Who is Salim Ahmed Salim?

Who is Salim Ahmed Salim?

Dua,
Nadhani kichwa cha mada hii kilisema MASHUJAA WETU!..
sasa nashangaa watu wanapoanza kuunda hoja ya Salim kuwa rais kesho sijui imetoka wapi.
Pili huyu Dada Asha kama anavyozungumza sielewi anachotaka kufahamu ikiwa Salim alipokuwa madarakani pengine yeye alikuwa badoi hajazaliwa ama ndoa akivaa nepi...

Asha Abdala,
Record ya Salim kama inavyojieleza ktk miaka hiyo sidhani kama dada Asha unaweza kutuambia data za hata Nyerere mwenyewe between late 60 hadi 80's maanake maswala ya uhuru wa nchi za kiafrica huko South bado hamzikubali kuwa ni mchango wake mkubwa kwa Africa. Sasa nambie Kikwete ana mchango gani ktk bara Afrika hadi kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumuiya yetu..
Hivi kweli mtu kama J.J Mnyika a,mbaye kaanza siasa akiwa na umri mdogo mnaweza kutuambia mchango wake leo hii ktk Tanzania?... sidhani hata kidogo kwa sababu wadanganyika wengi hatufuatilii vitu zaidi ya kutazama nani kaleta mboga mezani. Nina hakika huwezi kunambia mchango wa Mnyika ama kiongozi yeyote yule ktk taifa letu na Africa kiasi kwamba Wadanganyika wanaweza kubaliana na wewe mia kwa mia.
Samahani, lakini hiki ndicho nilichojifunza kuhusu Wadanganyika! hakuna mbora isipokuwa yule anayeubeba msalaba kwa ajili yetu..
Bahati mbaya ni kwamba hatuna Uhuru kamili hadi leo kwa hiyo bado tunamtafuta David ambaye ataweza kupambana na jitu hili la kutisha - CCM.

Komredi Mkandara:

Kuna mtu anaitwa Konrad Hermann Josef Adenauer. Alikuwa Chancellor wa kwanza wa serikali ya Ujerumani Magharibi baada ya vita vya pili vya dunia. Alichukuwa u-Chancellor akiwa na miaka 73 na aliongoza kwa miaka 13 na kuleta mabadiliko makubwa.

Ni afadhari mtu awe mzee kiumri lakini kijana katika kufikiri na kutenda kazi kuliko kuwa kijana wa umri lakini mzee wa kufikiri au kutenda kazi.
 
Field Marshall Es,
Mkuu nadhani hapa unachanganya vitu kabisa...
Hukuweza kuona Salim akifanya kitu ktk madhifa gani kiasi kwamba unajaribu kumlinganisha na Sokoine..

Sokoine ndiye aliyekuwa waziri mkuu wakati UDA ilipoanza (utaifishaji) na ndiye alikuwa waziri mkuu UDA ilipokufa hivyo alikuwa na ushindi gani ku replace Public transport na Daladala wakati tunaona nchi zote zilizoendelea zinatumia Public transport kama UDA tena karne hii ya Utandawazi..Je, to fail in one na kutafuta solution ya muda kujishikiza ambayo imekuwa ndio utaratibu kabisa ndio unaita ushindi? hivi kweli daladala ni ushindi mkubwa ktk kutatua swala la usafiri Dar! Je, linahusiana vipi na mafanikio ya waziri mkuu kitaifa!

Salim aliposhika madaraka ya waziri mkuu ilikuwa ktk transition ya kutoka Ujamaa kuingia mfumo mpya wa Ubepari na ktk hili mkuu alishika mwaka mmoja tu tofauti na Sokoine aliyeshika awamu mbili tofauti kwa jumla ya miaka miine nmdani ya Ujamaa pamoja na kwamba maisha yake yalikatizwa..

Na kama alivyosema Zitto, hata baada ya kuondoka uwaziri mkuu bado alishika nafasi ya naibu waziri mkuu chini ya Warioba jambo ambalo linaonyesha wazi uzoefu wake ktk kazi hiyo kumsaidia Warioba. Na ni katika wakati huo Warioba aliweza ku shine.
Kisha hizi habari za UN mbona mnataka kuzipindisha kiasi hicho?

Salim alikwenda UN mwaka 1976 na kukaa huko hadi early 80's hivyo swala la uongozi wake ndani ya Tanzania ilikuwa baada ya UN ndipo alishika nafasi za madaraka kama waziri mkuu na naibu, waziri wa Ulinzi na kadhalika hivyo mnaposema hizi habari za kupelekwa UN inaonyesha wazi mnajaribu kupotosha ukweli kama vile hakuwa nyumbani wakati wote.

Bila shaka mkuu, kiongozi yeyote anayekutana na matatizo ndio mnaweza kumwona zaidi kile alichokifanya tofauti na yule ambaye kila kitu kinakwenda sawa.. Huwezi ku account mazuri ya kiongozi kutokana na shida alizokutana nazo kama unavyuojaribu kumpamba Sokoine na ndicho nilichozungumza hapo juu kuwa yawezekana Pinda atakuja kumbukwa zaidi kutokana na matatizo tuliyokuwa nayo leo kuliko viongozi wengine waliotangulia..

Na hakuna mtu anayesema salim achukue urais isipokuwa anaweza sana kutoa mchango mkubwa ktk Tanzania ya kesho kwa sababu huyu mtu anafahamu jinsi mataifa makubwa wanavyofikiria kisha ni address nzuri kwa taifa letu nje... ana kila sifa za kiongozi kuwa shujaa wetu.

Mkuu mwenyewe unafahamu kuwa pamoja na kuwa wajamaa Tanzania bado tuliendelea kuheshimika na wala usijaribu kutudanganya kwamba Nyerere alikuwa na uwezo wa kumchagua Salim na kumpeleka UN kuwa - PRESIDENT wa UN SECURITY COUNCIL... mkuu hizi ni propaganda za hali ya juu sana dhidi ya Salim kwani Nyerere hakuwa na wala hawezi kuwa na madaraka hayo, na sidhani kama kuna mbongo yeyote anaweza pewa cheo hicho leo ama karne zijazo!
Acheni jamani kumpaka mtu tope hata kama hapendwi!
 
