Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

do we need a new synthesis of Ujamaa theory in light of what is going on today in the economic world?

Definately...

What is sad, is that the powerful always dictate terms. What the US is doing now, is trying to sort out the most powerful using socialist model BUT for the powerful. Sijasoma latest what is on the detail with the Wall Street "Deal", but no one doubts what will be the case with the most vulnerables.

Kwa Tanzania, I used to complain why we left Ujamaa kwenye katiba ya nchi. I realized sooner later that ni sawa kabisa. Lazima nchi iwe na direction, and kwa nchi yawatu wanyonge au less powerful, the power is unity and Ujamaa provides excellent vehicle kwa maendeleo, if it is organized well and allowed to be truely people's Ujamaa from grassroot up, and not elite Ujamaa.
 
Kuhani,
Nimetaka yote niliyoandika awali na majibu yako vionekana hapa. 'naivete' yangu imefanya niweke wino mwekundu kwa yale uliyosema na yangu wino mweusi, kama kutakuwa na mparaganyiko basi wasomaji waniwie radhi! Technolojia hizi tumejifunzia jikoni.

Quote:
Originally Posted by Bibi Ntilie

Mwalimu alikuwa na dhamira ya kuacha uongozi tangu miaka ya ’70 zaidi ya miaka 10 kabla ya kung’atuka mwaka 1985. Aliamini kwa dhati kabisa kwamba walikuwepo watu ambao wametajwa humu na baadhi ya wachangiaji, watu kama Marehemu Sokoine, Marehemu Mzee Bomani, Mzee Malecela, Mzee Job Lusinde, Dr. Salim Ahmed Salim, Judge Sinde Warioba, Mzee Cleopa Msuya na wengine ambao hadi leo hii bado...

Madai kama hayo, Bibi Ntilie, huwezi kuyasema kijuu juu hivyo bila substantiation. Katika chaguzi za Raisi, Nyerere alikuwa anashindana na kiboxi kitupu, hakuwahi hata kushindana na mtu. Ukisema alitaka kutoka miaka ya '70, ni jambo la ajabu kutamka. Ni kitu ambacho hakijawahi kusikika, ni bizarre!

Kuhani ‘Mkuu’,
Ni-substantiate nini? Kwamba waliotajwa si wazalendo wa kweli au Mwalimu alikuwa hashindani na ki-box kitupu!? Ni kazi yako wewe ku-substantiate kwa kutoa maelezo ya kina yatakayodhihirisha kukanusha niliyosema. Kuhusu Mwalimu kutaka kung’atuka, kwamba ‘ni kitu ambacho hakijawahi kusikika’ nayo ni bizarre pia. Kwa mtu ambaye anafuatilia kwa kina historia ya uongozi wa Mwalimu hangeweza kusema kwamba statement yangu ni bizarre. Ushauri wa bure: jaribu kufuatilia kwa kina mambo yanayohusu viongozi waasisi wa nchi si kuchimbua ya akina Carl Max na akina Che Gueverra pekee.

Quote:
...hivi wakati huo kabla ama baada ya Uhuru, wananchi wangapi walikuwa na uelewa kisiasa wa kuweza kuchangia mawazo kikamilifu katika kutunga kitu kama Azimio la Arusha ama mbinu za utekelezaji wake? Wananchi waliokuwa na uelewa wa hata namna masuala ya utawala ama mchezo wa siasa ulivyo walikuwa ni wachache mno.

Hao wachache hao waliokuwepo hao wengine tunauliza kwa nini hao wachache walifungwa, kufukuzwa kazi, kufungiwa vijijini au kwenye vyumba vya mateso vya giza?

Kuhani, katika harakati za kutafuta maendeleo ya nchi changa baada ya Uhuru kwa sababu za ‘ubinafsi’ walikuwepo wapinga maendeleo, wazuia maendeleo na juu hao walizuka wahaini.

Quote:
...Ndio hao walioibuka na kaulimbiu ya “Zidumu Fikra…” Hata humu tukianza kuimba “Zidumu Fikra za Mchungaji Kishoka” sidhani kwamba atatuambia ‘ah sitaki jamani’, tumeamua wenyewe hakutuomba wala kutulazimisha! Hata hivyo, Mwalimu alikuwa mwenye busara aliwahi kuikana kaulimbiu hiyo.

J.K. Nyerere angekataa kuimbiwa nyimbo za kusujudu watu wangeacha kumsujudia. Mkapa alikataa kuitwa "Mtukufu." Na watu wakakoma! Anashindwa hata na Mkapa? Hapo J.K. Nyerere amekuwa kama alifurahia kuwa a vain demigod, kimungu mtu!

Kweli hujui historia!
Wakati nchi inapata Uhuru, mie Bibi Ntilie nilikuwa darasa la 8. Lakini, kutokana na niliyoyasikia na kusoma kuhusu Mwalimu naweza kuandika yafuatayo: “Walikuwepo baadhi ya viongozi; Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, pamoja na watumishi walioteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini ambao walianza kutaka kuiga maisha ya Wakoloni. Hawakuelewa wajibu wao katika suala zima la kujenga nchi kwa misingi ya haki, usawa na kuheshimiana. Zilianza kujitokeza dalili za kuibuka tabaka la ‘Wazungu weusi’ waliojiona bora kuliko wananchi wengine, kutokana na nyadhifa zao.

Mwalimu alibaini kwamba hali hiyo isipodhibitiwa ingezorotesha sana juhudi za kujenga jamii yenye usawa na heshima kwa kila mtu. Halikadhalika, hali hiyo ilikuwa ikiharibu heshima ya Serikali mpya ya Jamhuri ya Tanganyika machoni pa Wakoloni ambao Mwalimu alikuwa amewaeleza wazi kwamba Waafrika wanaweza kujitawala wenyewe kwa misingi ya haki na usawa.

Mwalimu alichukua hatua ya kuwaandikia barua Mawaziri na viongozi wa ngazi zote Serikalini akiwaambia:

“....Ipo hali iliyojitokeza Serikalini ya kuchanganya hadhi na mbwembwe. Hali hii inabidi idhibitiwe vinginevyo itaharibu hadhi na heshima ya Serikali ya Jamhuri..... Upo mtindo ulioenea kwamba Waziri Mkuu, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na kadhalika wakifika kwenye mkusanyiko wowote wa watu nchini basi inabidi wimbo wa taifa uimbwe. Hiyo ni kuuvunjia heshima wimbo wa Taifa na kuufanya kama wimbo maarufu wa muziki!.... Matokeo ya mtindo huo, hadhi na heshima ya wimbo wa taifa hutoweka na wananchi huamua kuupuza na kutotoa heshima inayostahili kwa wimbo wa taifa lao....”

Mwisho wa barua ile aliwaasa viongozi kwa kuwaambia:

“Tuache mbwembe na tudharau mbwembe. Hadhi na heshima havihitaji mbwembwe... Ni jukumu letu kusitisha tabia hiyo....”

Kufuatia barua hiyo, Serikali ilichukua hatua mbali mbali za kujaribu kudhibiti hali iliyokuwa imejitokeza ya viongozi kutaka kuiga Uzungu na kuishi maisha ya kifahari. Serikali iliamuliwa Mawaziri wote watumie magari aina ya Pijo (Peugeot) ama Landrover badala ya kutumia Benz. Magari aina ya Benzi yalikuwa ghali na yalikuwa yakitumia fedha nyingi za kigeni kuyanunua. Alisitisha utumiaji wa fedha za kigeni kununulia mambo ya anasa. Alitaka fedha ambazo zingelitumika kuagiza mambo ya anasa ambayo yangeweza kununuliwa na wachache, zilielekezwa kwenye kuendesha shughuli za maendeleo ya walio wengi. Aliona haikuwa haki kundi dogo la viongozi liachiwe kufuja mali ya Taifa kwa kuishi kwa anasa wakati wananchi wengine wakiishi maisha duni.

Pamoja na hatua hizo Mwalimu aliamua kwa makusudi kupunguza mshahara wake, ilibidi Mawaziri nao wakubali kupunguza yao. Alijaribu kukataa ulinzi aliokuwa akipewa wa kumlinda. Lakini, hilo halikuwezekana. Ndugu Job Lusinde aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani aliyekuwa akishughulikia masuala ya Usalama wa Taifa wakati huo, alimwambia Mwalimu alipaswa kukubali kulindwa kwa sababu, aliyekuwa akilindwa ni Rais wa nchi sio ‘Julius’!

