Who created God? Who made him? Where did he come from?

Who created God? Who made him? Where did he come from?

nadhani mtu wa namna hiyo hayupo kuelewa... ukimuomba ushahidi kama limechomekwa kiujanja ujanja bado atakosa jibu! hawa watu ni watu wa ajabu sana, yaani mtu yupo radhi kuamini kwamba mambo fulani fulani yamechomekwa kiujanja ujanja kana kwamba alikuwepo enzi hizo... ila ukimwambia hivi anabisha
Hiyo ni tisa kumi ni pale anapokuja kukuona wewe ambae umeamua kuyaamini hayo maandiko kuwa sio mtu wa tafakuri wakati habari ya kuchomekewa maneno hata yeye ameisoma kama wewe ulivyosoma maandiko na akaamini kuwa ni kweli yamechomekewa kama wewe ulivyoamini kuwa maandiko hayo ni kweli

Akinya kuku kanya lakini akinya bata kaharisha

Kaazi kweli kweli ...!!
 
GOD IS NOT A CREATION

That means the WHOLE THREAD is Fallacious and abortive.

THESE ARE HIS WORDS:

Isaiah 46:5 "To whom will you compare me, count me equal, or liken me, so that I may be compared?
 
Ni Dhaifu sana huyo Ishmael kwanza anapanic mapema na kuanza kupayuka hovyo.Amekosa mwelekeo sasa anataka kujua jinsia za watu.Sijawahi ona udhaifu kama huu.

Hawa jamaa ni vichekesho,wanashindwa kumthibitisha mungu wao wanabaki kuandika taarabu humu.

Unafahamu kuwa huwezi jibu swali langu. TENA HATA MUNGU WAKO MAREHEMU DARWIN AJE HAPA, HATO WEZA JIBU SWALI LANGU.

SASA JIBU SWALI UNALO LIKIMBIA:

Are you are male or a female? PROVE IT TO ME THAT YOU ARE NOT A WOMAN.

Ni mwendo huo huo wa Fallacy bana. Fallacy inajibiwa na fallacy.
 
Mbona Hujathibitisha kwamba wewe n mmoja wa wale wamama wa kana moja.Ukithibithibitisha hilo basi nakujibu.Ukimaliza kumtaja marehem Darwin usisahau kumalizia na marehem yesu!.
 
nadhani mtu wa namna hiyo hayupo kuelewa... ukimuomba ushahidi kama limechomekwa kiujanja ujanja bado atakosa jibu! hawa watu ni watu wa ajabu sana, yaani mtu yupo radhi kuamini kwamba mambo fulani fulani yamechomekwa kiujanja ujanja kana kwamba alikuwepo enzi hizo... ila ukimwambia hivi anabisha

Mkuu sio kubisha, naamini Yesu aliongea kwa mifano tu kwani Gehanoni ilikuwepo kabla ya kuja na idea ya jehanam au sio!?
 
Mkuu hujanisaidia bado, unapojibu swali unaanza na Intro, unakuja na Definition, kisha unazama kwenye jibu, na mwisho unatoa conclusion ya jibu lako. Sasa mkuu wewe umeniatack kama ugomvi! Sijakuelewa hasaa!

mkuu utawazoea,huwa hawajibu bali waanza kumshambulia mtu badala ya hoja,kuna mmoja humu mtu akitoa hoja yeye anamuuliza jinsia
 
GOD IS NOT A CREATION

That means the WHOLE THREAD is Fallacious and abortive.

THESE ARE HIS WORDS:

Isaiah 46:5 "To whom will you compare me, count me equal, or liken me, so that I may be compared?

Hatuko hapa kum~compare mungu wa kuumwa na kitu kingne,tunataka ajitokeze yeye binafsi au kupitia mahali pengine ili tujue kuwa yupo
 
Ni heri uamini uwepo wa Mungu na kufuata matendo yake yanayoagizwa kupitia mitume ambyo kimsingi yanapatikana ktk vitabu takatifu.. Na usimkute... Kuliko kutoamini mwisho wa siku ukamkuta.. Utajinyea ahahahaha.. Kiiman Mungu hajaumbwa na yeyote.. Yeye ndo alfa na omega... Hawez fananishwa na kitu chochote...
 
