Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?

Jasusi,

Nani aliwekwa kizuizini bila mashitaka wakati wa McCarthyism ?

Zakumi,

Hilo kombora ni kali mno, sidhani kuna wengi wanaweza kuli handle hapa. Unafanya mchezo. Nimemuuliza Bubu Ataka Kusema juzi hapa, kama unabeza ubepari na unasema "mazuri ya ujamaa ni mengi mno kuliko mazuri ya ubepari" sasa kilichokufanya ukimbilie kwa mabepari ni nini? Oooh sijakimbia, sasa kumbe umefanya nini, unatafuta matibabu ya dharura Saint Thomas Hospital ? Wakaja ma defense attorney wake, wakina Pundit, ambao nao hilo kombora lime "hit home" kwa sababu inawezekana ndio wale wale waliokimbilia kwa mapepari halafu wanatukana ubepari. Wakashindwa kumtetea! Huwezi kuimba Ujamaa ujamaa, halafu umekimbilia kwa mabepari.
Sikujua tupo hapa kurusha makombora. Kusema kuwa Marekani nao walikuwa na kipindi chao cha "dark ages" si sawa na kupenda ujamaa.
Kuhani, kumtia mtu kizuizini bila kumfikisha mahakamani si kosa katika nchi ambayo mpaka leo mna sheria ya detention. Iondoeni hiyo sheria kwanza. At least Durado alitoka kizuizini na kupata au kuendelea na kazi yake. Wakati wa anti-communism hapa watu walipoteza kazi na kutengwa na jamii. Kuna watu waliowekwa ndani kwa kesi za kubambikiziwa. Tafiti utaona mwenyewe.
 
Nilichokipata kwenye hii thread nimekipata, nashukuru. Lakini nitatafuta muda siku nyingine nije niwajibu wote wanaomtukana Nyerere humu, maana wanaharibu historia kwa makusudi. Wapo vijana wengi wasiojua ukweli ama undani wa hali ya Tanganyika na Tanzania, na mazingira aliyokuwa nayo Mwalimu wakati ule kama kiongozi, sasa vijana hao wakisoma matusi anayotukanwa Nyerere humu watadhani ni ya kweli alifanya hayo ama alikuwa na roho hizo anazopakaziwa.

Kwa kipindi hiki mnisamehe tu sina muda wa kutosha kuandika details, lakini tuombe uzima, naapa kwa mizimu ya babu zangu nitarudi hapa nijibu post moja baada ya nyingine, hata kama thread imefungwa nitaianzisha upya.

Asanteni wakuu
 
Tatizo kubwa la Waafrika/Watanzania ni kuwa akitokea Mwafrika/Mtanzania anayejaribu kuvumbua kitu kinachotokana na mazingira ya Kiafrika/Kitanzania na kitakachofanya kazi Afrika/Tanzania basi anapigwa vita mpaka kaburini. Ila akitokea mzawa akaenda ASEAN kuomba sera ya MINITIGER2020 anaonekana wa maana. Tena mzawa mwingine akienda US kuomba dozi ya PRSP ili atengeneze MKUKUTA/NSGRP wa kuombea misaada kupitia kopo la maombi la HIPC anaonekana wa maana!

Mpaka leo tunajadili tuige kipi, cha magharibi au mashariki, badala ya kunoa bongo zetu na kuvumbua vya kwetu wenyewe. Hivi hizi nadharia za ubepari na usoshalisti/ukomunisti zinamsaidia nini mkulima wa pale kijijini Mtakuja? Ujamaa ilikuwa ni jitihada ya dhati ya kuvumbua mfumo wetu wenyewe wa maendeleo! Ndio maana hata Mwalimu alisisitiza kuwa anachukia 'dotrinaire socialism', yaani imani ya kisoshalisti, inayosema maisha yetu ni maisha ya migogoro ya watu/matabaka na unaoutukuza ubepari kwa kudai kuwa lazima tuwe kwanza mabepari alafu tupambane wee uchumi uanguke pwa kama unavyoanguka sasa duniani ndipo tuwe wasoshalisti. Ujamaa ulikuwa ni msingi wa usoshalisti wa Kiafrika wenye mantiki ya Kiafrika kwa ajili ya Mwafrika anayeishi Afrika kwenye mazingira ya Kiafrika (Rejea Ujamaa By Junious(Tusi) Nyerere)!

Fellow Africans/Tanzanians let us stop consuming the knowledge that we don't produce while we produce the knowledge that we don't consume, yaani, Waafrika/Watanzania wenzangu hebu tuache kufakamia maarifa ambayo hatujayavumbua na kuvumbua maarifa ambayo hatuyatumii!

Wewe bado unaboronga. Kwanza siasa na miundo ya jamii ni human behavior. Nyerere aliwaona watanzania naive (mafala) fulani. Watu wasiojua kunyonya na wavumilivu.

Kitu ambacho hakukijua ni kuwa watanzania wakipata nafasi nao wana-behave kama watawala.

Hivyo kuwa na siasa maalumu kwa ajili ya waafrika/watanzania ni upumbavu. Siasa ni lazima ziende na level ya watu ambao wakipata ujanja wanabadilika.

