Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

Lusajo,
Ndivyo China walivyofanya na nchi kama Maleysia, Vietnam na sasa Urusi wote wamefanya na mabadiliko tunayaona sio sisi tuliogawa kila kitu bila kuzingatia malengo ya nchi ila matakwa ya watu...Mfumo wa tanzania unajaribu kuwabadilisha watu na mazingira yawe sawa na yale ya nchi zilizoendelea wakati ni maendeleo ndio hubadilisha watu na Mazingira..
Kwa hiyo toka Ujamaa kosa kubwa tulilolifanya ni kujaribu kubadilisha watu na mazingira yetu ili yafanane na hao tunaowaiga ndipo tulipojikuta tumeshindwa kila kitu..
 
....keep debate alive what philosophy is the best lakini mifumo yote hiyo bila hard work and innovations ni zero,hizo philosophy kwenye vitabu bila hard work/innovations hazitupeleki popote na umaskini will continue to be our badge of honour!
 
Unachosema ni kuwa kwenye great depression sera mbaya za wakati huo ndizo zilisababisha hayo. Kilichotokea wakati wa great depression hakikutokana na tendo la Mungu (act of God) bali ni kutokana na uzembe wa wanadamu kuliacha soko liamue kile kitu. Na kutokana na kujifunza huko kama unavyosema hapa chini:

ni kweli. Wakati huo wa makosa ya sera zao za kibepari ambacho waliacha soko liamue kila kitu wamarekani walifikia mahali pa kuweka mipaka ya ununuzi wa vitu na upatikanaji wa vitu mbalimbali. Hilo lilifanyika pia wakati wa vita ya pili ya dunia. Nchi za kibepari Uingereza na Marekani zililazimika kufanya rationing ili kuhakikisha raia wake wanaishi maisha ya maana. Inasemwa hivi kuhusu rationing ya vita ya pili ya dunia kwa mujibu wa U-s-history.com

Kwanini nchi ya kibepari basi inalazimika kufanya rationing ya namna hiyo? Siyo wao tu bali hata Uingereza. Inasemwa hivi kwenye wikipedia kuhusu rationing ya Uingereza.

Sasa hawa unaowapigia debe kuwa ni mabepari waliona umuhimu wa kufanya rationing (mgao). Walifanya hivyo kwa sababu walipenda kuona watu wao wanagawiwa vitu; walifanya hivyo kwa sababu mgao uliwafanya waonekane na nguvu; waliona raha kuona watu wao wanadhalilika kwa kupanga foleni? Hapana! Walifanya hivyo kwa sababu ilikuwa ni muhimu vinginevyo katika mazingira ya namna hiyo watu wachache wenye uwezo ndio wangeweza kufanikiwa na kupata mahitaji yao.

Hilo la Waingereza na Wamarekani wewe utaona ni sawa na inakubalika lakini kwa Tanzania chini ya Mwalimu utaona ni baya ingawa Wamarekani na Waingereza walikuwa na control ya kutosha ya kutosababisha rationing. Sisi tulilazimika kuwa na rationing miaka ya mwanzoni ya 1980s sababu tumetoka kwenye vita ambayo tulitumia karibu mabilioni ya shilingi. Na tunapotoka hapa tunakutana na ukame wa 1982-1984. Watu wetu wanatishiwa na njaa, wachache wanaanza kutumia nafasi hiyo kujitengenezea fedha ya haraka haraka kutokana na misery ya watu wengine.

Wewe ungesema Nyerere angekaa pembeni na kuacha soko liamue; kwamba asingesababisha maduka ya kaya, RTC, na mgao wa mafuta na hata kulazimisha magari kutotembea siku ya Jumapili. Haya kwako unaona ni uonevu lakini yangefanywa na Wazungu ungesema "the stroke of genius".

