Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

Mwalimu alikuwa na dhamira ya kuacha uongozi tangu miaka ya ’70 zaidi ya miaka 10 kabla ya kung’atuka mwaka 1985. Aliamini kwa dhati kabisa kwamba walikuwepo watu ambao wametajwa humu na baadhi ya wachangiaji, watu kama Marehemu Sokoine, Marehemu Mzee Bomani, Mzee Malecela, Mzee Job Lusinde, Dr. Salim Ahmed Salim, Judge Sinde Warioba, Mzee Cleopa Msuya na wengine ambao hadi leo hii bado...

Madai kama hayo, Bibi Ntilie, huwezi kuyasema kijuu juu hivyo bila substantiation. Katika chaguzi za Raisi, Nyerere alikuwa anashindana na kiboxi kitupu, hakuwahi hata kushindana na mtu. Ukisema alitaka kutoka miaka ya '70, ni jambo la ajabu kutamka. Ni kitu ambacho hakijawahi kusikika, ni bizarre!

...hivi wakati huo kabla ama baada ya Uhuru, wananchi wangapi walikuwa na uelewa kisiasa wa kuweza kuchangia mawazo kikamilifu katika kutunga kitu kama Azimio la Arusha ama mbinu za utekelezaji wake? Wananchi waliokuwa na uelewa wa hata namna masuala ya utawala ama mchezo wa siasa ulivyo walikuwa ni wachache mno.

Hao wachache hao waliokuwepo hao wengine tunauliza kwa nini hao wachache walifungwa, kufukuzwa kazi, kufungiwa vijijini au kwenye vyumba vya mateso vya giza?

...Ndio hao walioibuka na kaulimbiu ya “Zidumu Fikra…” Hata humu tukianza kuimba “Zidumu Fikra za Mchungaji Kishoka” sidhani kwamba atatuambia ‘ah sitaki jamani’, tumeamua wenyewe hakutuomba wala kutulazimisha! Hata hivyo, Mwalimu alikuwa mwenye busara aliwahi kuikana kaulimbiu hiyo.

J.K. Nyerere angekataa kuimbiwa nyimbo za kusujudu watu wangeacha kumsujudia. Mkapa alikataa kuitwa "Mtukufu." Na watu wakakoma! Anashindwa hata na Mkapa? Hapo J.K. Nyerere amekuwa kama alifurahia kuwa a vain demigod, kimungu mtu!

Pengine Mwalimu alifanya makosa katika baadhi ya hatua alizochukua.

Hamna "pengine" hapo. Hakuna anaejadili kama Mwalimu alifanya makosa au la. Hilo halina mjadala. Ndio hayo makosa na mazuri tunayoyachambua.

Lakini, katika kuwashughulikia hao wanaodaiwa kufurukuta kuhoji, kama aliwapeleka ama aliwashitaki kwenye vikao vya Chama ikadhihirika ndani ya kikao kwamba wana makosa, wakahukumiwa na vikao hivyo, kosa la Mwalimu ni lipi?

Kosa lake ni kwamba vyombo hivi vya kushitaki watu vilikuwa kama institution zinazoitwa Mahakama za Kangaroo: Jaji, wakili, prosecutor, wazee wa baraza, court reporters na polisi wanaomlinda Jaji na mahakama wote lao moja.Yani, mshitaki, huyu J.K. Nyerere, amesha waweka waamuzi, wajumbe wa TANU, mfukoni. Wote wanamsikiliza yeye, vinginevyo waweza fungwa. Ndio hali ya hewa ilivyokuwa wakati ule era ya kuwekwa vizuizini kuzuiza hatari kutumia Sheria ya Vizuizi vya Mazuizi (Preventive Dentention Act). Ni kama unduli vile.

Niliwahi kusikia kwamba Jenerali Ulimwengu alikuwa mmoja wa Wabunge G… waliokuwa wanataka Tanganyika wakati ule. Inasemekana walikwenda Msasani kwa Mwalimu kuelezea greaviences zao zilizowafanya watake/kudai Tanganyika yao! Je, katika mkutano wao na Mwalimu hawakuwa na majadiliano naye, aliwaburuza tu wasomi wazima? Nasikia aliwashinda kwa kuwaambia jambo jepesi sana, Jenerali anaweza kutuambia kama ni kweli...