Vilevile waafrika tuna tofauti. Hakuna uvumbuzi utakao kuwa sawa kwa wamasai na wachagga kwa kipingi kimoja. Hivyo ni kuwa na akili fupi kufikiri mmakonde na msukuma wanaweza wakaendelea kwa siasa za aina moja.

Na mwisho kabisa. Wafumbuzi waafrika/watanzania wanaopigwa vita, wanajipiga vita wenyewe kwa sababu mbili muhimu. Kwanza wanachovumbua sio COST effective. Na vilevile hawajuhi ni siku gani kusimama pale majaribio yao yanaposhindwa. Chukua mfano wa Ujamaa. Serikali ilitumia mamilioni kufungua viwanda ambavyo havikusaidia taifa. Lakini kila viliposhindwa viliongezewa mitaji wakati kilimo mtu wa mgongo hakikupata kitu.

Sababu nyingine ni PRIDE. Mnafanya vitu kwa pride na sio kuboresha maisha yenu. Wote mnaomsifia Nyerere mnamsifia kwa sababu alifanya hivyo kuwakilisha watu weusi.

Tukiacha PRIDE na kuchukua ujamaa kama falsafa na kulinganisha wengine walifanya nini utaona kuwa ujamaa ulikuwa pure CRAP.

Wako

Rasputin The Evil Monk
 
Zakumi,Kuhani,

..nashukuru kwamba hata wewe umeona jinsi 'washabiki' wa Mwalimu walivyoikimbia ripoti ya wachumi toka Goteborg Univ na ESRF.

..ripoti hiyo inatoa mwangaza wa jinsi mijadala ya uendeshaji uchumi wa taifa letu ilivyokuwa ikiendeshwa wakati ule.

..zaidi ripoti inaelezea matatizo yaliyokuwepo, mapendekezo tofauti ya hatua za kuchukua, pamoja na maamuzi yaliyofikiwa kutokana na mapendekezo hayo.

..kuna wananchi walipoteza kazi/nyadhifa zao. kosa lao lilikuwa ni kumsihi Mwalimu kubadili mwenendo wa jinsi uchumi wetu ulivyokuwa ukiendeshwa.

..kuna walioitwa wasaliti, wakapakaziwa kwa wananchi, wakatengwa kisiasa, na kudhalilishwa ndani ya chama.

..Mwalimu alitekeleza ushauri mbaya, matokeo yake uchumi ukadidimia. lakini hakuna aliyewajibishwa badala yake watu hao hao wakapewa nafasi ya kutekeleza mapendekezo ambayo mwanzoni waliyopinga kwa nguvu zote.

..mazingira na mahusiano ya utendaji kazi na kisiasa wakati wa utawala wa Mwalimu hayaku-encorage mawazo mbadala, badala yake kulikuwa na mashindano ya kudumisha fikra za mwenyekiti--hata zile zilizokuwa na athari mbaya kwa uchumi.

Nao hao ndio waliokuwa wanamwaga mahela kusaidia serikali yake. Siku zote wanasema hapa wanasema kuwa nchi za Scandinavia ni kama zao na wajamaa watanzania. Lakini wakibondwa wanakaa kimya.
 
Jasusi,

Nani aliwekwa kizuizini bila mashitaka wakati wa McCarthyism ?

Zakumi,

Hilo kombora ni kali mno, sidhani kuna wengi wanaweza kuli handle hapa. Unafanya mchezo. Nimemuuliza Bubu Ataka Kusema juzi hapa, kama unabeza ubepari na unasema "mazuri ya ujamaa ni mengi mno kuliko mazuri ya ubepari" sasa kilichokufanya ukimbilie kwa mabepari ni nini? Oooh sijakimbia, sasa kumbe umefanya nini, unatafuta matibabu ya dharura Saint Thomas Hospital ? Wakaja ma defense attorney wake, wakina Pundit, ambao nao hilo kombora lime "hit home" kwa sababu inawezekana ndio wale wale waliokimbilia kwa mapepari halafu wanatukana ubepari. Wakashindwa kumtetea! Huwezi kuimba Ujamaa ujamaa, halafu umekimbilia kwa mabepari.

lol

Nostalgia ya ujamaa inawasumbua. Kuna siku nilikuwa narudi Tanzania na chanel moja ya ndege ikawa inapiga nyimbo ya Remmy (Narudi Songea). Basi nikajiona nasikiliza bonge la wimbo. Lakini zote zilikuwa ni emotions tu.

Na siku hizi wakipata visenti huku Marekani, wanataka nyumba zao ziwe kama za kimarekani. Luxury zote za kiMarekani wanataka kuzipeleka Tanzania.

Na wakienda kwenye benki za kibongo hata foleni hawataki kusimama. Wanataka wamepewe huduma kama wako Marekani.

Msigeuke jiwe.
 
Sikujua tupo hapa kurusha makombora. Kusema kuwa Marekani nao walikuwa na kipindi chao cha "dark ages" si sawa na kupenda ujamaa.
Kuhani, kumtia mtu kizuizini bila kumfikisha mahakamani si kosa katika nchi ambayo mpaka leo mna sheria ya detention. Iondoeni hiyo sheria kwanza. At least Durado alitoka kizuizini na kupata au kuendelea na kazi yake. Wakati wa anti-communism hapa watu walipoteza kazi na kutengwa na jamii. Kuna watu waliowekwa ndani kwa kesi za kubambikiziwa. Tafiti utaona mwenyewe.

