1.
Mkuu nadhani hapa unachanganya vitu kabisa...
Hukuweza kuona Salim akifanya kitu ktk madhifa gani kiasi kwamba unajaribu kumlinganisha na Sokoine..Sokoine ndiye aliyekuwa waziri mkuu wakati UDA ilipoanza (utaifishaji) na ndiye alikuwa waziri mkuu UDA ilipokufa hivyo alikuwa na ushindi gani ku replace Public transport na Daladala wakati tunaona nchi zote zilizoendelea zinatumia Public transport kama UDA tena karne hii ya Utandawazi..Je, to fail in one na kutafuta solution ya muda kujishikiza ambayo imekuwa ndio utaratibu kabisa ndio unaita ushindi? hivi kweli daladala ni ushindi mkubwa ktk kutatua swala la usafiri Dar! Je, linahusiana vipi na mafanikio ya waziri mkuu kitaifa!
Mkuu Bob,
Sokine ndiye aliyeanzisha usafiri wa Dala dala ambao to this day umekuwa one of the strengh ya effecency za katika wananchi wetu kufika kazini mapema au on time, kwa sababu ndio hasa sababu iliyomfanya Sokoine aaamue kuiruhusu dala dala, UDA na KAMATA, zilikuwa ni idea za Mwalimu. Taifa letu linaanzia makao makuu ya taifa, Darsalama, ndio mafanikio mengi ya kiongozi wa taifa, huanzia Darsalama na baadye kusambaa kwa taifa zima, lakini still unazo haki zote kama mwananchi kuyaona mafanikio ya Sokoine as you want, mimi kwenye hili ninasema kuwa Salim never did anything kwa taifa letu labda huko nje! Na kama ni ushujaa yeye ni shujaa wa Mwalimu, period!
2.
Salim aliposhika madaraka ya waziri mkuu ilikuwa ktk transition ya kutoka Ujamaa kuingia mfumo mpya wa Ubepari na ktk hili mkuu alishika mwaka mmoja tu tofauti na Sokoine aliyeshika awamu mbili tofauti kwa jumla ya miaka miine nmdani ya Ujamaa pamoja na kwamba maisha yake yalikatizwa..
Salim ameshika madaraka under Mwalimu, so was Sokoine, never under Mwalimu regime tuliwahi kuwa na transition ya kutoka ujamaa kwenda ubepari, lakini record za Sokoine ziko very clear as opposed na za Salim ambazo hazipo kabisa!
3.
Na kama alivyosema Zitto, hata baada ya kuondoka uwaziri mkuu bado alishika nafasi ya naibu waziri mkuu chini ya Warioba jambo ambalo linaonyesha wazi uzoefu wake ktk kazi hiyo kumsaidia Warioba. Na ni katika wakati huo Warioba aliweza ku shine.
Zitto ni kijana ambaye ameonyesha kufaa kwa siasa za taifa letu, muda wake mchache kwenye siasa zetu huwezi kulinganisha na muda wote wa Salim, kwa sababu angalau Zitto, ana a lot to show for than Salim, lakini pia Zitto, bado anahitaji darasa on historia ya siasa zetu, kumpenda Salim ni one thing, lakini kum-link Salim na siasa zetu local za taifa, ni another story of itself kwa sababu ukweli ni kwamba Salim hana uzoefu wowote na matatizo ya siasa zetu za bongo, zaidi tu ya kuwepo kwenye uongozi all his life kwa kubebwa na Mwalimu, hata Warioba naye ni hao hao waliokuwa wakibebwa na Mwalimu, lakini ilipofikia kusimama wenyewe they failed, sasa sisi wananchi hatuwezi kuwabeba wanasiasa wasioweza kusimama wenyewe, na bahati mbaya hayupo tena, kwa hiyo tutaendelea na wanasiasa kama kina Zitto, Slaa, Mwakyembe, Anne Kilango na wengineo ambao wako current with time, na wana uwezo wa kusimama ngangari na siasa zetu, huo usaidizi wa Salim kwa Warioba ulikuwa ni wa kupewa tu kama kawaida yake, na yule yule Mwalimu, aliyemhamishia OAU, sio sisi wananchi!
4.
Kisha hizi habari za UN mbona mnataka kuzipindisha kiasi hicho?..
Salim alikwenda UN mwaka 1976 na kukaa huko hadi early 80's hivyo swala la uongozi wake ndani ya Tanzania ilikuwa baada ya UN ndipo alishika nafasi za madaraka kama waziri mkuu na naibu, waziri wa Ulinzi na kadhalika hivyo mnaposema hizi habari za kupelekwa UN inaonyesha wazi mnajaribu kupotosha ukweli kama vile hakuwa nyumbani wakati wote.
