Kuhani
JF-Expert Member
- Apr 2, 2008
- 2,944
- 64
Mwalimu alikuwa na dhamira ya kuacha uongozi tangu miaka ya 70 zaidi ya miaka 10 kabla ya kungatuka mwaka 1985. Aliamini kwa dhati kabisa kwamba walikuwepo watu ambao wametajwa humu na baadhi ya wachangiaji, watu kama Marehemu Sokoine, Marehemu Mzee Bomani, Mzee Malecela, Mzee Job Lusinde, Dr. Salim Ahmed Salim, Judge Sinde Warioba, Mzee Cleopa Msuya na wengine ambao hadi leo hii bado...
Madai kama hayo, Bibi Ntilie, huwezi kuyasema kijuu juu hivyo bila substantiation. Katika chaguzi za Raisi, Nyerere alikuwa anashindana na kiboxi kitupu, hakuwahi hata kushindana na mtu. Ukisema alitaka kutoka miaka ya '70, ni jambo la ajabu kutamka. Ni kitu ambacho hakijawahi kusikika, ni bizarre!
...hivi wakati huo kabla ama baada ya Uhuru, wananchi wangapi walikuwa na uelewa kisiasa wa kuweza kuchangia mawazo kikamilifu katika kutunga kitu kama Azimio la Arusha ama mbinu za utekelezaji wake? Wananchi waliokuwa na uelewa wa hata namna masuala ya utawala ama mchezo wa siasa ulivyo walikuwa ni wachache mno.
Hao wachache hao waliokuwepo hao wengine tunauliza kwa nini hao wachache walifungwa, kufukuzwa kazi, kufungiwa vijijini au kwenye vyumba vya mateso vya giza?
...Ndio hao walioibuka na kaulimbiu ya Zidumu Fikra Hata humu tukianza kuimba Zidumu Fikra za Mchungaji Kishoka sidhani kwamba atatuambia ah sitaki jamani, tumeamua wenyewe hakutuomba wala kutulazimisha! Hata hivyo, Mwalimu alikuwa mwenye busara aliwahi kuikana kaulimbiu hiyo.
J.K. Nyerere angekataa kuimbiwa nyimbo za kusujudu watu wangeacha kumsujudia. Mkapa alikataa kuitwa "Mtukufu." Na watu wakakoma! Anashindwa hata na Mkapa? Hapo J.K. Nyerere amekuwa kama alifurahia kuwa a vain demigod, kimungu mtu!
Pengine Mwalimu alifanya makosa katika baadhi ya hatua alizochukua.
Hamna "pengine" hapo. Hakuna anaejadili kama Mwalimu alifanya makosa au la. Hilo halina mjadala. Ndio hayo makosa na mazuri tunayoyachambua.
Lakini, katika kuwashughulikia hao wanaodaiwa kufurukuta kuhoji, kama aliwapeleka ama aliwashitaki kwenye vikao vya Chama ikadhihirika ndani ya kikao kwamba wana makosa, wakahukumiwa na vikao hivyo, kosa la Mwalimu ni lipi?
Kosa lake ni kwamba vyombo hivi vya kushitaki watu vilikuwa kama institution zinazoitwa Mahakama za Kangaroo: Jaji, wakili, prosecutor, wazee wa baraza, court reporters na polisi wanaomlinda Jaji na mahakama wote lao moja.Yani, mshitaki, huyu J.K. Nyerere, amesha waweka waamuzi, wajumbe wa TANU, mfukoni. Wote wanamsikiliza yeye, vinginevyo waweza fungwa. Ndio hali ya hewa ilivyokuwa wakati ule era ya kuwekwa vizuizini kuzuiza hatari kutumia Sheria ya Vizuizi vya Mazuizi (Preventive Dentention Act). Ni kama unduli vile.
Niliwahi kusikia kwamba Jenerali Ulimwengu alikuwa mmoja wa Wabunge G waliokuwa wanataka Tanganyika wakati ule. Inasemekana walikwenda Msasani kwa Mwalimu kuelezea greaviences zao zilizowafanya watake/kudai Tanganyika yao! Je, katika mkutano wao na Mwalimu hawakuwa na majadiliano naye, aliwaburuza tu wasomi wazima? Nasikia aliwashinda kwa kuwaambia jambo jepesi sana, Jenerali anaweza kutuambia kama ni kweli...