Kuzidi kudhihirisha kwamba hakupenda tabia za mbwembwe na kutukuzwa, Mwalimu Nyerere alisitisha mambo mengi aliyoyaona hayakuwa na ulazima. Mojawapo lilikuwa ni kukataa kuitwa ‘Mtukufu Rais.’ Aliamini, heshima za aina hiyo hazikuwa na maana sana kwake. Kurahisisha mambo aliwaambia wananchi:

“...Niiteni ‘Mwalimu Nyerere’, inatosha. Maana hiyo ndiyo kazi yangu niliyoisomea na ndicho cheo changu cha kudumu...!”

Bwana Kuhani, mwenzio hizo quotes nimezipata kutoka kwenye kitabu kilichoandikwa na William Edget Smith na kutafsiriwa kwa Kiswahili na Mzee Paul Sozigwa mwaka 1977. Utapata fursa nzuri ya kumfahamu zaidi Mwalimu kupitia kitabu hicho. Smith alifanya utafiti mzuri kabisa kuhusu Mwalimu, bahati nzuri kwake, aliongea ana kwa ana na Mwalimu mwenyewe. Kwa hiyo challenge kwako ni kufanya utafiti kabla ya kukurupuka na maneno ya 'kusikia' kwamba Mkapa alikataa kuitwa Mtukufu. Alikuwa anarudia tu yaliyokwishwa asisiwa na Mwalimu!

Quote:
Pengine Mwalimu alifanya makosa katika baadhi ya hatua alizochukua.

Hamna "pengine" hapo. Hakuna anaejadili kama Mwalimu alifanya makosa au la. Hilo halina mjadala. Ndio hayo makosa na mazuri tunayoyachambua

Sawa.

Quote:
Lakini, katika kuwashughulikia hao wanaodaiwa kufurukuta kuhoji, kama aliwapeleka ama aliwashitaki kwenye vikao vya Chama ikadhihirika ndani ya kikao kwamba wana makosa, wakahukumiwa na vikao hivyo, kosa la Mwalimu ni lipi?

Kosa lake ni kwamba vyombo hivi vya kushitaki watu vilikuwa kama institution zinazoitwa Mahakama za Kangaroo: Jaji, wakili, prosecutor, wazee wa baraza, court reporters na polisi wanaomlinda Jaji na mahakama wote lao moja.Yani, mshitaki, huyu J.K. Nyerere, amesha waweka waamuzi, wajumbe wa TANU, mfukoni. Wote wanamsikiliza yeye, vinginevyo waweza fungwa. Ndio hali ya hewa ilivyokuwa wakati ule era ya kuwekwa vizuizini kuzuiza hatari kutumia Sheria ya Vizuizi vya Mazuizi (Preventive Dentention Act). Ni kama unduli vile.

Kuhani, usisahau kwamba tunaenda na wakati na pia hatua kwa hatua. Mababu zetu walikuwa na ‘mahakama’ zao chini ya mibuyu. Wajerumani na Waingereza walipotutawala walijenga vyumba vilivyoitwa mahakama lakini havikutumika ipasavyo. Wananchi waliteswa wakapigwa mijeledi nk. wakati mwingine bila kosa. Wapo waliopewa adhabu ya kuwabeba wazungu kwenye machela. Unataka tuamini kuwa Mwalimu aliwaelimisha ili awaweke mfukoni majaji, mawakili etc. wamsikilize yeye waweke watu vizuizini? You must be joking!

Quote:
Niliwahi kusikia kwamba Jenerali Ulimwengu alikuwa mmoja wa Wabunge G… waliokuwa wanataka Tanganyika wakati ule. Inasemekana walikwenda Msasani kwa Mwalimu kuelezea greaviences zao zilizowafanya watake/kudai Tanganyika yao! Je, katika mkutano wao na Mwalimu hawakuwa na majadiliano naye, aliwaburuza tu wasomi wazima? Nasikia aliwashinda kwa kuwaambia jambo jepesi sana, Jenerali anaweza kutuambia kama ni kweli...

Unajenga hoja yako ya msingi based on "kusemekana." Hilo ni tatizo hapo. Argument yako ya msingi ni kwamba J.K. Nyerere alikuwa ana accomodate mawazo ya wengine. Sasa ukitoa mifano ya hilo dai, huwezi kutumia hadithi za kusikia. Historia ya Tanzania ilivyopotoshwa ni kitu kinachotutatiza wengine, na sasa ukijenga hoja ya nini kilichojiri halafu unarudi huko huko kwenye kusikia unakuwa haujasema lolote la maana.

Kuhani, wataka kunilazimisha niseme ambayo sikusikia ama hayakusemwa? Mie sikuwa mmoja wa G.. Ndio maana nimeomba iwapo Jenerali (naongeza) na wengine waliokuwa kwenye kundi hilo kama watapenda, watueleze yaliyojiri.

Quote:
Watu ambao walidhani wanaweza kumshinda Mwalimu kwa hoja, walipoona kila wakijaribu anawaweka mahali wakajiona hoja zao hazina uzito, ndio hao wanaoeneza uvumi kwamba Mwalimu alikuwa akitoa laana za kisiasa! Walikuwa wakijimaliza wenyewe. Sisi hao hao tunaodai kwamba Mwalimu alikuwa akimaliza watu kisiasa, wakati mwingine tunamsifu kwamba alikuwa anaona mbali. Ukweli ndio huo!

Huo "ukweli" wako una mushkeli. Hiki cha Nyerere kuona mbali umekisema mara mbili humu. J.K. Nyerere aliona mbali kivipi?. Alivyoving'ang'ania toka mwanzo ndio vili feli baadae, kama unakumbuka yaliyojiri kuhusu fikra zake. Ni wakina Kambona ndio walikuwa wanamwambia Mzee hizi politics na policies zako zitatupoteza, zitatulostisha. Hakusikia. Kutokusikia sio baya sana. Uhasidi, kibaya zaidi, ni kuwafukuzisha nchini, kuwafungia kijijini (S. Mwijage, Balozi Tumbo na wengine wengi tu) au kuwafunga bila mashitaka (kina Eli Anangisye, Happy Maeda na wengine wengi tu). Wengine walikufa baada ya kuwekwa kwenye vyumba vya giza bila sababu zilizopitishwa mahakamani. Hasidi hana sababu. Hayawi hayawi yakawa: Yaliyohofiwa na kina Eli, Oscar, Kassanga, Kassela, Titi, na wengine wengi yakawa. Ufukara ukatujia. Kwa hiyo ukisema J.K. Nyerere alikuwa anaona mbali unakuwa....sijui nisemeje!

Leo tuko awamu ya nne ufukara ndio unazidi. Je, awamu ya pili, tatu,i na miaka mitatu ya awamu ya nne zimeshindwaje kuja na mu-arobaini wa ufukara?

Nikikwambia utasema ‘nimesikia’. Soma kitabu nilichokitaja huko juu. Mzungu huyo anaelezea yaliyotokea kuhusu hao uliowataja. Bila shaka waliokuwa wakimshauri Mwalimu vinginevyo walikuwa wakitaka politics za kibepari. Kenya hawakufuata politics za Ujamaa, leo hii hali ya wananchi walio wengi nchini Kenya ina tofauti gani na ya Watanzania walio wengi? Waliotiwa kizuizini na waliokimbia nchi 'nasikia' walikuwa wanataka kumpindua Mwalimu!

Quote:
Tukubaliane kwamba Mwalimu alikuwa binadamu na aliweza kukosea kama binadamu mwingine yeyote.

Kwamba J.K. Nyerere alikuwa binadamu halina mjadala. Hakuna aliyesema kuna binadamu hakosei. Tunakosea na kukosoana. Na ndio maana uko hapa unamtetea. Ingekuwa binadamu hakosolewi kwa sababu tu ni binadamu basi kusingekuwa kuna kitu kama vile kufukuzwa mtu kazi. Si binadamu bwana? Pointi yangu hapa, Bibi Ntilie, ni kwamba ni sawa kujadili makosa ya binadamu!

Mmmh, sijakuelewa.