Jehanam lilikuwa jina ambalo Yesu alilitumia kwa mahali pa adhabu ya mwisho kwa watu waovu.

Ni tafsiri ya kiyunani kutoka neno la kiebrania la bonde la Hinomu. Bonde la Hinomu lilikuwa mahali nje ya ukuta wa Yerusalem, kipindi wakati wa ibada ya sanamu Waisrael waliteketeza watoto wao kama sadaka kwa mungu Moleki

Yeremia 7:31 Nao wamepajenga mahali palipoinuka pa Tofethi, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwateketeza wana wao na binti zao motoni; jambo ambalo mimi sikuliagiza, wala halikuingia moyoni mwangu.

Mahali palipo fanyika mambo haya Mungu aliwaadhibu kwa mauaji makali sana Yeremia 7:32-34
32. Basi angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo katika siku hizo halitaitwa tena Tofethi, wala Bonde la mwana wa Hinomu bali litaitwa, Bonde la Machinjo; maana watazika watu katika Tofethi, hata hapatakuwapo mahali pa kuzika tena.

33.Na mizoga ya watu hawa itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi; wala hapana mtu atakayewafukuza.

34. Ndipo katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, nitaikomesha sauti ya kicheko na sauti ya furaha, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi; kwa maana nchi hiyo itakuwa ukiwa.

Baadae mahali hapo palikuwa sehemu ya kutupia takataka yote ya mji moto uliwaka huko bila kuzimika Yeremia 19:1-13

1. Bwana akasema hivi, Enenda ukanunue gudulia la mfinyanzi, ukachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa watu, na baadhi ya wazee wa makuhani;

2. ukatoke uende mpaka bonde la mwana wa Hinomu lililo karibu na mahali pa kuingia kwa lango la vigae, ukahubiri huko maneno nitakayokuambia,

3. ukisema, Lisikieni neno la Bwana, enyi wafalme wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Angalieni, nitaleta mabaya juu ya mahali hapa, ambayo mtu ye yote akisikia habari yake, masikio yake yatawaka.

4. Kwa sababu wameniacha mimi, nao wamepafanya mahali hapa kuwa mahali pageni, nao hapa wamewafukizia uvumba miungu mingine wasiowajua, wala wao, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda; nao wamepajaza mahali hapa damu ya wasio na hatia;

5. nao wamemjengea Baali mahali pake palipo juu, ili kuwachoma moto wana wao, wawe sadaka za kuteketezwa kwa Baali; tendo nisiloliamuru mimi, wala kulinena, wala halikuingia moyoni mwangu;

6. basi, angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo katika siku hizo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, wala Bonde la mwana wa Hinomu, bali, Bonde la Machinjo.

7. Nami nitalitangua shauri la Yuda na Yerusalemu mahali hapa; nami nitawaangusha kwa upanga mbele za adui zao, na kwa mkono wa watu watafutao roho zao; na mizoga yao nitawapa ndege wa angani na wanyama wakali wa nchi, iwe chakula chao.

8. Nami nitaufanya mji huu kuwa kitu cha kushangaza watu, na kuzomewa; kila mtu apitaye karibu nao atashangaa, na kuzomea kwa sababu ya mapigo yake.

9 Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawadhiikisha.

10 Ndipo hapo utalivunja gudulia lile, mbele ya macho ya watu wale waendao pamoja nawe,

11 na kuwaambia, Bwana wa majeshi asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyowavunja watu hawa, na mji huu, kama mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, kisichoweza kutengenezwa tena na kuwa kizima; nao watazika watu katika Tofethi hata hapatabaki mahali pa kuzika.

12. Hivyo ndivyo nitakavyopatenda mahali hapa, asema Bwana, nao wakaao humo, hata kufanya mji huu kuwa kama Tofethi;

13. na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa.

Kwanini basi jehanamu lilitumika na Yesu? kwasababu ya kuunganisha mambo yale na hukumu na kuteketeza jehanamu lilikuwa neno lililofaa kudokeza mahali au hali ya adhabu ya milele

Mathayo 10:28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.

Mathayo 18:9 Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto.

Mathayo 23:33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?

