Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

Nyani McCain said:
Some of you are so hung up on the past that you can't move forward with your lives. It's getting kinda old now...

Nyani McCain,

..i lived thr' the hardship brought on to us by Mwalimu's policies and decisions.

..sasa kuna ving'ang'anizi wanajaribu kutuambia kwamba tulikuwa na maisha mazuri kuliko wakati wowote.

..the country is trying to move on, lakini hawa 'watetezi' wa Mwalimu wa kila hali ndiyo wanataka kuturudisha kulekule tulikotoka.

Mwanakijiji,

..Mwalimu hakuwa straight forward ktk kukiri makosa na matatizo ya utawala wake.

..huoni kwamba hata anapokiri kukosea anafanya hivyo akiwa na vyombo vya habari vya nje, years after he resigned.

..Mwalimu alipaswa kutuangalia wa-Tanzania machoni, mwaka 1985 wakati anaondoka madarakani, na kutueleza kwamba amekosea, ameharibu, na anaondoka madarakani kwasababu ameshindwa, siyo kwasababu amechoka au ametawala kwa muda mrefu.
 
JokaKuu, ni wazi kuwa hujui Historia ya Nyerere au hujachukua muda kujifunza. Hakuna kiongozi wa Tanzania ambaye amekuwa straighforward na watu wake kama Nyerere. Umpende au usimpende, barua, maandishi, hotuba n.k vinapatikana kiurahisi tu kwa mtu yeyote anayetaka kumjua Mwalimu. Kuhusu yeye kukiri mapungufu au makosa ya uongozi wake, umewahi kuisikiliza hotuba yake ya Mei Mosi 1995 uwanja wa Sokoine pale Mbeya? Itafute.

Na kuhusu mwaka 1985 tafuta hotuba yake alipoagana na Jeshi la Magereza na utaona alichokisema wakati ule na no hakudai kuwa amechoka!
 
Nawashukuru nyote mlionitetea dhidi ya makombora ya Kuhani. Pengine Kuhani aelewe tu kuwa pamoja na kwamba hivi sasa niko jikoni nampikia mjukuu wangu, mambo haya ya kuingia kwenye discussion forums mie sio wa kuja! Tulikuwepo tangu enzi za Nyenzi.com. Kwa ubishi katika jambo ambalo ninalijua ukweli wake mie ndio mwenyewe! Siwezi kujitapa kwamba najua kila kitu kuhusu Mwalimu lakini kidogo ninachojua kinaniwezesha kuchangia kwa kujiamini kabisaa!

Naamini wengi ama baadhi ya wanaojadili humu ni watu ambao wanaangalia mambo yanavyokwenda kisiasa na hawana mahali pa kuweza kutoa mchango wao ama madukuduku yao. La msingi ni kuchangia na kuvumiliana tu.

Mie siasa ninayoijua kwa dhati kabisa ni ya Nyerere maana siku ya Uhuru nilivaa gauni lenye rangi ya bendera ya Tanganyika. Enzi hizo siasa za Nyerere zilikuwa zimemuingia kila mtu kwa sababu moja kubwa - zilikuwa ni siasa zilizojali sana welfare ya wananchi ambao wote walikuwa wa hali ya chini, wa matawi ya juu hawakuwepo enzi hizo.

Naweza pia nikasema kutokana na kufahamu kwa kuona mwenyewe nchi ilikuwa katika hali gani wakati tunapata Uhuru na juhudi gani zilifanywa na Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Mwalimu Nyerere ndani ya miaka 15 (awamu moja na nusu) baada ya Uhuru, yaliyofanywa yalikuwa ni mageuzi ya hali ya juu.

Ningeliweza kuorodhesha hapa mambo makubwa, moja baada ya jingine, yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere kutokana na utu aliokuwanao Mwalimu ambao ndio uliozaa Ujamaa aliojaribu kuujenga na Azimio la Arusha. Pamoja na kuwepo makosa ya kiutendaji yanayotajwa, Taifa lilisonga mbele.

Kama Kuhani haamini hilo, akafanye 'utafiti' na atagundua kwamba baada ya Azimio la Arusha uchumi wa nchi ulikua mwaka hadi mwaka mpaka mwaka 1977. Kuvunjika kwa Jumuiya ya Mashariki kuliyumbisha uchumi wetu, Vita vya Kagera vya 1978, kupanda kwa bei ya mafuta na janga la njaa tangu mwaka 1979 - 1983; ukichanganya na watu kutamani utajiri bila kuuhenyea vilichangia kuzorotesha kukua kwa uchumi na kufanya tusiweze kusonga mbele zaidi. Mwalimu, Ujamaa ama Azimio si sababu.