Ni lazima tutambue kuongoza Taifa siyo kama kibanda cha mtu. Leo hii Bush na wenzake wanavyohangaika kutuliza taifa lao siyo suala la ujamaa tena bali ni suala la survival of America kama tunavyoijua. Kama njia za kijamaa ambazo wanataka kutumia (kutaifisha mabenki kama walivyofanya Uingereza juzi au walivyofanya wa Marekani) kutasaidia kulilinda Taifa lao na mfumo wao wa kibepari well and good and more power to them. Lakini kama kesho ukisikia URT inataka kutaifisha NBC, Barclays n.k ili kuulinda uchumi na walaji bila ya shaka utapiga kelele kwamba wanataka kuturudisha kwenye ujamaa!

Binafsi sijasema hivyo lakini nakubaliana na wale ambao wanaona kinachotokea kweli nacho ni kutumia njia za kijamaa kuukoa ubepari! In other words that is the irony of ironies!

Hili ni swali la msingi kweli. Ujamaa wetu umetusaidia nini? Well, to tell you the truth haujatufanya tuwe maskini wa kupindukia! Siyo ujamaa uliofanya hivi kwa sababu Ubepari uliojaribiwa Kenya na Congo haukuwafanya wawe matajirri wa kupindukia na katika nchi zote tatu ni kundi la watu wachache tu bado ni matajiri. Huwezi kuelezea umaskini wetu kwa kuangalia Ujamaa kama vile usivyoweza kuelezea umaskini wa Kenya, Congo n.k kwa kuangalia Ubepari tu.

Hili linaweza kuwa kweli kwa kiasi fulani, lakini ubepari wao umejaa vikolombwezo vya ujamaa na kwa muda mrefu (kama wakati wa Clinton) na bila ya shaka chini ya Obama, sera za kijamaa zitaongoza Marekani. Wanapotukuza Capitalism siyo ule Ubepari tunaouzungumzia sisi kisiasa (political economy). Binafsi naamini kuna tofauti kubwa sana kati ya Ubepari na Capitalism. Litakuwa somo kwa siku nyingine. Binafsi naamini katika Capitalism na siyo katika Ubepari.

Hii ni kejeli kwa watanzania wanaosota mchana na usiku kufanya kazi na kujenga nchi na maisha yao. Unataka watu waamini kuwa Watanzania ni wavivu hadi walipokuja huku. Wengi wetu tunakumbuka jinsi wazee wetu walivyokuwa wanahangaika mchana na usiku kutengeneza mazingira ya kupata fedha za bila ya kutumia njia za mkato. Licha ya kuwa na ajira wengine wetu tulikuwa tunapelekwa kule kwenye mashamba kila weekend. Na wengine tulifundisha hii hard work kwa kupita na kuuza mchicha na nyanya mitaani na kufundishwa jinsi ya kutumia mitaji kwenye soko la Makorola pale.

Tatizo la Tanzania ndugu yangu siyo watu kutofanya kazi, ni kwamba inakubidiu ufanye kazi zaidi Tanzania kuweza kutengeneza maisha yako kuliko hapa Marekani. Mfumo wetu wa ajira na malipo katika Tanzania hauendani na ukweli wa jamii inayotoka kutengeneza maisha ya kisasa. Hivyo mtu anatumia nguvu nyingi kweli kuvuna kidogo wakati huku Marekani mtu anaweza kutengeneza fedha nyingi tu kwa kubonyeza vitufe viwili vitatu au kuketi kwenye kompyuta yake na kuangalia "buy" and then "sell"!

Wewe kweli huambiliki. Knowledge Base ya Wamarekani ni kubwa. Na mwenye knowledge siku zote ana-prevail.
 
..still naamini capitalism ni nzuri maana ina encourage/motivate hardwork/innovations kwa sababu system ina reward na kuna personal profit na kuna ile sense of individual responsibility,nature ya binadamu tunapenda freedom sio kubanwa banwa au kuambiwa cha kufanya kila wakati,capitalism imefanya mambo makubwa sana katika maendeleo ya binadamu duniani,ukitaka kuonja utamu wa capitalism ishi states!
 
Wewe kweli huambiliki. Knowledge Base ya Wamarekani ni kubwa. Na mwenye knowledge siku zote ana-prevail.