3. Salim amebebwa mno na Mwalimu, mpaka one has to wonder why? Aliyempeleka OAU ni Mwalimu, kwa kumtumia Mandela, baada ya kuona kuwa viongozi wengi wa CCM hawamtaki na walikuwa na sababu za msingi, ninasema Salim ni arrogant asingekuwa basi ange-humble himself na kujaribu ku-deal na his political past, lakini arrogantly, akaamua kumuamini Mwalimu tu kuwa siku zote atamsaidia, kwani sio siri kuwa Salim alihusika na siasa za Babu, na ni Babu personally na agenda zake ndiye aliyempeleka Salim na kina Mahafudhi kusomea u-Komandoo Cuba, ili warudi bongo one day na kuiondoa serikali ya mapinduzi visiwani and it happened, ingawa serikali kule haikuondolewa, sasa je Salim alihusika? sijui lakini ninajua kuwa kati ya aliokwenda nao Cuba kuna waliohusika including Babu mwenyewe, sasa haya sio majungu na CIA walikuwa wanayajua haya yote!

Mkuu kumbe Salim alisomea Ukomadoo!!, kwa hiyo Salim ni Komandoo au hakumaliza mafunzo ?
 
Wapendwa wana JF,
Nimeupenda sana mjadala huu,sio tu kwa sababu ya anayetajwa bali pia haja ya kutajwa kwake wakati huu.
Taifa letu,kama yalivyo mataifa mengine yaitwayo yanayoendelea, liko safarini kuelekea katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kwa bahati mabaya safari hii imekuwa ngumu na imesuasua sana. Ni jambo linalofurahisha kwamba, nyuma ya majadala huu naweza kuona jinsi watanzania tulivyotambua kwamba sababu kubwa ya kudorora kwa safari yetu ni uongozi dhaifu.

Kumbe tunao wajibu hapa wa kuhakikisha ijapo fursa nyingine ya uchaguzi hatutachukua risk ya kuacha watu wajitokeze tu (na kuuzia mbuzi kwenye gunia) bila sisi wenyewe kutambua na mapema nani atatupeleka tunapopataka.

Ni heri basi mjadala huu ukitufikisha mahali ambapo tunaweza kusema naam,SAS is the best we have, au tumtafute mwingine. itafaa pia tusiishie kuidentify, bali tufike mahali tutumie mamlaka tuliyonayo kumtuma kazi tunayomtaka aifanye (sisi wananchi ndio waajiri wa rais).

Mimi ni mmojawapo wa wenye imani na SAS, lakini nashawishika pia kwamba yeye peke yake hatoshi kuharakisha safari yetu. Kwa hiyo;
Naunga mkono combination ya SAS na SLAA
 
Asha,
What has Kikwete done for us kwa miaka yote aliyokuwa waziri wa mambo ya nje au ameifanyia nini Africa katika kipindi hicho? ABSOLUTE NOTHING!!!!

Lunyungu, Kusema Salim hakusaidia kuzuia Genocide ya Rwanda..inabidi tuangalie mfumo wa OAU ulivyokuwa isitoshe hawakuwa na makali yoyote ya kuintervene kijeshi but guess what? katibu mkuu wa UN kipindi hicho alikuwa anatokea Afrika(Boutros Boutros Ghali) what did he do? NOTHING!!!

Kuhusu yeye kuzungumzia ufisadi, si tumeona kila kiongozi aliyejaribu kuzungumzia tumempa majina ya kila aina..Kuanzia Butiku hadi Kawawa juzi...kwenye hili mimi naona bora akae kimya tuu manaa kwa CCM ilvyo lazima watasema anataka umaarufu kupitia issue za mafisadi and blah blah.
 
Mkuu Bob,

3. Salim amebebwa mno na Mwalimu, mpaka one has to wonder why? Aliyempeleka OAU ni Mwalimu, kwa kumtumia Mandela, baada ya kuona kuwa viongozi wengi wa CCM hawamtaki na walikuwa na sababu za msingi, ninasema Salim ni arrogant asingekuwa basi ange-humble himself na kujaribu ku-deal na his political past, lakini arrogantly, akaamua kumuamini Mwalimu tu kuwa siku zote atamsaidia, kwani sio siri kuwa Salim alihusika na siasa za Babu, na ni Babu personally na agenda zake ndiye aliyempeleka Salim na kina Mahafudhi kusomea u-Komandoo Cuba, ili warudi bongo one day na kuiondoa serikali ya mapinduzi visiwani and it happened, ingawa serikali kule haikuondolewa, sasa je Salim alihusika? sijui lakini ninajua kuwa kati ya aliokwenda nao Cuba kuna waliohusika including Babu mwenyewe, sasa haya sio majungu na CIA walikuwa wanayajua haya yote!

Field Marshall E.

Ukinipa nafasi yoyote ya kazi Tanzania. Nitaifanya vizuri tu lakini ninakuakikishia kuwa utapokea malalamiko kuwa mimi ni ARROGANT.

Viongozi wa juu wa Tanzania hawajuhi kufanya kazi na kumsingizia mtu anayefanya kazi kwa kufuata taratibu za kazi, kufika kazini mapema ARROGANT au mkoloni ni kitu cha kawaida.
 
Icadon,
Kuhusu yeye kuzungumzia ufisadi, si tumeona kila kiongozi aliyejaribu kuzungumzia tumempa majina ya kila aina..Kuanzia Butiku hadi Kawawa juzi...kwenye hili mimi naona bora akae kimya tuu manaa kwa CCM ilvyo lazima watasema anataka umaarufu kupitia issue za mafisadi and blah blah

Kisha basi Salim ana nafasi gani ndani ya chama na nje serikalini? atachekwa kama Warioba majuzi alipojitokeza makada wa CCM wakaanza kufufua visa vyake hali issue ilikuwa ni mafisadi ndani ya uongozi uliopo.

Tatizo kubwa letu sisi Watanzania ni pale tunapojenga hoja ya YESU kuwa mwenye kulaani awe wa kwanza kutupa jiwe!

hali tunashindwa kabisa kuelewa walioambiwa maneno hayo walikuwa wanaume wenye kuyatenda haya.
Salim hana nafasi ya uobngozi ndani ya serikali ya CCM jambo ambalo tumeshindwa kabisa kujiuliza WHY?....guys huyu jama aliwahi kuwa PRESIDENT wa UN suricury council sio sifa ya mchezo kabisa.