Quote:
Lakini, mengi aliyobuni Mwalimu, akafanya na kuyasimamia yalikuwa na mantiki sana na kwa kuwa alikuwa anaelewa kwamba analolisimamia na kulivalia njuga lilikuwa na manufaa kwa Taifa alilokuwa analiongoza, hoja za kumtaka awaze vinginevyo alikuwa hazikubali kwa sababu alikuwa anaona mbali na alikuwa anajua analofanya ni kwa nia njema na lengo zuri.

Unajua unapotoa kauli za juu juu kama hivyo kusifia vitu ambavyo viko kwenye utata na ubishani mkali kuna wengine tunakuona kama unachukulia mambo kirahisi rahisi, na kutokujali jali, unaonyesha naivete. Kuna tatizo hapo kudhani kwamba watu tutakusikiliza kumpamba J.K. Nyerere bila vidhibiti. Yani unakuwa mbali sana na watu walipofika katika mijadala kama hii. Kwa mfano, ukimtetea J.K. Nyerere kwa sababu alikuwa ana "nia njema na lengo zuri" ina maana wewe katika dunia yako mtu asingelaumiwa kwa kukosea, kama vile kazini tuseme, iwapo tu alikuwa ana nia nzuri. Hiyo mantiki sio wengi wataikubali.

Is it a big deal? Hii ni discussion forum, hawakusema watakaoingia humu sharti wawe na kiwango fulani cha elimu. Mie naamini uhuru wa kutoa mawazo ni wa watu wote hata sie tunaokosha masufuria. Inakuwaje ‘naivete’ yangu inakupa shida hata unapoteza muda wako kujibu kila kipengele?

Quote:
...Maandishi kama haya hayamtendei haki Mwalimu. Mara ngapi Mwalimu alikuwa akienda Chuo Kikuu kujadiliana na wasomi kuhusu mustakabali wa nchi?

Alienda kujadili mara sifuri. J.K. Nyerere alikuwa akienda Chuo Kikuu kugombeza watu tu, kama sio kuwachapa wakina marehemu Mwabulambo viboko matakoni! Hakwenda "kujadiliana na wasomi kuhusu mustakabali wa nchi"!

Naomba nirudie yaleyale usiyoyataka ‘nasikia’ Mwabulambo alichapwa kwa ‘utovu wa nidhamu’….. walipinga kwenda JKT na waliibuka na mabango yameandikwa “Afadhali wakati wa Mkoloni” yaliyomuudhi sana ‘Mwalimu’ wao aliyekuwa akijaribu kuwafundisha nchi HURU inavyopaswa kujitegemea. Wakoloni hawakuwahi kuchukua hatua za makusudi za kuwaelimisha Watanganyika iweje wao waseme afadhali wakati wa Mkoloni? Hata wewe Kuhani ungelikasirika na kuwachapa viboko! Kumbuka, wakati huo mwanafunzi kuchapwa viboko ilikuwa ruksa. Hata Wakoloni mentor wetu wa ‘haki za binadamu’ walitumia njia hiyo hiyo kuwafunza watu wazima nidhamu na si wanafunzi peke yao!

Quote:
Mlango wa Msasani ulikuwa wazi wakati wote lakini watu kwa woga wao wakawa hawathubutu kuomba kuonana na Mwalimu ili watoe mawazo yao. Wengine wakawa wanasingizia kwamba Butiku alikuwa akiwazuia kumuona Mwalimu! Wachache waliokuwa wakijiamini,

Maofisa wa serikali hawatakiwi kwenda nyumbani kwa Rais kujikomba komba undugu. Wanaongea rasmi bungeni, cabinet meetings, vikao vya chama, na kupitia official and expert recommendation kwenye makaratasi. Sio "kuomba kuonana Msasani... kusikilizwa kwa makini." Mambo ya Serikali hayaendeshwi hivyo.

Nadhani hapa nawe unadhihirisha naivety yako juu ya taratibu za utendaji katika ngazi za juu za Rais na Mawaziri. Maofisa wa Serikali ni watu wa ngazi ya chini kuweza kwenda moja kwa moja kwa Rais, labda Rais aamue kuwaita kwa sababu maalum na kwa kupitia kwa Waziri muhusika wa suala lenyewe. Mfano hai, Rais Kikwete akitaka kubadilisha Baraza la Mawaziri je atapeleka suala hilo Bungeni, kwenye Cabinet meeting, vikao vya Chama ama kutafuta official na expert recommendation kwenye makaratasi? Waziri Mkuu Pinda akiona kuna tatizo la mwenendo wa Waziri ama kiongozi yeyote mteuliwa na Rais atatumia makaratasi na vikao ulivyotaja? Waziri Mkulo akiwa Bungeni, alipotatizwa na suala la EPA alilipeleka kwenye vikao ama aliomba kuonana na Rais washauriane maana lilikuwa ni suala zito?

Quote:
Mwalimu alikuwa akiwasikiliza kwa makini sana. Mwalimu alikuwa akiwasikiliza wazee kwa vijana, hata wahudumu, wapishi, madobi, madreva n.k. na kufanyia kazi aliyoyapata kutoka kwao, sembuse viongozi wenziwe?

Madobi na wapishi! Hii pointi ni dhaifu sana kwa sababu unajipiga risasi mguuni kwa kuonyesha kwamba Nyerere alikuwa comfortable kujadili siasa na wahudumu na madereva. J.K. Nyerere mwenyewe angesikia unasema hivyo angekuruka. Tulitaka ajadili nyeti za Taifa na wabunge na viongozi wa mawizara na wakuu wa mashirika na maofisa wengine wa Chama na Serikali. Sio awa convince wapiga pasi au gardeners wa nyumbani kwake, na wapishi, Bibi Ntilie.

Kuhani, mimi ni naïve lakini wewe mwenzangu ni shallow minded. Kiongozi asiyewasikiliza wananchi hata wawe wadogo kiasi gani si kiongozi! Utajadili vipi nyeti za Taifa wakati majority wanaoliunda taifa hilo ndio hao watu wadogo? Kuna nyeti gani zisizohusu mustakabali wa wananchi including watu wadogo?

Quote:
Hivi ni kweli Mwalimu alikuwa akilizuia Bunge la chama kimoja kujadiliana juuya namna ya kuboresha ama kushughulikia matatizo ya ki-sera zilizolenga kumkomboa Mtanzania mpaka sera hizo zinakufa etc etc?

Alikuwa anazuia wanaopinga politics na policies zake Bungeni. Kuna vidhibiti vya kiutafiti vya wasomi wengine, sio makala ya Ulimwengu tu, vimewekwa humu.

Utafiti uliokamilika ni ule wa kuketi na muhusika anayefanyiwa utafiti ili naye aeleze juu ya yale yanayofanyiwa utafiti ama wale waliokuwa wakizungumza naye kwa karibu zaidi kujua mawazo yake. Utafiti mwingine unatawaliwa zaidi na hisia na mawazo ya mtafiti na watu wengine kuliko ukweli wenyewe.

Quote:
Viongozi wa mashirika na wananchi waliopewa na Serikali majukumu ya kuuza “nyama na chumvi” wangelikuwa ni watendaji wazalendo wenye uchungu wa dhati ya maendeleo ya nchi yao, mashirika yote yakaendeshwa kwa ufanisi uliodhamiriwa, leo hii Tanzania tungelikuwa wapi? Mameneja wangapi walijenga nyumba na kufuja fedha za mashirika, kufanya ubadhilifu wa kila aina kwa kutumia nafasi za uongozi walizopewa?

Sasa hapa, Bibi Ntilie, unakuwa unahamisha lawama kwenda kwa mafisadi wa Nyerere peke yao. Ni kweli kwamba viongozi walinuka rushwa wakati wa Nyerere administration, na mashirika hayakuendeshwa kwa ufanisi chini ya Nyerere administration, lakini hili halimaanishi kosa si la Nyerere pia. Makosa ni ya wote, lakini tunajadili sera na fikra za Nyerere hapa. Ni yeye ndie alikuwa dereva wa mashua. Yeye ndio alikuwa kiongozi. Sasa dereva wa mashua kwa nini wataka akae nyuma ?

Kuhani, Nadhani mie na wewe tunakubaliana jambo moja la msingi. Nyerere alikuwa binadamu. Kosa moja alilofanya ni kutotia ndani/kizuizini wale wote waliofilisi Mashirika. Angeweza kutumia Sheria ya Uhujumu Uchumi. Kosa la Mwalimu alikuwa akiwaangalia nyani usoni na kuwahurumia!