...mkuu unajua tatizo la wanaotetea ujamaa kama Mwanakijiji,wanaamini zile rushwa za mafisadi na umaskini wa kutupa ni matokeo ya capitalism kumbe ni ufisadi tuu unaofanywa na wengi wao ambao still wanaamini kwenye ujamaa,mataifa yaliyoendelea sio uchawi ni hardwork/innovation tuu ndio imewafikisha hapo sio blah blah tuu za namna ya kugawana na kumiliki kisichokuwepo au cha wengine!
 
..still naamini capitalism ni nzuri maana ina encourage/motivate hardwork/innovations kwa sababu system ina reward na kuna personal profit na kuna ile sense of individual responsibility,nature ya binadamu tunapenda freedom sio kubanwa banwa au kuambiwa cha kufanya kila wakati,capitalism imefanya mambo makubwa sana katika maendeleo ya binadamu duniani,ukitaka kuonja utamu wa capitalism ishi states!

Koba:

Hapa jamaa hawana cha kusema. Katika shule moja ya ubepari: Austrian School of Economics wamesema haya yote humu.

Mojawapo ni kuwa interest za kuchukua mikopo zinapokuwa chini, watu wanakopa sana na baadaye ku-creat crunch.

Baada ya septermber 11 na internet bubble burst, Bank Kuu ya Marekani ilishusha sana interest rate. Kushuka kwa interest rate kulifanya kukuza sekta zingine kwa kutumia mikopo. Na sasa tupo kwenye burst nyingine.

Waache wenye Ujamaa wa kutoka Chuo Kikuu Cha Chama Kivukoni.
 
...unajua tatizo la wanaotetea ujamaa kama Mwanakijiji,wanaamini zile rushwa za mafisadi na umaskini wa kutupa ni matokeo ya capitalism kumbe ni ufisadi tuu unaofanywa na wengi wao ambao still wanaamini kwenye ujamaa,mataifa yaliyoendelea sio uchawi ni hardwork/innovation tuu ndio imewafikisha hapo sio blah blah tuu za namna ya kugawana na kumiliki kisichokuwepo au cha wengine!

Mimi nadhani wanaotetea Ujamaa wengi hapa ni kwa sababu ya admiration waliokuwa nayo kwa hero wao aliyeasisi hiyo itikadi, Mwalimu Nyerere. Kama J.K. Nyerere angekuwa muasisi wa Ubeberu nadhani kina Mwanakijiji wangekuwa wanatetea ubeberu. Angekuwa Mkomunisti wangetetea ukomunisti. Nadhani wana blind affection for the great leader.
 