Hakuna makombora ni ukweli. WE dare to speak. Jesus aliacha maneno. Lakini wafuasi wake wakaendeleza.

Nyerere ni kama boxer Mike Tyson. Ana washabiki tu. Enzi zake Nyerere alifanya hivi, alifanya vile.

Ungekuwa ni mfuasi wa Nyerere, usingekaa Marekani. Lakini kwa sababu wewe ni mshabiki wake it doesn't matter where you live.
 
Nimekubali ushabiki wangu. Sitageuka kuwa Petro. Ninyi ndio mnaojua na kuhodhi ukweli.
 
Kuhani, kumtia mtu kizuizini bila kumfikisha mahakamani si kosa katika nchi ambayo mpaka leo mna sheria ya detention. Iondoeni hiyo sheria kwanza. At least Durado alitoka kizuizini na kupata au kuendelea na kazi yake.

Jasusi,

Sikia Mkuu. Ukishamfunga mtu jela bila mashitaka huwezi ukasema "at least alitoka kizuizini na kuendelea na kazi yake." Ni aibu kutetea ovu eti kwa sababu mngeweza kumnyang'anya na kazi pia. Ni unyama huo. Na vipi hao wengine ambao hamkuwarudishia kazi zao, na wale waliotoka hoi nusu ya kufa na magonjwa ya vifua kwa kufungiwa kwenye vyumba vya giza na vumbi na visivyo na hewa Oysterbay detention camp ?

Halafu ile sheria ya Mazuizi ya Kuzuia ilikuwa ni unjust law. Sehemu nyingine duniani inavyofanya kazi unaweza ku challenge kizuizi chako, kutumia Habeas Corpus proceedings. Lakini ya Tanzania ilikuwa inasema kinachoamuliwa na Rais ndio kimeshaamuliwa, imetoka. Hakuna due process protections kuhakikisha haki. Mpaka walipoibadilisha kuruhusu Habeas Corpus challenges mwaka 1985 wakati J.K. Nyerere anaondoka. Haikuwa sheria ya haki.

Halafu, hata kama ukisema ni sheria iliyokuwepo kwa hivyo sheria ni sheria, bado kinachosumbua na kinachoumiza sana ni kuwa sheria yenyewe haikufuatwa. Kwa mfano, kuna wakati political police wa J.K. Nyerere walikuwa wanasahau kupata muhuri au saini ya Nyerere kufanya preventive detention iwe halali. Mawakili wa waliowekwa kizuizini wana challenge mahakamani halafu henchmen wa Nyerere wanaiambia mahakama tutaleta muhuri ya Rais baadae. Yani dharau juu ya ubabe, ufidhuli juu ya uhasidi.

..the Court of Appeal declared that the detention order in this particular case was invalid for lack of a public seal. However, the detainee remained in custody. The state authorities had rushed to the President on his return to the country and obtained a new detention order which met all the requirements. (1)

Kuna siku detainee mmoja, Happy George Maeda, aliishinda state authority ya Nyerere mahakamani. Kumbe security forces zikawa zimeshajiandaa kutokushindwa. Alipoambiwa na jaji uko huru tu, ile anatoka kwenye ngazi za mahakama political police wa Nyerere wanae! Wakamkwida upya. Majaji wa Tanzania walisikitika mno. Jaji Mwesiumo anasema "hiyo sio dharau ya Mahakama tu, ila dharau ya sheria za nchi na Katiba yake." (2)

Halafu kuna sheria nyingine shemeji yake na hii ya preventive detention, ikiitwa The Deportation Ordinance of 1921. Inaruhusu Rais aamue kuku "deport" kutoka sehemu moja ya Tanganyika kwenda kwingine. Mara nyingi ulikuwa unafungiwa kijijini kwa Mama yako. Ilianza kutumiwa na wakoloni kuhamisha watemi walioonekana vurugu vurugu. Nyerere nae, masikini, akawa anaitumia! Kuna siku mwekwa kizuizini ali challenge deportation. Mahakama ikatuma summons kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza aje kujieleza imekuwaje hakuna muhuri na saini ya Raisi. Mkuu wa magereza alikuwa hana detention order. Hakujali, na mahakamani hakuja, akatuma photocopy ya detention order yenye muhuri na saini ya Rais iliyopigwa tarehe ya mbele zaidi ya alipotumiwa summons. Yaani siku mfungwa anawekwa kizuizini kulikuwa hakuna detention order, ila state authority ya Nyerere wakakimbia Ikulu na J.K. Nyerere akatia saini baada ya mtu kukamatwa. (3)

Unaweza kusema haya ni ma technicality tu. Lakini si hivyo. Jaji wa Mahakama Kuu alisema kwamba hata ukisahau kuanisha kijijiji unachoenda kumfungia muwekwa kizuizini hilo ni kosa la msingi. "the omission to specify the place to where the subject to the order and the warrant is to be sent, cannot be said to be a mere technicality, but is a material irregularity." (4)

Kwa hiyo utaona, Jasusi, hata ukisema hizi sheria za kihasidi ni halali, bado hawakufuata sheria zinavyosema. Sheria ya kikatili halafu wewe unaongeza ushetani juu yake. Matokeo yake ndio nusu-unduli wa ile enzi. J.K. Nyerere anasoma ninachoandika hapa kutoka kaburini, na anajua simsemei uongo. Simtukani, nasema yaliyojiri wakati wa era ya Preventive Detention Act of 1962. Mtu mwenye kuchonga chonga sana kama mimi wakati wa enzi za J.K. Nyerere ilikuwa jehanamu. Ndio maana nawaenzi hawa mababa zangu waliokuwa na kende za kuhojiana na J.K. Nyerere. Yeye Mwalimu, bahati mbaya, hakuwa nazo, ndio maana akawa anawatuma political police wakamate wabunge wanaochangia bajeti bungeni! Think about that!

