Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
BARUA KWA RAIS SAMIA SULUHU KUHUSU UFISADI KWENYE SUKARI
11 December 2021
Mheshimiwa Rais nakusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini ningependa badala ya kusema kazi Iendelee basi uitikie haki, ustawi wa watu na uhuru wa kweli.
Mheshimiwa Rais nina mengi ya kukueleza kuhusu nchi yetu lakini leo ningependa kukueleza moja ambalo ni maombi yangu kwamba utalifanyia kazi ili kuitoa nchi yetu katika uchafu huu mkubwa. Jambo hili ni ulanguzi katika bei ya sukari na ufisadi mkubwa uliopo katika eneo la bidhaa muhimu (nipatapo wasaa nitakuandikia barua zaidi kuhusu bidhaa nyingine kama mafuta ya kula). Nakiri kwamba bei ya bidhaa hizi inachangiwa na mwenendo wa bei ya soko la dunia lakini pia inachangiwa na ufisadi uliopo katika soko la ndani.
Kwenye sukari tuna kundi dogo la wazalishaji nchini na hawa wana kikundi chao ambacho kisheria si sahihi (cartel). Kikundi hiki kiko chini ya Seif Ally Seif ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Superdoll (wamiliki wa Mtibwa na Kagera Sugar). Bei za sukari zinaweza kupandishwa kwa namna mbili, kwanza kwa kuamua kiasi gani cha sukari viwanda vya ndani vizalishe, maana yake hapa unaamua kiasi gani cha sukari kiwe kwenye maghala.
Ukishaamua kiasi basi bei itapanda kuendana na kiasi. Maana yake ukiamua sukari uzalishe kidogo basi bei itapaa sababu bidhaa inakuwa chache na wahitaji ni wengi. Namna ya pili ni kushirikiana na watendaji walio serikalini kuhakikisha kwamba unapobana uzalishaji soko la ndani ili kuwe na uhaba na bei iwe juu basi serikali haitoi vibali kwa watu kuingiza sukari nchini sababu kwa kufanya hivyo uhaba hautakuwepo na bei unayotaka wewe itavurugika. Huo ndio mchezo unaochezwa Tanzania.
Ilikuwaje?
Endelea kusoma HAPA