Koba,
Kwanza umesema sio Ujamaa wala Ubepari unaweza kufanya kazi bila watu kufanya kazi kwa nguvu na Innovations. Hivi mkuu unataka kunambia Wachina walikuwa hawafanyi kazi kwa nguvu na Innovations..Mkuu kweli unafikiria kazi ngumu ama only hard workj people ndio wanakuwa rewarded na system ya Kibepari?...basi ingekuwa hivyo sisi wabeba box tungekuwa na mishahara mikubwa kuliko hao walikaa ofisini wakitumia muda mwingi kuagiza vitu toka China na Taiwan ambako pia watu wanafanya kazi masaa 16 kwa siku...
Huu msemo wa kusema ati ukitaka kuona utamu wa Ubepari ishi Marekani ni mawazo yako tu kwa sababu katika akili yako tayari umekwisha jenga maendeleo ni yanafanana vipi..Hakuna kitu cha maendeleo ambacho kipo Marekani hakipo nchi nyinginezo hasa Ulaya na Asia, tena naweza kusema kuna vitu vingi sana Ulaya na Asia ambavyo havipo Marekani..mfano garimoshi liendalo kwa kasi over 250km/hr.
Sasa tunarudi palepale kuwa ni WATU na MAZINGIRA ya Marekani ambayo yanawazingua wengi sana duniani ikiwa ni pamoja na diversity iliyopo. Marekani ni nchi iliyotengenezwa na wahamiaji, freedom iliyopo kwa raia wake nadhani huwezi kuipata sehemu yoyote ile kwa sababu hawa watu walipotaka kuijenga nchi yao walitazama kwanza uwezekano huo - Wahamiaji ktk mazingira mapya!
Hawakutaka kubadilisha watu wala mazingira yao yafanane na nchi nyingine yoyote isipokuwa Marekani ambayo ilikuwa ikipokea Immigrants toka Ulaya. They built their system kulingana na wao....walowezi wakaweza kuchukua madaraka ya nchi na kuitangaza nchi yao kama ilivyokuwa South Afrika na huwezi kuleta habari za Ujamaa mahala ambapo wewe mwenyewe ndiye mwizi, hivyo wakatumia UMOJA wa rangi yao na nguvu ya elimu waliyoivuta toka Ulaya kuanzisha makazi mapya.
Most of innovations Marekani zimevumbuliwa Ulaya ama wakazi wa Ulaya..Kwa hiyo ni vigumu sana kutambua mavuno ya Ubepari hali kuna watu walipoteza uhai wao. Tazama South Afrika na hata Israel wote hawa wamevuta innovations toka nje na kutumia wakazi wake utumwa - cheap labour na low maintanance kuweza kufanikisha..Sasa Bongo mkuu utamwibia nani kama sio ndugu yako! utamdharirisha nani kama sio jirani yako.. haya ndiyo yanayotokea hadi leo ktk Ubepari wakuiga hao kina Lowassa wanatuibia sisi, wanatuweka utumwani na kutangaza maendeleo... sijui hayo maendeleo ni ya familia zao ama yapi!..
Tunasahau sana kwamba haya tunayoyaona leo hii ni mavuno ya Ubepari uliotangulia ambao kwanza walituibia sana Afrika wakajenga uchumi wao tofauti na nchi kama Portugal na Spain ambao pamoja na kwamba walikuwa na kila kitu sawa na nchi nyingine za Ulaya lakini walishindwa kuiba uchumi wa nchi hizi kwa manufaa ya Spain na Portugal isipokuwa kuwa na koloni ambazo walifikiria watazitawala hadi kiyama...Leo hii wao miguu juu kama sisi.

Mkuu historia ni ndefu sana hakuna haja ya kwenda huko lakini pamoja na yote haya hakuna mtu anayesema Ubepari ni mbaya 100% laahasha kuna mazuri yake hasa pale inaporuhusu kushindana... Ni sawa na michezo - Kushindana ndiko kunakowajenga wachezaji na timu kuwa nzuri sana na zenye tamaa ya ushindi... mnaweka malengo kuwa mafanikio ni ushindi wa ligi kuu kwa hiyo mna train kwa kutazama dira...sasa hapo ndipo, vifaa, ujuzi, hard work na Innovation inapoingia kati baada ya kuweka malengo..

Tofauti na Ubepari Ujamaa unalemaza sana pale tunapokosa malengo ya mchezo, tunafanya mazoezi kwa ajili ya afya zetu, burudani ya halaiki (maonyesho) kuonyesha nani ngangari..ndio maana kama timu hatukuweza kupata improvement yoyote ktk ufanisi wa mchezo kwa sababu hatukuweza kucheza na nchi nyinginezo kupima uwezo wetu... Tunajipima nguvu zetu na hewa yaani mafanikio ya Tanzania yalipimwa kwa kutazama vitu ambavyo havi apply ktk maendeleo..Tazma iile picha ya mji wa Arusha baada ya Uhuru (kumbux2)...taa za umeme na barabara za lami tuliziita ni anasa tupu na sio maendeleo... mkuu sasa hapo kweli utasema elimu ya vitabu haikutupotosha!..haya ndio tuliyaona ktk UJAMAA......
 
..still naamini capitalism ni nzuri maana ina encourage/motivate hardwork/innovations kwa sababu system ina reward na kuna personal profit na kuna ile sense of individual responsibility,nature ya binadamu tunapenda freedom sio kubanwa banwa au kuambiwa cha kufanya kila wakati,capitalism imefanya mambo makubwa sana katika maendeleo ya binadamu duniani,ukitaka kuonja utamu wa capitalism ishi states!