(1 ) Attorney-General v. Lesinoi Ndeinai, [1980], Incarcerating the Innocent😛reventive Detention in Tanzania, The Johns Hopkins University Press. CHRIS PETER MAINA

( 2) Edward Mlaki and Liston Matemba v. Regional Police Commander Kilimanjaro Region and Secretary Regional Security Committee Kilimanjaro Region, High Court of Tanzania at Arusha, Misc. App No.38 of 1979.

( 3 ) High Court of Tanzania at Dar es Salaam, Misc. App No. 44 of 1979

( 4 ) In the Matter of an Application for a Writ of Habeas Corpus Subjiciendum and In the Matter of Detention of Winfred Ngonyani at Keko Remand Prison in Dar es Salaam, 1982. CHRIS PETER MAINA
 
Kuhani, mchungaji na wanamjdala wenzangu salute kwa michango mizuri!

Tatizo kubwa sisi waafrika hatuthamini utu wa watu wetu. Ni laana ambayo tumeshindwa kuiondoa. Ndo maana mpaka leo wananchi tunakuwa second class kwenye nchi yetu hata kwenye maamuzi muhimu yanayotuhusu! Mi ndiyo maana nimesema, sheria kandamizi ambazo zilipita enzi za Nyerere itatuchukua miongo mingi kuzibadirisha kwa sababu zinawafanya viongozi wetu wawe miungu watu. Na on record- nyingi ya hizo sheria alipitisha mzee wetu mpendwa! hivi leo CCM imejijenga kuanzia kijijini..ukija uchanguzi machinery zote za serikali zinakuwa agents wa CCM..kuanzia DC,DED,RC nk..haya hayakuanza leo. na vyeo vingi kama hivi viliundwa kumlinda mzee, otherwise how do you justify uwepo wa DC na RC? Kifupi mwalimu politicised all governement machineries. A no small feat kubadilisha! Mmoja atasema kwa nini tusibadilishe haya mambo waliobaki? Yes, probabably you are right, but think again landscape ya ushindani wa siasa Tanzania..utalielewa hilo! People are trying lakini kuna sheri kandamizi mno!

Hivi mchungaji, naomba nikuulize, 1995 ilikuwa ni hakika kabisa kwamba CCM waliiba kura Zanzibar mchana kweupe! Everybody knows. Nyerere alikuwa hai. Alifanya nini? Alikemea wizi na uvunjaji wa haki za wananchi? From 1995 election Zanzibar was never the same again! Muumba wetu alimwita miaka minne baadaye, lakini unaweza kunipa hata chembe ya juhudi za mwalimu katika kuaddress mgogoro wa Zanzibar? Infact alienda kuwasaidia WARUNDI kutatua migogoro yao.. (something good ofcourse;-)

Tatizo wengi humu tunajadili theories za ujamaa na ubepari kwa kutumia elimu yetu..kifupi we are just theoretical, lakini tunashindwa kung`amua kwamba kwa mwananchi wa kawaida anachokihitaji siyo hizi theories ni uhuru wa kuwa huru nchini mwake. Ndo maana leo hata viongozi wa upinzani (sorry ushindani) wakiongea bungeni wanaonekana kwamba hawana adabu. Mtu akiongea na mawazo mbadala utaambiwa huna shukrani, maana ulisomeshwa na CCM! Upo hapo? Mpaka leo nchini kwetu tunaona chochote kinachofanywa na serikali ni fadhila na wala si wajibu. Despite millions of tax payers money!

Kambarage alikuwa na nafasi kubwa sana ya kutujengea misingi ya demokrasia ya kwa kweli. Naamini Tanzania tungekuwa na demokrasia ya kweli mengine tungeyapata tuu. Jiulize Nyerere alianza kuwa VERY CRITICAL wa system na serikali alivyoondoka madarakani! Can we say that was a smart move? Sidhani mi nailinganisha hiyo na akina Warioba, Sumaye, Msuya et al ambao leo hii ndo wanapaza sauti dhidi ya ufisadi na utawala wa kimabavu lakini hao hao walipokuwa madarakani ndo walikuwa mabaradhuli wa kufa! Kwa hiyo kwa mwendo huo, cycle haiishi..akina Pinda wa leo ndo watakuwa macritic wa serikali kesho..and on and on...

All in all, I always appreciate Nyerere kama kiongozi wetu na michango yake kwa taifa letu, lakini nadiffer na wenzangu wanapotaka (Speak no evil, see no evil against Mwalimu).