Yakobo 3:6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.

sasa hilo jina sahihi katika kutumika kwa mfano we ulitaka Yesu atumie jina gani? Kufuatana na Agano jipya, adhabu ya Ziwa la Moto(Jehanamu) ni mahali pa mateso Inafananishwa na kuteketea milele bila ya kukoma

Mathayo 13:42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Ufunuo 20:10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.

Panafananishwa na giza la milele

Mathayo 8:12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Mathayo 22:13 Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Na kutengwa kwa milele na Mungu na baraka zake

2 Wathesalonike 1:9 watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;

Yesu.wakati anaanza kuhubiri akiwa na 30th tayari neno jehanam lilikuwa maarufu,hata noah alipitia kipindi ambacho jehanam ya takataka ilikuwepo,kutokana na yesu kutumia jina jehanam basi leo kila mtu analeta ushuhuda kuwa kaenda jehanam na heaven,je stori hizo znaendana na uhalisia wa biblia?nadhan hapa mkuu wa chuo unajua naongelea nini,kama umefuatilia research za after life kubaliana na mimi haya yote ni ideas tuu bongo za watu zmeathrka na haya
 
Ni heri uamini uwepo wa Mungu na kufuata matendo yake yanayoagizwa kupitia mitume ambyo kimsingi yanapatikana ktk vitabu takatifu.. Na usimkute... Kuliko kutoamini mwisho wa siku ukamkuta.. Utajinyea ahahahaha.. Kiiman Mungu hajaumbwa na yeyote.. Yeye ndo alfa na omega... Hawez fananishwa na kitu chochote...

Naomba waamin wenzako wakusahihishe maana unathibitisha kuwa mnaamini kwasababu ya uoga,hujuh ukfa unaenda wap,inaonyesha hata wewe hujuh kama yupo,ondoa uoga uwe huru
 
Yesu.wakati anaanza kuhubiri akiwa na 30th tayari neno jehanam lilikuwa maarufu,hata noah alipitia kipindi ambacho jehanam ya takataka ilikuwepo,kutokana na yesu kutumia jina jehanam basi leo kila mtu analeta ushuhuda kuwa kaenda jehanam na heaven,je stori hizo znaendana na uhalisia wa biblia?nadhan hapa mkuu wa chuo unajua naongelea nini,kama umefuatilia research za after life kubaliana na mimi haya yote ni ideas tuu bongo za watu zmeathrka na haya
Sijakataa kwamba neno Jehanamu halikuwepo, ila nimekuwekea historia ya Jehanamu na kwanini Yesu alilitumia hilo neno, halafu kitu kingine inawezekana unachanganya haya maneno mawili KUZIMU na JEHANAMU, hivyo vitu viwili ni tofauti! pia kuna PARADISO na KUZIMU, lakini JEHANAMU ni tofauti na KUZIMU, sasa hao wanaoenda Jehanamu dah! hapo sijui...
 
Mkuu wa chuo,wakati nikiwa mkristo nilikuwa nawaambia watu kuwa sisi waamin tunamuaibisha mungu,matendo yetu hayaendan na idea ya mungu inavyopaswa awe,baada ya kujua kuwa hayupo leo naendelea kuona tatizo hilohilo,waamin wanamuibisha mungu wao mwenyewe ambaye kwangu siamn kama yupo,naomba ujibu maswali haya,
mungu ana roho chafu?kwanini kwenye kitabu cha isaya alimtuma roho huyo kumuingia mtawala?je kama mungu ndiye muumba kwanini asiwe responsible kwa maovu na magumu wanayopitia wanadam ikiwa kathbtsha kuwa chafu ni yeye anayewatumia watu?
 
Huku Mtaani kuna hoteli inaitwa Nile

Ikipita miaka 2000 halafu mtu akaja na kusema kuwa hakukuwahi kuwa na mto unaoitwa Nile bali kulikuwa na hoteli iliyokuwa inaitwa Nile na ile hoteli ilikuwa na mambomba makubwa ambayo watu waliyafananisha mambomba hayo na mto na hicho ndicho kilichotokea mambomba yale kuitwa mto nile na hakujawahi kuwepo mto halisi ulioitwa hivyo,[halafu wakati huo kuwe hakuna ushahidi wa kuwahi kuwepo mto Nile ila upo wa kuwepo hoteli]

Je,huyo jamaa atakuwa yupo sahihi kwasababu tu hakuna ushahidi wa kisayansi wa uwepo wa mto Nile?

