...Great depression ilitokana na market crisis kama inayoendelea sasa,na walichofanya ni sawa na wanachofanya sasa hivi (bailout) na kuweka more regulations kwenye markets
Unachosema ni kuwa kwenye great depression sera mbaya za wakati huo ndizo zilisababisha hayo. Kilichotokea wakati wa great depression hakikutokana na tendo la Mungu (act of God) bali ni kutokana na uzembe wa wanadamu kuliacha soko liamue kile kitu. Na kutokana na kujifunza huko kama unavyosema hapa chini:
,Americans wanatumia sana past experience kusolve matatizo yao,
ni kweli. Wakati huo wa makosa ya sera zao za kibepari ambacho waliacha soko liamue kila kitu wamarekani walifikia mahali pa kuweka mipaka ya ununuzi wa vitu na upatikanaji wa vitu mbalimbali. Hilo lilifanyika pia wakati wa vita ya pili ya dunia. Nchi za kibepari Uingereza na Marekani zililazimika kufanya rationing ili kuhakikisha raia wake wanaishi maisha ya maana. Inasemwa hivi kuhusu rationing ya vita ya pili ya dunia kwa mujibu wa U-s-history.com
With the onset of World War II, numerous challenges confronted the American people. The government found it necessary to ration food, gas, and even clothing during that time. Americans were asked to conserve on everything. With not a single person unaffected by the war, rationing meant sacrifices for all. In the spring of 1942, the Food Rationing Program was set into motion.
Kwanini nchi ya kibepari basi inalazimika kufanya rationing ya namna hiyo? Siyo wao tu bali hata Uingereza. Inasemwa hivi kwenye wikipedia kuhusu rationing ya Uingereza.
Rationing in the United Kingdom is the series of food rationing policies put in place by the government of the United Kingdom during certain wartime periods of the 20th century [1].
Sasa hawa unaowapigia debe kuwa ni mabepari waliona umuhimu wa kufanya rationing (mgao). Walifanya hivyo kwa sababu walipenda kuona watu wao wanagawiwa vitu; walifanya hivyo kwa sababu mgao uliwafanya waonekane na nguvu; waliona raha kuona watu wao wanadhalilika kwa kupanga foleni? Hapana! Walifanya hivyo kwa sababu ilikuwa ni muhimu vinginevyo katika mazingira ya namna hiyo watu wachache wenye uwezo ndio wangeweza kufanikiwa na kupata mahitaji yao.
Hilo la Waingereza na Wamarekani wewe utaona ni sawa na inakubalika lakini kwa Tanzania chini ya Mwalimu utaona ni baya ingawa Wamarekani na Waingereza walikuwa na control ya kutosha ya kutosababisha rationing. Sisi tulilazimika kuwa na rationing miaka ya mwanzoni ya 1980s sababu tumetoka kwenye vita ambayo tulitumia karibu mabilioni ya shilingi. Na tunapotoka hapa tunakutana na ukame wa 1982-1984. Watu wetu wanatishiwa na njaa, wachache wanaanza kutumia nafasi hiyo kujitengenezea fedha ya haraka haraka kutokana na misery ya watu wengine.
Wewe ungesema Nyerere angekaa pembeni na kuacha soko liamue; kwamba asingesababisha maduka ya kaya, RTC, na mgao wa mafuta na hata kulazimisha magari kutotembea siku ya Jumapili. Haya kwako unaona ni uonevu lakini yangefanywa na Wazungu ungesema "the stroke of genius".
Ni lazima tutambue kuongoza Taifa siyo kama kibanda cha mtu. Leo hii Bush na wenzake wanavyohangaika kutuliza taifa lao siyo suala la ujamaa tena bali ni suala la survival of America kama tunavyoijua. Kama njia za kijamaa ambazo wanataka kutumia (kutaifisha mabenki kama walivyofanya Uingereza juzi au walivyofanya wa Marekani) kutasaidia kulilinda Taifa lao na mfumo wao wa kibepari well and good and more power to them. Lakini kama kesho ukisikia URT inataka kutaifisha NBC, Barclays n.k ili kuulinda uchumi na walaji bila ya shaka utapiga kelele kwamba wanataka kuturudisha kwenye ujamaa!
mnaosema bailout ni kuelekea communism
Binafsi sijasema hivyo lakini nakubaliana na wale ambao wanaona kinachotokea kweli nacho ni kutumia njia za kijamaa kuukoa ubepari! In other words that is the irony of ironies!
hamjui kilichotokea during great depression,niambie ujamaa wetu umetusaidia nini hiyo miaka karibu 50 ya uhuru zaidi ya kutufanya maskini kupindukia na vitegemezi,
Hili ni swali la msingi kweli. Ujamaa wetu umetusaidia nini? Well, to tell you the truth haujatufanya tuwe maskini wa kupindukia! Siyo ujamaa uliofanya hivi kwa sababu Ubepari uliojaribiwa Kenya na Congo haukuwafanya wawe matajirri wa kupindukia na katika nchi zote tatu ni kundi la watu wachache tu bado ni matajiri. Huwezi kuelezea umaskini wetu kwa kuangalia Ujamaa kama vile usivyoweza kuelezea umaskini wa Kenya, Congo n.k kwa kuangalia Ubepari tu.
kubali America is great kutokana na capitalism
Hili linaweza kuwa kweli kwa kiasi fulani, lakini ubepari wao umejaa vikolombwezo vya ujamaa na kwa muda mrefu (kama wakati wa Clinton) na bila ya shaka chini ya Obama, sera za kijamaa zitaongoza Marekani. Wanapotukuza Capitalism siyo ule Ubepari tunaouzungumzia sisi kisiasa (political economy). Binafsi naamini kuna tofauti kubwa sana kati ya Ubepari na Capitalism. Litakuwa somo kwa siku nyingine. Binafsi naamini katika Capitalism na siyo katika Ubepari.
hardwork haiui na wabongo wengi walioamua kufuata sheria na kuweka bidii 100,000$ salary sio issue...bongo njaa tupu maisha mazuri ni kwa wezi tuu na wachache sana wenye bahati
Hii ni kejeli kwa watanzania wanaosota mchana na usiku kufanya kazi na kujenga nchi na maisha yao. Unataka watu waamini kuwa Watanzania ni wavivu hadi walipokuja huku. Wengi wetu tunakumbuka jinsi wazee wetu walivyokuwa wanahangaika mchana na usiku kutengeneza mazingira ya kupata fedha za bila ya kutumia njia za mkato. Licha ya kuwa na ajira wengine wetu tulikuwa tunapelekwa kule kwenye mashamba kila weekend. Na wengine tulifundisha hii hard work kwa kupita na kuuza mchicha na nyanya mitaani na kufundishwa jinsi ya kutumia mitaji kwenye soko la Makorola pale.
Tatizo la Tanzania ndugu yangu siyo watu kutofanya kazi, ni kwamba inakubidiu ufanye kazi zaidi Tanzania kuweza kutengeneza maisha yako kuliko hapa Marekani. Mfumo wetu wa ajira na malipo katika Tanzania hauendani na ukweli wa jamii inayotoka kutengeneza maisha ya kisasa. Hivyo mtu anatumia nguvu nyingi kweli kuvuna kidogo wakati huku Marekani mtu anaweza kutengeneza fedha nyingi tu kwa kubonyeza vitufe viwili vitatu au kuketi kwenye kompyuta yake na kuangalia "buy" and then "sell"!