Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Kwa mujibu wa Ripoti ya mwaka 2019 ya Shirika la Afya Duniani (WHO), matumizi ya pombe, hata kwa viwango vidogo, yanaweza kuleta madhara ya kiafya, lakini madhara makubwa zaidi yanatokana na unywaji wa kupitiliza, wa mara kwa mara na kwa kiasi kikubwa.
Pia, takwimu hizo zinaonyesha kuwa duniani kote, vifo milioni 2.6 vilihusishwa na unywaji wa pombe, ambapo milioni 2 vilikuwa ni kwa wanaume na milioni 0.6 kwa wanawake.
Aidha, takwimu kutoka Ourworldindata.com zinaonesha kuwa kufikia mwaka 2019, Tanzania ilikuwa nchi ya 28 duniani na ya 3 barani Afrika kwa kiwango cha matumizi ya pombe.
Aidha, takwimu kutoka Ourworldindata.com zinaonesha kuwa kufikia mwaka 2019, Tanzania ilikuwa nchi ya 28 duniani na ya 3 barani Afrika kwa kiwango cha matumizi ya pombe.