekula kibano (house arrest) huku akiondolewa njia zozote ambazo anaweza kuwasiliana na mtu, ili waweze kukata wale wote waliokuwa wananmpa nguvu au kumsaidia kwa namna moja au nyingine kwa chochote alichokuwa anapanga.
Pia soma https://www.jamiiforums.com/threads...-yanafanyika-kinyume-na-matakwa-yake.2466930/
I mean ukijiweka kwenye nafasi yake, na anamuona Nchimbi kama tishio, baada ya kumbananisha lazima kwanza uzuie njia zozote ambazo anaweza kuwasiliana na umma au jumuiya za kimataifa, then utaanza kufuatilia nani alikuwa anamsupport au kumpa bichwa kwenda kinyume na yeye, then unaangalia nani anamdhara kati ya hao ili uwashughulikie pia kwa kuwa wanaweza kuharibu mipango yako and may be hata kukuchomoa hapo ulipo. Unaendelea kumshikilia mpaka uhakikishe umekata mabawa yake yote ili asiweze kuruka.
Ila kwa upande mwingine kumuweka Nchimbi kwenye kibano (kama ni kweli), Makamu wa Rais ambaye huna kitu solid ambacho unaweza kutumia dhidi yake, unakuwa unazidi kujichimbia shimo na kuonekana huna nia ya kushusha joto linaloendelea nchini.
Ni kweli anaenda kuangushiwa jumba bovu la mauaji ya Oktoba 29? Baada ya kutangazwa uamuzi wa kumvua uanachama Nchimbi, kuna magazeti yameanza kuandika kuwa mambo yameanza kufichuka na kuhusanisha ushiriki wa Nchimbi kwenye matukio hayo - kwahiyo wanamwanchia Lissu, anavikwa yeye zigo, nchi inapata mtu wa kumlaumu halafu mambo yanaisha hivyo tunarudi kwenye furaha eti?
Tukirudi kwenye suala la msingi; NCHIMBI YUPO WAPI?