Naomba nifunguke kidogo nielezee kile ninachokifahamu kuhusu ili sakata!!
Mgogoro katika ndoa ya Mbasha na Florah ulianza kushika kasi mwaka jana mara baada ya Florah na Mumewe kuhamia kuanza kusali
kanisani kwa GWAJIMA (ufufuo na Uzima - Kawe) wakitokea kanisa la MITO YA BARAKA (kariakoo)! Inasemekana kuwa mara baada ya kuhamia kanisani hapo kwa mualiko wa Gwajima (aliwaombe waje kusali kwake), mchungaji Gwajima alimfanya Florah kama kiongozi wa Ibada ya SIFA na KUABUDU katika mikutano yake!!
Kama ni mfuatiliaji wa haya mambo utakumbuka kuwa mwaka jana Florah alizunguka Tanzania nzima akiwa na Gwajima wakifanya mikutano ya Injili!! Baada ya Muda kidogo Mchungaji Gwajima alimpeleka Florah London kwaajili ya masomo kitendo ambacho
inasemekana kilipingwa sana na mumewe Mbasha! Ikumbukwe kuwa GWAJIMA haiwezi kupita miezi miwili pasipo kwenda UK coz
amefungua kanisa kule (GLORY OF CHRIST - UK)!! So katika kipindi ambacho Florah alikuwa London, walikuwa wanaonana mara nyingi sana na GWAJIMA...
Baada ya Florah kurudi Tanzania, ndipo akaanza hii ziara ya kuzunguka mikoani na GWAJIMA... inasemekana kuwa katika kipindi
hiki ndipo mahusiano ya kindoa kati ya Florah na mumewe yalizorota zaidi... baada ya ziara kuisha Florah alirudi nyumbani lakini she wasn't the same (nisiseme zaidi)!
Baada ya mikwaruzano ya hapa na pale, ndipo Florah akaenda kukaa hotelini na inasemekana hoteli ilikuwa inalipiwa na mchungaji GWAJIMA. Ikumbukwe kuwa ni swala la kawaida kwa Gwajima kuwalipia bills mbalimbali viongozi wake wa huduma hapo kanisani kwa mfano ana mchungaji anaitwa MAXMILLIAN MACHUM, amempangishia nyumba ya ghorofa pale Ubungo na wachungaji wake wote wapatao thelethini amewanunulia magari!!
Lakini hata hivyo hii hatua yake ya kumpangia hoteli mke wa mtu ilizua maswali mengi sana...