Kwa mara ya pili au ya tatu nakubaliana na wewe!! I'll choose "compassionate" capitalism over socialism on any given day.
 
swali ambalo hatuna budi kukabiliana nalo ni hili: tumeona kuanguka kwa Ujamaa na vile vile mafanikio yake (China, Cuba, Vietnam, Spain, na nchi za Nordic) na tumeona pia mafanikio makubwa ya umtajisho (don't ask), sisi Tanzania tunajifunza nini? Je ni kitu gani ambacho tunapaswa kukichukua na kuona kinafaa? Je suala la kutaifisha mabenki na taasisi za fedha ni baya kama ambayo wakosoaji wa Mwalimu walikuwa wanasema lakini leo mataifa yao yanataifisha taasisi hizo?

Koba unapozungumzia regulations unazungumzia mkono wa serikali kuwa involved katika sekta binafsi; lakini wakati huo huo wakuu hawa wanataka nchi zetu to deregulate our industry na kuruhusu competition n.k Je ni kwa kiasi gani serikali iingilie kati taasisi binafsi?

Hivi majuzi serikali imetoa ruzuku kwa ATCL na TRL kuna watu walipinga au waling'aka kwanini serikali isaidie kampuni binafsi; kuna watu waliwahi kusuggest kuiacha ATCL icollapse je hoja zao bado zipo?

Je katika nchi zetu hizi serikali bado iingilie kati sekta binafsi kwenye mambo ya regulations na ikibidi "bailing them out". Najiuliza kwanini Tanzania haikuingilia kuokoa makampuni yaliyofanya vibaya wakati ule na tukaambiwa tuyauze kwenye kisingizio cha "uchumi wa soko" na "ushindani"?
 
Mwanakijiji,
Siyo kwamba tu hayo mashirika tuliyauza. Tuliyauza kwa bei ambayo ni kama tuliyagawa bure. Matokeo yake leo ni nini? Tanzania imeongeza production? Jibu ni hapana. Mengine wameyageuza kuwa maghala ya kuingizia bidhaa kutoka nje.
 
Wewe kweli huambiliki. Knowledge Base ya Wamarekani ni kubwa. Na mwenye knowledge siku zote ana-prevail.

mwisho utasema ni kwa sababu wazungu! hivi hiyo knowledge base imetoka mbinguni? Hivi unajua kuna vyuo vikuu vingapi Nigeria na watu wangapia wana angalau digrii moja? Hivi kama ni elimu tu kuna nchi zinawasomi wengi na nyingine zinawasomi wachache relative to their population. Usomi peke yake hautoshi kuibadli nchi kuwa ya kisasa.

Leo hii Rwanda itaipita Tanzania katika kila kitu, Namibia iko juu yetu kwa mbali tu, so is Botswana. Lakini unataka kusema kuwa wako mbali sana kwenye ellimu kuliko sisi?
 
Mwanakijiji,
Siyo kwamba tu hayo mashirika tuliyauza. Tuliyauza kwa bei ambayo ni kama tuliyagawa bure. Matokeo yake leo ni nini? Tanzania imeongeza production? Jibu ni hapana. Mengine wameyageuza kuwa maghala ya kuingizia bidhaa kutoka nje.

Jasusi, naamini wale waliolipeleka taifa kwenye ubepari (ule unyonyaji) waliamini kabisa kuwa katika ubepari ni wao watafanikiwa (it turned out to be true). Hawakulipeleka Taifa kwenye umtajisho (capitalism). Wengi waliuelewa ubepari kama ule unyonyaji hawakuuelewa umtajisho. Matokeo yake, Taifa letu limegeuka kuwa na wanyonyaji wachache ambao wanajiita "wawekezaji" na wale wamtajisho wachache wamebakia kuitwa "wajasiriamali" yaani entrepreneurs. Wale wachache waliokuwa capitalists ndio wale wale walioanza tangu enzi za ujamaa, kina Mengi na wenzake.

