1
. Ni kweli kabisa Salim hawezi kushika Urais wa Bongo kwa sababu ya Uharamu wa siasa zetu, sasa nikitazama swala hili kwa makini inaonyesha wazi unajaribu kuhalalisha vitendo vya kina Kikwete na Mkapa kuwa ndio wanaume na wanatakiwa wanaume wengine kina Slaa kwa kupitia mlango huo huo kupigana na viongozi kama Mkapa.
Mkuu Bob,
Heshima mbele bro, sivihalalishi vitendo vya kihuni kwenye siasa zetu, kama ambavyo siwezi kuhalalisha uhuni kwenye siasa za UN ambako Salim, aligombea kama alivyogombea bongo na kufanyiwa uhuni kama wa bongo, huo hapana siuhalalishi, lakini ninasema hivi tuliyonayo as far as siasa zetu, hatukuyaomba, lakini tunayo, sasa wanaume imara kama Dr. Slaa na Dr. Mwakyembe, hukaa chini na kutafakari what to do ili ku-deal na situation, lakini sio kukimbilia nje na kusubiri uchaguzi, ndio maana sasa tuko kwenye siasa mpya za kusafisha mafisadi,
Salim, alipaswa kutuongoza kwenye vita hivi hasa baada ya yaliyomkuta kule Dodoma, unafikiri kwa nini alinyamaza tu na kulia nyumbani kwake na mkewe? Alijua akifungua mdomo watammaliza, yaaani angalau hata Sumaye ni kidume kidogo maana yeye alisema kidogo, siasa za kihuni hatukuziomba lakini tunazo tayari sasa dawa ni kuwachagua kina Dr. slaa na Dr. Mwakyembe, wanaonekana kuziweza ili watufikishe to the next level, kwa sababu kuna wananchi kama mimi ambao tunaamini kuwa ukisafisha tu viongozi wabovu, basi bongo kila tatizo litajipanga lenyewe!
2.
Mkuu tuzungumze kwa kuwatazama watanzania wenyewe kwanza. Hizi habari za kuchukua Ikulu by any means necessary zinaweza kumharibia mtu kama Dr. Slaa kwa sababu kinachogomba hapa ni uwezo wa mtu KUONGOZA..na sifa za kiongozi ni ktk usukani na kubadilisha gear sio swala nla nani anaonekana vizuri akiwa ktk driver's seat.
Mkuu Bob,
Point safi, lakini bongo sasa hivi tunahitaji dawa ya mafisadi kwanza, CV ya Salim ni nzito sana lakini ni kwa huko nje na the worst thing you can do sasa hivi kwa siasa za bongo ni kujaribu kuleta diplomasia kwa mafisadi, hawa kina Chenge, Mkapa, Yona wanahitaji Dr. Slaa au Dr. Mwakyembe, WAjerumani bila ya Hitler wasingefikia walipo sasa alikuja at the right time, lakini aliharibu tu kuua, US ilikuwa inamhitaji Bush kupambana na kina Osama, kama ni uongozi kwa bongo haiwezi ku-get better than Dr. Slaa na Dr. Mwakyembe, wanaoweza siasa za kumkoma nyani, ama sivyo taifa litaishia kukomwa na nyani, hatuwezi ku-afford that sasa hivi tunahitaji kiongozi wa kuweza kumkoma nyani giladi kama Dr. Slaaa na Dr. Nwakyembe!
3.
Hawa wajinga walikimbilia mlango wa dereva kuendesha mwenyewe hawajui hivyo haiwezi kuwa sifa kwa Slaa naye akimbilie tu usukani kugombana na washenzi.
Hawa wote ulowataja ni watu ambao sote tulidhani wana liseni ya kuendesha kumbe fake... na mada hii inazungumzia zaidi uwezo wa mtu kuendesha, sasa kama Salim liseni anayo na umekubali anaweza kuendesha gari hili isipokuwa hana Ubavu wa kupambana na madereva wabaya, sidhani kama utakuwa umetusaidia ktk hoja hii.
Sasa mkuu ili uwe na leseni ya bongo si lazima ushindane na washenzi madereva wa bongo, sasa Salim aliipataje hiyo leseni bila kuwashinda washenzi wa bongo? Ina maana moja tu kuwa hana hiyo leseni?
4.
Nitarudia kusema kwamba Ushujaa wa Salim na uwezo wa kuongoza Tanzania anao na pengine ana qualify zaidi kuliko kiongozi yeyote tuliye naye leo hii isipokuwa wakati wake umeshapita.
Salim ana sifa nyingi sana huko nje maana ndio wanaoujua uwezo wake kikazi bongo hatumjui, na besides hata shule yake ni suspect pia kwa sababu ameisoma akiwa kuanzia ofisa wa ubalozi na balozi tayari, hapa bongo tunao watu kama Dr. Mwakyembe wamesoma shule toka kuanzia umri wa kwenda shule, hizi shule za kusoma ukiwa balozi tayari ndio maana inakuwa taaabu sana kuziweza siasa zetu!
