Who is MIZENGO PINDA? (private & Public)

Who is MIZENGO PINDA? (private & Public)

Mtu kashakwambia kafundishwa kazi na Lowassa, Ben Mkapa, Ngwilizi, Andy Chenge unategemea nini?

Frankly mimi ningekuwa comfortable na backbencher kua PM kuliko hawa tunaowajua.

Uliona confirmation speech alivyokuwa ana ji shoot himself in the foot bila hata kuulizwa? Je kama kungekuwa n some real confirmation process ingekuwaje?

Jamaa ni Sumaye wa Kikwete.Kikwete kashtuka kuweka mjanja kama Lowassa soo ngoja niweke mkalamba nimpeleke peleke.


Unajua tatizo moja kubwa sana katika utawala wa CCM ni kuwaweka kando watu wenye uwezo hasa kuanzia utawala wa Mkapa. In fact Lowasa kuwa PM was rather exceptional. Kwa akili, uwezo na ujasiri aliokuwa nao Lowasa kwa utaratibu wa kawaida wa CCM asingewezekana awe PM. Hata ndani ya CCM wengi watakwambia kwamba Lowasa ana uwezo mkubwa sana kuliko aliyekuwa boss wake na kwa sababu hii hakufaa kuwa PM kwa utaratibu unwritten wa CCM. Of course tatizo la Lowasa ni huko kupenda kwake mali na kuamua kuzisaka kwa kila njia ikiwemo wizi wa hela za nchi.

Sasa huyu Pinda tunajua ni very poor thinker and a very bad implementer. Hata kutafsiri mambo ya kawaida kabisa kunampa shida. Utakumbuka mapema mwaka 2006 aliagizwa aangalie uwezekano wa kuimarisha serikali za mitaa. Lakini kwa uwezo mdogo alio nao yeye akafikiri hii inamaanisha kumuongezea madaraka waziri wa serikali za mitaa. Kwa hiyo akaibuka na mswada wa sheria unaotaka kumpa mamlaka waziri wa serikali za mitaa kuteua madiwani kumi katika kila halmashauri. This was the most ridiculous bill proposed by a minister in contemporary Tanzania. Sasa some of us tukiona mtu kama huyu anapewa u-PM tunajua ndiyo hivyo tena tunarudi kwenye enzi za Sumaye za kuwa na symbolic PM ambaye kazi yake ni kufungua makongamano ya ukimwi. Huyu hana tofauti yeyote na Sumaye kiuwezo; tofauti pekee ni kwamba yeye angalau sio mlafi na hivyo hana historia ya kuiba, which of course is good. But as far as u-PM is concerned we should not expect anything from him apart from seeing a docile PM office and once again a disturbingly very powerful president doing all PM functions!

ok, sasa tunakuja kwenye issue yenyewe ya kujiuzulu u-PM bwana Lowas, did he do the right thing-absolutely yes! Lakini speech yake ilikuwa ya kitoto. Ukisoma ile speech ni kama vile anazira baada ya kuwa implicated katika ile scandal rather than kujiuzulu. Sababu ya msingi kabisa ya yeye kujiuzulu ni ukweli kwamba kwa revealations za kamati ile ni wazi kwamba wananchi wasingeweza tena kuwa na imani na ofisi ya PM bila kujali kama yale madai ni ya kweli au la. Sasa kwa mtu mwenye uelewa wa kawaida wa kiuongozi huwezi kuendelea kufanya kazi ya wananchi ambayo wananchi unaowafanyia hiyo kazi hawana imani na wewe. Of course nakubaliana naye kwamba it's wrong for the Mwakyembe committee to reach such grave conclusions without having interogated the PM in person, if this assertion is at all true. This is unethical in any kind of investigation or any sort of activity that involves some sort of research. In regardless of the obviousness of the evidence the committee thought was there to implicate the PM, they should have sought his explanation. This is very much a common sense issue and you dont need to be lawyer to understand it. Kwa hiyo utaona kwamba kulikuwa na some sort of being overwhelmed and obsessed kwa upande wa kamati. Pamoja na yote haya, Lowasa hawezi kujitetea kwamba hahusiki na uhuni ule wa Richmond maana ushahidi ulikuwa wazi hata kabla ya kamati hii; walichofanya kamati ni kuthibitisha kile ambacho tulikuwa tunakijua.

