Lole Gwakisa:
Dira bila kuwa na expertise ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Hivyo mimi sio mshabiki wa siasa za dira. Nina sababu muhimu lakini kuzielezea kwake itabidi niumize kichwa kidogo kitu ambacho siko tayari kukifanya kwa sasa.
Tukirudi kwenye mada wanasema: All politics is local. Kwa maoni yangu sioni ubaya wa aliyosema Mwinyi kwa sababu hotuba yake aliitoa kwa hard core CCM supporters wakiwa wana-sherehekea miaka 32 ya kuanzishwa kwa chama chao.
Mheshimiwa Zakumi, bila dira ya kule tuendako, kwa hakika hata ile hatua tupigazo ni za kuzunguka pale tulipo.
This is a very serious issue, na sikubaliani kabisa kuwa inabidi uwe msomi wa kupidukia ndio upate dira.Ndio wasomi watasaidia kujaza details za utekelezaji wa dira hiyo.
Kwa mfano,mtu unapooa unategemea watu muwe wengi kenye nyumba hivyo basi, mzee wa nyumba ni jukumu lake kutengeneza dira ya kukidhi matakwa ya kuwa baada ya miaka kadhaa mtakapopata watoto, inabidi kufanya kazi kwa bidii au biashara ili kumudu maisha na kusomesha watoto na pengine ingalau ziada ya maendeleo ya baadaye.Huu ni mfano mdogo tu tena wa maisha ya kila siku.
Dira ni mpango tu wa kimaisha na kisiasa yenye details nyingi sana,.
Kinachohitajika ni kuwa na mpango na kuwa committed kwa mpango hua wa kimaisha na kisiasa.Hili ndo linakosekana.
Kwa kukosa hilo kila kiongozi ana mipango yake ya kibinafsi, anayetaka kutawala tu haya, anyetaka kuiba/kufisadi haya, miiko ya kimaisha/kiutawala hakuna.
Hivi tutapata kigugumizi kikubwa sana kudhibiti matukio yasiyo tarajiwa katika jamii.Kwa mfano siyo bure kuwa:
mapigano kati ya wakulima na wafugaji yanaongezeka, wakati wafugaji wanaruhusiwa kuzurura na mifugo yao nchi nzima,
-kuna viongozi wanajitwalia mali ya umma/au kutumia madaraka vibaya kupindukia bila uongozi kustukia jambo hili mpaka wananchi wanapoanza kulalama
-mwongozo wa kiuchumi/viwanda kutokuwa na strategy zinazolenga maendeleo ya wananchi,
The list is endless!
Mheshimiwa Zakumi,birthday celebrations for its sake haileti maana sana bila kujua kule utakako na kule uelekeako , hasa kwa chama cha siasa.