'Siri' ama msingi wa mafanikio ya kukua kwa uchumi kwa miaka yote hiyo ilikuwa ni siasa ya Ujamaa iliyozaa Azimio la Arusha na kupelekea Serikali kuchukua hatua za makusudi kudhibiti njia kuu za uchumi.

Hata kama Kuhani hataki kukubali kwa sababu zake binafsi, Mwalimu alikuwa kiongozi aliyekubalika sana kwa sababu alijali wananchi aliokuwa akiwaongoza na mikakati yake yote ukiwemo Ujamaa na Azimio aliibuni kwa maslahi ya wananchi na si kwa maslahi yake binafsi, ama watoto wake, Wazanaki wenziwe ama marafiki. Kiongozi yoyote anayetaka kuiongoza nchi kwa mafanikio asijaribu kuvaa viatu vya Mwalimu maana vyaweza visimtoshe, lakini anaweza akafuata nyayo za Mwalimu katika misingi ya utu na kujali mustakabali wa wananchi wote, na kudhihirisha kwamba anajali zaidi wale wa hali ya chini ambao ndio majority.

Bibie:

Umefika wakati tuambizane ukweli. Kuna ukweli kuwa uchumi wa Tanzania ulionyesha kukua mpaka miaka ya katikati ya 1970.

Swali linalokuja, je ni kitu gani kilichangia ukuaji wa uchumi huo ? Katika posti yako unalipongeza Azimio la Arusha. Lakini huo sio ukweli.

Pesa za misaada na mikopo zinahesabiwa katika ongezeko la pato la nchi. Na Takwimu zinaonyesha kabisa kuwa kuanzia kipindi cha 1968 mpaka 1977, Tanzania ilipewa misaada na mikopo mingi.

Hivyo ongezeko la uchumi uliloona halitokani na juhudi za watanzania katika vijiji vya ujamaa. Linatokana na misaada na mikopo.

Hata Mobutu Seseko katika kipindi cha hichohicho alifanya mabadiliko makubwa sana Zaire. Na hiki ni kipande cha Rais wa Marekani kukaribisha Mobutu tarehe August 4, 1970: Mr. President, Since I came into office over 18 months ago, you are the youngest head of state to be honored in this room, and you represent the youngest nation, but though you are a young man and you come from a young nation, there are things we can learn from you. Tomorrow, I have a meeting scheduled with my cabinet on the budget. I find in studying your administration that you not only have a balanced budget but a favored balanced of trade and I had like to know your secret before our meeting with the cabinet.

Hivyo Bibie sio Tanzania peke yake iliyofanya vizuri katika kipindi hicho na sio siasa za Ujamaa zilizofanya hivyo. Kuna mahela kibao tu yaliokuja Africa kutoka taasisi za fedha za kidunia na vilevile wafadhili wa vita baridi.

Uchumi wowote uliokuwa kwa kutegemea misingi ya ndani ya nchi, ukipata matatizo mara nyingi unaji-sahihisha ukipata matatizo fulani.

Lakini uchumi uliokuwa kwa kutegemea streoids (misaada) kutoka nje una matatizo yake.
 
Mimi nimemwelewa Jokakuu. Anachozungumzia ni responsibility na accountability. Mtu kama umeharibu, achia ngazi na kubali kuwa umeharibu na unaondoka na sio uachie ngazi kwa sababu umekaa muda mrefu. Kila mara watu mnaitisha baadhi ya viongozi wajiuzulu kwa sababu ya kushindwa kufanya kitu/ kazi fulani sasa kwa nini Nyerere awe exception.
 
Mwanakijiji,

..labda kwa standards zako Mwalimu alikuwa straight forward ktk kukiri kushindwa kwa utawala wake.

..hotuba ya mei mosi mbeya, miaka 10 tangu aondoke madarakani, niliisikiliza na haikuniridhisha ktk suala zima la Mwalimu kukiri kwamba aliharibu uchumi wa nchi.

..hiyo ya Magereza nakiri kwamba sijawahi kuisikia. unaweza kutuletea hapa jamii forums??