Now should we smile that our cry for Lowasa to go has finally been heeded to and that a new cabinet is in the offing? My answer here is absolutely yes but for different reasons. It is not that this will help to end ufisadi in our country, no. As I have repeatedly said in the past, ufisadi hauwezi kwisha katika ile nchi kwa kukata matawi au kwa kuwatoa samaki wanaonekana wana sumu au wameoza. Ukweli ni kwamba tatizo la ufisadi katika nchi yetu ni la kimfumo zaidi kuliko hali ya kwamba ni la watu wachache katika system. Madamu ni CCM hii inaendelea kuwa ndani ya nyumba bado tutaendelea kupambana nalo kwa sababu players watabaki hao akina Pinda ambao wameshiriki ufisadi moja kwa moja au kwa kufumba macho wakati ufisadi ukitendeka. Na sababu ingine ya msingi ni kwamba CCM ya leo haiwezi kushinda uchaguzi katika Tanzania ya leo bila ufisadi. Kwa hiyo CCM wanajua kuumaliza kabisa ufisadi itakuwa sawa na kukata mti walioukalia.

Lakini kwa maana ya utawala bora na kukuza demokrasia, lazima tukiri kwamba hili tukio limetupeleka hatua moja mbele kabisa. Katika bara letu la Afrika nchi yetu inakuwa ya pili kwa kiongozi mwenye uzito wa waziri mkuu kujiuzulu kwa sababu za rushwa. Nilipokuwa Abuja, Nigeria juzi niliona jinsi ambavyo TV za huku zilivyoshtushwa na waziri mkuu wetu kujiuzulu na jinsi ambavyo jambo hili lilizua mazungumzo miongoni mwa wananchi wa jiji la Abuja. Yaani walikuwa hawaamini kwamba katika bara hili waziri mkuu anaweza kujiuzulu kwa sababu ya rushwa. Kwa hiyo tumepiga hatua na kwa kiasi fulani tumetoa somo kubwa sana kwa nchi zingine katika swala la uwajibikaji. Ni kweli pia kwamba jambo hili litahuisha sana utendaji na taswira ya serikali ya Rais Kikwete. Sasa JK kapata nafasi ingine tena ya kusawazisha mambo katika utawala wake, swali ataitumia? Ngoja tusikilizie.

Wapo watakaouliza je upinzani watakuwa na ajenda bado? Mimi kwa maoni yangu ni kwamba hili ni jambo jema kwa upinzani kwa sababu ajenda ya ufisadi ilikuwa inakula muda wa upinzani katika kufanya kazi za kawaida za kisiasa. Sasa tunategemea tunapoelekea huko 2010 from today tuanze kuona vyama vyetu vya siasa vinaanza kushindana kutoa mawazo ya namna ya kuitoa Tanzania hapa tulipo. Kazi ya kuikosoa na kuizodoa serikali imekwishaonekana sana. Sasa nafikiri wananchi sasa wangependa kuona kwamba vyama vyetu sio tu kwamba ni parties against something (in this case ufisadi), lakini pia parties for something. Wakati umefika tuwape wananchi falsafa na mkakati wetu wa kumaliza umaskini, kuboresha huduma za jamii, etc ili waanze kutu-judge kwa haya.

Sasa kuna kila dalili kwamba hivi karibuni kitaeleweka!
 
What he stands for

2008-02-09 09:13:36
Angel Navuri said:


wmkuu108037yu9.jpg


Credit: IPP media

The new Prime Minister, Mizengo Pinda, yesterday pledged to closely work with Members of Parliament in what he described as a ``united parliament`` so as to relieve millions of Tanzanians from deepening poverty, coupled with a high cost of living, unemployment and other social-economic problems.