Friends, make no mistake no body hates Mwalimu as a human being, lakini hapa tunajaribu kuangalia sisi kama taifa tulijikwaa wapi na kujikuta hapa tulipo? na wengi tuna majibu tofauti, lakini ukweli unabaki, somewhere tulijikwaa. Sasa kama hatuwezi kukubaliana ni wapi tulipojikwaa, basi tushikane mikono tuendelee na safari tukiwa makini tusijikwae tena. Maana kila mmoja wetu ana jibu lake ni wapi tulijikwaa. Hiyo itatusaidia mbele ya safari.

Nadhani kuna haja ya kuwa na elimu ya uraia kuangalia ni wapi demokrasia ya nchi yetu imetoka na inaelekea. ukisoma mijadala ya bunge kuanzia uhuru mpaka leo utagundua ni wapi tumetoka. Hizi theories za ujamaa zitakuwepo tuu as long as tunaishi kama binadamu. Harafu sidhani ni vema kumlinganisha Nyerere na viongozi wa kiafrika..cha muhimu ni kuangalia alichokifanya kilikuwa na maslahi kwetu kama wananchi au la? maana in Africa viongozi wengi walikuwa madikteta, lakini haihalalishi udikteta wa mzee wetu. Huwezi kupima ufya yako kwa kujilinganisha na mgonjwa! Definetely utakuwa na nafuu!

Kiuchumi Nyerere alijitahidi sana kuwa creative-unfortunately hakufanikiwa. Kwa upande wa demokrasia, ningekuwa mwalimu wa Sayansikimu ningempa alama ya D.
 
Mtazamo wako Masanja kuhusu Nyerere unafanana na wa kwangu. In fact mimi namwona Nyerere kama a failure. Nitamwonaje successful leader kama sisi aliotuongoza ni maskini hohe hahe, kuanzia akilini(zimelala) hadi umasikini wa mali na kipato?

Binafsi siwezi kwenda kinyume na dhamiri (conscience) yangu na kuanza kumshabikia JKN wakati naamini alitu-let down. Hata "pride" aliyotujengea, haikuwa na misingi. Ilijengwa hewani.
 
Masanja na Invicible,

Nashukuru kwa kuingia ndani na kuchangia kuhusiana na hoja hii. Hoja imepoteza dira kutokana na kuanza kurudia yale tuliyoyasema kwenye thread nyingine kuhusu Nyerere.

Nia yangu narudia tena kwa kila mtu ilikuwa ni kutaka kujua chimbuko na asili la Nyerere kuukimbilia Ujamaa na Kujitegemea na hata kuishia kutuletea Azimio la Arusha.

Yamekuja mawazo mengi na katika mdahalo wa upi ungekuwa mfumo mzuri wa Tanzania, tukaingia katika mambo ya utawala wa Nyerere kama kiainishi cha kuonyesha ni vipi mifumo mingine isingefanikiwa kwa kuzimwa kama mshumaa na Nyerere na wafuasi wake.

Binafsi, nakubali, kuna mambo ambayo sikubaliani na Nyerere na jinsi alivyoyafanya na najiuliza uamuzi wake ulikuwa ni kwa sababu gani? ni ulevi wa madaraka au woga?

Suala la Zanzibar 1995, ilipaswa asimame juu ya mawingu n akumfungashia virago Salmin Amour! Sasa sijui ni kamari gani alicheza kumrudisha Salmin maana ZEC na CCM walikimbilia Butiama kutaka ushauri na ndipo matokeo yakatangazwa.

Hili nitalipinga daima, pamoja na utamaduni ulioendelea wa kupuuza wananchi ingawa alijitahidi sana kukikaripia chama baada ya kuondoka madarakani.

Nyerere angeamua kuachana na kuiokoa CCM kisiasa na kiushawishi kila mara, yaliyotufikia hapa ya udhalimu wa Serikali na CCM hasa kutuhujumu na ukosefu wa uongozi bora yasingetokea!
 
[QUOTE

Nyerere angeamua kuachana na kuiokoa CCM kisiasa na kiushawishi kila mara, yaliyotufikia hapa ya udhalimu wa Serikali na CCM hasa kutuhujumu na ukosefu wa uongozi bora yasingetokea![/QUOTE]

Asante sana mchungaji.
 
Kuhani said:
Halafu ile sheria ya Mazuizi ya Kuzuia ilikuwa ni unjust law. Sehemu nyingine duniani inavyofanya kazi unaweza ku challenge kizuizi chako, kutumia Habeas Corpus proceedings. Lakini ya Tanzania ilikuwa inasema kinachoamuliwa na Rais ndio kimeshaamuliwa, imetoka. Hakuna due process protections kuhakikisha haki. Mpaka walipoibadilisha kuruhusu Habeas Corpus challenges mwaka 1985 wakati J.K. Nyerere anaondoka. Haikuwa sheria ya haki.

Kuhani,

..sasa hayo uliyaeleza ni tisa, kumi ni lile zoezi la kukamata wahujumu uchumi.

..wananchi wanakamatwa mbele ya watoto wao usiku wa manane. WHY?

..walidai zoezi la kukamata wahujumu uchumi ndiyo muarubaini wa matatizo ya uchumi wa Tanzania.