Quote:
Kama Wachina wameweza kujipatia maendeleo ya kiuchumi haraka, sisi ambao tunaambiwa kiongozi wetu alikuwa akiwaiga wao na kusikiliza kila alilosema, ilikuwaje na tulishindwaje kuwa kama Wachina?

Wachina, Bibi Ntilie, hawakupata maendeleo kwa sababu ya vijiji vya ujamaa. Tena ni baada ya kuanza ku reverse mifumo inayofanana na ujamaa, hususan mashamba ya vijiji vya kisoshalisti, miaka ya mwisho ya '70 ndio walianza kuona mafanikio. Na siku hizi Uchina imeanza kufanana na ubepari katika mgawanyo wa mapato.

Kuhani, kuna watu wamesema Mwalimu alikuwa influenced na siasa za Wachina na wakati huo Wachina walikuwa Wajamaa. Na kama tungeliwaiga Wachina katika hayo unayosema walifanya bila shaka tungelikuwa mbali kama wao, au sio?

Graph mie wa jikoni sielewi. Ninachoelewa ni kwamba mwaka jana nilikuwa nanunua mchele safi unaonukia wa Kyela kwa sh. 400 kilo. Mwaka huu mchele huo naununua kwa kilo Sh. 1,200. Akina Bibi Ntilie hatushoni tena nguo mpya tunavaa mitumba kafa ulaya. Lakini, jinsi mambo yalivyobadilika, kuna mitumba inatoka kwa Watanzania wenzetu wanaoishi kwa kuangalia fashion toka Ulaya ambazo ni nguo zao zikiwa out of fashion tunauziwa kama mitumba!

Kwa hiyo, mengi ya unayoyadai kuhusu J.K. Nyerere yana mapungufu makubwa, halafu kinachosikitisha, na wakati mwingine kughafirisha, ni kwamba umeyachukulia kijuu juu tu. Na katika mkanganyiko wa masikitiko na maghafirisho hayo unajikuta mtu unapoteza civility na kujibu dismissively, kama pale awali, na nasema tena, unisale kwa hilo.

Civility na naivety hapa si pahala pake ni majadiliano tu.

Zidumu Fikra za Jamiiforums!
 
Hapo mkuu haijakaa sawa, the ishu hapa sio kizazi kizima please, the ishu inapaswa kua mafanikio na mapungufu ya Mwalimu, as a leader,

Ninasema inapaswa kwa sababu so far ni mapungufu tu yanayojadiliwa, mkuu Zakumi ni kweli kwamba hakukuwa na hta moja zuri la Mwalimu unaloliona leo? I mean lets say kwamba your argument ni valid kwamba kizazi cha Mwalimu kilikuwa na papara,

Can you real argue politically tena on a serious note kwamba, kizazi cha Mwalimu, kilikuwa na papara, comparing to kizazi cha kasi mpya na ari mpya?

Halafu ninaamini kuwa nyinyi wote huko on your side ni wasomi, hivi kweli jamani ni lini tuliacha ku-compare na ku-contrast, katika kujaribu ku-present a big picture ya utawala wa kisiasa uliowahi kuwepo kwenye power? Mbona hatulinagnishi kabisa na utawala wa Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete? I mean sasa una present vipi a paper ya critique bila ya kulinganisha?



Field Marshall ES:

Matatizo ya watu wanaompenda Nyerere ni emotion issues. Hata Rev. Kishoka, mwanzilishi wa mada, naona naye yupo kwenye kundi hilo.

Mada hii ni ya Falsafa ya Ujamaa na Nyerere. Katika miaka ya utawala wake, Nyerere alifanya mambo mengi mazuri. Mengi ya hayo mazuri hayana uhusiano wowote na Ujamaa.

Kwa mfano kuwa mstali wa mbele katika ukombozi wa nchi za Kiafrika ni jambo moja kubwa sana. Lakini ule sio Ujamaa.

Kwa mfano Tanzania ilipata matatizo ya njaa mara nyingi wakati wa utawala wake. Na yeye hakuona aibu kutafuta chakula hata katika nchi za kibepari hili wananchi wake wapone njaa. Hicho ni kitendo kizuri lakini huo sio Ujamaa.

Mlolongo wa mambo mazuri unaweza kuendelea lakini hayana uhusiano wowote hule na Ujamaa.

Watanzania ni sawa na wamarekani wengi tunapokuja katika masuala ya kisiasa. Emotions zinatawala na hatuko independent kuchambua mada iliyo mkononi.

Mipango mikubwa ya Ujamaa ilikuwa katika kipindi cha miaka kumi tu 1967 mpaka 1977 tu. Na kwa nchi changa kama Tanzania mipango hiyo kwa pamoja katika kipindi kifupi ilikuwa ni kutwanga maji kwenye kinu.

Simeni hivi kwa sababu naangalia Ujamaa miaka zaidi ya 20 toka kushindwa kwake. Bali, kuna hoja nyingi zilizotolewa wakati hulehule wa mipango hili ambazo zilisema kuwa mambo haya hayawezekani.

Mfano ni Elimu ya UPE. Wataalamu wa mambo ya elimu walipendekeza mpango uwe wa miaka ishirini. Lakini Nyerere alikataa na kusema kuwa mpango huo unaweza kutekelezwa kwa miaka saba tu. Matokeo yake tuna mfumo mzima wa elimu wenye kujali wingi kuliko ubora.
 
1.
Kwa mfano kuwa mstali wa mbele katika ukombozi wa nchi za Kiafrika ni jambo moja kubwa sana. Lakini ule sio Ujamaa.

2.
Kwa mfano Tanzania ilipata matatizo ya njaa mara nyingi wakati wa utawala wake. Na yeye hakuona aibu kutafuta chakula hata katika nchi za kibepari hili wananchi wake wapone njaa. Hicho ni kitendo kizuri lakini huo sio Ujamaa.

Mkuu Zakumi,

With all due respect, yaani haya tu ndio umeyaona yalikuwa ni mazuri ya Mwalimu?

By the way, are this points mazuri ya Mwalimu or what?
 
Taasisi,
Nimefurahi kukuona tena ukumbini!...Karibu mkuu usipotee hivyo.

Wanabodi,
Kuhusiana na Nyerere!.. yangu macho maanake naona tumeshindwa kutenganisha Nyerere na Ujamaa wala Ujamaa toka kwa Nyerere, kisha cha ajabu zaidi tunajiuliza alipata wapi vision hiyo..
Ama kweli kazi ipo.
 
1. Bwana Kuhani, mwenzio hizo quotes nimezipata kutoka kwenye kitabu kilichoandikwa na William Edget Smith na kutafsiriwa kwa Kiswahili na Mzee Paul Sozigwa mwaka 1977. Utapata fursa nzuri ya kumfahamu zaidi Mwalimu kupitia kitabu hicho. Smith alifanya utafiti mzuri kabisa kuhusu Mwalimu, bahati nzuri kwake, aliongea ana kwa ana na Mwalimu mwenyewe. Kwa hiyo challenge kwako ni kufanya utafiti kabla ya kukurupuka na maneno ya 'kusikia' kwamba Mkapa alikataa kuitwa Mtukufu. Alikuwa anarudia tu yaliyokwishwa asisiwa na Mwalimu!

2. Is it a big deal? Hii ni discussion forum, hawakusema watakaoingia humu sharti wawe na kiwango fulani cha elimu. Mie naamini uhuru wa kutoa mawazo ni wa watu wote hata sie tunaokosha masufuria. Inakuwaje ‘naivete’ yangu inakupa shida hata unapoteza muda wako kujibu kila kipengele?

3. Naomba nirudie yaleyale usiyoyataka ‘nasikia’ Mwabulambo alichapwa kwa ‘utovu wa nidhamu’….. walipinga kwenda JKT na waliibuka na mabango yameandikwa “Afadhali wakati wa Mkoloni” yaliyomuudhi sana ‘Mwalimu’ wao aliyekuwa akijaribu kuwafundisha nchi HURU inavyopaswa kujitegemea. Wakoloni hawakuwahi kuchukua hatua za makusudi za kuwaelimisha Watanganyika iweje wao waseme afadhali wakati wa Mkoloni? Hata wewe Kuhani ungelikasirika na kuwachapa viboko! Kumbuka, wakati huo mwanafunzi kuchapwa viboko ilikuwa ruksa. Hata Wakoloni mentor wetu wa ‘haki za binadamu’ walitumia njia hiyo hiyo kuwafunza watu wazima nidhamu na si wanafunzi peke yao!