NB:

..Mwalimu ktk moja ya hotuba zake za 'kuaga' alisema: "...si kama nakwepa kutumwa, ila ninaomba tupate mwingine..." is that being straight forward kwa mtu aliyeharibu uchumi??

..halafu uliona wapi mtu aliyeharibu kazi anazunguka ndani na nje 'kuaga'?

..nadhani hata wa-Tanzania wenyewe we havent come to terms na matatizo yetu.
 
I tried and I couldn't find any......can you help?

will do that when i get the time.

BTW,Mwalimu Nyerere Foundation wanakaribia kufungua library yake pale kwenye ofisi zao.They have over 2000 speeches written and taped,and some videos as well.
 
Hotuba yoyote ambayo ingetolewa wakati mwalimu alipokuwa hai ingekuwa ya kujikomba tu.Nyerere alikuwa dikteta aliyeogopwa na kila mtu hata baada ya kung'atuka hakutaka kupumzika.Ile tabia ya kuwa na power hakuiacha kamwe,bado alijiona yeye ni yeye tu.

1984 watanzania wengi walikuwa maskini wakitembea karibu na uchi.Kila kitu cha matumizi ya kawaida katika maisha,kuanzia chakula hadi mavazi vilikuwa ni bidhaa adimu.

Ukitaka kumjua Nyrere alikuwa mtu wa aina gani usiende mbali chunguza hali za wanae.Kama alishindwa kuwalea hao angeweza vipi kutawala nchi?

Makongoro,Madaraka na wengineo hakuna hata mmoja aliyeweza kupata elimu ya maana.

Kama unashindwa kulea familia nchi utaiweza?Msinifanye nikalia kwa uchungu maana enzi zile zilikuwa za ukiritimba wa kila kitu.Bunge lilikuwa rubber stamp,Vyama vingi vilipigwa marufuku,hakuna magazeti ila ya chama na serikali tu na mambo mengi ya kidikteta.

Nawaonea wivu vijana wetu wa sasa kwani wanakuwa na fikra huru,wanaweza kujadili kwa wazi bila hfu ya kuswekwa ndani.

Wanaweza kupiga kelele hadi kiongozi akasikia lakini yule mzee alikuwa Mr.Haambiliki.

Kila jina lake linapotajwa linanikumbusha uoza wa siasa za kishenzi za kuwazuia watu kusafiri,kuwawekea vizuizi vya barabarani wasiuze mahindi yao..n.k.
Nakumbuka uoza wa kununua bidhaa kwa kuomba vibali iwe ni betri za radio au gari.

Nyinyi vijana mnaosoma historia iliyoandikwa chini ya mfumo na sera zake hamuwezi kumjua vizuri Nyerere.Waulizeni kina Zacharia Hans na wenzake ni kitu gani kilichowafanya watake kumpindua huyu mchonga meno.
 
Madaraka anayo MA. Anna Nyerere anayo MA. John Nyerere na Andrew Nyerere walikuwa pilots katika JWTZ. Kwa hiyo usizuge watu hapa.
 
will do that when i get the time.

BTW,Mwalimu Nyerere Foundation wanakaribia kufungua library yake pale kwenye ofisi zao.They have over 2000 speeches written and taped,and some videos as well.

Kwanini wasipeleke kwenye makumbusho ya taifa?
 
..Mwalimu hakuwa straight forward ktk kukiri makosa na matatizo ya utawala wake.

Joka kuu, ona J.K. Nyerere alichosema:

"If I had my time over again, I would do it much the same way,"

"What would I have changed if I had my time over again?...Not much."

"They keep saying you've failed. But what's wrong with urging people to pull together? Did Christianity fail because the world isn't all Christian?"

Published October 24, 1990, New York Times, By PAUL LEWIS

Nitajie nani aliwekwa kizuizini kwa kujadiliana issues enzi za Mwalimu.

Jasusi,

Mwinyijuma Othuman Upindo, A.F. Mkenda , Wolfagang Dourado, Ndugu Kaneno, Eli Anangisye, Happy George Maeda, Ndugu Bakampenja, Melek Mzirai Kangero, Ndugu Choga, K.L. Bazigiza….(Mkenda na Bazigiza ni wanafunzi waliotofautiana na Chama cha Nyerere kuhusu maswala ya vijana!)

Nimeacha majina mengine makubwa makubwa mengi tu ya watu ambao walikamatwa na political police wa Nyerere ambayo nadhani unayajua vizuri tu.
 