Unajenga hoja yako ya msingi based on "kusemekana." Hilo ni tatizo hapo. Argument yako ya msingi ni kwamba J.K. Nyerere alikuwa ana accomodate mawazo ya wengine. Sasa ukitoa mifano ya hilo dai, huwezi kutumia hadithi za kusikia. Historia ya Tanzania ilivyopotoshwa ni kitu kinachotutatiza wengine, na sasa ukijenga hoja ya nini kilichojiri halafu unarudi huko huko kwenye kusikia unakuwa haujasema lolote la maana.

Watu ambao walidhani wanaweza kumshinda Mwalimu kwa hoja, walipoona kila wakijaribu anawaweka mahali wakajiona hoja zao hazina uzito, ndio hao wanaoeneza uvumi kwamba Mwalimu alikuwa akitoa laana za kisiasa! Walikuwa wakijimaliza wenyewe. Sisi hao hao tunaodai kwamba Mwalimu alikuwa akimaliza watu kisiasa, wakati mwingine tunamsifu kwamba alikuwa anaona mbali. Ukweli ndio huo!

Huo "ukweli" wako una mushkeli. Hiki cha Nyerere kuona mbali umekisema mara mbili humu. J.K. Nyerere aliona mbali kivipi?. Alivyoving'ang'ania toka mwanzo ndio vili feli baadae, kama unakumbuka yaliyojiri kuhusu fikra zake. Ni wakina Kambona ndio walikuwa wanamwambia Mzee hizi politics na policies zako zitatupoteza, zitatulostisha. Hakusikia. Kutokusikia sio baya sana. Uhasidi, kibaya zaidi, ni kuwafukuzisha nchini, kuwafungia kijijini (S. Mwijage, Balozi Tumbo na wengine wengi tu) au kuwafunga bila mashitaka (kina Eli Anangisye, Happy Maeda na wengine wengi tu). Wengine walikufa baada ya kuwekwa kwenye vyumba vya giza bila sababu zilizopitishwa mahakamani. Hasidi hana sababu. Hayawi hayawi yakawa: Yaliyohofiwa na kina Eli, Oscar, Kassanga, Kassela, Titi, na wengine wengi yakawa. Ufukara ukatujia. Kwa hiyo ukisema J.K. Nyerere alikuwa anaona mbali unakuwa....sijui nisemeje!

Tukubaliane kwamba Mwalimu alikuwa binadamu na aliweza kukosea kama binadamu mwingine yeyote.

Kwamba J.K. Nyerere alikuwa binadamu halina mjadala. Hakuna aliyesema kuna binadamu hakosei. Tunakosea na kukosoana. Na ndio maana uko hapa unamtetea. Ingekuwa binadamu hakosolewi kwa sababu tu ni binadamu basi kusingekuwa kuna kitu kama vile kufukuzwa mtu kazi. Si binadamu bwana? Pointi yangu hapa, Bibi Ntilie, ni kwamba ni sawa kujadili makosa ya binadamu!

Lakini, mengi aliyobuni Mwalimu, akafanya na kuyasimamia yalikuwa na mantiki sana na kwa kuwa alikuwa anaelewa kwamba analolisimamia na kulivalia njuga lilikuwa na manufaa kwa Taifa alilokuwa analiongoza, hoja za kumtaka awaze vinginevyo alikuwa hazikubali kwa sababu alikuwa anaona mbali na alikuwa anajua analofanya ni kwa nia njema na lengo zuri.

Unajua unapotoa kauli za juu juu kama hivyo kusifia vitu ambavyo viko kwenye utata na ubishani mkali kuna wengine tunakuona kama unachukulia mambo kirahisi rahisi, na kutokujali jali, unaonyesha naivete. Kuna tatizo hapo kudhani kwamba watu tutakusikiliza kumpamba J.K. Nyerere bila vidhibiti. Yani unakuwa mbali sana na watu walipofika katika mijadala kama hii. Kwa mfano, ukimtetea J.K. Nyerere kwa sababu alikuwa ana "nia njema na lengo zuri" ina maana wewe katika dunia yako mtu asingelaumiwa kwa kukosea, kama vile kazini tuseme, iwapo tu alikuwa ana nia nzuri. Hiyo mantiki sio wengi wataikubali.