Unajenga hoja yako ya msingi based on "kusemekana." Hilo ni tatizo hapo. Argument yako ya msingi ni kwamba J.K. Nyerere alikuwa ana accomodate mawazo ya wengine. Sasa ukitoa mifano ya hilo dai, huwezi kutumia hadithi za kusikia. Historia ya Tanzania ilivyopotoshwa ni kitu kinachotutatiza wengine, na sasa ukijenga hoja ya nini kilichojiri halafu unarudi huko huko kwenye kusikia unakuwa haujasema lolote la maana.
Watu ambao walidhani wanaweza kumshinda Mwalimu kwa hoja, walipoona kila wakijaribu anawaweka mahali wakajiona hoja zao hazina uzito, ndio hao wanaoeneza uvumi kwamba Mwalimu alikuwa akitoa laana za kisiasa! Walikuwa wakijimaliza wenyewe. Sisi hao hao tunaodai kwamba Mwalimu alikuwa akimaliza watu kisiasa, wakati mwingine tunamsifu kwamba alikuwa anaona mbali. Ukweli ndio huo!
Huo "ukweli" wako una mushkeli. Hiki cha Nyerere kuona mbali umekisema mara mbili humu. J.K. Nyerere aliona mbali kivipi?. Alivyoving'ang'ania toka mwanzo ndio vili feli baadae, kama unakumbuka yaliyojiri kuhusu fikra zake. Ni wakina Kambona ndio walikuwa wanamwambia Mzee hizi politics na policies zako zitatupoteza, zitatulostisha. Hakusikia. Kutokusikia sio baya sana. Uhasidi, kibaya zaidi, ni kuwafukuzisha nchini, kuwafungia kijijini (S. Mwijage, Balozi Tumbo na wengine wengi tu) au kuwafunga bila mashitaka (kina Eli Anangisye, Happy Maeda na wengine wengi tu). Wengine walikufa baada ya kuwekwa kwenye vyumba vya giza bila sababu zilizopitishwa mahakamani. Hasidi hana sababu. Hayawi hayawi yakawa: Yaliyohofiwa na kina Eli, Oscar, Kassanga, Kassela, Titi, na wengine wengi yakawa. Ufukara ukatujia. Kwa hiyo ukisema J.K. Nyerere alikuwa anaona mbali unakuwa....sijui nisemeje!
Tukubaliane kwamba Mwalimu alikuwa binadamu na aliweza kukosea kama binadamu mwingine yeyote.
Kwamba J.K. Nyerere alikuwa binadamu halina mjadala. Hakuna aliyesema kuna binadamu hakosei. Tunakosea na kukosoana. Na ndio maana uko hapa unamtetea. Ingekuwa binadamu hakosolewi kwa sababu tu ni binadamu basi kusingekuwa kuna kitu kama vile kufukuzwa mtu kazi. Si binadamu bwana? Pointi yangu hapa, Bibi Ntilie, ni kwamba ni sawa kujadili makosa ya binadamu!
Lakini, mengi aliyobuni Mwalimu, akafanya na kuyasimamia yalikuwa na mantiki sana na kwa kuwa alikuwa anaelewa kwamba analolisimamia na kulivalia njuga lilikuwa na manufaa kwa Taifa alilokuwa analiongoza, hoja za kumtaka awaze vinginevyo alikuwa hazikubali kwa sababu alikuwa anaona mbali na alikuwa anajua analofanya ni kwa nia njema na lengo zuri.
Unajua unapotoa kauli za juu juu kama hivyo kusifia vitu ambavyo viko kwenye utata na ubishani mkali kuna wengine tunakuona kama unachukulia mambo kirahisi rahisi, na kutokujali jali, unaonyesha naivete. Kuna tatizo hapo kudhani kwamba watu tutakusikiliza kumpamba J.K. Nyerere bila vidhibiti. Yani unakuwa mbali sana na watu walipofika katika mijadala kama hii. Kwa mfano, ukimtetea J.K. Nyerere kwa sababu alikuwa ana "nia njema na lengo zuri" ina maana wewe katika dunia yako mtu asingelaumiwa kwa kukosea, kama vile kazini tuseme, iwapo tu alikuwa ana nia nzuri. Hiyo mantiki sio wengi wataikubali.
...Maandishi kama haya hayamtendei haki Mwalimu. Mara ngapi Mwalimu alikuwa akienda Chuo Kikuu kujadiliana na wasomi kuhusu mustakabali wa nchi?
Alienda kujadili mara sifuri. J.K. Nyerere alikuwa akienda Chuo Kikuu kugombeza watu tu, kama sio kuwachapa wakina marehemu Mwabulambo viboko matakoni! Hakwenda "kujadiliana na wasomi kuhusu mustakabali wa nchi"!
