WHO: Hata kwa Viwango vidogo Matumizi ya Pombe yanaweza kuleta madhara ya kiafya

WHO: Hata kwa Viwango vidogo Matumizi ya Pombe yanaweza kuleta madhara ya kiafya

Mngejua wanawakataza ili wawapole figo zenu mngeendelea kunywa ipo hv wewe unaetunza afya kwa ukamilifu siku ukiugua ukalazwa docta anakuja na bomb la sumu anakupiga matakon jamaa kwaheli kumbe kuna kibosile kahonga m25 figo ake imefel nyie hamuon watu wanakufa kwa homa ndogo sana nimempoteza broo kwa uzembe wa kuitunza afya kaugua tumempeleka hospital kwahel na alikuwa wala pombe wala dem wala chochote hatumii ila baba yangu mwaka wa 69 huu ukiongeza na yake jumla 88 anakula pombe oya walevi tule pombe hawa who wana wivvu
 
Kwa mujibu wa Ripoti ya mwaka 2019 ya Shirika la Afya Duniani (WHO), matumizi ya pombe, hata kwa viwango vidogo, yanaweza kuleta madhara ya kiafya, lakini madhara makubwa zaidi yanatokana na unywaji wa kupitiliza, wa mara kwa mara na kwa kiasi kikubwa.​

Pia, takwimu hizo zinaonyesha kuwa duniani kote, vifo milioni 2.6 vilihusishwa na unywaji wa pombe, ambapo milioni 2 vilikuwa ni kwa wanaume na milioni 0.6 kwa wanawake.

Aidha, takwimu kutoka Ourworldindata.com zinaonesha kuwa kufikia mwaka 2019, Tanzania ilikuwa nchi ya 28 duniani na ya 3 barani Afrika kwa kiwango cha matumizi ya pombe.​
Kwakweli hakuna adui mbaya wa binadamu ambaye hatumtambui kama POMBE! Pombe ni mbaya jamani! Ubaya wa pombe unakamata fikra! Pombe Ikishakamata fikra zako inakulazimisha uitetee na kuipigania huku ikiendelea kuharibu afya na uchumi wako!
 
Back
Top Bottom