...Maandishi kama haya hayamtendei haki Mwalimu. Mara ngapi Mwalimu alikuwa akienda Chuo Kikuu kujadiliana na wasomi kuhusu mustakabali wa nchi?

Alienda kujadili mara sifuri. J.K. Nyerere alikuwa akienda Chuo Kikuu kugombeza watu tu, kama sio kuwachapa wakina marehemu Mwabulambo viboko matakoni! Hakwenda "kujadiliana na wasomi kuhusu mustakabali wa nchi"!

Mlango wa Msasani ulikuwa wazi wakati wote lakini watu kwa woga wao wakawa hawathubutu kuomba kuonana na Mwalimu ili watoe mawazo yao. Wengine wakawa wanasingizia kwamba Butiku alikuwa akiwazuia kumuona Mwalimu! Wachache waliokuwa wakijiamini,

Maofisa wa serikali hawatakiwi kwenda nyumbani kwa Rais kujikomba komba undugu. Wanaongea rasmi bungeni, cabinet meetings, vikao vya chama, na kupitia official and expert recommendation kwenye makaratasi. Sio "kuomba kuonana Msasani... kusikilizwa kwa makini." Mambo ya Serikali hayaendeshwi hivyo.

Mwalimu alikuwa akiwasikiliza kwa makini sana. Mwalimu alikuwa akiwasikiliza wazee kwa vijana, hata wahudumu, wapishi, madobi, madreva n.k. na kufanyia kazi aliyoyapata kutoka kwao, sembuse viongozi wenziwe?

Madobi na wapishi! Hii pointi ni dhaifu sana kwa sababu unajipiga risasi mguuni kwa kuonyesha kwamba Nyerere alikuwa comfortable kujadili siasa na wahudumu na madereva. J.K. Nyerere mwenyewe angesikia unasema hivyo angekuruka. Tulitaka ajadili nyeti za Taifa na wabunge na viongozi wa mawizara na wakuu wa mashirika na maofisa wengine wa Chama na Serikali. Sio awa convince wapiga pasi au gardeners wa nyumbani kwake, na wapishi, Bibi Ntilie.

Hivi ni kweli Mwalimu alikuwa akilizuia Bunge la chama kimoja kujadiliana juuya namna ya kuboresha ama kushughulikia matatizo ya ki-sera zilizolenga kumkomboa Mtanzania mpaka sera hizo zinakufa etc etc?

Alikuwa anazuia wanaopinga politics na policies zake Bungeni. Kuna vidhibiti vya kiutafiti vya wasomi wengine, sio makala ya Ulimwengu tu, vimewekwa humu.

Viongozi wa mashirika na wananchi waliopewa na Serikali majukumu ya kuuza “nyama na chumvi” wangelikuwa ni watendaji wazalendo wenye uchungu wa dhati ya maendeleo ya nchi yao, mashirika yote yakaendeshwa kwa ufanisi uliodhamiriwa, leo hii Tanzania tungelikuwa wapi? Mameneja wangapi walijenga nyumba na kufuja fedha za mashirika, kufanya ubadhilifu wa kila aina kwa kutumia nafasi za uongozi walizopewa?

Sasa hapa, Bibi Ntilie, unakuwa unahamisha lawama kwenda kwa mafisadi wa Nyerere peke yao. Ni kweli kwamba viongozi walinuka rushwa wakati wa Nyerere administration, na mashirika hayakuendeshwa kwa ufanisi chini ya Nyerere administration, lakini hili halimaanishi kosa si la Nyerere pia. Makosa ni ya wote, lakini tunajadili sera na fikra za Nyerere hapa. Ni yeye ndie alikuwa dereva wa mashua. Yeye ndio alikuwa kiongozi. Sasa dereva wa mashua kwa nini wataka akae nyuma ?

Kama Wachina wameweza kujipatia maendeleo ya kiuchumi haraka, sisi ambao tunaambiwa kiongozi wetu alikuwa akiwaiga wao na kusikiliza kila alilosema, ilikuwaje na tulishindwaje kuwa kama Wachina?