Maswala ya Rwanda inajulikana vizuri jihihada za Mwalimu na Salim kuwaweka hapa jamaa kiti kimoja isipokuwa M7 na watu wake walikuwa na agenda zao. Je, mlitaka tuvamie Rwanda na jeshi la wapi UN, OAU ama Tanzania, maanake sielewi lawama hizi zilimtaka Salim afanye kitu gani.
 
wandugu,

..Raisi wa UN-Security Council ni nafasi ya mzunguko kwa wananchama wa UN.

..Nchi ikipata nafasi ya kuingia Security Council basi Balozi wa nchi husika ana nafasi ya kuwa Raisi wa Security Council. Tena nadhani..nadhani, nafasi ya Uraisi huwa ni suala la mwezi mmoja tu.

..Tangu Uhuru Tanzania tumepata nafasi ya kuwa kwenye security council mara 2. Katika vipindi hivyo mabalozi wetu walikuwa Salim Salim, na Dr.Mahiga. Wote walipata heshima ya ku-serve kama maraisi wa Security Council.

..Tanzania tulipigana sana ili China ijiunge UN na zaidi iwe permanent member wa security council.

..Watanzania waliamini kwamba Salim Salim ni mgombea wao kuwa SG UN. lakini nchi za magharibi zilimuona kama mgombea wa China na nchi zenye mlengo wa kushoto.

..Kwa kifupi candidacy ya Salim Salim kuwa UN SG, na kushindwa kwake, haielezei uwezo wake, wala mapungufu yake. How close he got to become the UN SG, na kushindwa kwake, kunaelezea zaidi siasa za vita baridi zilizokuwa zikiendelea wakati ule.

NB:

..Kenya walikuwa na nafasi either ya kuingia UN Security Council, au kuwa Raisi wa SC, lakini for some reasons hawakuchukua nafasi hiyo.

..Kwa kifupi mimi naona haya masuala ya diplomacy yanatugharimu mno Watanzania. Hebu fikiria ziara za Raisi Kikwete kama mwenyekiti wa AU zinatugharimu kiasi gani. Chunguza ziara ya Mwalimu Nyerere kuzunguka dunia nzima ku-promote South-South ilitugharimu kiasi gani.

..Mimi nafikiri Tanzania inahitaji Raisi ambaye hatajaribu to fit into Nyerere shoes when it comes to world politics and international diplomacy.

..Tanzania tulipata kuitwa na "Mecca of Africa's liberation."

..Katika zama hizi mpya tunahitaji kuwa "Mecca" ya nyanja tofauti kama viwanda, kilimo, uvuvi, mabenki, bandari, elimu ya Juu, sayansi etc etc.
 
Icadon,
..
Kisha basi Salim ana nafasi gani ndani ya chama na nje serikalini?..atachekwa kama Warioba majuzi alipojitokeza makada wa CCM wakaanza kufufua visa vyake hali issue ilikuwa ni mafisadi ndani ya uongozi uliopo.
Tatizo kubwa letu sisi Watanzania ni pale tunapojenga hoja ya YESU kuwa mwenye kulaani awe wa kwanza kutupa jiwe!..
hali tunashindwa kabisa kuelewa walioambiwa maneno hayo walikuwa wanaume wenye kuyatenda haya.
Salim hana nafasi ya uobngozi ndani ya serikali ya CCM jambo ambalo tumeshindwa kabisa kujiuliza WHY?....guys huyu jama aliwahi kuwa PRESIDENT wa UN suricury council sio sifa ya mchezo kabisa... Maswala ya Rwanda inajulikana vizuri jihihada za Mwalimu na Salim kuwaweka hapa jamaa kiti kimoja isipokuwa M7 na watu wake walikuwa na agenda zao... Je, mlitaka tuvamie Rwanda na jeshi la wapi UN, OAU ama Tanzania.. maanake sielewi lawama hizi zilimtaka Salim afanye kitu gani.

Nabii apokelewa nyumbani kwake. Yule si mtoto wa seremala tu.
 
wandugu,

..Raisi wa UN-Security Council ni nafasi ya mzunguko kwa wananchama wa UN.

..Nchi ikipata nafasi ya kuingia Security Council basi Balozi wa nchi husika ana nafasi ya kuwa Raisi wa Security Council. Tena nadhani..nadhani, nafasi ya Uraisi huwa ni suala la mwezi mmoja tu.

..Tangu Uhuru Tanzania tumepata nafasi ya kuwa kwenye security council mara 2. Katika vipindi hivyo mabalozi wetu walikuwa Salim Salim, na Dr.Mahiga. Wote walipata heshima ya ku-serve kama maraisi wa Security Council.

..Tanzania tulipigana sana ili China ijiunge UN na zaidi iwe permanent member wa security council.

..Watanzania waliamini kwamba Salim Salim ni mgombea wao kuwa SG UN. lakini nchi za magharibi zilimuona kama mgombea wa China na nchi zenye mlengo wa kushoto.

..Kwa kifupi candidacy ya Salim Salim kuwa UN SG, na kushindwa kwake, haielezei uwezo wake, wala mapungufu yake. How close he got to become the UN SG, na kushindwa kwake, kunaelezea zaidi siasa za vita baridi zilizokuwa zikiendelea wakati ule.

NB:

..Kenya walikuwa na nafasi either ya kuingia UN Security Council, au kuwa Raisi wa SC, lakini for some reasons hawakuchukua nafasi hiyo.

..Kwa kifupi mimi naona haya masuala ya diplomacy yanatugharimu mno Watanzania. Hebu fikiria ziara za Raisi Kikwete kama mwenyekiti wa AU zinatugharimu kiasi gani. Chunguza ziara ya Mwalimu Nyerere kuzunguka dunia nzima ku-promote South-South ilitugharimu kiasi gani.

..Mimi nafikiri Tanzania inahitaji Raisi ambaye hatajaribu to fit into Nyerere shoes when it comes to world politics and international diplomacy.

..Tanzania tulipata kuitwa na "Mecca of Africa's liberation."

..Katika zama hizi mpya tunahitaji kuwa "Mecca" ya nyanja tofauti kama viwanda, kilimo, uvuvi, mabenki, bandari, elimu ya Juu, sayansi etc etc.

