Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,956
Mtu kashakwambia kafundishwa kazi na Lowassa, Ben Mkapa, Ngwilizi, Andy Chenge unategemea nini?
Frankly mimi ningekuwa comfortable na backbencher kua PM kuliko hawa tunaowajua.
Uliona confirmation speech alivyokuwa ana ji shoot himself in the foot bila hata kuulizwa? Je kama kungekuwa n some real confirmation process ingekuwaje?
Jamaa ni Sumaye wa Kikwete.Kikwete kashtuka kuweka mjanja kama Lowassa soo ngoja niweke mkalamba nimpeleke peleke.
Unajua tatizo moja kubwa sana katika utawala wa CCM ni kuwaweka kando watu wenye uwezo hasa kuanzia utawala wa Mkapa. In fact Lowasa kuwa PM was rather exceptional. Kwa akili, uwezo na ujasiri aliokuwa nao Lowasa kwa utaratibu wa kawaida wa CCM asingewezekana awe PM. Hata ndani ya CCM wengi watakwambia kwamba Lowasa ana uwezo mkubwa sana kuliko aliyekuwa boss wake na kwa sababu hii hakufaa kuwa PM kwa utaratibu unwritten wa CCM. Of course tatizo la Lowasa ni huko kupenda kwake mali na kuamua kuzisaka kwa kila njia ikiwemo wizi wa hela za nchi.
Sasa huyu Pinda tunajua ni very poor thinker and a very bad implementer. Hata kutafsiri mambo ya kawaida kabisa kunampa shida. Utakumbuka mapema mwaka 2006 aliagizwa aangalie uwezekano wa kuimarisha serikali za mitaa. Lakini kwa uwezo mdogo alio nao yeye akafikiri hii inamaanisha kumuongezea madaraka waziri wa serikali za mitaa. Kwa hiyo akaibuka na mswada wa sheria unaotaka kumpa mamlaka waziri wa serikali za mitaa kuteua madiwani kumi katika kila halmashauri. This was the most ridiculous bill proposed by a minister in contemporary Tanzania. Sasa some of us tukiona mtu kama huyu anapewa u-PM tunajua ndiyo hivyo tena tunarudi kwenye enzi za Sumaye za kuwa na symbolic PM ambaye kazi yake ni kufungua makongamano ya ukimwi. Huyu hana tofauti yeyote na Sumaye kiuwezo; tofauti pekee ni kwamba yeye angalau sio mlafi na hivyo hana historia ya kuiba, which of course is good. But as far as u-PM is concerned we should not expect anything from him apart from seeing a docile PM office and once again a disturbingly very powerful president doing all PM functions!
ok, sasa tunakuja kwenye issue yenyewe ya kujiuzulu u-PM bwana Lowas, did he do the right thing-absolutely yes! Lakini speech yake ilikuwa ya kitoto. Ukisoma ile speech ni kama vile anazira baada ya kuwa implicated katika ile scandal rather than kujiuzulu. Sababu ya msingi kabisa ya yeye kujiuzulu ni ukweli kwamba kwa revealations za kamati ile ni wazi kwamba wananchi wasingeweza tena kuwa na imani na ofisi ya PM bila kujali kama yale madai ni ya kweli au la. Sasa kwa mtu mwenye uelewa wa kawaida wa kiuongozi huwezi kuendelea kufanya kazi ya wananchi ambayo wananchi unaowafanyia hiyo kazi hawana imani na wewe. Of course nakubaliana naye kwamba it's wrong for the Mwakyembe committee to reach such grave conclusions without having interogated the PM in person, if this assertion is at all true. This is unethical in any kind of investigation or any sort of activity that involves some sort of research. In regardless of the obviousness of the evidence the committee thought was there to implicate the PM, they should have sought his explanation. This is very much a common sense issue and you dont need to be lawyer to understand it. Kwa hiyo utaona kwamba kulikuwa na some sort of being overwhelmed and obsessed kwa upande wa kamati. Pamoja na yote haya, Lowasa hawezi kujitetea kwamba hahusiki na uhuni ule wa Richmond maana ushahidi ulikuwa wazi hata kabla ya kamati hii; walichofanya kamati ni kuthibitisha kile ambacho tulikuwa tunakijua.
Now should we smile that our cry for Lowasa to go has finally been heeded to and that a new cabinet is in the offing? My answer here is absolutely yes but for different reasons. It is not that this will help to end ufisadi in our country, no. As I have repeatedly said in the past, ufisadi hauwezi kwisha katika ile nchi kwa kukata matawi au kwa kuwatoa samaki wanaonekana wana sumu au wameoza. Ukweli ni kwamba tatizo la ufisadi katika nchi yetu ni la kimfumo zaidi kuliko hali ya kwamba ni la watu wachache katika system. Madamu ni CCM hii inaendelea kuwa ndani ya nyumba bado tutaendelea kupambana nalo kwa sababu players watabaki hao akina Pinda ambao wameshiriki ufisadi moja kwa moja au kwa kufumba macho wakati ufisadi ukitendeka. Na sababu ingine ya msingi ni kwamba CCM ya leo haiwezi kushinda uchaguzi katika Tanzania ya leo bila ufisadi. Kwa hiyo CCM wanajua kuumaliza kabisa ufisadi itakuwa sawa na kukata mti walioukalia.
Lakini kwa maana ya utawala bora na kukuza demokrasia, lazima tukiri kwamba hili tukio limetupeleka hatua moja mbele kabisa. Katika bara letu la Afrika nchi yetu inakuwa ya pili kwa kiongozi mwenye uzito wa waziri mkuu kujiuzulu kwa sababu za rushwa. Nilipokuwa Abuja, Nigeria juzi niliona jinsi ambavyo TV za huku zilivyoshtushwa na waziri mkuu wetu kujiuzulu na jinsi ambavyo jambo hili lilizua mazungumzo miongoni mwa wananchi wa jiji la Abuja. Yaani walikuwa hawaamini kwamba katika bara hili waziri mkuu anaweza kujiuzulu kwa sababu ya rushwa. Kwa hiyo tumepiga hatua na kwa kiasi fulani tumetoa somo kubwa sana kwa nchi zingine katika swala la uwajibikaji. Ni kweli pia kwamba jambo hili litahuisha sana utendaji na taswira ya serikali ya Rais Kikwete. Sasa JK kapata nafasi ingine tena ya kusawazisha mambo katika utawala wake, swali ataitumia? Ngoja tusikilizie.
Wapo watakaouliza je upinzani watakuwa na ajenda bado? Mimi kwa maoni yangu ni kwamba hili ni jambo jema kwa upinzani kwa sababu ajenda ya ufisadi ilikuwa inakula muda wa upinzani katika kufanya kazi za kawaida za kisiasa. Sasa tunategemea tunapoelekea huko 2010 from today tuanze kuona vyama vyetu vya siasa vinaanza kushindana kutoa mawazo ya namna ya kuitoa Tanzania hapa tulipo. Kazi ya kuikosoa na kuizodoa serikali imekwishaonekana sana. Sasa nafikiri wananchi sasa wangependa kuona kwamba vyama vyetu sio tu kwamba ni parties against something (in this case ufisadi), lakini pia parties for something. Wakati umefika tuwape wananchi falsafa na mkakati wetu wa kumaliza umaskini, kuboresha huduma za jamii, etc ili waanze kutu-judge kwa haya.
Sasa kuna kila dalili kwamba hivi karibuni kitaeleweka!