4. Kuhani, mimi ni naïve lakini wewe mwenzangu ni shallow minded. Kiongozi asiyewasikiliza wananchi hata wawe wadogo kiasi gani si kiongozi! Utajadili vipi nyeti za Taifa wakati majority wanaoliunda taifa hilo ndio hao watu wadogo? Kuna nyeti gani zisizohusu mustakabali wa wananchi including watu wadogo?

5. Kuhani, Nadhani mie na wewe tunakubaliana jambo moja la msingi. Nyerere alikuwa binadamu. Kosa moja alilofanya ni kutotia ndani/kizuizini wale wote waliofilisi Mashirika. Angeweza kutumia Sheria ya Uhujumu Uchumi. Kosa la Mwalimu alikuwa akiwaangalia nyani usoni na kuwahurumia!

6. Civility na naivety hapa si pahala pake ni majadiliano tu.
Zidumu Fikra za Jamiiforums!

Bibi Ntilie,

Heshima mbele na nimekukubali, Salute!
 
Rev,Kishoka unayo haki ya kujiuliza maswali hayo.Na kusema kweli swali unalojiuliza wewe bado lina nisumbua.Lakini katika utafiti wangu nilipata jibu,ambalo hata hivyo bado nalifanyia kazi.Jibu hilo msingi wake ulitokana na maneno ya Nyerere mwenyewe,kwamba 'tusidhani wakoloni wame "give up"ndoto yao ya kututawala, isipokuwa wamekwenda kujipanga,na utumwa wa pili utakuwa mbaya zaidi kuliko wa kwanza."Sasa nilidhani maneno haya yalikuwa na msingi fulani,na nikagundua baadaye kwamba kweli yalikuwa na msingi fulani.Katika utafiti wangu niligundua kwambe yale ya China,Urusi iliyosambaratika,Nazi Germany,Cuba,Angola,Mozambique,Zaire ya Mobutu,Tanzania ya Nyerere na mengine mengi yalikuwa majaribio ya wakubwa 'of a wider agenda.'Nenda TARGETS OF THE ILLUMINATI AND THE COMMITTEE OF 300 uone.Si unajua unapofanya kitu kikubwa lazima ufanye jaribio 'on a smaller scale' ili kuona kama litafanikiwa au la.Kama utasoma 'link' hiyo hapo juu utagundua kwamba wakubwa hawa nia yao ni SERIKALI MOJA YA DUNIAau wakati mwingine wanaita 'New World Order'.Na katika serikali hiyo utawala utakuwa wa ki-imla.Kwa hiyo wanachofanya sasa ni kujaribu kujua 'human behaviour' katika 'scenarios' za aina mbalimbali za ki-imla.Ya Nyerere ilikuwa 'scenario' moja wapo.Kama unataka kujua hao wakubwa nenda www.thewatcherfiles.com/bloodlines/introduction.htm


Waungwana,

Ni nani na ni misingi gani ya utashi iliyojijenga kwenye akili za Julius Kambarage wa Nyerere kutuletea Ujamaa na Kujitegemea na hata Azimio la Arusha?

Wengi tunadhania kuwa ni safari yake ya China 1966. Wengine wanadai ni wale ma-Labor na Socialist wa Uingereza.

Tunajua kuwa tumeangalia sana Ujamaa wetu na Azimio kwa mkao wa Great Leap Forward na Cultural Revolution za China ya Mao na Leninism/Stalinism ya Command Economy, New Economic Policy, Collective farming, na hata matunda ya Bolshevik revolution na sera kama Prodrazvyorstka!

Tukija huku kwetu Afrika tunadai kuna Ujamaa wa Kiafrika, Pan Africanism na mengine mengi.

Lakini bado nafikiri ni kitendawili kwetu kuwa ni ushawishi gani na kwa maono gani Nyerere alikaa chini na kutuletea Ujamaa na Kujitegemea na Azimio la Arusha?

Nikirudia Historia na kuangalia kinachotokea Marekani kiuchumi mwaka huu na nyakati hizi, narudi kujiuliza, falsafa za kiuchumi na kujenga jamii za Marekani zilimkosha Mwalimu Nyerere hasa kuangalia Historia ya great depression?

Je FDR (Franklin Delano Roosevelt) na New Deal yake, Fransiscans/Jesuit philosophy na hata Keynesian Policies zilimbadilisha vipi huyu Mkulu wetu? Planned Economy za National Recovery Administration wakati wa Great Depression ya Marekani na hata Public Works ya Nazi German vilikuwa na nafasi gani?Je alichungulia Front Populaire ya Leon Blum wa Ufaransa na kudonoa mambo kadhaa?

Je kujinasua kwa Marekani baada ya Uhuru wake kutoka Uingereza na kujijenga kama taifa linalojitegemea na si kutegemea falme ya Uingereza na kiburi cha Kimarekani pia kilichangia kumjenga Nyerere kuwa na kiburi cha masikini jeuri?

Twajua Julius Nyerere alikuwa mwana historia mzuri hata ukiangalia na kumpima kutafsiri kwake kwa Julius Kaisari na Mfanyabiashara wa Venisi kazi za William Shakespear zinaonyesha ni influence gani ya fasihi, historia na falsafa alikuwa nayo.


Je Keynes alikuwa na infuence gani kwa Nyerere ambaye alisoma fasihi, historia , uchumi na falsafa alipokuwa Makerere na hata Edinburgh?

What about Wealth of nations, je Nyerere alifanya modification ya principles za Adam Smith akipewa baraka na Labor Party ya Uingereza chini ya ushawishi wa Mama Joy Wickens? Maana ukiangalia Azimio la Arusha, pamoja na kuuzwa kuwa linapiga vita Ubepari, in fact linaruhusu ubepari na mfumo wa Kibepari kwa kiasi fulani hasa linaposema kuwa Viongozi wasiwe na zaidi ya hisa katika makampuni mawili!

Je Plato, Aristotle, Socrates, Ghandi na hata Yesu au Mtume Mohamed wali-play part gani kum-influence Nyerere?

Je alisoma sana Das Kapital na Communist Manifesto ya Karl Marx, akamchanganya Trosky na Friederich Engels?

Je sisi kama Taifa kwa kumfuata Kiongozi wetu tulikuwa ni majaribio (experiment) ambayo mataifa makubwa yalikaa kando kuangalia huyu mwanafalsafa na mwanamapinduzi wa Afrika akikoroga na kuunganisha mifumo ya kiuchumi ya Ubepari, Ukabaila, Ukomunisti na Ujamaa na kuunda Ujamaa wa Kiafrika ambao ulilenga kwenye kujitegema na hata kuzaa Azimio la Arusha kubana tabaka la viongozi na kuhamasisha umiliki wa mali kwa umma na si watu binafsi?

Tumeegemea sana kusema tumeunda Ujamaa wetu kutokana na ziara yake ya China na kuharibika kwa uhusiano wetu na Uingereza kulikotokea kipindi hicho hicho.

Je inawezekana kuwa kiwango kikubwa cha falsafa zake za Ujamaa na Azimio ni mgawanyiko sawa wa influence za magharibi wakati wa depression na mashariki wakati wa uprising na mapinduzi?
 
1.

2.

Mkuu Zakumi,

With all due respect, yaani haya tu ndio umeyaona yalikuwa ni mazuri ya Mwalimu?

By the way, are this points mazuri ya Mwalimu or what?

Mtaacha lini kuwa na emotions. Nilichotoa ni mifano. Na nia kuonyesha mambo mazuri aliyofanya kwa misingi ya kibinadamu na kiutu na ambayo hayausiani na falsafa ya Ujamaa au Azimio la Arusha.


Na kuhusu uzuri wa mifano, usiwe na wasiwasi hiyo ni mifano mizuri sana kuonyesha kuwa alikuwa ni mtu mwenye kujali maisha. Wajamaa wengine kama wale waEthiopia waliachia watu kufa kwa kutotaka kuomba misaada.