Wachina, Bibi Ntilie, hawakupata maendeleo kwa sababu ya vijiji vya ujamaa. Tena ni baada ya kuanza ku reverse mifumo inayofanana na ujamaa, hususan mashamba ya vijiji vya kisoshalisti, miaka ya mwisho ya '70 ndio walianza kuona mafanikio. Na siku hizi Uchina imeanza kufanana na ubepari katika mgawanyo wa mapato.

ravallion1a.jpg

Kwa hiyo, mengi ya unayoyadai kuhusu J.K. Nyerere yana mapungufu makubwa, halafu kinachosikitisha, na wakati mwingine kughafirisha, ni kwamba umeyachukulia kijuu juu tu. Na katika mkanganyiko wa masikitiko na maghafirisho hayo unajikuta mtu unapoteza civility na kujibu dismissively, kama pale awali, na nasema tena, unisale kwa hilo.
 
Nyani ( I hate to call you Mc Pain)
Sasa ile nidhamu ya woga ilitoka wapi? Was it Nyerere's eyes? Maana kuna wakati niliongea na Nyirabu (rip) na akasema kabla ya kwenda kuonana na Nyerere alikuwa anapiga simu Ikulu kuwauliza wasaidizi wake Nyerere yuko katika mood gani siku hiyo. Why? Watu wengi sana nimepata kusikia wakiitwa Ikulu walikuwa wakitetemeka.

Nidhamu ya woga sina hakika ilitoka wapi. Labda ni Ndivyo Yulivyo au ni learned behavior. Ila hai make sense kwa nini watu wapige simu kuulizia yuko kwenye mood gani na kutetemeka wakiitwa ikulu. Labda ile hadithi ya Nyerere kuwacharaza watu mboko ilikuwa ni ya kweli la sivyo sioni sababu ya mtu kutetemeka akiitwa ikulu.
 
Alienda kujadili mara sifuri. J.K. Nyerere alikuwa akienda Chuo Kikuu kugombeza watu tu, kama sio kuwachapa wakina marehemu Mwabulambo viboko matakoni! Hakwenda "kujadiliana na wasomi kuhusu mustakabali wa nchi"!

Marekebisho hapo, aliowachapa viboko aliwachapia Ikulu, sio Mlimani huo ni uongo wa makusudi au kutokujua, Mwalimu alikuwa ni mkuu wa Chuo mlimani,

enzi hizo ilikuwa inaruhusiwa kuchapa viboko wanafunzi na hakukuwa na limit ni wanafunzi gani wanaruhusiwa au kutoruhusiwa, sikubaliani na watu wazima kuchapwa viboko lakini bado kuna nafasi ya kumuelewa Mwalimu on this,

Lakini hakumchapa mtu Mlimani, that is not true!
 
Maofisa wa serikali hawatakiwi kwenda nyumbani kwa Rais kujikomba komba undugu. Wanaongea rasmi bungeni, cabinet meetings, vikao vya chama, na kupitia official and expert recommendation kwenye makaratasi. Sio "kuomba kuonana Msasani... kusikilizwa kwa makini." Mambo ya Serikali hayaendeshwi hivyo.

Hii sio hoja makini, mafanikio machache ya rais Mwinyi yalitokana na tabia ya rais Mwinyi kwenda kila Jumapili pale kwenda Lummumba, kusikiliza maoni ya wananchi na viongozi, uso kwa uso,

Kuna masuala ambayo ni official yanatakiwa ikiwezekana yamalizwe kiserikali, lakini rais siku zote hana muda wa kutosha on that, kwa hiyo sio ajabu wananchi na viongozi kuomba kwenda kumuona rais nyumbani, kwa sababu kwa sheria zetu ni kwamba rais yuko on duty 24 hours a day, kwa hiyo hata kukutana naye popote pale haibadilishi anything as far as umuhimu wa yeye rais kusikiliza na kutolea maamuzi any of your comlains kwa sababu rais anaweza kutoa amri akiwa popote pale na ikawa valid sio lazima awe ofisini,

Kwa hiyo si wkeli kwua mambo ya serikali ni lazima yaendeshwe kwenye Ikulu tu, as far as rais is concerned!
 
Zakumi,
Hindsight is always 20/20. You can afford to say that now from the comforts of hindsight.