CC: Mkuu wa chuo Ishmael 2013 TanzaniaLaw Mutabaruka .......!!
hatakuwa sahihi...

Inawezekana neno Jehanum ilitokana na eneo la kuchomea taka lenye Jina hilo ama lugha ya kitu kinachoteetea ama vyovyote vile.. lakini Mungu akasema kuwa jehanum ya wenye dhambi ipo kupitia lugha ya watu husika ili waelewe. Sasa kutengeneza hisia kuwa jehanum haipo kwa hoja kuwa ni eneo fulani duniani..bado haina mashiko. Kwani watu wa wakati huo hawakuwa ignorance wasiweze kujua sehemu ya taka na jehanum halisi. Sio story ya kudanganya watoto wadogo.Jehanum ipo na hii tunapaswa kuiamini kwa mujibu wa Imani.
 
Jehanam ni nini?ukitoa tafsir halisi utagundua ni tofauti ya kidin
 
Jehanam ni nini?ukitoa tafsir halisi utagundua ni tofauti ya kidin
Mkuu sijaisoma maana halisi a hii kitu lakini nikitumia mainstream thinking and understanding ningeweza kusema ni moto unaounguza milele kwa wale watenda dhambi na shetani siku ya mwisho
 
Mkuu sijaisoma maana halisi a hii kitu lakini nikitumia mainstream thinking and understanding ningeweza kusema ni moto unaounguza milele kwa wale watenda dhambi na shetani siku ya mwisho

Si kweli kaka,jehanam lilikuwaga eneo nje ya lango la kuinglia jerusalem,hapo ndo taka zote za mji zlpokuwa znatupwa na kutokana na hili hzo taka zilikuwa znachomwa moto,sasa nadhani unaweza kutazamia moto.utokanao na taka na mji mzma,watu walipaogopa kutokana na joto kali la pale,sasa watumishi wa huyu aitwae mungu ndipo waliolpoanza kuwatisha watu kuwa ukifanya dhambi utaenda jehanam,kabla ya hapo hapakuwa na jehanam kwahyo jehanam ya kidin iliundwa kipind hicho,hakuna.jehanam hakuna heaven na hakuna mungu,KAMA YUPO NAOMBA UNIPE TOFAUTI TANO ZINAZOONEKANA KIMACHO KATI TA WEWE MUUMINI NA MIMI NISIYEAMINI
 
Mkuu swali gumu sana kwa Mungu asiyebagua..Emanuel.
Kwani huwaangazia jua lake wabaya kwa wema. Labda ujiulize wewe binafsi dhamiri yako haina shaka hata tone?
 
Mkuu wa chuo,wakati nikiwa mkristo nilikuwa nawaambia watu kuwa sisi waamin tunamuaibisha mungu,matendo yetu hayaendan na idea ya mungu inavyopaswa awe,baada ya kujua kuwa hayupo leo naendelea kuona tatizo hilohilo,waamin wanamuibisha mungu wao mwenyewe ambaye kwangu siamn kama yupo,naomba ujibu maswali haya,
mungu ana roho chafu?kwanini kwenye kitabu cha isaya alimtuma roho huyo kumuingia mtawala?je kama mungu ndiye muumba kwanini asiwe responsible kwa maovu na magumu wanayopitia wanadam ikiwa kathbtsha kuwa chafu ni yeye anayewatumia watu?

kwanza kabisa nashindwa kuelewa ulikuwa mkristo wa namna gani? kama umeshindwa kutofautisha kati ya JEHANAMU NA KUZIMU! unasema umegundua kwamba Mungu Hayupo hebu leta uthibitisho kama hayupo... ni sawa na Ishmael anavyowaambia kipofu anasema hakuna Mwezi utafanyaje kumthibitishia!? Nimekujibu swali kuhusiana na Jehanamu naona bado unang'ang'ania nalo kuuliza tena huko chini...
 
Back
Top Bottom