Mwishoni naomba mrudi kwenye mada.
 
Field Marshall ES:

Matatizo ya watu wanaompenda Nyerere ni emotion issues. Hata Rev. Kishoka, mwanzilishi wa mada, naona naye yupo kwenye kundi hilo.

Mada hii ni ya Falsafa ya Ujamaa na Nyerere. Katika miaka ya utawala wake, Nyerere alifanya mambo mengi mazuri. Mengi ya hayo mazuri hayana uhusiano wowote na Ujamaa.

Kwa mfano kuwa mstali wa mbele katika ukombozi wa nchi za Kiafrika ni jambo moja kubwa sana. Lakini ule sio Ujamaa.

Kwa mfano Tanzania ilipata matatizo ya njaa mara nyingi wakati wa utawala wake. Na yeye hakuona aibu kutafuta chakula hata katika nchi za kibepari hili wananchi wake wapone njaa. Hicho ni kitendo kizuri lakini huo sio Ujamaa.

Mlolongo wa mambo mazuri unaweza kuendelea lakini hayana uhusiano wowote hule na Ujamaa.

Watanzania ni sawa na wamarekani wengi tunapokuja katika masuala ya kisiasa. Emotions zinatawala na hatuko independent kuchambua mada iliyo mkononi.

Mipango mikubwa ya Ujamaa ilikuwa katika kipindi cha miaka kumi tu 1967 mpaka 1977 tu. Na kwa nchi changa kama Tanzania mipango hiyo kwa pamoja katika kipindi kifupi ilikuwa ni kutwanga maji kwenye kinu.

Simeni hivi kwa sababu naangalia Ujamaa miaka zaidi ya 20 toka kushindwa kwake. Bali, kuna hoja nyingi zilizotolewa wakati hulehule wa mipango hili ambazo zilisema kuwa mambo haya hayawezekani.

Mfano ni Elimu ya UPE. Wataalamu wa mambo ya elimu walipendekeza mpango uwe wa miaka ishirini. Lakini Nyerere alikataa na kusema kuwa mpango huo unaweza kutekelezwa kwa miaka saba tu. Matokeo yake tuna mfumo mzima wa elimu wenye kujali wingi kuliko ubora.

Zakumi,

Sijawahi kusikia hata mara moja duniani kuwa emotional kuhusu kitu ni kosa. Kosa ni pale unaporuhusu emotion zikupofushe na kukosa mwelekeo kabisa kama tulivyoona hapo awali katika mjadala huu.

Mimi nimefaidikia na Ujamaa wa Nyerere na Azimio lake, ndio maana nipo hapa nilipo na nabaini ni vipi Ujamaa na Azimio lingefanikiwa zaidi au mapungufu yake.

Watanzania tunamlaumu sana Nyerere kutokana na Umasikini na kuzorota kwa maendeleo kisa eti ni Siasa za Ujamaa na Kujitegemea na Azimio la Arusha.

Nikijiuliza kilichotokea Marekani leo kwa Uchumi wake kuangamia katika mfumo wa Kibepari hata kurudi kwenye great depression na kilichofanywa na Serikali enzi zile na wanachokifanya sasa najiuliza ni kosa ni sera, itikadi za Kibepari au ni ukosefu wa uongozi mzuri na udhibiti?

Kwenye Azimio la Arusha ambalo ndio blue print ya Taifa baada ya Katiba yetu, tulikiri "ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora"

Kushindwa kwa Tanzania kuwa na maendeleo mazuri na ya uwiano ya kiuchumi hakutokani na Sera, Itikadi, Ujamaa au Azimio la Arusha.

Ni kutokana na uhaba na ufinyu wa vitu hivyo vinne tulivyosema kuwa ni muhimu ili tupate maendeleo.

Labda mtu atasema tungeongeza mtaji, lakini mtaji wetu ni watu na ardhi tuliyonayo.

Tukiangalia maana ya watu, si idadi pekee kutokana na Sensa. Watu ni wale wenye uwezo wa kufanya kazi, wenye upeo wa kuelewa majukumu na kuweza kutumia ubunifu, juhudi na hata maarifa ili kuwa wazalishaji mali.

Watu hawa wasingeweza kupata maarifa na uwezo wa kuwa na juhudi, ubunifu, na ufanisi kama wasingeelimishwa. Ndio maana jambo la kwanza lililofanywa wakati wa Azimio ni pamoja na kutaifisha mashule ili Serikali na mtaji wake mdogo itoe na kusambaza maarifa kwa wananchi wake ili wawe tayari kimawazo na kwa ufanisi kuwa wazalishaji na kushiriki katika kuchangia ujenzi wa Taifa kwa umahiri na utaalamu na si kwa mbinu za kijima.

Utakumbuka miaka ile ya awali Nyerere alisema, wakati wenzetu wanapaa, sisi tunatembea, inabidi tukimbie (not sure the exact phrase, mwenye nayo na aibandike hapa) kuwafikia. Sasa namna ya kuwafikia mojawapo ni kuboresha watu kwa kuwapa elimu na afya ili waweze kushiriki katika ujezi wa TGaifa, iwe ni kwenye Kilimo, Ufugaji, Biashara, Viwanda au shughuli nyinginezo.

Tunapokuwa kwenye Ardhi, Tanzania tunabahati ya kuwa na rasilimali nyingi za kutosha kutufanya tuwe Taifa linalojitosheleza. Ndio kwa awali tulipokea misaada ili tupate nafasi ya kujizindua kwa kuwa mkoloni alituacha kwenye uchumi na uzalishaji duni. Ukiangalia Kenya na hata Uganda wakati wanapata Uhuru na kufananisha na Tanzania kiuchumi, utagundua kuwa Tanzania tulikuwa nyuma sana kuliko wenzetu. Hata Msumbiji na Kongo, zilikuwa zimeshapata miuondombinu mizuri ya uzalishaji mali, iwe ni barabara, nishati, ujenzi wa miji, mashule, zahanati, viwanda na mengineyo. Sisi tulikuwa na miundombinu ya kujishikiza na Muingereza alituachia viraka alivyoanzisha Mjerumani!

Siasa safi, tulikuwa nayo, na ndio chimbuko la kutaka kujenga nchi ya Kijamaa na Kujitegemea. Maazimio yote uliyoyataja pamoja na sear nyingine ni msingi wa Siasa Safi.

Siasa Safi ni kile kinachoundwa na Chama na uongozi wa Chama. Ndio ushindani wa vyama vingi uliondolewa na TANU (not Nyerere alone) kutokana na mazingira tuliyokuwa nayo nyakati hizo na yaliyokuwa yanatokea si Tanzania tuu, hata kwenye nchi jirani.

Bahati yetu nzuri, hatukufikia hatua ya Marekani ya Civil War kati ya Yankees na Confederates, North na South, maana historia ilishatufundisha kwenye uchanga wa Taifa, mkoroganyo wa itikadi ni sumu na tayari tulishaona matokeo ya kukosekana na mshikamano wa kisiasa kutokana na vita baridi. Hivyo kuepoka vurugu hizo kwenye uchanga wetu ukiambatanisha na unyonge na umasikini, uamuzi wa TANU ambayo ilikuwa chama Tawala kufuta mfumo wa vyama vingi ili kujenga stability, ulikuwa ni haki kwa nyakati hizo.

Suala halikuwa ni kuuwa ushindani, bali kuzuia na kuiepusha Tanzania kuingia katika misukosuko ya kiitikadi kama nchi nyingine zilizyoingia na kupata matatizo.

Lakini ushindani ulibakia ndani ya Chama tawala TANU na ni humo ndani yake ambao ilitegemewa kuwa wale wenye msimamo tofauti na sera na fikra za Mwenyekiti, ama wangewasilisha na kutetea maoni yao na kuyaoanisha na mfumo tuliokuwa tunaujenga na si kufanya mambo kwa uhaini.

Kuna listi ambayo Kuhani kaiweka hapa ya watu takribani 12 ambao eti walipingana na TANU (yeye anasema ni Nyerere) ambao waliposhindwa hoja walifukuzwa uanachama na wengine kuwekwa vizuizini. Swali linabakia hata Kambona aliyekimbilia Uingereza, je yeye alipinga Ujamaa na alikuwa na sera gani kwa Mtanzania? Hata hao wengine ambao kuna wengine walikimbila nje ya nchi, ni sera na itikadi gani walizokuwa nazo ambazo walizifanyia kazi na hata kujaribu kuziuza kwa Watanzania na wakashindwa kutokana na Watanzania kuamini ujamaa?