Na wale ambao mara nyingi wanajifanya wao ndio capitalists mambo leo ndio waliotumia EPA na madili ya shortcut kutengeneza mitaji yao. Miongoni mwao ndio kina Chenge, Mkono, na wenzao.
 
Damn it, 10 pages of Nani zaidi! sorry guys, maboksi yalinizidi.

Kinachonifurahisha hapa ni jinsi Watanzania tulivyo ama ni wajinga, limbukeni au tumechanganyikiwa.

Lets get this Straight talk straight!

TUnakimbilia kutaka maendeleo na ufanisi sawa na wa Marekani au wa kibepari huku tukiwa bado tuna uchanga na uduni wa kutumia zana za kijima.

At this minute, Mwalimu Nyerere ndiyo kinara wa matatizo yote hasa ya kiuchumi ya Tanzania. Je sisi kama Taifa tuna sehemu gani katika matatyizo haya?

Let say that Ujamaa was wrong, what about Kujitegemea? Why kujitegemea never succeded? was it Nyerere's fault? and lets not talk about Serikali or the system itself, turudi katika nafsi zetu mtu mmoja mmoja. Je tutatafuta sababu nyingine za kudai tumeshindwa kujifunza kujitegemea kwa kuwa Nyerere alileta Ujamaa au kutupeleka vijiji vya ujamaa?

If that is the case, are we dumb enough to declare that makovu ya Siasa za Nyerere hata Vaseline haiwezi kuyatoa? Nyerere died almost 10 years ago, Mtanzania kafanya nini kwa nafsi moja au nafsi mkusanyiko kama jamii na taifa kujitegemea?

Wamarekani walipopata Uhuru wao, hawakuwa matajiri usiku wa pili, walichokivuna katika miaka 200 ni matunda ya kuchapa kazi pamoja na unyonyaji.

Ubepari, sawa na Ujamaa(wa kirusi si sa Kiafrika), ni mifumo ya Kinyonyaji ambayo mmoja unaonekana ni bora kuliko mwingine kwa kuwa anayenyonya ni Serikali na mwingine ni watu binafsi.

Marekani haikufika hapa bila kupitia misukosuko, shida au dhiki. Hata leo hii, pamoja na Utajiri wake wote, bado leo hii kuna umasikini wa hali ya juu katika baadhi ya wananchi wake kuliko hata Tanzania.

Tunaposema Maendeleo, tunamaanisha maendeleo ya namna gani? Tunapima maendeleo kwa mizani gani? ni vipengele vya namna gani?

Ni maendeleo ya Uchumi tuu? what about umoja wetu?

Je tujiulize wakati Marekani ilipopata Uhuru, kazi yake ya kwanza ilikuwa nini? je ni vikwazo gani viongozi wa kwanza wa Marekani walivikuta? Je Marekani ilikuwa na matatizo na mazingira ambayo Tanzania ilikuwa nayo? au walipopata Uhuru tayari nchi ilikuwa imepiga hatua mbele?

Hata China na Urusi na ujamaa wao, tayari nchi zao zilikuwa zimepuga hatua kubwa sana, na kukutana na vishawishi, majaribu, shida ma balaa nyingine ambazo zimewarudisha nyuma.

Sasa sisi tunaikana Historia ya dunia hii kwa kutaka kujenga Taifa kamili lenye viongozi Malaika wasio na makosa au kila walichokisema na kuahidi kitimilike na kinyume cha hayo, basi ni kosa na tutanyooshea vidole milele.

Lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya Nyerere na kikwete ikiwa kuna watakaosema tumwachie Kikwete naye afanye makosa kama Nyerere, Mwinyi na Mkapa.

Mswahili anasema kosa si kulifanya kwa mara ya kwanza, bali ni kulirudia kosa.

Tumefika hapa tulipo ambapo mimi Mndengereko nalonga na Msukuma bila woga huku nimekaa na mke wangu wa Kinyaturu. Hiyo pekee ni maendeleo makubwa.

