Who is Salim Ahmed Salim?

Who is Salim Ahmed Salim?

Kalamu,
Salim hawezi kusema Urais wa kununua ikiwa hana ushahidi na Takrima ilikuwa halali. Kumbukeni Field Marshall Es aliwahi sema Kikwete hakuvunja sheria yeyote ya chama na tulizungumzia mengi ambayo kusema kweli sote tulikuja kubali wenyewe kuwa maswala mengine ya ndani ya chama ni ya chama hayahusiani na sisi tulioko nje.

Utaratibu wa kura ndani ya CCM sii jukumu letu kuutazama na kama una mashaka na chaguzi za ndani ya CCM basi nenda vyama vingine vyenye uwazi zaidi, hata ukienda Chadema ama CUF utakuta kuna baadhi ya sheria za uchaguzi wa viongozi wao una utata na sidhani kama Dr. Slaa anaweza kusimama hapa na kuzungumzia ubaya wa uchaguzi wa viongozi ndani ya Chadema hali yeye mwenyewe alishiriki kuunda sheria hizo.

Ye, Salim alitegemea kwamba atauzika na ngoma itabakia kati yake na Kikwete lakiniCCM kwa ujeuri walimwacha Mwakyembe na wagombea wengine pale kuchukua kura za Salim. Trust me, wajumbe wote ambao hawakumpigia kura Kikwete walitazama nje yake na kukuta mlolongo watu.

Ni mbinu ya kisheria iliyomwangusha Salim kisheria hata hivyo alikuwa bado mtu wa pili, kama wangefikia mtu mbili mkuu, uchawi wa Mtandao usingefanya kazi.

Sasa alalamike kitu gani?
 
1
. Ni kweli kabisa Salim hawezi kushika Urais wa Bongo kwa sababu ya Uharamu wa siasa zetu, sasa nikitazama swala hili kwa makini inaonyesha wazi unajaribu kuhalalisha vitendo vya kina Kikwete na Mkapa kuwa ndio wanaume na wanatakiwa wanaume wengine kina Slaa kwa kupitia mlango huo huo kupigana na viongozi kama Mkapa.

Mkuu Bob,

Heshima mbele bro, sivihalalishi vitendo vya kihuni kwenye siasa zetu, kama ambavyo siwezi kuhalalisha uhuni kwenye siasa za UN ambako Salim, aligombea kama alivyogombea bongo na kufanyiwa uhuni kama wa bongo, huo hapana siuhalalishi, lakini ninasema hivi tuliyonayo as far as siasa zetu, hatukuyaomba, lakini tunayo, sasa wanaume imara kama Dr. Slaa na Dr. Mwakyembe, hukaa chini na kutafakari what to do ili ku-deal na situation, lakini sio kukimbilia nje na kusubiri uchaguzi, ndio maana sasa tuko kwenye siasa mpya za kusafisha mafisadi,

Salim, alipaswa kutuongoza kwenye vita hivi hasa baada ya yaliyomkuta kule Dodoma, unafikiri kwa nini alinyamaza tu na kulia nyumbani kwake na mkewe? Alijua akifungua mdomo watammaliza, yaaani angalau hata Sumaye ni kidume kidogo maana yeye alisema kidogo, siasa za kihuni hatukuziomba lakini tunazo tayari sasa dawa ni kuwachagua kina Dr. slaa na Dr. Mwakyembe, wanaonekana kuziweza ili watufikishe to the next level, kwa sababu kuna wananchi kama mimi ambao tunaamini kuwa ukisafisha tu viongozi wabovu, basi bongo kila tatizo litajipanga lenyewe!

2.
Mkuu tuzungumze kwa kuwatazama watanzania wenyewe kwanza. Hizi habari za kuchukua Ikulu by any means necessary zinaweza kumharibia mtu kama Dr. Slaa kwa sababu kinachogomba hapa ni uwezo wa mtu KUONGOZA..na sifa za kiongozi ni ktk usukani na kubadilisha gear sio swala nla nani anaonekana vizuri akiwa ktk driver's seat.