Ukichunguza, hao 12 na waliofuatia, hawakuwa na Sera au Itikadi yeyote wala utashi wa kimapinduzi na falsafa kuliongoza Taifa. Wao walichokuwa nacho ni kuupinga Ujamaa, Azimio na Nyerere lakini hawakuwa na lolote la kumuuzia Mtanzania apate chaguo. Maana kama walikuwa na sera au falsafa, wakati masharti yalipolegea 1992, wangerudi wakiwa na nguvu kubwa ya ushawishi na kutuuzia sera ambazo zilikimbizwa na Nyerere kwa miaka 25.

Leo hii mawazo na Siasa zao tulizonyimwa na TANU 1965-67 zingekuwa ndio chimbuko la kweli la upinzani Tanzania.

Uongozi bora, hapa ndipo tatizo kubwa lilipo kwa Tanzania. Si nyakati zile tulipoimba ili tuendelee na kulikumbatia Azimio na Ujamaa, bali ni mpaka leo.

Hatuwezi kumlaumu Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete pekee kwa kuwa eti wao walikuwa ni Maraisi na Wenyekiti wa Chama tawala.

Uongozi si wa mtu mmoja ni jumuisho la watu na wanakuwa na mtu mmoka amnaye ni kinara na msimamizi ambaye anabeba sauti za Chama na Serikali.

Kama yalivyotokea kwa Nyerere, hata Kikwete amerithi ugonjwa huo wa kukuta kuwa yeye ni Kiongozi na walio wasaidizi wake, hawana ufanisi, juhudi, hawajitumi na si wakweli kuwa wako pamoja na nahodha wao.

Tofauti ya Nyerere na waliomfuatia hasa Mkapa na Kikwete, ni kuwa alikuwa na uwezo wa kushawishi na alilena kulitumikia Taifa na si Chama au kikundi maalumu cha marafiki.

Bibi Ntilie kanukuu vizuri waraka wa Nyerere dhidi ya "Wazungu Weusi" viongozi ambao walijiona kuwa wao ndio wenye haki na mamlaka pekee ya kuila ile keki ya Taifa.

Wengi wao ama kutokana na udhaifu wa upeo wa kielimu na Utendaji, walifikai kuharibu kabisa maana ya Ujamaa, Azimio na hata utimilizaji wa Sera.

Tatizo letu hata leo ni kufikiri kuwa kazi hii ni ya Rais pekee, na wengine waachiwe huru na hawapaswi kuwajibishwa.

Tofauti yetu leo na wakati wa Nyerere hata Mwinyi ni kuwa sisi kama Taifa, tumeamka na kuwa makini kukemea juhudi za kuua maendeleo zinazofanywa na viongozi wetu huku wakishirikiana na mafisadi.

Naamini kama Nyerere angekuwa kwenye madaraka leo hii, asingelipuuzia vilio vya wananchi na hata nguvu zetu kuwajibisha Viongozi na Serikali jinsi Mkapa na Kikwete walivyofanya kwa ufanisi wa hali ya juu. Hilo ndilo linalomtofautisha Nyerere na waliomfuatia hasa Mkapa na Kikwete.

Tunamsingizia kuwa Nyerere ni haambiliki kwa kuwa ni viongozi walewale "wazungu weusi" ambao waliwekewa vipengele maalum kwenye Azimio la Arusha kuwadhibiti ambao walishindwa kufanya kazi zao na kutimiza majukumu na ili kukwepa lawama na kuwajibika, wakamtuhumu Mwalimu kwa kila kitu.

Ni mpaka pale tutakapokuwa na tabaka la viongozi bora wenye maadili, wenye upeo, wepesi wa kufanya maamuzi magumu, wenye kujituma, ufanisi na kujihakiki na kuwjibika, ndipo Tanzania inaweza kuamka tena na kuwa Taifa la Kijamaa na Kujitegemea na tutaweza kuushinda Umasikini, Unyonge, Maradhi na Ujinga.

La sivyo, hata huu uchumi tulionao wa soko huru na utandawazi ni kazi bure, kwa kuwa tunajua kuwa si Sera au Itikadi za siasa zinazorudhisha maendeleo nyuma bali ni sisi kama Watu na Viongozi.

Hivyo emotion zangu ni kutokana na kuwa tunaukwepa ukweli wa mambo na kukimbilia kulundika lawama kwa mtu mmoja huku wa kuwajibika ni sisi sote.
 
Zakumi nakubaliana na wewe hapo ndipo walipompatia Haille Selasie...
 
Rev,Kishoka unayo haki ya kujiuliza maswali hayo.Na kusema kweli swali unalojiuliza wewe bado lina nisumbua.Lakini katika utafiti wangu nilipata jibu,ambalo hata hivyo bado nalifanyia kazi.Jibu hilo msingi wake ulitokana na maneno ya Nyerere mwenyewe,kwamba 'tusidhani wakoloni wame "give up"ndoto yao ya kututawala, isipokuwa wamekwenda kujipanga,na utumwa wa pili utakuwa mbaya zaidi kuliko wa kwanza."Sasa nilidhani maneno haya yalikuwa na msingi fulani,na nikagundua baadaye kwamba kweli yalikuwa na msingi fulani.Katika utafiti wangu niligundua kwambe yale ya China,Urusi iliyosambaratika,Nazi Germany,Cuba,Angola,Mozambique,Zaire ya Mobutu,Tanzania ya Nyerere na mengine mengi yalikuwa majaribio ya wakubwa 'of a wider agenda.'Nenda TARGETS OF THE ILLUMINATI AND THE COMMITTEE OF 300 uone.Si unajua unapofanya kitu kikubwa lazima ufanye jaribio 'on a smaller scale' ili kuona kama litafanikiwa au la.Kama utasoma 'link' hiyo hapo juu utagundua kwamba wakubwa hawa nia yao ni SERIKALI MOJA YA DUNIA.Na katika serikali hiyo utawala utakuwa wa ki-imla.Kwa hiyo wanachofanya sasa ni kujaribu kujua 'human behaviour' katika 'scenarios' za aina mbalimbali za ki-imla.Ya Nyerere ilikuwa 'scenario' moja wapo.Kama unataka kujua hao wakubwa nenda The 13 Illuminati Bloodlines - Introduction


Ndugu:

Ndio maana tunapigwa magoli kila siku. Siku zote mnaimba nyimbo za ukoloni kurudi.

Kutawala makoloni IS TOO EXPENSIVE and INHUMAN. Kuna njia bora zaidi za kunyonya watu nazo ni kuwapa uhuru na bendera bila kuelewa siri ya urembo wa kujitawala.
 
Ndugu:

Ndio maana tunapigwa magoli kila siku. Siku zote mnaimba nyimbo za ukoloni kurudi.

Kutawala makoloni IS TOO EXPENSIVE and INHUMAN. Kuna njia bora zaidi za kunyonya watu nazo ni kuwapa uhuru na bendera bila kuelewa siri ya urembo wa kujitawala.

Zakumi,

Sasa kama unalielewa hilo, ni ubaya gani uliofanywa kuunda mfumo wetu huru wa kisiasa na kiuchumi kwa kudonyoa kutoka kwa kila mtu?

Maana mantiki makubwa ya kuanzisha thread hii pamoja na kuwa ni kumjadili Nyerere na kilichojenga mawazo yake, ni kujifunza kuwa Tanzania na hasa Nyerere alipoleta Ujamaa na Kujitegemea hata Azimio la Arusha, nini hasa ilikuwa influence yake?

Ndiyo maana kwemye listi yangu nimemuweka Adam Smith, John Milton Keynes, Theodore Roosevvelt, Mao, Lenin, Stalin, Marx, Ghandi na wengine na kujiuliza je tunavyokimbilia kuwpa credit China na Urusi kwa ukomunisti tunakosea huku kumbe resource za siasa yetu ya Ujamaa ambayo ni unique ni tamaduni na miundombinu asili ya Waafrika na mapokeo ya yetu kutoka kwa watu wa Magharibi na Mashariki?
 