..nakumbuka kuna Mzee mmoja wa miaka kama 90 akiitwa Kengeremingi. walimkamata porini na maelfu ya ngombe wakadai ni mhujumu uchumi. sasa nijiuliza: what did he have to do with the inflation that was off the roof? what did he have to do with factories that were undercapitalized and underutilized?

..lakini siyo huyo tu. kuna meneja wa Tacoshili alikataa kusafirisha saruji kwasababu kiwanda cha wazo walikuwa wadaiwa sugu. meneja huyo alikamatwa ni kuwekwa ndani zaidi ya miaka miwili akisubiri mashtaka ya uhujumu uchumi. baadaye akaonekana hana hatia, na serikali haikumfidia chochote.

..matukio ya kionevu kama niliyoyaeleza hapo juu yalikuwa mengi, tena nchi nzima.

..lakini zoezi la kuhujumu uchumi siyo kwamba lilikuwa na maana yoyote ile kiuchumi, bali hata kisheria lilikuwa batili.

..nina hakika "watetezi" wa Mwalimu bado wanaamini kwamba zoezi lile lilikuwa na lengo la kuokoa uchumi wetu. zaidi, wanaamini kwamba lilifanikiwa.
 
..nina hakika "watetezi" wa Mwalimu bado wanaamini kwamba zoezi lile lilikuwa na lengo la kuokoa uchumi wetu. zaidi, wanaamini kwamba lilifanikiwa.

The Serpent General,

This is where you go wrong assuming that everything that was done during Nyerere era is merry and dandy and we the Pro-Nyerere are dumb enough to play blind on injustices or wrong doings!

Uhakika umepotoka hapa rafiki yangu!
 
Wewe bado unaboronga [...] Wako Rasputin The Evil Monk

Kumbe ni wewe Tuta, nilikuwa nakutafuta sana na wale wapinzani wenzako wa JKN kule DHB ya enzi zile. Kumbuka mlikubali wito wangu wa kurejea Tanzania tunoe bongo zetu, tuangalie wapi tulijikwaa na tusawazishe pale JKN alipochemka. Najua mna uchungu sana na JKN tena uchungu binafsi unaochochewa na aliyowafanyia aidha ninyi, wazazi wenu,ndugu zenu au marafiki zenu wa karibu hasa wale waliokuwa wameanza kuwini maisha wakati wengine wanalosti. Msameheni tu mzee wa watu. Na yeye pia alikuwa anataka tuwe na 'wini-wini situesheni'.

Sasa rudini jamani rudini nyumbani tulete hayo mabadiliko ili tuondoe ule ubaya wote ambao mnadai tumerithi kutoka kwa JKN, yaani woga wa kuthubutu, ukosefu wa ufanisi kazini, ukiritimba wa mawazo n.k. Ila mkumbuke daima lazima tuanze mwanzo na mwanzo wa Tanzania ni JKN na sera zake za Ujamaa na Kujitegemea. Lazima tuanze kwa kuangalia asili ya fikra na dhana za JKN kwa undani kama swali kuu la mada hii ya Mchungaji inavyoonesha.

Narudia tena kuwa JKN mwanzoni hakuwa na nia kabisa ya kuwaburuza Watanzania ndio maana kwenye toleo la mwaka 1967 la kijitabu chake cha sera cha 'Socialism and Rural Development', yaani 'Ujamaa na Maendeleo Vijijini' alisema kila jamii itabidi ibuni mbinu zake yenyewe kuendelea maana huwezi kuwa na mbinu hiyo hiyo ya maendeleo kwa Mmasai aliyebobea zaidi kwenye ufugaji na Mnyakyusa ambaye amejikita zaidi kwenye ukulima.

Sasa tujiulize ilikuwaje ghafla katika miaka ya 70 JKN aliingiwa nini akilini mpaka akakubali viongozi waanze kutumia nguvu za dola kulazimisha wananchi waende kuishi misituni?Nini kilisababisha fikra za JKN zibadilike na aanze kutekeleza yale ambayo hakuyadhamiria hapo awali? Hivi hayo mawazo yake ya mwanzo nayoyanukuu hapo chini kutoka kwenye hicho kijitabu chake cha sera yana tatizo gani - mbona mengine wanayaiga kwenye hizi refomuzi tulizoletewa na hao hao ambao sasa wanabeiliauti na kutaifisha makampuni yao?

"But we must add to these [three] principles [of the Ujamaa family] the knowledge and the instruments necessary for the defeat of the poverty which existed in traditional African society. In other words, we must add those elements which allow for increased output per worker, and which make a man's efforts yield more satisfactions to him."

"We must take our traditional system, correct its shortcomings, and adapt to its service the things we can learn from the technologically developed societies of other continents."

"It is obvious, however, that with the variations in potential in soils and in social customs, it would be absurd to set down one pattern of progress or one plan which must be followed by everyone."

"What is necessary is the objective of an ujamaa commuity. The interim steps and the detailed organization should be adapted to the local circumstances - which includes an understanding of the people's traditional attitudes as well as the degree of the people's political understanding and their acceptance of this social objective"

"It is essential to realize that within the unity of Tanzania there is also such diversity that it would be foolish for someone in Dar es Salaam to try to draw up a blueprint for the crop production and social organization which has to be applied to every corner of our large country"

"Principles of action can be set out, but the application of these principles must take into account the different geographical and geological conditions in different areas, and also the local variations in the basically similar traditionals structures."