Hayo mambo ya ku-fit Nyerere shoes sitaki kusikia. Mtaturudisha kwenye enzi ya kubweka kwenye majukwaa ya kimataifa wakati ndani ya nchi hakuna kitu kinachoendelea.

Kinachotakiwa sasa ni decentralization na kufanya taasisi zingine za umma kama bunge, wakuu wa mikoa au wilaya kuwa na professionals watakaofanya kazi kwa kuwajibika.
 
Badohamna mtu aliyejibu achievements zake kwa mwananchi wa Tanzania (bara au zanzibar)...kazi yake ni ya kiheshima and he is a career diplomat, just as Kikwete has been a career politician but with poor results,

Salim kuamuru wanaovaa magunia waletewe mitumba quite frankly is not something i can count as a significant achievement.

I need to see an attribute of development that can be directly linked to Dr. Salim,

we have seen what happens when you elect a Public face without measuring their deeds. Dr. Salim was atthe OAU at the timewhere we witnessed some of the Worst atrocities this continent has everseen...maybe he was just powerless, maybe he tried...but i need a link,amemsaidiaje mzanzibari au mtanzania bara mwenzake since (whether as a diplomat or a politician or even as a retiree)
 
1.
Mkuu nadhani hapa unachanganya vitu kabisa...
Hukuweza kuona Salim akifanya kitu ktk madhifa gani kiasi kwamba unajaribu kumlinganisha na Sokoine..Sokoine ndiye aliyekuwa waziri mkuu wakati UDA ilipoanza (utaifishaji) na ndiye alikuwa waziri mkuu UDA ilipokufa hivyo alikuwa na ushindi gani ku replace Public transport na Daladala wakati tunaona nchi zote zilizoendelea zinatumia Public transport kama UDA tena karne hii ya Utandawazi..Je, to fail in one na kutafuta solution ya muda kujishikiza ambayo imekuwa ndio utaratibu kabisa ndio unaita ushindi? hivi kweli daladala ni ushindi mkubwa ktk kutatua swala la usafiri Dar! Je, linahusiana vipi na mafanikio ya waziri mkuu kitaifa!

Mkuu Bob,

Sokine ndiye aliyeanzisha usafiri wa Dala dala ambao to this day umekuwa one of the strengh ya effecency za katika wananchi wetu kufika kazini mapema au on time, kwa sababu ndio hasa sababu iliyomfanya Sokoine aaamue kuiruhusu dala dala, UDA na KAMATA, zilikuwa ni idea za Mwalimu. Taifa letu linaanzia makao makuu ya taifa, Darsalama, ndio mafanikio mengi ya kiongozi wa taifa, huanzia Darsalama na baadye kusambaa kwa taifa zima, lakini still unazo haki zote kama mwananchi kuyaona mafanikio ya Sokoine as you want, mimi kwenye hili ninasema kuwa Salim never did anything kwa taifa letu labda huko nje! Na kama ni ushujaa yeye ni shujaa wa Mwalimu, period!

2.
Salim aliposhika madaraka ya waziri mkuu ilikuwa ktk transition ya kutoka Ujamaa kuingia mfumo mpya wa Ubepari na ktk hili mkuu alishika mwaka mmoja tu tofauti na Sokoine aliyeshika awamu mbili tofauti kwa jumla ya miaka miine nmdani ya Ujamaa pamoja na kwamba maisha yake yalikatizwa..

Salim ameshika madaraka under Mwalimu, so was Sokoine, never under Mwalimu regime tuliwahi kuwa na transition ya kutoka ujamaa kwenda ubepari, lakini record za Sokoine ziko very clear as opposed na za Salim ambazo hazipo kabisa!

3.
Na kama alivyosema Zitto, hata baada ya kuondoka uwaziri mkuu bado alishika nafasi ya naibu waziri mkuu chini ya Warioba jambo ambalo linaonyesha wazi uzoefu wake ktk kazi hiyo kumsaidia Warioba. Na ni katika wakati huo Warioba aliweza ku shine.

Zitto ni kijana ambaye ameonyesha kufaa kwa siasa za taifa letu, muda wake mchache kwenye siasa zetu huwezi kulinganisha na muda wote wa Salim, kwa sababu angalau Zitto, ana a lot to show for than Salim, lakini pia Zitto, bado anahitaji darasa on historia ya siasa zetu, kumpenda Salim ni one thing, lakini kum-link Salim na siasa zetu local za taifa, ni another story of itself kwa sababu ukweli ni kwamba Salim hana uzoefu wowote na matatizo ya siasa zetu za bongo, zaidi tu ya kuwepo kwenye uongozi all his life kwa kubebwa na Mwalimu, hata Warioba naye ni hao hao waliokuwa wakibebwa na Mwalimu, lakini ilipofikia kusimama wenyewe they failed, sasa sisi wananchi hatuwezi kuwabeba wanasiasa wasioweza kusimama wenyewe, na bahati mbaya hayupo tena, kwa hiyo tutaendelea na wanasiasa kama kina Zitto, Slaa, Mwakyembe, Anne Kilango na wengineo ambao wako current with time, na wana uwezo wa kusimama ngangari na siasa zetu, huo usaidizi wa Salim kwa Warioba ulikuwa ni wa kupewa tu kama kawaida yake, na yule yule Mwalimu, aliyemhamishia OAU, sio sisi wananchi!

4.
Kisha hizi habari za UN mbona mnataka kuzipindisha kiasi hicho?..
Salim alikwenda UN mwaka 1976 na kukaa huko hadi early 80's hivyo swala la uongozi wake ndani ya Tanzania ilikuwa baada ya UN ndipo alishika nafasi za madaraka kama waziri mkuu na naibu, waziri wa Ulinzi na kadhalika hivyo mnaposema hizi habari za kupelekwa UN inaonyesha wazi mnajaribu kupotosha ukweli kama vile hakuwa nyumbani wakati wote.