5.
Hizo hadithi za watum kuandika kitabu kuonyesha uzinzi wake na kadhalika ni hadithi za jikoni mkuu kwa sababu nani kweli atakaa hapa na kusoma kitabu kinachomzungumzia Salim nyumba alizowahi kupita....wengine hapa tunakaa kimya tu mbona tunajua relation ya Mwinyi alipokuwa akija mtaa wa Mahiwa Kariakoo kuvizia mke wa pili. Nyerere mwenyewe hakuwa safi, huyo Mkapa ndio usiseme kabisa maanake inasemekana alikuwa akipiga mke wa Mramba wakiwa bado ktk ndoa. Kikwete ndio kabisaaa yaani ktk maswala hayo hakuna msafi
Hapa nilikuwa ninajibu hoja ya mkuu mmoja kuhsusu Salim, kuandika kitabu ambacho litawachafua viongozi wengine wa Afrika, nikasema hawezi maana ana uchafu mwingi sana ambao haujawahi kutolewa nje, the point unayo-miss hapo ni kwamba akiandika anything, kutakuwa na majibu na hatayapenda kuanzia uwezo wake wa kazi mpaka his personal life kama kiongozi maana kwenye siasa ni fair game!
6.
na siasa za Zanzibar huwezi kabisa kumweka ktk kundi moja na wahuni wengine kwa sababu hakuwa na Muda wa kuishi Zanzibar wala kuendeleza siasa za Zainzibar akiwa nchi za nje...
Salim ni mwananchi wa huko visiwani, amefanya kazi huko kwenye siasa za 60s kabla Mwalimu hajamkimbiza nje, amehusika mpaka na siasa za mahizbu na mentor wake Babu, ndiye alitempeleka Cuba, ambako CIA walimuona kwa mara ya kwanza na kuanza kuwa na interest naye na kumfuatilia since then, mimi sijawahi kusikia mwanasiasa kama Salim, asiyekubalika kwao yaaani sisi bara ndio iwe kazi yetu kubeba wasiokubalika huko visiwani? Salim aende agombee urais wa visiwani alikotokea na kuzaliwa, huku Bara tunawafagilia kina Dr. slaa na Dr. Mwakyembe watoto wa nyumbani!
7.
Sema nachomkubali ni tabia yake akiwa kazini ya kutokubali upuuzi wa kujuana na ku favour mtu kwa sababu tu mnatoka nchi moja. Wapo Wadanganyika kibao wamefanya nae kazi na wamemshtumu sana na hata kumwita arrogant kwa sababu hakuwajali ama kuwapendelea wao kama Watanzania... Hii ndio hulka ya Mdanganyika yaani akisha kuwa ndugu yako anataka anina fulani ya attention na p[engione kujikosha kuwa mnafahamiana.. Salim ni mtu asiyependa uvivu ktk kazi, mpango wa kusukana nywele kazini na hadithi za saloon ama migahawani.
Mkuu wangu this is what you only know kuhusu Salim, one side of the story waliofanya kazi naye kule Adis wanasema vingine kabisa mkuu, na mpaka leo hajaweza ku-explain mlinzi wake yule mbongo alikufaje kule Adis, kama kuajiri aliajiri waarabu wengi sana wa Oman kule OAU, Watu wa West Afrika moja ya sifa yao kubwa ni kusaidia wananchi wa nchi zao wakipata nafasi huko nje, sasa kweli unasema kuwa Salim kutowasaidia wabongo huko nje ni sifa kubwa ya kumpa urais wa bongo?
8.
Hizi zote ni sifa ambazo kwa sababu sio reflection yetu sisi basi bila shaka naweza kukubali kuwa hafai kuwa kiongozi na wala hastahili sifa za Ushujaa wa mdanganyika mvuvi wa kufikiri. Kwani hata Kinjeketile anaweza kuitwa shujaa pamoja na kwamba matokeo ya mbinu zake zilitughalimu zaidi kimwili lakini pia zilitufumbua macho zaidi ya kuelewa kuwa wazungu walikuja kututawala na sio wapita njia ama wahamiaji (immigrant) ktk makazi yetu. Kifikra aliweza kutukomboa zaidi kama matunda ya vita ile ya Majimaji.
Hapana Kinjeketile ni kama Nyerere, waliyoyafanya wakati ule yanaweza kuonekana kuwa ni ujinga kwa wakati huu, lakini they did what they could, kutokana na mazingara na wakati, na kama Salim sio reflection yetu basi angepewa ukatibu wa UN na anowa-reflect, sasa na CV yote hiyo ilikuwaje wakamnyima ni kwa sababu hafafanani nao kabisa mkuu, na sisi bongo ndio kabisaaa labda huko visiwani ndio atafaaa kuwa rais!
Mengi zaidi siwezi kuyatoa, ila ninaaamini kwenye siasa ipo siku yatatoka tu yena wazi, otherwise darasa zito mkuu! Kesho mkuu!