"For example, in the Kilimanjaro Region not only is the practice of individual land-holding [Kihamba system] almost universal, but also there is no unused land on the mountain. This affects social attitudes and create some family problems which do not exist in those parts of Tanzania where a young man can get land of his own quite near to his father's farm as soon as he is ready to start his own family. Again, some part of our country suffer from great water shortage or uncertainty; their agricultural organization, their density of population - and thus their social organization - must inevitably take account of these facts, just as the organization in well-watered areas must take advantage of its greater potential. All these things affect what can be grown, and the degree of investment in land or the implements which is necessary for a given output. It would be absurd to try and settle all these questions from Dar es Salaam, particularly as such variations as those of the type of soil sometimes occur within a very small area. Local initiatives and self-reliance are essential"

"The social customs of the people also vary to some extent. The Masai are traditionally a nomadic cattle people; their family structure, their religious beliefs, and other things, have been shaped by this fact. They are therefore somewhat different from the social beliefs and organization of, for example, the traditionally agricultural Wanyakyusa. The steps which will be necessary to combine increased output with social equality may therefore also vary; the important thing is that the methods adopted should not be incompatible with each other, and should each be appropriate for the attainment of the single goal in a particular circumstance."

"'[T]here must also be an efficient and democratic system of local government, so that our people make their own decisions on the things which affect them directly, and so that they able to recognize their own control over community decisions and their own responsibility for carrying them out."

"In Tanzania it is clear that as a general rule new development of this kind should be operated by the public, although some private or joint private and public investment may be appropriate in certain cases where expertise or capital is an immediate problem."

"Marketing must be properly organized so that, even while our nation is in grip of international market forces which contol world prices, still we get the maximum possible for our goods, and our producers - that is, our farmers - get a fair return for their contribution to the national wealth."

Haya mambo JKN aliyafikiria 1967!Huyu Mzee aliona mbali sana! 'He wa far ahead of his time - it seems he is even far ahead of our time'! Ndio maana bado hatumuelewi, labda tutamuelewa mwaka 2050 baada ya MDGs2015, MKUKUTA2005+, MINITIGER2020 na VISION2025 kutimiza ile methali ya 'mbio za sakafuni huishia ukingoni'!Nadhani aliliona hilo ndio maana alisisitiza kuwa 'mwisho wa siku tutayarudia maadili na misingi muhimu ya Ujamaa'!Na mwisho wa siku ndio huu wa EPA, KAGODA, RICHMOND, MEREMETA,TANGOLD, BUZWAGI, TULAWAKA,....,!
 
Kwahiyo aliona mbali akampa nchi Mkapa kwasababu ya Kiwira Tangold etc ?
 
Kwahiyo aliona mbali akampa nchi Mkapa kwasababu ya Kiwira Tangold etc ?

Hapana mkuu, alituwezesha tuchague 'the lesser evil', yaani uovu mdogo zaidi kati ya maovu mengi makubwa...hebu imajini richi boizi tu meni wangechukua inji hii wakati ule...kumbuka nilisema aliona mbali sikusema aliona ndani...si rahisi kujua ndani ya moyo wa mwanadamu kuna nini...ni vigumu kujua lini moyo wa mwanadamu utabadilika kama kinyonga...usiusemee moyo...ila kwa matendo yao utawajua...kwa wakati ule matendo yao aliyajua...aliyaona...
 
Mwalimu nina mrespect with all due respect...(May he rest in Peace)
Ila angetakiwa aanzishe yeye mwenyewe chachu ya mabadiliko na si kukaa pembeni eti kudai kuwa mabadiliko yatatokea ndani ya ccm na huku ufisadi nje nje...Imani na wananchi wa aina mbali mbali ilishamtoka..Ufisadi ulikuwa unatokea aliuona lakini hakuthubutu kukaribisha mawazo tofauti...Same major problem iliyomkosanisha na wapambanaji wenzake.
Alikumbatia unazi wa chama kuliko hali halisi..Remember Mrema?
Yani yeye hakuona ilikuwa right kwa Mrema kupinga kina Chavda?
Mimi mwenyewe nilikuwa bwana mdogo sana tu lakini alichofanya Mrema ndicho wanachofana kina Slaa,Zitto na Mbowe hivi sasa...

Kwahiyo mwalimu alikuwa na yeye na unazi kwasana tu na ndio tatizo tulilo nalo...Unazi wa chama mbele..Taifa nyuma.
 
Mwalimu nina mrespect with all due respect...
Ila angetakiwa aanzishe yeye mwenyewe chachu ya mabadiliko na si kukaa pembeni eti kudai kuwa mabadiliko yatatokea ndani ya ccm na huku ufisadi nje nje...Imani na wananchi wa aina mbali mbali ilishamtoka..Ufisadi ulikuwa unatokea aliuona lakini hakuthubutu kukaribisha mawazo tofauti...Same major problem iliyomkosanisha na wapambanaji wenzake. Alikumbatia unazi wa chama kuliko hali halisi..Remember Mrema? Yani yeye hakuona ilikuwa right kwa Mrema kupinga kina Chavda? Mimi mwenyewe nilikuwa bwana mdogo sana tu lakini alichofanya Mrema ndicho wanachofana kina Slaa,Zitto na Mbowe hivi sasa...Kwahiyo mwalimu alikuwa na yeye na unazi kwasana tu na ndio tatizo tulilo nalo...Unazi wa chama mbele..Taifa nyuma.