Pinda promised to push for solid unity among the state pillars - executive, judiciary and parliament - for the betterment of the lives of Tanzanians.
``The focus should be to bring better lives to all Tanzanians and safeguard interests our political parties. We need to be united, especially on matters of national importance,`` he said, adding that he would cooperate and work hand in hand with ministers, MPs in Parliament, as well as meeting the expectations of the President and Tanzanians generally. ``This is the toughest assignment, but I will try as much as possible to move at par with the fast-tracking spirit and determination of the president,`` he added.

He said the country expected much from leaders and legislators, and that it was time ``we, in the leadership, should deliver to their expectations and drive them out of numerous problems.`` Pinda advised the incumbent permanent secretaries and would-be ministers to respect expert advice on technical issues of national interest. ``We have to instill discipline in the public systems we need to work and correct problems of state organs pointed out in the parliamentary select committee report and others related public institutions. I am sure, if we do this there will be changes in the operations and performance of the government systems,``he said.

Pinda challenged MPs to forget the past and concentrate on the task ahead of serving the nation.
Hayo ndiyo maneno ya waziri Mkuu mpya.

Kitila

Thanks kwa maoni yako hapo juu, natumaini na wengine wanaomfahamu vizuri wataweka maoni yao hapa.
 
The new Prime Minister, Mizengo Pinda, yesterday pledged to closely work with Members of Parliament in what he described as a ``united parliament`` so as to relieve millions of Tanzanians from deepening poverty, coupled with a high cost of living, unemployment and other social-economic problems

Kwa maneno mengine ni huu ndio wakati muafaka wa kutambua sekta zote ambazo sio rasmi, ili kuona vipi zitaweza kuinua hali ya maisha ya mtanzania.
 
Kitila,

thanx for a comprehensive, good analysis. Have a drink, bill on me.
 
Kitila thanks for this, it takes somebody principled to write this about Lowassa

Of course nakubaliana naye kwamba it's wrong for the Mwakyembe committee to reach such grave conclusions without having interogated the PM in person, if this assertion is at all true. This is unethical in any kind of investigation or any sort of activity that involves some sort of research. In regardless of the obviousness of the evidence the committee thought was there to implicate the PM, they should have sought his explanation. This is very much a common sense issue and you dont need to be lawyer to understand it. Kwa hiyo utaona kwamba kulikuwa na some sort of being overwhelmed and obsessed kwa upande wa kamati. Pamoja na yote haya, Lowasa hawezi kujitetea kwamba hahusiki na uhuni ule wa Richmond maana ushahidi ulikuwa wazi hata kabla ya kamati hii; walichofanya kamati ni kuthibitisha kile ambacho tulikuwa tunakijua.

I have been saying the same all along, ila ukisema hivyo unaambiwa wewe ni Lowassa sympathiser/apologist.The rights to a hearing is a basic one and as you put it, was not afforded Lowassa.My thing is now they have iven Lowassa something to save face on unnecessarily.
 
-This is unethical in any kind of investigation or any sort of activity that involves some sort of research.
Nimetoa mfano wa scandal ya Watergate ambapo kamati ya uchunguzi haikumhoji rais isipokuwa kamati ya senate baada ya uchunguzi kuwakilishwa!.... hamkutoa jibu!
 
"Sikiliza huyu Mizengo haiwezekani akawa ni Clean kama ambavyo unataka tuamini na only time will tell kama ni Mizengo au atakuwa ni Mizengwe"

Inaelekea haupo analytical because you ta side just because you fill so ,nikuulize kama hauna vigezo vya kutueleza kwanini hayuko clean at we just wait time will tell.Nadhani hii ni ile tabia ya kupinga kila kitu!!!!
 