Bob, usikasirike mkuu nothing personal hapa, Salim alikuwa Egypt alikopelekwa na Mwalimu akiwa ni his early 20s, na sio kwamba aligombea hiyo nafasi au kwamba kulikuwa na wa-Tanzania wengi wenye huo umri waliopewa nafasi kama yake nationally, na Mwalimu, yeye alikuwa special wa Mwalimu, na baadaye akamuhamishia UN ambako kwa kushirikiana na Russia with China, under siasa za dunia za Cold War, Salim akashamiri sana huko lakini sio kwenye siasa nyumbani ambazo bado aliendelea kuwa mgeni hadi leo hii, huu ni ukweli hakuna anayejaribu kupotosha anything, Salim bado ni mgeni kwa wa-Tanzania wengi kwa sababu ya either his arrogancy au uwezo mdogo wa uongozi wa siasa za national, kwani angeweza akafanya maajabu mengi sana kuliko Sokoine, lakini leo tunamkumbuka Sokoine, lakini sio Salim!

5.
Bila shaka mkuu, kiongozi yeyote anayekutana na matatizo ndio mnaweza kumwona zaidi kile alichokifanya tofauti na yule ambaye kila kitu kinakwenda sawa.. Huwezi ku account mazuri ya kiongozi kutokana na shida alizokutana nazo kama unavyuojaribu kumpamba Sokoine na ndicho nilichozungumza hapo juu kuwa yawezekana Pinda atakuja kumbukwa zaidi kutokana na matatizo tuliyokuwa nayo leo kuliko viongozi wengine waliotangulia..
Na hakuna mtu anayesema salim achukue urais isipokuwa anaweza sana kutoa mchango mkubwa ktk Tanzania ya kesho kwa sababu huyu mtu anafahamu jinsi mataifa makubwa wanavyofikiria kisha ni address nzuri kwa taifa letu nje... ana kila sifa za kiongozi kuwa shujaa wetu.

Angekuwa anafahamu mataifa makubwa yanavyofikiri, basi angweza kuwa katibu wa UN, ni kina Asha Migiro ndio wanaojua jinsi mataifa makubwa yanavyofikiria, mimi siamini kuwa Salim ana anything to offer kwa taifa letu, huyu akiwa Adis ameshindwa hata kuajiri sisi wa-Tanzania wenziwe kumsaidia kazi, lakini akaajiri watu wengi kutoka kwenye Arab World, halafu amekutwa na aibu nyingi sana kule ambazo hazisemwi tu hadharani akiwa Adis, na siwezi kuwa wa kwanza kuyasema hapa, Salim amelitumikia taifa letu vya kutosha, lakini akili ya kutuendeleza mbele ya hapa hana, kwanza yeye hatujui sisi wananchi wa Tanzania, na sisi hatumjui sasa atatuongoza vipi? Wanaomjua ni wananchi wa huko nje! Historia ya siasa yetu iko very clear kwamba Sokoine hana mpinzani!

6.
Mkuu mwenyewe unafahamu kuwa pamoja na kuwa wajamaa Tanzania bado tuliendelea kuheshimika na wala usijaribu kutudanganya kwamba Nyerere alikuwa na uwezo wa kumchagua Salim na kumpeleka UN kuwa - PRESIDENT wa UN SECURITY COUNCIL... mkuu hizi ni propaganda za hali ya juu sana dhidi ya Salim kwani Nyerere hakuwa na wala hawezi kuwa na madaraka hayo, na sidhani kama kuna mbongo yeyote anaweza pewa cheo hicho leo ama karne zijazo!
Acheni jamani kumpaka mtu tope hata kama hapendwi!

Mkuu Bob,

Hakuna nayepiga propaganda wala kupika hadithi, kwa sababu Salim sio contender sasa hivi wa anything bongo, sina sababu ya kumdanganya anyone hapa ila nina sababu za kusema ukweli nioujua juu ya Salim kwamba hana uwezo wa kuliongoza taifa letu, UN alipelekwa na Mwalimu, urais wa Security Council hata Balozi Mahiga juzi alikuwa, ni haki ya taifa letu kule kutokana na rotation za nafasi hiyo kwa kila nchi duniani ambayo ni member wa UN, lakini it has nothing to do na Salim kama kiongozi, ila alikuwa tu ni muwakilishi wetu kule ndio maana akawa this time Mahiga ndiye aliyekuwepo kule ndio maana akawaa, sasa uongo na hizo propaganda zinatoka wapi?

Hakuna anyempaka matope, ila rekodi yake kisiasa inampaka matope yeye mwenyewe na wale wanaoajribu kum-promote, kwamba uongozi wa kubebwa una faida na madhara yake, yanyomkuta sasa Salim ndio madahara yake, now this has nothing to do na kumpenda au kutompenda!
 
Badohamna mtu aliyejibu achievements zake kwa mwananchi wa Tanzania (bara au zanzibar)...kazi yake ni ya kiheshima and he is a career diplomat, just as Kikwete has been a career politician but with poor results,

Salim kuamuru wanaovaa magunia waletewe mitumba quite frankly is not something i can count as a significant achievement.

I need to see an attribute of development that can be directly linked to Dr. Salim,

we have seen what happens when you elect a Public face without measuring their deeds. Dr. Salim was atthe OAU at the timewhere we witnessed some of the Worst atrocities this continent has everseen...maybe he was just powerless, maybe he tried...but i need a link,amemsaidiaje mzanzibari au mtanzania bara mwenzake since (whether as a diplomat or a politician or even as a retiree)
Kama alivyodokeza Mhe.Zitto, muda wake katika nafasi kubwa ya madaraka na wajibu wa nyumbani ulikuwa mfupi sana alichoweza kufanya katika huo muda mfupi (miaka ya 1980) kimetajwa.
Nadhani Mwalimu hakumpendelea tu kijana Salim(22) bali aliuona na kuutambua uwezo wake. kadhalika hata mataifa ya nje yaliutambua uwezo huo, vinginevyo wangekuwa wana lao jambo kumpa majukumu mazito sana katika umri mdogo.
Angalia alipewa majukumu gani na alishiriki shughuli zipi katika umri wa miaka 30 tu;