Jasusi:

Hivi vitu vyote vilikuwepo. Na kuna nchi zilizotumia models kunyanyua nchi zao. Chukua mfano wa India ambayo ilikuwa inakabiliwa na matatizo ya ukosefu wa chakula mpaka miaka ya sabini. Ni green revolution iliyofanya India ijitegemee.

Tatizo la viongozi wa Afrika asa Kizazi cha Nyerere, walitumia muda mrefu ku-reinvent the wheel wakati solutions zipo.

Vilevile Nyerere angekuwa amekaa madarakani kwa miaka kumi ningekubaliana na usemi. Mtu amekaa madarakani kwa miaka 25 na kushindwa kupata hindsight.
 
So how long did it take India from Independence to get to Green Revolution?

On the other hand, ungeniambia kuwa Tanzania tuliji stretch kupita kiasi hasa kuhakikisha kuwa nchi za Afrika zina kuwa huru kwa kuwasaidia kiuchumi, kijeshi na kisiasa Zimbabwe, Afrika Kusini, Msumbiji, Angola na wenginewe na hivyo kujijengea uadui na Makaburu na kuvuja uchumi kusaidia wengine na si kujijenga sisi wenyewe ningekuelewa.

Lakini nitarudi kwenye swali ambalo nimeendelea kuuliza Watanzania wanaolaumu Umasikini wa Tanzania kwa Nyerere.

Nyerere alistaafu Uraisi miaka 23 iliyopita, akajivua Uenyekiti wa Chama karibu miaka 20 iliyopita, na Mungu kamwita mahali pema peponi miaka 9 iliopita.

NI vipi basi bado tunachechemea na tumeshindwa kusahihisha makosa ya Mwalimu?

Tumeambiwa hapa kuwa Wananchi waliupenda na kuuimba Ujamaa, lakini walikuwa wazito kufanya kazi au kuuamini na kuutumikia. Sasa tuna mfumo wa soko huria na Ubepari Uchwara, mbona hatuoni mabadiliko yeyote kwa Mtanzania?

Kwa kweli matatizo yetu ya unyonge na umasikini yaliletwa na Nyerere, sasa tuko huru. Fikra zake kaondoka nazo. Hata Ujamaa na Azimio kaondoka navyo, je ni msukumo gani tulionao Tanzania kujiendeleza na kujikwamua kiuchumi?

Jee wale adui Njaa, Umasikini, Maradhi, Ujinga na Unyonge walikuwa ni maadui wa itikadi na fikra za Nyerere pekee? Je kwa kufa kwa Ujamaa na Azimio la Arusha tiba dhidi ya hawa maadui imepatikana?

Je waliomfuatia Mwinyi, Mkapa na Kikwete, wao walikuwa na wana ushawishi gani wa kisiasa na itikadi kutuongoza? who influenced them?
 
Jasusi:

Hivi vitu vyote vilikuwepo. Na kuna nchi zilizotumia models kunyanyua nchi zao. Chukua mfano wa India ambayo ilikuwa inakabiliwa na matatizo ya ukosefu wa chakula mpaka miaka ya sabini. Ni green revolution iliyofanya India ijitegemee.

Tatizo la viongozi wa Afrika asa Kizazi cha Nyerere, walitumia muda mrefu ku-reinvent the wheel wakati solutions zipo.

Vilevile Nyerere angekuwa amekaa madarakani kwa miaka kumi ningekubaliana na usemi. Mtu amekaa madarakani kwa miaka 25 na kushindwa kupata hindsight.

Bado hindsight ni 20/20. Was it Gandhi who started the green revolution in
India or the following generation of leaders? Viongozi wa kizazi cha Nyerere walikuwa pioneers au trailblazers. Lakini at least walikuwa na vision. What is the vision of the current leadership?
 
.

Swadakta. Hamna mtu level-headed hapa na menye civility kama Rev. Kishoka. Lakini kwenye mijadala inayogusa hisia zake kama huu, anashindwa kuwa consistently even-tempered. Inasikitisha.

Kuhani,

I have never seen you be so emotional and loose your composure like this! Infact you came back and responded to Bibi Ntilie with sort of soft touch words, but you are still high on nitro of emotions.

Ukiachia hao jamaa zako waliofungwa, let me change the direction of the thread na kutumia approach ya Tutu ya truth and reconciliation.