Labda tumesahau historia ya Mwafrika tangu zama za mawe na kuijumuisha na mahusiano yetu na ugeni wa kikoloni mpaka leo hii.

Je kuna uwezekano kuwa kufeli kwa Ujamaa kulitokana si kwa sera au fikra za Nyerere tuu, bali ni pamoja na hali halisi ya Uafrika wetu ambayo Nyani anaukiri kuwa "Ndivyo Tulivyo"?

Natamani sana Mkandara angeingia humu na kumwaga hoja kwa kutumia falsafa yake ya Watu na Mazingira, labda tungeweza kupata kasura fulani ka mwelekeo.

Leo hii tunasimanga detention act za Tanzania, lakini Patriotic Act ya Marekani tunaiamini kuwa itatulinda tunaoishi Marekani kupata balaa la Ugaidi!

In any society, even a liberal and progressive society like USA, if you are a dissident, you are an enemy. Take a look of the praised Capitalistic America with its attitudes towards minorities, communist or even muslims!

I guess using the Kuhani words of shame "Naive or Naivette" it is us who are in complete denial of man history, in relationship to ours.

Yes I am an ardent Mwalimu fan, and there are things I did not agree with him and that does not make me an out of touch Mdingi mla Chumvi or Haambiliki!

Kila serikali na wananchi hufanya makosa, kama Zakumi alivyosema, je tumejifunza nini kutokana na makosa yetu? Jee awamu tatu zilizomfuata Mwalimu Nyerere zimefanya nini kusahihisha makosa ya awali?

Je sisi ambao leo hii tunashangilia "uhuru" wa kulonga na kuchambua mambo, tumepata mabadiliko gani ya nafsi kuwa watu huru wenye kujitegemea na hivyo kuwa mfano wa kuigwa na wenzetu milioni karibu 30 ambao bado ni waoga kama Kikokiko wa The Gods must be Crazy?

Nafurahia kuwa tunajadili na kutoa hoja pamoja na vijembe vinavyotoka.

Lakini bado swali la awali ni je inawezekana kuwa Ujamaa wetu na Kujitegemea pamoja na Azimio la Arusha ni mkorogo wa mambo mengi na falsafa nyingi duniani na kama wale panya wa maabara kupima muundo wetu mpya wa kisiasa na uchumi, tulipewa pesa nzyingi za utaifiti (misaada) lakini priority zetu zikatuzidi uwezo?
 
So lets check history again, calvin Coolidge na Herbet Hoover waliokuwa maraisi wa Marekani wakati Great depression inaanza walikuwa Republicans ambao ndio Neo Capitalist ambao hawataki kusikia Regulations!

Sasa tuseme kuanguka kwa Uchumi kwa mara nyingine nchi ikiwa chini ya Republicans ni bahati mbaya au Republicans hawana uwezo kuongoza?

Je Republicans ni sawa na TANU na CCM? if so where is our equivalent to Democratic Party of USA?

In other words, Ujamaa wa TANU/CCM na Ubepari wa Republicans ni sawa!
 
Hivi kwanini tulitangaza Azimio la Arusha?

Kwa sababu kati ya 1961 na 1966 nchi ilimshinda Mwalimu maana:

1.Wakoloni waliendela kututawala 1961
2.Waafrika walidai Afrikanaizesheni 1962
3.Wabenzi walizidi kujilimbikizia mali 1963
4.Wanajeshi waliamua kumpindua 1964
5.Wamagharibi walimbania misaada 1965
6.Wanafunzi Mlimani walimgomea 1966

Mwalimu akachoka akaona sasa kha inabidi 'tukimbie wakati wengine wanatembea' ili:

1. Watanzania wamiliki pamoja njia kuu za uchumi
2. Watanzania waache kutegemea misaada ya nje
3. Watanzania wawe na viongozi wasio mafisadi
4. Watanzania wawe na jamii isiyo na matabaka
5. Watanzania wajiletee maendeleo yao wenyewe
6. Watanzania wawe na umoja na uhuru wa kweli

Hizo ndio sababu za kuleta Azimio ambalo Mwalimu alisema mwisho wa siku tutarejea maadili na misingi yake:

http://www.hartford-hwp.com/archives/30/049.html
 
So lets check history again, calvin Coolidge na Herbet Hoover waliokuwa maraisi wa Marekani wakati Great depression inaanza walikuwa Republicans ambao ndio Neo Capitalist ambao hawataki kusikia Regulations!