• While serving at the United Nations, he was Chairman of the United Nations Special Mission to Niue in June/July 1972;
• Drafting Committee Chairman of the Political Committee of the Ministerial Conference of Non-Aligned States, Georgetown, Guyana (August 1972);
• Chairman of the Political Committee of the International Conference of Experts in Support of the Victims of Colonialism and Apartheid in southern Africa, Oslo (April 1973);
• 1975 Chairman of the Security Council's Committee on Sanctions against Southern Rhodesia;
• President of the Security Council (January 1976);
• Chairman of the high-level Ad HOC Group of the Special Committee of 24 visiting the United Kingdom, the United Republic of Tanzania, Zambia, Botswana, Mozambique and Ethiopia (April/May 1976);
• Chairman of the Drafting Committee of the Fifth Conference of Heads of State or Government of the non-Aligned States, Colombo (August1976),
• and Vice-President of the International Conference in support of the people of Zimbabwe arid Namibia and Chairman of the Committee of the Whole of that Conference, held in Maputo, Mozambique (may 1977).
Since his appointment as Ambassador at the United Nations he has attended the following:
• Pacem en Maribus, Valleta, Malta (May 1970);
• Governing Council of the United Nations Development Programme (UNDP), Geneva (June 1970);
• Liberation Committee session, Algiers (July 1970);
• OAU Assembly of Heads of State or Government, Addis Ababa (September 1970);
• United Nations Security Council meeting, Addis Ababa (January /February 1972);
• Preparatory Committee Meetings of Non-Aligned States, Georgetown (February 1972),
• Kuala Lumpur (Mat 1972) and Kabul (May 1973); OAU Liberation Committee session, Accra (January 1973);
• United Nations Security Council meeting, Panama City (March 1973);
• Tenth Ordinary Session of the OAU Assembly of Heads of State or Government, Addis Ababa (May 1973);
• Fourth Summit Conference of Non-Aligned States, Algiers (September 1973); world Congress of Peace Forces, Moscow (October 1973) ;
• Co-ordinating Bureau of Non-Aligned Sates, Algiers (March 1974) ;
• OAU Liberation Committee session, Dar es Salaam (January 1975);
• Meeting of Co-ordinating Bureau of the Non-Aligned States, Havana (March 1975);
• Extraordinary Session of OAU Council of Ministers, Dar es Salaam (April 1175);
• Commonwealth Heads of Government Conference, Kingston (May 1975);
• International Seminar on the Eradication of Apartheid and in Support of the Struggle for Liberation in South Africa, Havana (May 1976);
• Co-ordinating Bureau of Non-Aligned States, Algiers (May/June 1976);
• Thirteenth Ordinary Session of the OAU Assembly of Heads of State or Government, Port Louis Mauritius (July 1976);
• Head of Tanzanian observer delegation to the Geneva Conference on Southern Rhodesia (October/December 1976);
• First Afro-Arab Summit Conference, Cairo (March 1977);
• Co-ordinating Bureau of Non-Aligned States, New Delhi (April 1977);
• Twenty-Ninth Ordinary Session of the OAU Liberation Committee and of the OAU Council of Ministers, Libreville (June 1977);
• Fourteenth Ordinary Session of the OAU Assembly of Heads of State or Government, Libreville (July 1977);
• World Conference for Action against Apartheid, Lagos (August 1977);
• Fifteenth Ordinary Session of the OAU Assembly of Heads of State or Government, Khartoum (July 1978); session of the OAU Liberation Committee, (June 1979);
• Tenth Ordinary Session of the OAU Assembly of Heads of State or Government, Monrovia (June 1979);
• and the Sixth Conference of Heads of State or Government of the Non-Aligned States, Havana (September 1979).
 
Ukinipa nafasi yoyote ya kazi Tanzania. Nitaifanya vizuri tu lakini ninakuakikishia kuwa utapokea malalamiko kuwa mimi ni ARROGANT. Viongozi wa juu wa Tanzania hawajuhi kufanya kazi na kumsingizia mtu anayefanya kazi kwa kufuata taratibu za kazi, kufika kazini mapema ARROGANT au mkoloni ni kitu cha kawaida.

Mimi binafsi ninamuita Salim kuwa ni arrogant, kwa sababu baada ya kushindwa uchaguzi wa rais Dodoma, akakasirika na kusema kwamba hataki tena siasa za bongo, na kwamba hataki tena hata kuonana na Mkapa, sasa hii kweli inaweza kuwa ni sprit ya a good politician kwa taifa letu?

Hata baada ya kushindwa kwenye uchaguzi, bado Malecela alikubali kumsaidia Salim dakika za mwisho, yaaani siku mbili za mwisho, ambazo zilimsaidia Salim kuweza hata kupata zile kura 500, pamoja na all the nasty kampeni ambazo Salim alikuwa amezifanya behind the scene against Malecela, ikiwa ni pamoja na kumuandika kakitabu kachafu ambako kalikuwa traced kwake Salim, alikoka-print from London, lakini akajaribu kukifanya kionekane kimeandikwa na Kiwete, confronted with facts akashindwa cha kusema, lakini aliposhindwa tu ule uchaguzi akamkasirikia kila mtu, badala ya kujikasirikia mwenyewe, kwamba hana tu uwezo wa kuwa rais wa bongo, kwa sababu kuwa na uwezo huo ni pamoja na kushinda ile mizengwe ya ndani ya CCM,

Kuingia kwenye uchaguzi ukashindwa na kuleta hasira, maana yake ni moja tu kwamba wewe ni arrogant uliyeamini kuwa utashinda tu maana wewe una akili sana kuliko wagombea wengine, hatuhitaji viongozi wa namna hii bongo, Love or hate him, Kikwete alishinda uchaguzi wa rais, labda anayo mapungufu kwenye uongozi wake kitu ambacho ni wazi kwa marais wote waliowahi kututawala. Salim baada ya kushindwa alitakiwa kusimama kidete na kuanza kujitayarisha na uchaguzi ujao, sio kukimbilia Abuja!

tha man is arrogant!
 
1.
Kama alivyodokeza Mhe.Zitto, muda wake katika nafasi kubwa ya madaraka na wajibu wa nyumbani ulikuwa mfupi sana alichoweza kufanya katika huo muda mfupi (miaka ya 1980) kimetajwa.
Nadhani Mwalimu hakumpendelea tu kijana Salim(22) bali aliuona na kuutambua uwezo wake.

