Unachosema ni kuwa kwenye great depression sera mbaya za wakati huo ndizo zilisababisha hayo. Kilichotokea wakati wa great depression hakikutokana na tendo la Mungu (act of God) bali ni kutokana na uzembe wa wanadamu kuliacha soko liamue kile kitu. Na kutokana na kujifunza huko kama unavyosema hapa chini:
ni kweli. Wakati huo wa makosa ya sera zao za kibepari ambacho waliacha soko liamue kila kitu wamarekani walifikia mahali pa kuweka mipaka ya ununuzi wa vitu na upatikanaji wa vitu mbalimbali. Hilo lilifanyika pia wakati wa vita ya pili ya dunia. Nchi za kibepari Uingereza na Marekani zililazimika kufanya rationing ili kuhakikisha raia wake wanaishi maisha ya maana. Inasemwa hivi kuhusu rationing ya vita ya pili ya dunia kwa mujibu wa U-s-history.com
Kwanini nchi ya kibepari basi inalazimika kufanya rationing ya namna hiyo? Siyo wao tu bali hata Uingereza. Inasemwa hivi kwenye wikipedia kuhusu rationing ya Uingereza.
Sasa hawa unaowapigia debe kuwa ni mabepari waliona umuhimu wa kufanya rationing (mgao). Walifanya hivyo kwa sababu walipenda kuona watu wao wanagawiwa vitu; walifanya hivyo kwa sababu mgao uliwafanya waonekane na nguvu; waliona raha kuona watu wao wanadhalilika kwa kupanga foleni? Hapana! Walifanya hivyo kwa sababu ilikuwa ni muhimu vinginevyo katika mazingira ya namna hiyo watu wachache wenye uwezo ndio wangeweza kufanikiwa na kupata mahitaji yao.
Hilo la Waingereza na Wamarekani wewe utaona ni sawa na inakubalika lakini kwa Tanzania chini ya Mwalimu utaona ni baya ingawa Wamarekani na Waingereza walikuwa na control ya kutosha ya kutosababisha rationing. Sisi tulilazimika kuwa na rationing miaka ya mwanzoni ya 1980s sababu tumetoka kwenye vita ambayo tulitumia karibu mabilioni ya shilingi. Na tunapotoka hapa tunakutana na ukame wa 1982-1984. Watu wetu wanatishiwa na njaa, wachache wanaanza kutumia nafasi hiyo kujitengenezea fedha ya haraka haraka kutokana na misery ya watu wengine.
Wewe ungesema Nyerere angekaa pembeni na kuacha soko liamue; kwamba asingesababisha maduka ya kaya, RTC, na mgao wa mafuta na hata kulazimisha magari kutotembea siku ya Jumapili. Haya kwako unaona ni uonevu lakini yangefanywa na Wazungu ungesema "the stroke of genius".
Ni lazima tutambue kuongoza Taifa siyo kama kibanda cha mtu. Leo hii Bush na wenzake wanavyohangaika kutuliza taifa lao siyo suala la ujamaa tena bali ni suala la survival of America kama tunavyoijua. Kama njia za kijamaa ambazo wanataka kutumia (kutaifisha mabenki kama walivyofanya Uingereza juzi au walivyofanya wa Marekani) kutasaidia kulilinda Taifa lao na mfumo wao wa kibepari well and good and more power to them. Lakini kama kesho ukisikia URT inataka kutaifisha NBC, Barclays n.k ili kuulinda uchumi na walaji bila ya shaka utapiga kelele kwamba wanataka kuturudisha kwenye ujamaa!
Binafsi sijasema hivyo lakini nakubaliana na wale ambao wanaona kinachotokea kweli nacho ni kutumia njia za kijamaa kuukoa ubepari! In other words that is the irony of ironies!
Hili ni swali la msingi kweli. Ujamaa wetu umetusaidia nini? Well, to tell you the truth haujatufanya tuwe maskini wa kupindukia! Siyo ujamaa uliofanya hivi kwa sababu Ubepari uliojaribiwa Kenya na Congo haukuwafanya wawe matajirri wa kupindukia na katika nchi zote tatu ni kundi la watu wachache tu bado ni matajiri. Huwezi kuelezea umaskini wetu kwa kuangalia Ujamaa kama vile usivyoweza kuelezea umaskini wa Kenya, Congo n.k kwa kuangalia Ubepari tu.
