Sawa mkuu tuachane na Pinda kidogo hapa.
Umesema na kunitolea mfano.. sawa je, sii kweli watu wenye ukimwi wanaruhusiwa kuoana wao wenyewe hata ktk nchi hizo zilizoendelea ambazo mnajaribu kuchukua tamaduni zao?...ain't we making them a family?
Ikiwa Ukimwi upo ktk jamii yangu ningekuwa na uamuzi mimi peke yangu na sio wale wasiokuwemo, na labda ikawapo sheria ya sisi kutotoka nje ingewakinga wengine kutopata vile vile wale wa nje kuwa salama kwao kwa kutotoka nje.... Kifupi nisingeoa kabisa na salama kwangu na wale wa nje!...
Utamaduni huu wa kuoa mdogo wa mke wako ni utaratibu wa baadhi makabila na wana kila sababu hna haki kama kabila kuendeleza wanaoyaamini, sii jukumu letu sisi kuwa judge kwani hata sisi ktk makabila yetu tuna mabaya. Hakuna utamaduni iliokuwa civilized ktk sura pana isipokuwa tunapojaribu kuchanganya tamaduni za mzungu kuwa ndio civilization...
Sasa nambie kuna mapungufu gani ktk familia ya Pinda kutokana na yeye kumwoa mdogo wake mkewe, na kama hakuna baya lililokwisha tokea, tuna base mjadala huu ktk vitu gani haswa.. Mbona wapo watu Tanzania wameoa first cousin. Waislaam kuoa wake wanne haya yote ukiyatazama kwa mtazamo wako yanaweza kuwa na madhara...hivyo, Nyerere, Mkapa, JK na Mwinyi hawakufaa kuwa marais kwa sababu tunaweza pata mapungufu yao ktk ngono ambazo tunazipa Ustaarabu wa kuchonga.