Mkiangalia hii ramani (shukrani kwa mchongoma) mtaona jinsi gani Tanzania enzi ya Mjerumani na hata Muingereza jinsi ilivyotajiri.

Naileta hapa ili tunapoliangalia suala la Ujamaa na kuangalia zitendea kazi tulivyokuwa navyo nyakati zile na nyakati hizi tuone ni vipi Watu na Viongozi walishindwa kuleta maendeleo na si Ardhi au Siasa!

2564d1222296085-tukumbuke-zamani-historia-ya-taifa-letu-katika-picha-b00313-p04424.jpg
 
Zakumi,

Sasa kama unalielewa hilo, ni ubaya gani uliofanywa kuunda mfumo wetu huru wa kisiasa na kiuchumi kwa kudonyoa kutoka kwa kila mtu?

Maana mantiki makubwa ya kuanzisha thread hii pamoja na kuwa ni kumjadili Nyerere na kilichojenga mawazo yake, ni kujifunza kuwa Tanzania na hasa Nyerere alipoleta Ujamaa na Kujitegemea hata Azimio la Arusha, nini hasa ilikuwa influence yake?

Ndiyo maana kwemye listi yangu nimemuweka Adam Smith, John Milton Keynes, Theodore Roosevvelt, Mao, Lenin, Stalin, Marx, Ghandi na wengine na kujiuliza je tunavyokimbilia kuwpa credit China na Urusi kwa ukomunisti tunakosea huku kumbe resource za siasa yetu ya Ujamaa ambayo ni unique ni tamaduni na miundombinu asili ya Waafrika na mapokeo ya yetu kutoka kwa watu wa Magharibi na Mashariki?

Kosa ni kuunda mfumo na kusema kuwa mfumo huu ni perfect kwa maisha yetu na tuulinde kwa juhudi zote. Matokeo juhudi kubwa zinafanyika kuulinda mfumo na sio kuimplement mfumo wenyewe.

Kwa mfano mfumo wa Ujamaa ulitakiwa utumike kuinua maisha ya mtanzania. Lakini ilifika kipindi watanzania wakawa wanatumia muda mwingi ku-prove kuwa ujamaa ni mtindo wa maisha. Kilichotakiwa ni kuutumia ujamaa kama vile mabepari wanavyotumia capital kujipatia faida.

Mfano huu ni sawa na mfugaji mwenye ng'ombe mmoja na anayetumia muda mwingi kumchunga ng'ombe wakati ng'ombe mwenyewe hana faida. Na hapa ng'ombe anakuwa mfugaji kwa sababu ndiye mwenye kufaidika.


Tukirudi kwenye swali lako. Mfumo wa maisha unategemea sana na tabia za binadamu katika kipindi husika. Mfumo wa Ujamaa uli-base sana kwenye misingi ya tabia za mwAfrica wakati wa ukoloni.

Waafrika wengi walisahau tofauti zao wakati wanapigani uhuru. Lakini baada ya uhuru tabia za Mwafrika zimebadilika sana. Mahitaji ya mwafrika yameongezeka. Mwafrika anataka kuwa na nyumba nzuri, gari, kushindana na jirani yake na kukwepa kulipa kodi. Zile anasa tulizoziona kama ni tabia za kikoloni sasa hivi zimejaa vichwani mwa watanzania na hivyo ku-invalidate misingi ambayo ingeweza kuujenga ujamaa.


Kipindi cha sasa ambacho mtanzania anaonyesha tabia zake halisi za kibinadamu bila kubanwa na mazingira aliyowekewa na mkoloni ndio wakati mzuri wakuja na falsafa.
 
Kosa ni kuunda mfumo na kusema kuwa mfumo huu ni perfect kwa maisha yetu na tuulinde kwa juhudi zote. Matokeo juhudi kubwa zinafanyika kuulinda mfumo na sio kuimplement mfumo wenyewe.

Kwa mfano mfumo wa Ujamaa ulitakiwa utumike kuinua maisha ya mtanzania. Lakini ilifika kipindi watanzania wakawa wanatumia muda mwingi ku-prove kuwa ujamaa ni mtindo wa maisha. Kilichotakiwa ni kuutumia ujamaa kama vile mabepari wanavyotumia capital kujipatia faida.

Mfano huu ni sawa na mfugaji mwenye ng'ombe mmoja na anayetumia muda mwingi kumchunga ng'ombe wakati ng'ombe mwenyewe hana faida. Na hapa ng'ombe anakuwa mfugaji kwa sababu ndiye mwenye kufaidika.


Tukirudi kwenye swali lako. Mfumo wa maisha unategemea sana na tabia za binadamu katika kipindi husika. Mfumo wa Ujamaa uli-base sana kwenye misingi ya tabia za mwAfrica wakati wa ukoloni.

Waafrika wengi walisahau tofauti zao wakati wanapigani uhuru. Lakini baada ya uhuru tabia za Mwafrika zimebadilika sana. Mahitaji ya mwafrika yameongezeka. Mwafrika anataka kuwa na nyumba nzuri, gari, kushindana na jirani yake na kukwepa kulipa kodi. Zile anasa tulizoziona kama ni tabia za kikoloni sasa hivi zimejaa vichwani mwa watanzania na hivyo ku-invalidate misingi ambayo ingeweza kuujenga ujamaa.


Kipindi cha sasa ambacho mtanzania anaonyesha tabia zake halisi za kibinadamu bila kubanwa na mazingira aliyowekewa na mkoloni ndio wakati mzuri wakuja na falsafa.

Swadakta, tupo kwenye ukurasa mmoja sasa kuwa si siasa bali ni Watu na Viongozi na nikiongeza falsafa ya Mkandara Mazingira!
 
Rev.Kishoka,
Katika ramani ya mkoloni naona kuna barabara inayoitwa Great North Road hiyo barabara bado ipo kweli ama ndio imekufa kutokana na Usanii wa mwafrika, kisha huko upande wa Mbeya/Sumbawanga nimeona kuna Gold mine imeitwa Lupa hiyo ndio wapi?..
 
Rev.Kishoka,
Katika ramani ya mkoloni naona kuna barabara inayoitwa Great North Road hiyo barabara bado ipo kweli ama ndio imekufa kutokana na Usanii wa mwafrika, kisha huko upande wa Mbeya/Sumbawanga nimeona kuna Gold mine imeitwa Lupa hiyo ndio wapi?..
Ni ya Chunya Mbeya, imeshamalizika, yamebaki mashimo. Nadhani ndio yatakuwa hayo kwa sababu ni ya zamani kidogo.
 
Nadhani ni ile nidhamu yetu ya woga ndio iliofanya wengi wasithubutu kuzichallenge hoja za Nyerere hence kuaminika kuwa hoja zake ni kali. Pia sidhani katika nchi ya watu millioni 30 kusiwe na watu hata kumi wanaoweza kwenda toe to toe na Nyerere. Angalia jinsi watu wanavyojadiliana kwa uhuru hapa...enzi za Nyerere kulikuwa na uhuru kama huu kweli?


Kama uko huru kwelikweli weka jina lako la kweli....muulize Invicible na mwenzake walivyokombwa na polisi....enzi hizo za Mwalimu kulikuwa na internet?

Au unamaanisha 'uhuru' unaousema tunao sasa hivi,tunaweza kukutana wote humu na kuongelea yoyote tunayoongelea humu kwenye threads tofauti bila woga lets say,pale Diamond jubilee? Trust me,wote tutajikuta tuko polisi!
 
Kama uko huru kwelikweli weka jina lako la kweli....muulize Invicible na mwenzake walivyokombwa na polisi....enzi hizo za Mwalimu kulikuwa na internet?

Au unamaanisha 'uhuru' unaousema tunao sasa hivi,tunaweza kukutana wote humu na kuongelea yoyote tunayoongelea humu kwenye threads tofauti bila woga lets say,pale Diamond jubilee? Trust me,wote tutajikuta tuko polisi!

Na wakati wa Mwalimu tungeweza kuyasema haya hapo Diamond Jubilee bila kuwekwa kizuizini, au sielewi?
 
Na wakati wa Mwalimu tungeweza kuyasema haya hapo Diamond Jubilee bila kuwekwa kizuizini, au sielewi?

Inaonekana huelewi. Nitajie nani aliwekwa kizuizini kwa kujadiliana issues enzi za Mwalimu.
 
Back
Top Bottom