Katika hilo kundi mwondoe Eli Anangisye. Huyu kesi yake ilikuwa tofauti. Alishiriki katika njama za Kambona kutaka kupindua serikali. Choga naye. Dourado kesi yake siijui. Mimi si mfuatiliaji sana wa mambo ya Zanzibar.
Lakini kitu ambacho nataka kusema ni lazima tuelewe hali iliyokuwepo Afrika kote wakati huo. Nkrumah alipinduliwa na jeshi aliloliamini. Ahmed Ben Bella alipinduliwa na right-hand man wake. Nyerere alishtuka pale balozi wa Algeria Dar-es-Salaam aliporudi nyumbani kuwa Foreign Minister katika serikali iliyompindua Ben Bella. Gamal Nasser alikuwa ameshamalizwa na njama za Marekani na Mayahudi. Kambona alijaribu mara mbili kupindua serikali. Nakumbuka katika interview na Peter Enahoro mwaka 1971 kuadhimisha miaka kumi ya uhuru Mwalimu aliulizwa ataje baadhi ya mafanikio yake akajibu "we have survived." The fact that survival was measured as success says a million to me. Kwa hiyo kama kuwatia kizuizini kulisadia survival ya serikali so be it.
 
Regardless of whether it was warranted or not?
 
...Grandioso!!!!
 
Mc Palin,
That is debatable. Whether it was warranted. Sidhani watu walikamatwa kiholela tu mitaani na kuswekwa lupango bila hatia.

Wewe umesema kama alifanya hivyo ili ku survive ni sawa tu. Kwa hiyo ni sawa kuweka watu vizuizini hata kama hakuna ushahidi ili u-survive?
 
Wewe umesema kama alifanya hivyo ili ku survive ni sawa tu. Kwa hiyo ni sawa kuweka watu vizuizini hata kama hakuna ushahidi ili u-survive?

Hapana. Read again my following sentence. Siamini kuwa watu waliwekwa kizuizini hivi hivi tu bila kuwepo ushahidi.
 
Jasusi and Inc.

Kwa data zako na za wenzako mnaomuunga mkono sana Nyerere, inaonyesha mmekula chumvi nyingi.

Swali langu ni kuwa Nyerere aling'atuka na kurudi kijiji Butiama, mtarudi lini vijiji hili mfuate nyayo zake?

Wote mnaomsifia Nyerere hapa, ni wapigaji kelele na porojo tu. Sioni mfano wowote unaoonyesha kuwa kuna wanaomfuata.
 
Jasusi,

..inaelekea wewe umevaa 'miwani ya mbao,' na 'kumimina zege 'kwenye masikio.

..kuna postings ambazo zinawataja wabunge waliochukuliwa hatua na Nyerere/TANU kwa kuikosoa serikali bungeni.

..hatua hizo ilikuwa ni pamoja na kufukuzwa ktk chama na wengine kuwekwa kizuizini.

..wakati huo kulikuwa hakuna kinga kwa wabunge kwa yale watakayoongea ndani ya bunge.

..mimi naamini Nyerere alikuwa akiipenda hii sheria ya kusweka watu kizuizini. nasema hivyo kwa sababu aliitumia kwa wapinzani wake. hii ni tofauti na mtazamo wake kuhusu sheria ya kunyonga, ambayo tunaelewa kabisa hakuipenda na aliitumia kwa nadra kabisa kabisa.

NB:

..halafu napenda niulize kuhusu suala la Sheikh Khassim Hanga. alifariki katika mazingira gani? alifariki mikononi mwa serikali ya Karume, au serikali ya Nyerere?

..inasemekana mara ya mwisho Hanga kuonekana hadharani ilikuwa ni ktk mkutano wa hadhara ambapo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alimsema vibaya.
jokaKuu,
Hanga alifariki mikononi mwa serikali ya Karume. Nyerere ni kweli alimsetiri Hanga Dar-es-Salaam, lakini katika kesi ya uhaini wa Kambona Hanga alikuwa mshirika wa Kambona. Karume akamwambia Nyerere nilikwambia huyo mtu wako hana akili "not exact quotes" na kwa kweli Nyerere alimwita Hanga mjinga au mpumbavu kwenye mkutano wa hadhara na kumrejesha Zanzibar. Sina miwani ya mbao ndugu yangu. Maybe I was closer to some events than you think.
 
Back
Top Bottom