Which engineering field has the best scope?


Watu wengine kwani ukisema unaishi chumbageni utadharauliwa? Njoo tu ukasome unachotaka huwezi kuamuliwa na mtu kuhusu maisha yako
 
Hivi hakuna visas restriction kwenye employments?! Ni kitu gani kinawashinda uhamiaji kuweka vikwazo kwenye kazi zinazoweza kufanywa na watanzania wenyewe? Rate of unemployment is very high Tanzania, vijana wenzangu wamemaliza chuo kikuu lakini wapo vijiweni kutokana na uhaba wa ajira, halafu wageni wanakuja kufanya hizo kazi kwa viwango duni...inasikitisha!
 
Mkuu samahani, hivi Mech engineering ndo ufundi makenika? Kama ndio vipi opportunities unazoongelea ni car garages ama??
ME sio machines na magari, ni very broad field, ukiangalia karibu vitu vingi ninavyokuzunguka mechanical engineer wamehusika kwa kiasi fulani kudesign.Kwa mfano switch ya umeme "on and off" button ni ME, robot, injection molding systems,computer keyboard ni ME hata kwenye Oil and gas wana play part kubwa.Lakini tatizo letu Bongo hatuko kwenye kudesign, huko tumewaachia wazungu, sisi tupo kwenye spanner zaidi.
 

Mungu akubariki, hasa kwa kuitumia elimu yako kwa ajili ya kuelimisha na wengine, Nice job brother
 
Watu wengine kwani ukisema unaishi chumbageni utadharauliwa?
hawezi dharauliwa, ila hii ni sehemu ambayo amtu ana uhuru wa kusema anachojiskia ila asivunje sheria na katika hili sidhani kama mleta mada kakosea!!
Njoo tu ukasome unachotaka huwezi kuamuliwa na mtu kuhusu maisha yako
naamini hata wewe kuna kipindi uliomba ushauri, nadhani ungetofautisha kati ya USHAURI na KUAMULIWA MAISHA mkuu!!
 
Hivi hakuna visas restriction kwenye employments?! Ni kitu gani kinawashinda uhamiaji kuweka vikwazo kwenye kazi zinazoweza kufanywa na watanzania wenyewe?
kisha akaniambia machenical Eng nzuri ijapo limeshikwa na Wachina, sio kwa ubora wao wa kazi bali vifaa walivyonavyo na mitaji wanayo dhaminiwa na selkari yao.
haya ni maneno yaliyotajwa na mdau hapo juu... you have a good observation!! cha kwanza kujua ni kwamba sisi(tanzania) ni nci inayohitaji misaada toka kwa nchi washirika...nikupe mfano, kuna project labda ya kujenga mabwawa na china ikafadhili hiyo project, je unadhani hiyo tenda watapewa wachina au wazawa? jibu unalo...

Kuna factor nyingine ya capital hapa naongelea mitambo ya ujenzi, kwa hapa nyumbani tuna project inaefanywa kule bagamoyo, na hii project inahitaji contractor mwenye vifaa vya kisasa kitu ambacho kwa mainjia au makampuni ya ndani kiasi flani ni ngumu kupata, na wageni mara nyingi huwaga wanafadhiliwa na serikali zao in terms of capital!! na hii kiasi flani inawasaidia kuwin tenda mbali mbali!! na kuhusu swala la visa restrictions kwa nchi kama yetu ni ngumu ku-impliment sheria kama hizo hasa kwa wageni wa mataifa makubwa!!
Rate of unemployment is very high Tanzania, vijana wenzangu wamemaliza chuo kikuu lakini wapo vijiweni kutokana na uhaba wa ajira, halafu wageni wanakuja kufanya hizo kazi kwa viwango duni...inasikitisha!
I concur with you, but this is our home land and that is the reality ..ila sio kigezo cha kutopambana!!
 
Watu wengine kwani ukisema unaishi chumbageni utadharauliwa? Njoo tu ukasome unachotaka huwezi kuamuliwa na mtu kuhusu maisha yako
Ni sehemu gani kwenye posts zangu zimekupa impression nipo Chumbageni? Kama ningekuwa Chumbageni isingenipa tatizo kuandika hivyo kwa sababu sidhani watu hapa wanachangia kwa sababu mwanzisha thread yupo sehemu fulani. Angalia thread nyingine na utaelewa ninachosema.
 
Haya makampuni ya barabara and the like ni sawa, hata Membe akiwafuata uko China kwenye maofisi yao kuwapa viza ni sawa tu. Tatizo langu ni hawa wawekezaji wadogo wadogo wa kichina,kwa mafano wamachinga au kama "NI MTAZAMO TU" alivyosema mention hapo juu, wapo pia kwenye biashara ya garages.Sidhani biashara kama hizi sisi wabongo hatuna ujuzi au mtaji.Serikali wangeweka kipengele cha kiasi cha mtaji kwenye maombi ya viza za biashara.Lakini ili alinitatizi kutimiza ndoto yangu, kama wazungu wanavyosema " If you can't stand the heat, get out of the kitchen", nipo tayari kupambana.
 
Nimetolea mfano tu wa makazi sikumaanisha kuwa unakaa huko nilipokusema.

 
I hope I am not late to advise you, lakini kama uko nje ya Tanzania na unataka kurudi bongo, usisome any of the field ulizoweka hapo. Soma Petroleum Engineering.
 
Civil mtu anajiajiri vipi...naomba kamfano hata kamoja tu kanatosha
Note:ieleweke kuwa lengo langu ni kujua tu jinsi mtu anavojiajiri na sio kuonesha kuwa mtu hawezi jiajiri na civil..

unafungua kampuni inaitwa hardman general supplies&civil engineering, hapo utapewa tenda kujenga hadi barabara za mtaani, nyumba za serikali, na za wananchi
 
I hope I am not late to advise you, lakini kama uko nje ya Tanzania na unataka kurudi bongo, usisome any of the field ulizoweka hapo. Soma Petroleum Engineering.
Hauja chelewa... bado nina muda kidogo.
Nitaangalia hiyo kozi.
Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…