Jamaa alikuwa Usalama wa taifa na mpaka sasa ni afisa Mwandamizi tena Waziri mkuu .unatgememea angesoma saa ngapi?>kwani ukona alivyoongea jana.Yeyes siyo Mwanasiasa

Kwani kusoma mpaka uwe mwanasiasa? Kuna courses nyingi tu pale Open University. Kwa siku hizi kukaa na bachelor degree miaka 30 bila hata kusoma ka certificate (post graduate certificate) ni uvivu wa hali ya juu.

Wengine tunaita continous improvement, sasa utaimpove vipi wakati hutaki kujiendeleza?
 
Kazi kweli kweli!

Mkandara,

Kwa umbea niliopewa mimi ni kwamba huyo mdogo mtu ambaye aliolewa na Pinda baada ya dada yake kufariki na yeye alishafariki. Nimefikisha ujumbe.

Sasa kitengo cha uchunguzi cha JF ingieni kazini na kutuletea ukweli.

Binafsi naona kuwa na ngoma sio issue labda issue ni hiyo ya kuoa mara ya pili wakati unajua unaumwa. Kama hiyo ni kweli basi itakuwa issue. Vinginevyo, hata kama ana ngoma bado ana uwezo wa kuchapa kazi miaka mingi ijayo. Siku hizi kuna madawa na watu wanaishi miaka mingi tu.
 
Pinda anaweza kuutumia uzoefu wake kwa namna mbili..
1)Ya kwanza ni kutumia uzoefu wake kwenye masuala ya kisheria ambapo atafanikisha kuwafikisha mafisadi mbele ya sheria bila kuvunja sheria.
2)Pili anaweza kutumia uzoefu wake wa masuala ya usalama wa taifa na kuwadhibiti wapinzani,kuhakikisha usiri na kuwashughulikia wale wote wanaovujisha nyeti!
NI WAZI UPANDE WA WAZALENDO NI NAMBA MOJA!WILL HE BE ABLE TO TAKE THE RESPONSIBILITIES THAT WE EXPECT HIM TO DO!WE'LL WAIT AND SEE!
 
nakuunga mkono mkuu kwa hoja hii.

Hivi kweli wana JF tunaanza kujadili vazi la mtu siku ya kwanza tu na ku discredit? kweli tuko makini kiasi gani? Kama ni sifa ya PM kuvaa vizuri, huyo aliyevaa vizuri ameufanyia nini umma wa waTanzania?

Hivi tunajua kweli tunachokihitaji sisi watanzania toka kwa viongozi wetu? Inawezekana kweli kiongozi avae vema, lakini lazima liwe jambo la kwanza kabisa ambalo kwa upeo wetu ndiyo tuanze kulitazama? haya mambo dada zetu kule sekondari ndo walikuwa wanagombania...kusemana kwa mavazi na kupendeza.

Pinda ni waziri wa TAMISEMI na mmoja kati ya mawaziri wachache waliohamia Dodoma. Siku ya kwanza tu watu mnataka awe kama hao mnaoishi nao USA, UK au Ufaransa?

Je tusingeweza kusema kuwa kuvaa kwake leo kunaonyesha kuwa si mpenda makuu, mtu mwenye maisha ya kawaida sana, japo ameitumikia Ikulu kwa muda mrefu sana? Je tusingeweza kumpa muda kidogo halafu tuone kama hatabadilika na kupiga mapigo ya ki PM, kama akipenda? JK anaapiga suti, kuna watu tunamwita mzee wa maonyesho ya suti...hivi tunataka nini lakini jamani?

huyo anavaa mavazi ya kiafrica kama suti za nyerere,kaunda na vile vile mandele alikuwa hapendi suti sana ,kule Nigeria wanavaa kivyao huyo jamaa kuwa Ulaya naye kashajifanya Mzungu ebu mpashe kaka
 
Kuondoa hiki kiwingu- basi PM apime ngoma na matokeo yawekwe wazi!

Tusije ingia gharama siku za karibuni as a country kutafuta tena PM mwingine... our country is so poor and we can can not afford!

Ashauriwe apime ngoma na majibu watu wajue ili kuondoa duku duku!