Sasa tuseme kuanguka kwa Uchumi kwa mara nyingine nchi ikiwa chini ya Republicans ni bahati mbaya au Republicans hawana uwezo kuongoza?

Je Republicans ni sawa na TANU na CCM? if so where is our equivalent to Democratic Party of USA?

In other words, Ujamaa wa TANU/CCM na Ubepari wa Republicans ni sawa!

Hapana bana...wakati wa depression raisi wa Marekani alikuwa FDR na alihutubia taifa kupitia luninga. Check your facts again.
 
mwisho utasema ni kwa sababu wazungu! hivi hiyo knowledge base imetoka mbinguni? Hivi unajua kuna vyuo vikuu vingapi Nigeria na watu wangapia wana angalau digrii moja? Hivi kama ni elimu tu kuna nchi zinawasomi wengi na nyingine zinawasomi wachache relative to their population. Usomi peke yake hautoshi kuibadli nchi kuwa ya kisasa.

Leo hii Rwanda itaipita Tanzania katika kila kitu, Namibia iko juu yetu kwa mbali tu, so is Botswana. Lakini unataka kusema kuwa wako mbali sana kwenye ellimu kuliko sisi?

Mjomba unazidi kuboronga na usipindishe post yangu. Kuna tofauti kubwa sana kati ya KNOWLEDGE AND EDUCATION.

Nigeria au Tanzania kuna vyuo vya elimu, vinavyowasaidia watu kuelimika katika fani mbalimbali. Lakini suala nililozungumzia ni KNOWLEDGE. University zote zinafundisha general education au theories ya displine fulani. Na mfano mkubwa ni mijadala ya hapa JF. Lakini kwenye applications au kutatua matatizo unatakiwa uwe na SPECIALIZED KNOWLEDGE kitu ambacho waMarekani wanacho cha kutosha.

Suala la Tanzania kupitwa na nchi zingine ni suala la PUT YOUR MONEY WHERE YOUR MOUTH IS.
 
Kwa sababu kati ya 1961 na 1966 nchi ilimshinda Mwalimu maana:

1.Wakoloni waliendela kututawala 1961
2.Waafrika walidai Afrikanaizesheni 1962
3.Wabenzi walizidi kujilimbikizia mali 1963
4.Wanajeshi waliamua kumpindua 1964
5.Wamagharibi walimbania misaada 1965
6.Wanafunzi Mlimani walimgomea 1966

Mwalimu akachoka akaona sasa kha inabidi 'tukimbie wakati wengine wanatembea' ili:

1. Watanzania wamiliki pamoja njia kuu za uchumi
2. Watanzania waache kutegemea misaada ya nje
3. Watanzania wawe na viongozi wasio mafisadi
4. Watanzania wawe na jamii isiyo na matabaka
5. Watanzania wajiletee maendeleo yao wenyewe
6. Watanzania wawe na umoja na uhuru wa kweli

Hizo ndio sababu za kuleta Azimio ambalo Mwalimu alisema mwisho wa siku tutarejea maadili na misingi yake:

The Heart of Africa. Interview with Julius Nyerere on Anti-Colonialism

Companero:

Wewe unatumia misuli sana kijana. Umefika wakati uanze kutumia akili. Unaposema njia kuu za uchumi, je unaweza kuzitaja ni njia zipi?

kumbuka wakulima wadogo wadogo wa Kahawa wanaweza kuliletea pato kubwa taifa na kulifanya zao hilo kuwa moja ya njia kuu za uchumi. Je inabidi watanzania kumiliki uzalishaji na uuzaji wa zao hilo kwa pamoja?
 
Back
Top Bottom