Umesema kuna watu wengi waliwekwa kizuizini na hata kufia huko. Ukiondoa kina Anangisywe tunaowafahamu, wengin ni kina nani?

Umeonyesha kuwa ukatili wa Nyerere kugandamiza haki za binadamu na ubabe ni karibu sawa na kile kikosi cha Simba cha Amini na hata mimi taswira ninazozipata ni zile za kina Bishop Luwum, ni picha kutoka kitabu cha Henry Kyemba. Je una maana Tanzania tulifika huko?

Je wale wote ambao unadai waliteswa na kuuwawa na Nyerere, familia zao ziko wapi nyakati hizi kuishtaki Serikali, kwa kuwa Nyerere alikuwa ni Serikali?

Je kama muathirika, umechukua hatua gani ya kusahihisha hilo jambo machoni pa Watanzania wote kwa kutaka hata katume kaundwe kuchunguza tuhuma?

Unajua kuwa hizi ni tuhuma za mauaji na ni mpaka kuwe na ushahidi na vithibitisho ndipo utakuwa ni ukweli?

Pole kwa yanayokusibu mpaka ukaghafilika namna hii. Lakini usipoteze utu wako.
 
1.
Unajenga hoja yako ya msingi based on "kusemekana." Hilo ni tatizo hapo. Argument yako ya msingi ni kwamba J.K. Nyerere alikuwa ana accomodate mawazo ya wengine. Sasa ukitoa mifano ya hilo dai, huwezi kutumia hadithi za kusikia. Historia ya Tanzania ilivyopotoshwa ni kitu kinachotutatiza wengine, na sasa ukijenga hoja ya nini kilichojiri halafu unarudi huko huko kwenye kusikia unakuwa haujasema lolote la maana.

2.
Alienda kujadili mara sifuri. J.K. Nyerere alikuwa akienda Chuo Kikuu kugombeza watu tu, kama sio kuwachapa wakina marehemu Mwabulambo viboko matakoni! Hakwenda "kujadiliana na wasomi kuhusu mustakabali wa nchi"!

Another one, hapa unamlaumu Bibi Ntilie kuwa amejenga hoja based on habari ya kusikia, great!

Halafu na wewe mwenyewe tena unajenga hoja hapo quote ya chini on habari kama ile unayomlaumu Bibi Ntilie, ya kusikia unless unaweza ku-prove hapa JF kuwa ulikuwepo wakati Mwalimu anamchapa viboko Marehemu Mwabulambo,

Otherwise, my point ni kwamba katika siasa unaweza kujenga hoja kwa habari ya kusikia zaidi kuliko kuona, na ndio hasa uti wa mgongo wa analysis zetu hapa JF, ni habari za kusikia isipokuwa unawaachia wananchi wasomaji kuamua how wanataka ku-deal na context ya hoja zako, kwenye argument.

Thanx!
 
Madai kama hayo, Bibi Ntilie, huwezi kuyasema kijuu juu hivyo bila substantiation. Katika chaguzi za Raisi, Nyerere alikuwa anashindana na kiboxi kitupu, hakuwahi hata kushindana na mtu. Ukisema alitaka kutoka miaka ya '70, ni jambo la ajabu kutamka. Ni kitu ambacho hakijawahi kusikika, ni bizarre!

I mean here is another one, si kweli kuwa Mwalimu hakuwahi kushindana na mtu, that is wrong kwa sababu historia iko very clear kuwa kuelekea uhuru Mwalimu alishindana na vyama vingi vingine vya siasa, lakini yeye na TAA ndio wakaibuka washindi, ingawa in a small picture you might have a point, lakini in the bigger picture hapana Mwalimu aliwahi kushindana na vyama vingine vya siasa.

Thanx!
 
Kwamba J.K. Nyerere alikuwa binadamu halina mjadala. Hakuna aliyesema kuna binadamu hakosei. Tunakosea na kukosoana. Na ndio maana uko hapa unamtetea. Ingekuwa binadamu hakosolewi kwa sababu tu ni binadamu basi kusingekuwa kuna kitu kama vile kufukuzwa mtu kazi. Si binadamu bwana? Pointi yangu hapa, Bibi Ntilie, ni kwamba ni sawa kujadili makosa ya binadamu!