Bob, usikasirike mkuu nothing personal hapa, Salim alikuwa Egypt alikopelekwa na Mwalimu akiwa ni his early 20s, na sio kwamba aligombea hiyo nafasi au kwamba kulikuwa na wa-Tanzania wengi wenye huo umri waliopewa nafasi kama yake nationally, na Mwalimu, yeye alikuwa special wa Mwalimu, na baadaye akamuhamishia UN ambako kwa kushirikiana na Russia with China, under siasa za dunia za Cold War, Salim akashamiri sana huko lakini sio kwenye siasa nyumbani ambazo bado aliendelea kuwa mgeni hadi leo hii, huu ni ukweli hakuna anayejaribu kupotosha anything, Salim bado ni mgeni kwa wa-Tanzania wengi kwa sababu ya either his arrogancy au uwezo mdogo wa uongozi wa siasa za national, kwani angeweza akafanya maajabu mengi sana kuliko Sokoine, lakini leo tunamkumbuka Sokoine, lakini sio Salim!
5.
Bila shaka mkuu, kiongozi yeyote anayekutana na matatizo ndio mnaweza kumwona zaidi kile alichokifanya tofauti na yule ambaye kila kitu kinakwenda sawa.. Huwezi ku account mazuri ya kiongozi kutokana na shida alizokutana nazo kama unavyuojaribu kumpamba Sokoine na ndicho nilichozungumza hapo juu kuwa yawezekana Pinda atakuja kumbukwa zaidi kutokana na matatizo tuliyokuwa nayo leo kuliko viongozi wengine waliotangulia..
Na hakuna mtu anayesema salim achukue urais isipokuwa anaweza sana kutoa mchango mkubwa ktk Tanzania ya kesho kwa sababu huyu mtu anafahamu jinsi mataifa makubwa wanavyofikiria kisha ni address nzuri kwa taifa letu nje... ana kila sifa za kiongozi kuwa shujaa wetu.
Angekuwa anafahamu mataifa makubwa yanavyofikiri, basi angweza kuwa katibu wa UN, ni kina Asha Migiro ndio wanaojua jinsi mataifa makubwa yanavyofikiria, mimi siamini kuwa Salim ana anything to offer kwa taifa letu, huyu akiwa Adis ameshindwa hata kuajiri sisi wa-Tanzania wenziwe kumsaidia kazi, lakini akaajiri watu wengi kutoka kwenye Arab World, halafu amekutwa na aibu nyingi sana kule ambazo hazisemwi tu hadharani akiwa Adis, na siwezi kuwa wa kwanza kuyasema hapa, Salim amelitumikia taifa letu vya kutosha, lakini akili ya kutuendeleza mbele ya hapa hana, kwanza yeye hatujui sisi wananchi wa Tanzania, na sisi hatumjui sasa atatuongoza vipi? Wanaomjua ni wananchi wa huko nje! Historia ya siasa yetu iko very clear kwamba Sokoine hana mpinzani!
6.
Mkuu mwenyewe unafahamu kuwa pamoja na kuwa wajamaa Tanzania bado tuliendelea kuheshimika na wala usijaribu kutudanganya kwamba Nyerere alikuwa na uwezo wa kumchagua Salim na kumpeleka UN kuwa - PRESIDENT wa UN SECURITY COUNCIL... mkuu hizi ni propaganda za hali ya juu sana dhidi ya Salim kwani Nyerere hakuwa na wala hawezi kuwa na madaraka hayo, na sidhani kama kuna mbongo yeyote anaweza pewa cheo hicho leo ama karne zijazo!
Acheni jamani kumpaka mtu tope hata kama hapendwi!
Mkuu Bob,
Hakuna nayepiga propaganda wala kupika hadithi, kwa sababu Salim sio contender sasa hivi wa anything bongo, sina sababu ya kumdanganya anyone hapa ila nina sababu za kusema ukweli nioujua juu ya Salim kwamba hana uwezo wa kuliongoza taifa letu, UN alipelekwa na Mwalimu, urais wa Security Council hata Balozi Mahiga juzi alikuwa, ni haki ya taifa letu kule kutokana na rotation za nafasi hiyo kwa kila nchi duniani ambayo ni member wa UN, lakini it has nothing to do na Salim kama kiongozi, ila alikuwa tu ni muwakilishi wetu kule ndio maana akawa this time Mahiga ndiye aliyekuwepo kule ndio maana akawaa, sasa uongo na hizo propaganda zinatoka wapi?
Hakuna anyempaka matope, ila rekodi yake kisiasa inampaka matope yeye mwenyewe na wale wanaoajribu kum-promote, kwamba uongozi wa kubebwa una faida na madhara yake, yanyomkuta sasa Salim ndio madahara yake, now this has nothing to do na kumpenda au kutompenda!