Hili linaweza kuwa kweli kwa kiasi fulani, lakini ubepari wao umejaa vikolombwezo vya ujamaa na kwa muda mrefu (kama wakati wa Clinton) na bila ya shaka chini ya Obama, sera za kijamaa zitaongoza Marekani. Wanapotukuza Capitalism siyo ule Ubepari tunaouzungumzia sisi kisiasa (political economy). Binafsi naamini kuna tofauti kubwa sana kati ya Ubepari na Capitalism. Litakuwa somo kwa siku nyingine. Binafsi naamini katika Capitalism na siyo katika Ubepari.
Hii ni kejeli kwa watanzania wanaosota mchana na usiku kufanya kazi na kujenga nchi na maisha yao. Unataka watu waamini kuwa Watanzania ni wavivu hadi walipokuja huku. Wengi wetu tunakumbuka jinsi wazee wetu walivyokuwa wanahangaika mchana na usiku kutengeneza mazingira ya kupata fedha za bila ya kutumia njia za mkato. Licha ya kuwa na ajira wengine wetu tulikuwa tunapelekwa kule kwenye mashamba kila weekend. Na wengine tulifundisha hii hard work kwa kupita na kuuza mchicha na nyanya mitaani na kufundishwa jinsi ya kutumia mitaji kwenye soko la Makorola pale.
Tatizo la Tanzania ndugu yangu siyo watu kutofanya kazi, ni kwamba inakubidiu ufanye kazi zaidi Tanzania kuweza kutengeneza maisha yako kuliko hapa Marekani. Mfumo wetu wa ajira na malipo katika Tanzania hauendani na ukweli wa jamii inayotoka kutengeneza maisha ya kisasa. Hivyo mtu anatumia nguvu nyingi kweli kuvuna kidogo wakati huku Marekani mtu anaweza kutengeneza fedha nyingi tu kwa kubonyeza vitufe viwili vitatu au kuketi kwenye kompyuta yake na kuangalia "buy" and then "sell"!
Wewe kweli huambiliki. Knowledge Base ya Wamarekani ni kubwa. Na mwenye knowledge siku zote ana-prevail.
..still naamini capitalism ni nzuri maana ina encourage/motivate hardwork/innovations kwa sababu system ina reward na kuna personal profit na kuna ile sense of individual responsibility,nature ya binadamu tunapenda freedom sio kubanwa banwa au kuambiwa cha kufanya kila wakati,capitalism imefanya mambo makubwa sana katika maendeleo ya binadamu duniani,ukitaka kuonja utamu wa capitalism ishi states!
...unajua tatizo la wanaotetea ujamaa kama Mwanakijiji,wanaamini zile rushwa za mafisadi na umaskini wa kutupa ni matokeo ya capitalism kumbe ni ufisadi tuu unaofanywa na wengi wao ambao still wanaamini kwenye ujamaa,mataifa yaliyoendelea sio uchawi ni hardwork/innovation tuu ndio imewafikisha hapo sio blah blah tuu za namna ya kugawana na kumiliki kisichokuwepo au cha wengine!
..still naamini capitalism ni nzuri maana ina encourage/motivate hardwork/innovations kwa sababu system ina reward na kuna personal profit na kuna ile sense of individual responsibility,nature ya binadamu tunapenda freedom sio kubanwa banwa au kuambiwa cha kufanya kila wakati,capitalism imefanya mambo makubwa sana katika maendeleo ya binadamu duniani,ukitaka kuonja utamu wa capitalism ishi states!
Mwanakijiji,swali ambalo hatuna budi kukabiliana nalo ni hili: tumeona kuanguka kwa Ujamaa na vile vile mafanikio yake (China, Cuba, Vietnam, Spain, na nchi za Nordic) na tumeona pia mafanikio makubwa ya umtajisho (don't ask), sisi Tanzania tunajifunza nini? Je ni kitu gani ambacho tunapaswa kukichukua na kuona kinafaa? Je suala la kutaifisha mabenki na taasisi za fedha ni baya kama ambayo wakosoaji wa Mwalimu walikuwa wanasema lakini leo mataifa yao yanataifisha taasisi hizo?