Kaka kumbuka Mwalimu alisema CCM sio mama yake...kumbuka alichangia kumjenga Mrema...Umesahau vile vikao vyake na Mzee wa Kiraracha pale Msasani/Butiama...Ni kweli aliibeba sana CCM kwenye matatizo yake hasa kuhusu OIC, G55 na CUF...Ila wakati wa vyama vingi CCM haijawahi kupata mpinzani/kritiki mkubwa kuliko yeye...Yeye ndiye aliyekisafisha CCM pale mafisadi walipotaka kuchukua nchi wakati wa uchaguzi ule ambao Mzee wa Guta alipata asilimia 20...Cheki mwenyewe beti hizo hapo chini kutoka katika katika kitabu chake cha kiushairi cha Tanzania!Tanzania! uone jinsi alivyokichambua chama kama karanga...

Hivi Chama SISIEMU
Hakina jambo haramu?
Kila wapendacho watu
Ni kuntu kwa Chama chetu?

Wengi wakisha amua,
Mama yako kumuua,
Kwa kuwa wao ni wengi,
Utashiriki, hupingi?

Pindi zianzapo nyimbo
Za kugawana majimbo,
Chama hiki yumbayumba
Kitaanza kuziimba?

Huo ndio uongozi
Wa Chama cha Mapinduzi?
Chama cha wapenda vyeo,
Wasio na mwelekeo?

Sharia yao matumbo,
kwa hili na kila jambo?
La msimamo hawana,
Huuza hata wanina?
 
Kwahiyo mwalimu alikuwa na yeye na unazi kwasana tu na ndio tatizo tulilo nalo...Unazi wa chama mbele..Taifa nyuma.

Na dondoo nyingine inayoonesha kuwa Mwalimu alijitahidi kusafisha chama hii hapa kutoka kwenye kitabu chake cha 'Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania':

Hatuwezi kuachia utamaduni wa woga ukawa ni mbinu au sifa mpya ya uongozi. Na sasa lazima tukiri kwamba utamaduni huu wa woga unaanza kuwa ni sehemu ya tatizo letu la kitaifa. Nilisema awali kwamba nilionana na baadhi ya Wabunge wenye hoja ya Utanganyika. Wote walipokwisha kutoa dukuduku zao kuhusu madhambi ya Serikali, niliwaambia: "Waheshimiwa Wabunge, yote mliyoyasema ni sababu nzuri za kuchukua hatua za kuwadhibiti Viongozi wahusika; kwa nini badala ya kufanya hivyo mnachukua hatua za kutaka kuigawa nchi?" Jibu lao: "Viongozi wakisemwa wanakuwa wakali sana!" Viongozi wetu nao nilipowauliza: "Kwa nini hamkupinga hoja ya Wabunge kama tulivyokuwa tumekubaliana, na badala yake mkaamua kuikubali?" Jibu lao: "Wabunge hao walipotoka kwako Msasani walikuwa wakali kama mbogo!"Na wajumbe wa Kamati Kuu ukiwauliza: "Kwa nini hamkukataa pendekezo la Serikali la kukubali hoja ya Serikali Tatu?" Jibu lao: "Wakubwa walikwisha kukubaliana, sisi, tungeweza kufanya nini?" Hata mtu mmoja hakuweza kupaaza sauti na kusema: Hivi sivyo? Hii ndio demokrasia mpya na mbinu mpya ya kukabiliana na Mfumo wa Vyama Vingi? Huko ndio kwenda na wakati?

Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio ulifanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona Chama makini cha upinzani; na wala dalili zozote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasiwasi!

Mwalimu wa watu alijitahidi, tena hiko chama mpaka kilimliza siku moja kikaoni maana viongozi walizidu kumkaidi kwa sababu alikuwa ameng'atuka. Alitaka sana mabadiliko ndio maana mjumbe mmoja wa G55 anasema kumbe Mwalimu alipowaita pale Msasani nia yake hasa ilikuwa kujenga mazingira yakayowafanya watoke CCM ili waunde chama kitakacholeta upinzani wa kweli. Hakika Mwalimu aliona mbali na alikuwa na alilia sana na mwelekeo wetu wa kifisadi - hebu angalia hizi beti zinazohitimisha hicho kitabu zinavyoonesha jinsi alivyozilani hila za mafisadi na kutuombea heri katika kukabiliana nao:

Ole wake Tanzania
Tusipoisaidia!
Niwezalo nimefanya:
Kushauri na kuonya.

Nimeonya: Tahadhari!
Nimetoa ushauri:
Nimeshatoka kitini;
Zaidi nifanye nini?

Namlilia Jalia
Atumulikie njia;
Tanzania ailinde,
Waovu wasiivunde.

Nasi tumsaidie,
Yote tusimwachie!
Amina, tena Amina!
Amina tena na tena!
 
Back
Top Bottom