Hakuna nilichodai hapo ambacho hakina uthibitisho.
Nimeweka vielelezo vya wanaojua kuliko mimi, wasomi wanaonizidi, maandishi ya waliofanyiwa huo unduli wa mawazo (kama sio unduli period) na J.K. Nyerere, na watafiti waliompenda J.K. Nyerere.
Sasa wewe ukija hapa kutuambia eti Mzee Bomani kakwambia J.K. Nyerere alikuwa anasikia ya watu isipokuwa tatizo ni kwamba Watanzania wenzake walikuwa hawawezi kujenga hoja huko ni kupumbazika (hoodwinked).
Utanambiaje Nyerere alikuwa haogopi hoja za wengine wakati Mwanasheria Mkuu mstaafu katika kongamano la Tanganyika Law Society anatoa hotuba kujadili kuboreshwa kwa Katiba, kutoka hapo Mwanasheria Mkuu J.S. Warioba anaagiza awekwe kizuizini, na J.K. Nyerere kweli nae anatia saini preventive detention order ? (2)
Mbunge Eli Anangisye, anaongea bungeni kuhusu fiscal policy ya Nchi, anatoka hapo anakamatwa ! Ndugu zangu, umesikia hilo, kuchangia kikao cha bajeti Bungeni! (3)
Hebu imagine! Sekunde mbili, u pose u imagine. Mbunge! Sisemi waliotuhumiwa na uhani, sijui Bibi Titi, sisemi Otini Kambona, na McGhee na Mattaka na Banyikwa. No, wabunge wanaochangia bajeti!
At a meeting of the National Executive Committee held in Tanga last October, nine TANU members were expelled. They included ...the former TANU Youth League Secretary and MP, Mr. E. Anangisye , who was in detention and apparently was closely connected with Kambona. The other seven who were expelled were all Members of Parliament who had been outspoken on various issues. Two had objected to the way that Ujamaa villages were being set up in their region, West Lake; another had complained about lack of freedom within the party and had objected to the failure of Zanzibar to carry out elections. The MPs who were expelled lost their seats in the National Assembly. They were not accused of specific violations of the Arusha provisos on economic accumulation but were said by party newspaper to have "grossly violated the Party creed both in their actions and attitudes, all of which sum up to a very clear opposition to the Party and its policies."( 1 )
Nimesema siwezi kufunga kamba za viatu vya Nyerere, lakini, tusiongopeane kuhusu yaliyojiri. Tusishtuke tukisikia mtu anasema hero fulani sio hero, au hakupata sifa fulani tulizodhani kapata. Ndio nchi nyingine zilivyoendelea hivyo, kutoogopa kuchambuana na kukosoana na kuambiana ukweli. Ndiko tunakokwenda huko, na watu watazidi kuongezeka Tanzania wanaosema kuwa mambo sio kama, na hayakuwahi kuwa kama, tulivyoimbishwa toka utotoni. Msiogope ukweli!
( 1 ) Foreign Affairs; April 1969 Edition; pg. 545-
(2) Chris Maina Peter; Incarcerating the Innocent: Preventive Detention in Tanzania; 1997 The Johns Hopkins University Press, Human Rights Quarterly 19.1 (1997) 113-135
(3 )Raymond F. Hopkins, The role of an MP in Tanzania, Swarthmore College; Ludovick S Mwijage, The dark side of Nyerere's Legacy;