Koba unapozungumzia regulations unazungumzia mkono wa serikali kuwa involved katika sekta binafsi; lakini wakati huo huo wakuu hawa wanataka nchi zetu to deregulate our industry na kuruhusu competition n.k Je ni kwa kiasi gani serikali iingilie kati taasisi binafsi?
Hivi majuzi serikali imetoa ruzuku kwa ATCL na TRL kuna watu walipinga au waling'aka kwanini serikali isaidie kampuni binafsi; kuna watu waliwahi kusuggest kuiacha ATCL icollapse je hoja zao bado zipo?
Je katika nchi zetu hizi serikali bado iingilie kati sekta binafsi kwenye mambo ya regulations na ikibidi "bailing them out". Najiuliza kwanini Tanzania haikuingilia kuokoa makampuni yaliyofanya vibaya wakati ule na tukaambiwa tuyauze kwenye kisingizio cha "uchumi wa soko" na "ushindani"?
Wewe kweli huambiliki. Knowledge Base ya Wamarekani ni kubwa. Na mwenye knowledge siku zote ana-prevail.
Mwanakijiji,
Siyo kwamba tu hayo mashirika tuliyauza. Tuliyauza kwa bei ambayo ni kama tuliyagawa bure. Matokeo yake leo ni nini? Tanzania imeongeza production? Jibu ni hapana. Mengine wameyageuza kuwa maghala ya kuingizia bidhaa kutoka nje.
Hivi kwanini tulitangaza Azimio la Arusha?
So lets check history again, calvin Coolidge na Herbet Hoover waliokuwa maraisi wa Marekani wakati Great depression inaanza walikuwa Republicans ambao ndio Neo Capitalist ambao hawataki kusikia Regulations!
Sasa tuseme kuanguka kwa Uchumi kwa mara nyingine nchi ikiwa chini ya Republicans ni bahati mbaya au Republicans hawana uwezo kuongoza?
Je Republicans ni sawa na TANU na CCM? if so where is our equivalent to Democratic Party of USA?
In other words, Ujamaa wa TANU/CCM na Ubepari wa Republicans ni sawa!
mwisho utasema ni kwa sababu wazungu! hivi hiyo knowledge base imetoka mbinguni? Hivi unajua kuna vyuo vikuu vingapi Nigeria na watu wangapia wana angalau digrii moja? Hivi kama ni elimu tu kuna nchi zinawasomi wengi na nyingine zinawasomi wachache relative to their population. Usomi peke yake hautoshi kuibadli nchi kuwa ya kisasa.
Leo hii Rwanda itaipita Tanzania katika kila kitu, Namibia iko juu yetu kwa mbali tu, so is Botswana. Lakini unataka kusema kuwa wako mbali sana kwenye ellimu kuliko sisi?
Kwa sababu kati ya 1961 na 1966 nchi ilimshinda Mwalimu maana:
1.Wakoloni waliendela kututawala 1961
2.Waafrika walidai Afrikanaizesheni 1962
3.Wabenzi walizidi kujilimbikizia mali 1963
4.Wanajeshi waliamua kumpindua 1964
5.Wamagharibi walimbania misaada 1965
6.Wanafunzi Mlimani walimgomea 1966
Mwalimu akachoka akaona sasa kha inabidi 'tukimbie wakati wengine wanatembea' ili:
1. Watanzania wamiliki pamoja njia kuu za uchumi
2. Watanzania waache kutegemea misaada ya nje
3. Watanzania wawe na viongozi wasio mafisadi
4. Watanzania wawe na jamii isiyo na matabaka
5. Watanzania wajiletee maendeleo yao wenyewe
6. Watanzania wawe na umoja na uhuru wa kweli
Hizo ndio sababu za kuleta Azimio ambalo Mwalimu alisema mwisho wa siku tutarejea maadili na misingi yake:
The Heart of Africa. Interview with Julius Nyerere on Anti-Colonialism