Mlango wa Msasani ulikuwa wazi wakati wote lakini watu kwa woga wao wakawa hawathubutu kuomba kuonana na Mwalimu ili watoe mawazo yao. Wengine wakawa wanasingizia kwamba Butiku alikuwa akiwazuia kumuona Mwalimu! Wachache waliokuwa wakijiamini,
Maofisa wa serikali hawatakiwi kwenda nyumbani kwa Rais kujikomba komba undugu. Wanaongea rasmi bungeni, cabinet meetings, vikao vya chama, na kupitia official and expert recommendation kwenye makaratasi. Sio "kuomba kuonana Msasani... kusikilizwa kwa makini." Mambo ya Serikali hayaendeshwi hivyo.
Mwalimu alikuwa akiwasikiliza kwa makini sana. Mwalimu alikuwa akiwasikiliza wazee kwa vijana, hata wahudumu, wapishi, madobi, madreva n.k. na kufanyia kazi aliyoyapata kutoka kwao, sembuse viongozi wenziwe?
Madobi na wapishi! Hii pointi ni dhaifu sana kwa sababu unajipiga risasi mguuni kwa kuonyesha kwamba Nyerere alikuwa comfortable kujadili siasa na wahudumu na madereva. J.K. Nyerere mwenyewe angesikia unasema hivyo angekuruka. Tulitaka ajadili nyeti za Taifa na wabunge na viongozi wa mawizara na wakuu wa mashirika na maofisa wengine wa Chama na Serikali. Sio awa convince wapiga pasi au gardeners wa nyumbani kwake, na wapishi, Bibi Ntilie.
Hivi ni kweli Mwalimu alikuwa akilizuia Bunge la chama kimoja kujadiliana juuya namna ya kuboresha ama kushughulikia matatizo ya ki-sera zilizolenga kumkomboa Mtanzania mpaka sera hizo zinakufa etc etc?
Alikuwa anazuia wanaopinga politics na policies zake Bungeni. Kuna vidhibiti vya kiutafiti vya wasomi wengine, sio makala ya Ulimwengu tu, vimewekwa humu.
Viongozi wa mashirika na wananchi waliopewa na Serikali majukumu ya kuuza nyama na chumvi wangelikuwa ni watendaji wazalendo wenye uchungu wa dhati ya maendeleo ya nchi yao, mashirika yote yakaendeshwa kwa ufanisi uliodhamiriwa, leo hii Tanzania tungelikuwa wapi? Mameneja wangapi walijenga nyumba na kufuja fedha za mashirika, kufanya ubadhilifu wa kila aina kwa kutumia nafasi za uongozi walizopewa?
Sasa hapa, Bibi Ntilie, unakuwa unahamisha lawama kwenda kwa mafisadi wa Nyerere peke yao. Ni kweli kwamba viongozi walinuka rushwa wakati wa Nyerere administration, na mashirika hayakuendeshwa kwa ufanisi chini ya Nyerere administration, lakini hili halimaanishi kosa si la Nyerere pia. Makosa ni ya wote, lakini tunajadili sera na fikra za Nyerere hapa. Ni yeye ndie alikuwa dereva wa mashua. Yeye ndio alikuwa kiongozi. Sasa dereva wa mashua kwa nini wataka akae nyuma ?
Kama Wachina wameweza kujipatia maendeleo ya kiuchumi haraka, sisi ambao tunaambiwa kiongozi wetu alikuwa akiwaiga wao na kusikiliza kila alilosema, ilikuwaje na tulishindwaje kuwa kama Wachina?
Wachina, Bibi Ntilie, hawakupata maendeleo kwa sababu ya vijiji vya ujamaa. Tena ni baada ya kuanza ku reverse mifumo inayofanana na ujamaa, hususan mashamba ya vijiji vya kisoshalisti, miaka ya mwisho ya '70 ndio walianza kuona mafanikio. Na siku hizi Uchina imeanza kufanana na ubepari katika mgawanyo wa mapato.
Kwa hiyo, mengi ya unayoyadai kuhusu J.K. Nyerere yana mapungufu makubwa, halafu kinachosikitisha, na wakati mwingine kughafirisha, ni kwamba umeyachukulia kijuu juu tu. Na katika mkanganyiko wa masikitiko na maghafirisho hayo unajikuta mtu unapoteza civility na kujibu dismissively, kama pale awali, na nasema tena, unisale kwa hilo.