Nakemea kwa nguvu yote hii tabia ya wasioelimika ya kuwanyanyapaa wenye virusi ,ikomeeeeeeeee
 
" na PM anayeonyesha poor judgement katika prsentation (kuvaa) anaweza kuonyesha poor judgement hata katika presentation ya documents Paris Club na World Bank huko."

Mbona Nyerere,mareheremu Kabila,Kaunda walikuwa wanavaa style ya ant-uzungu ,vile vile Mandela hupendelea kuvaa mashati ya maua,Fidel castro -Kombati mbona hamuwasemi ? vipi viongozi wanaigeri wanavaaje si kivyao .Wewe kama unatukuza uzungu na kuukana Uafrika kivyako sio wote
 
Madiba alipoanza kuvaa mashati yake walimsema sana. Sasa limekuwa vazi la heshima. Mwalimu na 'Chou in lai' zake, hakuna aliyemsema, tulimzoea. Wolfowitz anavaa soksi zenye matundu lakini hakuna anayebisha intellect yake. Sasa vazi la waziri mkuu ni lipi? Suti za Armani? Muache a'form identity yake'. Mimi hata akija na msuli, ili mradi akaonyesha uadilifu kazini na uwezo makini wa kuunganisha jamii ya kitanzania sina tatizo nae. Pengine tunahitaji Andre 3000 wetu anayejua hali ya watanzania na aliye accessible na watu. Naamini huko Paris Club ( si anaenda waziri wa fedha huko na si PM)wanaheshimu intellect na sio mavazi. Muacheni kwanza tuone uwezo wake. Huko kupanga pamba kutakuja au hakutakuja.Could't care less!

KABISA Nakuunga MKONO

Vipi Mahtma Gandh alikua akivaaje? was he not good upstairs?
 
KABISA Nakuunga MKONO

Vipi Mahtma Gandh alikua akivaaje? was he not good upstairs?
I almost mentioned Mahatma Gandhi..but you already did!ITS TRUE!ILA AFANYE YALE TUNAYOTARAJIA SI KAUNDA SUTI WALA NINI ZITAKAZOMLINDA!
 
Kuondoa hiki kiwingu- basi PM apime ngoma na matokeo yawekwe wazi!

Tusije ingia gharama siku za karibuni as a country kutafuta tena PM mwingine... our country is so poor and we can can not afford!

Ashauriwe apime ngoma na majibu watu wajue ili kuondoa duku duku!

Jamani acheni unyanyapaa! Nadhani mnahitaji testimony za watu kama kina Joseph Kato na Alex Marjery kugundua kuwa tabia mnayofanya hapa ni mbaya sana. Joseph Kato ni miongoni mwa watanzania wa awali kabisa kujitokeza mbele ya umma na kujitangaza wazi kuwa ni waathirika wa virusi vya UKIMWI, na binafsi nimeonana naye na kuzungumza naye mara kadhaa. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1995, wakati huo afya yake haikuwa nzuri na alituambia aligundua tatizo lake 1987 baada ya kifo cha mkewe na mwanae mchanga. Akajiunga na wenzie wakaanzisha SHDEPHA+. Leo hii ni zaidi ya miaka 20 imepita, ukimwona Kato huwezi kuamini kama ana tatizo lolote, achilia mbali HIV. Vivyo hivyo kwa Alex Marjery, mtanzania pia ambaye alishuhudia kuwa ni miaka 10 sasa tangu ajijue ana HIV, lakini ukimwona ana shepu ya "baunsa" bila dalili yoyote ya nje. Ujumbe: Kwanza, wako watu wengi sana huko mtaani wenye HIV ambao hawana ujasiri huo wa kujitangaza (kinyume na kina Kato na Marjery), na si ajabu ndio wanaonyanyapaa wenzao ilhali hali zao hawazijui. Pili, watu wenye HIV wanaweza kuendelea na kazi zao vizuri tu. Joseph Kato angekuwa waziri mkuu alipojigundua ana HIV miaka 20 iliyopita, leo hii angekuwa waziri mkuu mstaafu aliyetumikia sawa na vipindi vinne vya miaka 5 kila kimoja, na angekuwa anagombea urais (angekuwa hajatuambia kuhusu shida yake wala tusingejua, na tungemchagua kama kawaida). Hadi ninapoandika ujumbe huu, Joseph Kato amekuwa mwenyekiti wa chama cha wanaoishi na HIV (SHDEPHA+) tangu kuanzishwa kwake hadi leo, na yuko active sana katika mapambano dhidi ya UKIMWI katika ngazi mbalimbali za kitaifa na kimataifa.