Very strong, lakini it is about time sasa tukasikia toka kwako the otherside of Mwalimu, maana tumekuwa used na kukusikia kwenye one side ya mapungufu yake, labda haitakuwa vibaya for once tukasikia the otherside kutoka kwako!
 
Bado hindsight ni 20/20. Was it Gandhi who started the green revolution in
India or the following generation of leaders? Viongozi wa kizazi cha Nyerere walikuwa pioneers au trailblazers. Lakini at least walikuwa na vision. What is the vision of the current leadership?

Nyerere hakuwa technocrat (period). Alikuwa na vision lakini vision zake zilikuwa impractical to implement.

Kizazi cha Nyerere kilikuwa na pupa za maendeleo bila kuwa mipango yoyote ya kuendeleza maendelo hayo.

Katika kipindi kisichozidi miaka kumi alikuwa na mipango ifuatayo:
azimio la Arusha
Azimio la Musoma
Vijiji vya Ujamaa
Operesheni maduka
Mamlaka za Mazao
UPE
N.K

Niambie visionary gani huyo kabla mpango mmoja aujaota mizizi mpango mwingine umeanza.
 
...a visionary who is impatient with the level of development. A visionary who had ideas about development, that's who!
 
Kizazi cha Nyerere kilikuwa na pupa za maendeleo bila kuwa mipango yoyote ya kuendeleza maendelo hayo.

Hapo mkuu haijakaa sawa, the ishu hapa sio kizazi kizima please, the ishu inapaswa kua mafanikio na mapungufu ya Mwalimu, as a leader,

Ninasema inapaswa kwa sababu so far ni mapungufu tu yanayojadiliwa, mkuu Zakumi ni kweli kwamba hakukuwa na hta moja zuri la Mwalimu unaloliona leo? I mean lets say kwamba your argument ni valid kwamba kizazi cha Mwalimu kilikuwa na papara,

Can you real argue politically tena on a serious note kwamba, kizazi cha Mwalimu, kilikuwa na papara, comparing to kizazi cha kasi mpya na ari mpya?

Halafu ninaamini kuwa nyinyi wote huko on your side ni wasomi, hivi kweli jamani ni lini tuliacha ku-compare na ku-contrast, katika kujaribu ku-present a big picture ya utawala wa kisiasa uliowahi kuwepo kwenye power? Mbona hatulinagnishi kabisa na utawala wa Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete? I mean sasa una present vipi a paper ya critique bila ya kulinganisha?

Zakumi,

Nyerere alikuwa mjamaa na alisema kuwa Ujamaa ni Imani na ni watu. Alileta mfumo wa ujamaa akiamini ni njia ya kujenga taifa linalojitegemea.

Wamarekani walisema ubepari ndio njia pekee ya mafanikio na maendeleo, wakaruhusu soko huria na watu kujifanyia wanavyotaka.

Sasa common denominator hapa ni hizo unazosema, chakula, paa na afya, sisi Tanzania tulipokuwa na sera za kutoa afya na elimu bure, tulikoromewa kwa ni makosa makubwa.

Kweli ilikuwa makosa makubwa kwa kuwa hatukuwa na mtaji wa kutosha, lakini ili kuwa ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kuwa kila mtu anapata furs ya kusoma na kuwa na afya njema.

Marekani, elimu ya msingi na sekondari ni bure, afya pamoja na kuwa kila mtu anahitaji bima, bado kama huna bima unaweza kwenda tibiwa hospitali bure.

Swali ni kwa nini iwe sawa kwa Marekani kuwa na elimu bure na hata huduma za afya bure lakini iwe ni sumu kwa Tanzania? tutang'ang'ania kuwa Tanzania haikuwa na mtaji wa kutosha? je kujenga nchi na taifa tukiwa na watu wenye siha bora na elimu tungefanikiwa vipi kama tungesema kila mtu alipie ili kunusuru viwanda na kujijenge utajiri?

Rev:

Kama ujamaa ni imani basi toka mwanzo ilitakiwa isiwe sio siasa ya kutawala nchi.

Imani siku zote ni RIGID. Na kutokana na fikra zake kuwa siasa za kuleta maendeleo ya kuaminiwa na Nyerere mwenyewe alikuwa RIGID.
 
Back
Top Bottom