Mkuu heshima mbele, Mwalimu alionea wapi uwezo wa Salim akiwa na miaka 22? Kwani kwenye hiyo miaka 22 alikuwa amewahi kufanya nini kwa taifa na akiwa kwenye nafasi ipi? Nijuavyo mimi ni kwamba Salim, alijihusisha na siasa za Sultani na Weusi huko Visiwani, na Mwalimu alimuokoa tu kabla hajapewa dharuba za hizo siasa,

Halafu wakuu acheni kututisha na jina la Zitto, naona linatolewa na kila mchangiaji anayemuunga mkono Salim, na uongozi wake wa kubebwa na Mwalimu, akisema Zitto haina maana basi ndio authority kwenye ishu, cha muhimu ni hoja, swali langu kwako mkulu ni vipi wa-Tanzania wengine waliokuwa in their 20s hawakuchaguliwa na kupewa na nafasi na Mwalimu, kama Salim?

2.
kadhalika hata mataifa ya nje yaliutambua uwezo huo, vinginevyo wangekuwa wana lao jambo kumpa majukumu mazito sana katika umri mdogo. Angalia alipewa majukumu gani na alishiriki shughuli zipi katika umri wa miaka 30 tu;

Hili mkuu hatulikatai, ni kweli alifanya mengi mazito huko nje ambako ndiko hasa anakoheshimika, lakini kwa bahati mbaya hakutufanyia lolote bongo ndio maana hatuwezi kumpa uongozi wa juu kama urais kwa sababu hatumjui kama anvyojulikana huko nje!
 
1.

Mkuu heshima mbele, Mwalimu alionea wapi uwezo wa Salim akiwa na miaka 22? Kwani kwenye hiyo miaka 22 alikuwa amewahi kufanya nini kwa taifa na akiwa kwenye nafasi ipi? Nijuavyo mimi ni kwamba Salim, alijihusisha na siasa za Sultani na Weusi huko Visiwani, na Mwalimu alimuokoa tu kabla hajapewa dharuba za hizo siasa,

Halafu wakuu acheni kututisha na jina la Zitto, naona linatolewa na kila mchangiaji anayemuunga mkono Salim, na uongozi wake wa kubebwa na Mwalimu, akisema Zitto haina maana basi ndio authority kwenye ishu, cha muhimu ni hoja, swali langu kwako mkulu ni vipi wa-Tanzania wengine waliokuwa in their 20s hawakuchaguliwa na kupewa na nafasi na Mwalimu, kama Salim?

2.

Hili mkuu hatulikatai, ni kweli alifanya mengi mazito huko nje ambako ndiko hasa anakoheshimika, lakini kwa bahati mbaya hakutufanyia lolote bongo ndio maana hatuwezi kumpa uongozi wa juu kama urais kwa sababu hatumjui kama anvyojulikana huko nje!

That goes with Mkapa and Kikwete as well.....
Kuhusu ajira kwa Watanznaia OAU, kile ni chombo cha Afrika nzima nadhani kila mwafrika ana haki ya kupewa ajira kama anameet qualifications, au tulitaka afanye kama aliyofanya Mama Mongellah?
 
Mimi binafsi ninamuita Salim kuwa ni arrogant, kwa sababu baada ya kushindwa uchaguzi wa rais Dodoma, akakasirika na kusema kwamba hataki tena siasa za bongo, na kwamba hataki tena hata kuonana na Mkapa, sasa hii kweli inaweza kuwa ni sprit ya a good politician kwa taifa letu?

Hata baada ya kushindwa kwenye uchaguzi, bado Malecela alikubali kumsaidia Salim dakika za mwisho, yaaani siku mbili za mwisho, ambazo zilimsaidia Salim kuweza hata kupata zile kura 500, pamoja na all the nasty kampeni ambazo Salim alikuwa amezifanya behind the scene against Malecela, ikiwa ni pamoja na kumuandika kakitabu kachafu ambako kalikuwa traced kwake Salim, alikoka-print from London, lakini akajaribu kukifanya kionekane kimeandikwa na Kiwete, confronted with facts akashindwa cha kusema, lakini aliposhindwa tu ule uchaguzi akamkasirikia kila mtu, badala ya kujikasirikia mwenyewe, kwamba hana tu uwezo wa kuwa rais wa bongo, kwa sababu kuwa na uwezo huo ni pamoja na kushinda ile mizengwe ya ndani ya CCM,

Kuingia kwenye uchaguzi ukashindwa na kuleta hasira, maana yake ni moja tu kwamba wewe ni arrogant uliyeamini kuwa utashinda tu maana wewe una akili sana kuliko wagombea wengine, hatuhitaji viongozi wa namna hii bongo, Love or hate him, Kikwete alishinda uchaguzi wa rais, labda anayo mapungufu kwenye uongozi wake kitu ambacho ni wazi kwa marais wote waliowahi kututawala. Salim baada ya kushindwa alitakiwa kusimama kidete na kuanza kujitayarisha na uchaguzi ujao, sio kukimbilia Abuja!

tha man is arrogant!

Kuna ubaya gani mtu akiwa arrogant na ana-deliver. Tony Blair ni Arrogany, Barack Obama Arrogant.
 
1.
That goes with Mkapa and Kikwete as well.....

Great, ila sikumbuki Kiwete na Mkapa, wakiwa viongozi wa taifa in their 20S!

2.
Kuhusu ajira kwa Watanznaia OAU, kile ni chombo cha Afrika nzima nadhani kila mwafrika ana haki ya kupewa ajira kama anameet qualifications,

Kutowaajiri wa-Tanzania kwa sababu ya waa-Afrika wengine wenye qoualifications ni one thing kama ingewa kweli, lakini kitendo chake cha kuwaajiri waa-Arab wa Oman, ambao wengi wao ushahidi mwingi wa uchunguzi ulibaini kuwa wana mizizi na watawala wa zamani wa visiwani haikumsaidia kabisa Salim na kugombea urais wa Tanzania, kupitia CCM ndio wengine tunasema kuwa hatufai ni kwa sababu yako mengi sana ya Salim ambayo hayajasemwa wazi hadharani, lakini wajumbe wengi wa NEC wanayajua vizuri, na ndio maana hata Mwalimu mwenye hakuweza kubishana sana waliokuwa wakimpinga Salim ndani ya CCM, hasa watu kama Natepe, Nassor Moyo, Jumbe, Mwakanjuki, Sepetu, Bakari, Salmin, na wengineo!

