Bibi Ntilie said:
Kama Kuhani haamini hilo, akafanye 'utafiti' na atagundua kwamba baada ya Azimio la Arusha uchumi wa nchi ulikua mwaka hadi mwaka mpaka mwaka 1977. Kuvunjika kwa Jumuiya ya Mashariki kuliyumbisha uchumi wetu, Vita vya Kagera vya 1978, kupanda kwa bei ya mafuta na janga la njaa tangu mwaka 1979 - 1983; ukichanganya na watu kutamani utajiri bila kuuhenyea vilichangia kuzorotesha kukua kwa uchumi na kufanya tusiweze kusonga mbele zaidi. Mwalimu, Ujamaa ama Azimio si sababu.
'Siri' ama msingi wa mafanikio ya kukua kwa uchumi kwa miaka yote hiyo ilikuwa ni siasa ya Ujamaa iliyozaa Azimio la Arusha na kupelekea Serikali kuchukua hatua za makusudi kudhibiti njia kuu za uchumi.
Bibi Ntilie,
..baada ya azimio la arusha tulianza harakati za kujenga viwanda, which i believe was a good decision.
..lakini azimio hilo hilo, utaifishaji wa mashamba makubwa, na operesheni vijiji, vilisababisha mazao ya katani, na korosho kuanguka.
..hasara za matukio hayo zinafichwa na mafanikio ya muda mfupi ya ujenzi wa viwanda, na kupanda kwa bei ya kahawa[coffee boom] ya miaka ile.
..unajua tatizo lingine la Mwalimu lilikuwa ni kuvuruga hata pale ambapo things were working fine ilimradi tu atekeleze itikadi zake.
..alichopaswa kufanya Mwalimu ni kuanzisha mashamba mapya ya mkonge, siyo kutaifisha yale yaliyokuwa yakizalisha na kuchangia ktk pato la taifa.
..Mwalimu pia hakupaswa kwenda kuswaga watu na kupeleka kwenye vijiji vya ujamaa, huku wakiacha mazao na ardhi zao un-attended.
..Mwalimu hakupaswa kuvunja vyama vya ushirika. mimi nilifikiri ushirika ni moja kati ya misingi ya ujamaa. kuna vyama vya ushirika vilivyovunjwa vilikuwa na umri wa zaidi ya miaka 30.
NB:
..Mwalimu aliondoka wakati nchi ina hali mbaya kabisa kiuchumi. inflation ilikuwa ktk double-digits, viwanda vilikuwa vimesimama, hazina ilikuwa haina akiba ya fedha kulipia bidhaa muhimu kama mafuta.
..kitu cha ajabu kabisa Mwalimu hakujiuzulu kutokana na makosa yake ktk kuongoza nchi na kuendesha uchumi. wakati anaondoka alipaswa kueleza bayana kwamba alikuwa ameharibu na ameshindwa, badala yake akasema anangatuka kwasababu ametawala kwa muda mrefu.
..Mwalimu angetuangalia machoni wa-Tanzania na kutueleza kwamba amekosea, na angeachana na propaganda zake na visingizio, tusingekuwa na mjadala huu. vilevile angeisaidia nchi hii kusonga mbele, na kuepukana na makosa yake.