Nimetoa mifano hiyo miwili tu ya watu ambao wamekubali kwa hiari yao kufahamika katika jamii licha ya unyanyapaa uliopo ili kuisaidia jamii, lakini watu hawa ni ushuhuda kuwa kuathirika na HIV hakumwondolei binadamu utu wake na wala hakumfutii uwezo wake wa kuitumikia nchi.

Kwa hiyo haya maneno ya kusema mtu apimwe HIV ili ati "msijekuingia gharama siku za karibuni" ni maneno tukanishi, ya kifedhuli, ya kibaguzi yenye kunyanyapaza na kudunisha utu. Tumeshuhudia watu wengi wakifa na tumeingia gharama nyingi za mazishi, kuajiri upya n.k kutokana na vifo vilivyosababishwa na ajali, kisukari, stroke, malaria nk, na wote hao wamekufa na kuwaacha wenye HIV wakiendelea na maisha duniani. Upimaji wa HIV kwa lengo la kuepuka "kuingia gharama siku za hivi karibuni" ungetusaidiaje katika matukio kama yaliyowakuta Marehemu Juma Akukweti na Salome Mbatia? Hebu jamani acheni tabia hii ni mbaya sana!
 
ni ukweli ulio wazi kuwa kuondoa hili tatizo la richmond ..KWA KIASI KIKUBWA ALIYEKUWA WAZIRI MKUU LOWASSA ALIKUWA AKIIDHIBITI NCHI..YAANI ALIKUWA AKIMFUNIKA JK KIUTENDAJI...KWA KIASI FULANI JK ALIKUWA AKIFURAHIA HALI HIYO MWANZO..KWA KUWA ILIMUWEZESHA KUSAFIRI MUDA MREFU TU....NA MAMBO YALIKUWA MAZURI...

TATIZO LILIANZA KUJITOKEZA MWANZONI..MWA LAST YEAR AMBAPO BAADHI YA MAWAZIRI WAANDAMIZI KAMA HUYU WA KUSAFIRI..PAMOJA NA WASHAURI WASIO RASMI WALIPOANZA KUMNANGA JK KUWA WATU WANASEMA JAMAA ANAKUFUNIKA,MARA JEURI ANAFANYA MAMBO ANAVYOTAKA,..MARA HAFUATI MAAMUZI YA BARAZA..ETS...HII ILIANZA KUZOROTESHA MAHUSIANO YA WAWILI HAWA...

KWA KIASIKIKUBWA MUUNGWANA HII RIPOTI ALIIONA MWANZO NDO MAANA RIPOTI YA HOTUBA YA MWISHO WA MWEZI huu aliongelea baadhi ya vipengele vya ripoti hii mf...kutofautisha biashara na siasa..imekuja gundulika hili ni moja ya pendekezo la kamati..

kwa kifupi jk hakupenda kumsaidia lowassa ..angependa kum,uokoa hasa ukizingatia kuwa ni msiri wake aliyeongoza kampeni zake tangu mwaka 1995...na kukosana na watu wengi kwa ajili yake..ie sumaye ..amabaye wanatoka eneo moja..angeweza kufanya yafuatayo...

1]angeweza kuamua kuifilisi au kuikataa richmond pale tu minongono ilipoanza mwaka jana...