3.
au tulitaka afanye kama aliyofanya Mama Mongellah?

Hapana tusingependa ayafanye ya wizi kama wa Mama Mongella, ambaye anatuhumiwa kwa wizi huko OAU!
 
1.
Kuna ubaya gani mtu akiwa arrogant na ana-deliver.

Tatizo ni ame-deliver wapi? nje? au ndani ya taifa lake? Kwa sababu kwenye siasa ni kama kwenye maisha, unavuna ulichopanda, kama ulipanda nje utavuna huko huko, na kama ulipanda bongo kama Kikwete, basi unavuna bongo!

2.
Tony Blair ni Arrogany, Barack Obama Arrogant.

Hawa ni arrogants walioweza kuchaguliwa locally kwanza, Salim ni arrogant ambaye hakuwahi kuchaguliwa zaidi ya kubebwa na Mwalimu, ndiyo tofauti yao, yaaani wenziwe u-arrogant wao una base za kuchaguliwa na kukubalika na wananchi, yeye ana u-arrogant wa kukubalika nje na sio locally, ndio maana hawezi kushinda uchaguzi wa local, labda huko nje anakosifika sana!
 
Kama alivyodokeza Mhe.Zitto, muda wake katika nafasi kubwa ya madaraka na wajibu wa nyumbani ulikuwa mfupi sana alichoweza kufanya katika huo muda mfupi (miaka ya 1980) kimetajwa.

Nadhani Mwalimu hakumpendelea tu kijana Salim(22) bali aliuona na kuutambua uwezo wake. kadhalika hata mataifa ya nje yaliutambua uwezo huo, vinginevyo wangekuwa wana lao jambo kumpa majukumu mazito sana katika umri mdogo.
Angalia alipewa majukumu gani na alishiriki shughuli zipi katika umri wa miaka 30 tu;

While serving at the United Nations, he was Chairman of the United Nations Special Mission to Niue in June/July 1972;
Drafting Committee Chairman of the Political Committee of the Ministerial Conference of Non-Aligned States, Georgetown, Guyana (August 1972);
Chairman of the Political Committee of the International Conference of Experts in Support of the Victims of Colonialism and Apartheid in southern Africa, Oslo (April 1973);
1975 Chairman of the Security Council's Committee on Sanctions against Southern Rhodesia;
President of the Security Council (January 1976);
Chairman of the high-level Ad HOC Group of the Special Committee of 24 visiting the United Kingdom, the United Republic of Tanzania, Zambia, Botswana, Mozambique and Ethiopia (April/May 1976);
Chairman of the Drafting Committee of the Fifth Conference of Heads of State or Government of the non-Aligned States, Colombo (August1976),
and Vice-President of the International Conference in support of the people of Zimbabwe arid Namibia and Chairman of the Committee of the Whole of that Conference, held in Maputo, Mozambique (may 1977).
Since his appointment as Ambassador at the United Nations he has attended the following:
Pacem en Maribus, Valleta, Malta (May 1970);
Governing Council of the United Nations Development Programme (UNDP), Geneva (June 1970);
Liberation Committee session, Algiers (July 1970);
OAU Assembly of Heads of State or Government, Addis Ababa (September 1970);
United Nations Security Council meeting, Addis Ababa (January /February 1972);
Preparatory Committee Meetings of Non-Aligned States, Georgetown (February 1972),
Kuala Lumpur (Mat 1972) and Kabul (May 1973); OAU Liberation Committee session, Accra (January 1973);
United Nations Security Council meeting, Panama City (March 1973);
Tenth Ordinary Session of the OAU Assembly of Heads of State or Government, Addis Ababa (May 1973);
Fourth Summit Conference of Non-Aligned States, Algiers (September 1973); world Congress of Peace Forces, Moscow (October 1973) ;
Co-ordinating Bureau of Non-Aligned Sates, Algiers (March 1974) ;
OAU Liberation Committee session, Dar es Salaam (January 1975);
Meeting of Co-ordinating Bureau of the Non-Aligned States, Havana (March 1975);
Extraordinary Session of OAU Council of Ministers, Dar es Salaam (April 1175);
Commonwealth Heads of Government Conference, Kingston (May 1975);
International Seminar on the Eradication of Apartheid and in Support of the Struggle for Liberation in South Africa, Havana (May 1976);
Co-ordinating Bureau of Non-Aligned States, Algiers (May/June 1976);
Thirteenth Ordinary Session of the OAU Assembly of Heads of State or Government, Port Louis Mauritius (July 1976);
Head of Tanzanian observer delegation to the Geneva Conference on Southern Rhodesia (October/December 1976);
First Afro-Arab Summit Conference, Cairo (March 1977);
Co-ordinating Bureau of Non-Aligned States, New Delhi (April 1977);
Twenty-Ninth Ordinary Session of the OAU Liberation Committee and of the OAU Council of Ministers, Libreville (June 1977);
Fourteenth Ordinary Session of the OAU Assembly of Heads of State or Government, Libreville (July 1977);
World Conference for Action against Apartheid, Lagos (August 1977);
Fifteenth Ordinary Session of the OAU Assembly of Heads of State or Government, Khartoum (July 1978); session of the OAU Liberation Committee, (June 1979);
Tenth Ordinary Session of the OAU Assembly of Heads of State or Government, Monrovia (June 1979);
and the Sixth Conference of Heads of State or Government of the Non-Aligned States, Havana (September 1979).

It seems still we are going around in circles, many of those chairmanships, he got by the virtue of his position, wako wengi wameongoza kamati na mikutano..even Idi amin was at one point the chairman of OAU. to do all that at a young age i commend him but, like Field Marshal Es said, wengi Nyerere aliwachagua wakiwa wadogo wakapewa kazi hizo, wako wakina Mkapa, Marehemu Magombe na wengine wengi.

Hiyo List umeweka inaonekana he has more experiences attending and arranging international meetings, again ni nini kimemsaidia mwananchi wa Tanzania?

Akiwa waziri mkuu, ni nini aliwasaidia wazanzibari, au watanzania...alikuwa waziri for 9 yrs 1980-1989 (including being prime minister) what were his achievements...many have used the excuse kuwa alikuwa nje...i think 9 yrs as a minister in different ministries and a politician hapa nyumbani surely he should have something to account for.
 
Back
Top Bottom