Hakuna popote nilipofanya corona politics. Mimi ninakataa double standards (na motives) za WHO na maagents wao katika kutengeneza mazingira kuonekana kwamba waafrika tunahitaji vaccine ya corona wakati huo huo hiyo vaccination tunaambiwa tutaipata baadaye sana. Ni bahati tu kwamba hata hiyo vaccination hatuihitaji (maana tayari miili yetu ilishajenga herd immunity tangi corona version 1), lakini kama kweli maisha ya waafrika yangekuwa na thamani kiasi hicho WHO ingepigia kelele kuwepo na usawa kwa aina ya vaccine ya corona wanayopaswa kuchanjwa watu wote. Si tunaishi dunia moja? Na kupambana na kirusi cha aina moja?
Na kama kisingizio kitakuwa sijui economics za nchi husika, na storage requirements za vaccinne, basi hiyo ndiyo ikuonyeshe kwamba kila nchi itapambana na corona kwa style yake kutokana na mazingira yake. Tangu siku ya kwanza tulisema kwamba corona tutapambana nayo the African way, nyie mnataka kutulazimishia tupambane nayo kwa namna wazungu wanavyotaka. Kwani kuna shida yoyote mpaka sasa kwa namna tulivyopambana nayo?
So point yangu inabaki. Vaccine siyo kipaumbele chetu katika kupambana na corona. Na kama itabidi tutafute vaccine, itabidi tuitafute kwa terms zetu sio zile tunazolazimishiwa. Vaccine za China hazina uwazi? Wao (wachina) wamechanjwa na vaccine kutoka wapi? Na kama unatilia shaka sayansi ya China mangapi made in China unayatumia kila siku?
Ukoloni wa mzungu kwa mwafrika ulimfanya kitu kibaya sana asee!