2]angeweza kuharakisha mabadiliko ya baraza la mawaziri kabla ripoti haijatolewa ..na ikibidi kumuondoa waziri mkuu na kumpumzisha..hii ingepunguza munkari ya wabunge...

3]kama alivyofanya kwa ripoti ya BOT ambayo inagusa pesa za kampeni..angeweza kuamua kuchukua jukumu la KUUNDA TUME YA RAIS YA RICHMONE..HAPA INA MAANA MAPENDEKEZO YOTE ANGEPEWA YEYE...NA ANGECHUKUA HATUA ..AMABAPO RAIS HALAZIMIKI KUSEMA SABABU ZA KUCHUKUA HATUA...NA ANGEVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI...

kwa kikwete kushindwa kufanya hayo amemsababishia LOWASSA KIFO CHA JUMLA CHA KISIASA...so kama kweli bado alikuwa ni rafiki yake..na alidhamini mchango wake..hadi anaupata urais angeweza kumtoa bila kumsababishia kifo cha kisiasa....tena bila kupewa haki ya kusikilizwa....PAMOJA NA KUWA NI WAZI MAKOSA ANAYO!!!!..

KWA HALI KAMA HII UHUSIANO WA HAWA MARAFIKI WA ZAMANI HAUTAKUWA ULE WA MWANZO..HAPA JF HAPO NYUMA TULIFANYA UCHAMBUZI ..TUAKAONA TATHMINI RAIS HATAKI KUENDELEA NA LOWASSA TANGU MWAKA JANA...NA KUNA WATU HAPA TUKAWA NA MAONI KUWA JK HAWEZI KUMUONDOA LOWASSA KATIKA MAZINGIRA YA KAWAIDA KWA KUWA AMEONEKANA NA UMAARUFU KUMSHINDA KIUTENDAJI....SANASANA LOWASSA ANA BAHATI ANAGALAU AMEONDOKA KWA KIFO CHA KISIASA...ANGEENDELEA KUONA UGUMU NA AIBU YA MUMWAMBIA AONDOKE ..MUUNGWANA ANGEWEZA KUFIKIRIA OPTION MBAYA KULIKO HII .....

KWA MAANA HIYO LOWASSA ASAHAU TENA SIASA..ABAKIE NA BIASHARA..HII NI KWA WOTE PAMOJA NA ROSTAM NA KARAMAGI!!
 
huyo anavaa mavazi ya kiafrica kama suti za nyerere,kaunda na vile vile mandele alikuwa hapendi suti sana ,kule Nigeria wanavaa kivyao huyo jamaa kuwa Ulaya naye kashajifanya Mzungu ebu mpashe kaka

Tatizo siyo mavazi ya kiafrika, nimeongelea hili, mbona hata mzee Malecela anavaa suti zake na watu hatusemi, kwa sababu mzee anajua etiquette na anpangilia vitu.

Tatizo langu ni ile kuvaa suti tacky bila shati halafu kivest cheupe kinaonekana, on his confirmation day no less.

Clearly he is no Mandela when it comes to dress.
 
Mbona Nyerere,mareheremu Kabila,Kaunda walikuwa wanavaa style ya ant-uzungu ,vile vile Mandela hupendelea kuvaa mashati ya maua,Fidel castro -Kombati mbona hamuwasemi ? vipi viongozi wanaigeri wanavaaje si kivyao .Wewe kama unatukuza uzungu na kuukana Uafrika kivyako sio wote

Unapofanya kitu fanya kitu kamili, unapovaa combat vaa combat na mabuti,Castro akivaa combat na mabuti, au track suit na sneakers mimi sioni ajabu, sio combat na moccassin au track suit na moccassin.

Alichofanya Pinda ni kuvaa suti na white tshirt inayoonekana,impossibly repulsing.

I will say this again and again, kabla ya kujibu angalia confirmation speech kwanza ujue ninachoongelea.

Siku atatokea Waziri Mkuu amevaa chpi nje tutasema "anti-western" style poa tu.
 
Back
Top Bottom