Mkuu Bob,

Point safi, lakini bongo sasa hivi tunahitaji dawa ya mafisadi kwanza, CV ya Salim ni nzito sana lakini ni kwa huko nje na the worst thing you can do sasa hivi kwa siasa za bongo ni kujaribu kuleta diplomasia kwa mafisadi, hawa kina Chenge, Mkapa, Yona wanahitaji Dr. Slaa au Dr. Mwakyembe, WAjerumani bila ya Hitler wasingefikia walipo sasa alikuja at the right time, lakini aliharibu tu kuua, US ilikuwa inamhitaji Bush kupambana na kina Osama, kama ni uongozi kwa bongo haiwezi ku-get better than Dr. Slaa na Dr. Mwakyembe, wanaoweza siasa za kumkoma nyani, ama sivyo taifa litaishia kukomwa na nyani, hatuwezi ku-afford that sasa hivi tunahitaji kiongozi wa kuweza kumkoma nyani giladi kama Dr. Slaaa na Dr. Nwakyembe!


3.
Hawa wajinga walikimbilia mlango wa dereva kuendesha mwenyewe hawajui hivyo haiwezi kuwa sifa kwa Slaa naye akimbilie tu usukani kugombana na washenzi.
Hawa wote ulowataja ni watu ambao sote tulidhani wana liseni ya kuendesha kumbe fake... na mada hii inazungumzia zaidi uwezo wa mtu kuendesha, sasa kama Salim liseni anayo na umekubali anaweza kuendesha gari hili isipokuwa hana Ubavu wa kupambana na madereva wabaya, sidhani kama utakuwa umetusaidia ktk hoja hii.

Sasa mkuu ili uwe na leseni ya bongo si lazima ushindane na washenzi madereva wa bongo, sasa Salim aliipataje hiyo leseni bila kuwashinda washenzi wa bongo? Ina maana moja tu kuwa hana hiyo leseni?

4.
Nitarudia kusema kwamba Ushujaa wa Salim na uwezo wa kuongoza Tanzania anao na pengine ana qualify zaidi kuliko kiongozi yeyote tuliye naye leo hii isipokuwa wakati wake umeshapita.

Salim ana sifa nyingi sana huko nje maana ndio wanaoujua uwezo wake kikazi bongo hatumjui, na besides hata shule yake ni suspect pia kwa sababu ameisoma akiwa kuanzia ofisa wa ubalozi na balozi tayari, hapa bongo tunao watu kama Dr. Mwakyembe wamesoma shule toka kuanzia umri wa kwenda shule, hizi shule za kusoma ukiwa balozi tayari ndio maana inakuwa taaabu sana kuziweza siasa zetu!


5.
Hizo hadithi za watum kuandika kitabu kuonyesha uzinzi wake na kadhalika ni hadithi za jikoni mkuu kwa sababu nani kweli atakaa hapa na kusoma kitabu kinachomzungumzia Salim nyumba alizowahi kupita....wengine hapa tunakaa kimya tu mbona tunajua relation ya Mwinyi alipokuwa akija mtaa wa Mahiwa Kariakoo kuvizia mke wa pili. Nyerere mwenyewe hakuwa safi, huyo Mkapa ndio usiseme kabisa maanake inasemekana alikuwa akipiga mke wa Mramba wakiwa bado ktk ndoa. Kikwete ndio kabisaaa yaani ktk maswala hayo hakuna msafi

Hapa nilikuwa ninajibu hoja ya mkuu mmoja kuhsusu Salim, kuandika kitabu ambacho litawachafua viongozi wengine wa Afrika, nikasema hawezi maana ana uchafu mwingi sana ambao haujawahi kutolewa nje, the point unayo-miss hapo ni kwamba akiandika anything, kutakuwa na majibu na hatayapenda kuanzia uwezo wake wa kazi mpaka his personal life kama kiongozi maana kwenye siasa ni fair game!

6.
na siasa za Zanzibar huwezi kabisa kumweka ktk kundi moja na wahuni wengine kwa sababu hakuwa na Muda wa kuishi Zanzibar wala kuendeleza siasa za Zainzibar akiwa nchi za nje...

Salim ni mwananchi wa huko visiwani, amefanya kazi huko kwenye siasa za 60s kabla Mwalimu hajamkimbiza nje, amehusika mpaka na siasa za mahizbu na mentor wake Babu, ndiye alitempeleka Cuba, ambako CIA walimuona kwa mara ya kwanza na kuanza kuwa na interest naye na kumfuatilia since then, mimi sijawahi kusikia mwanasiasa kama Salim, asiyekubalika kwao yaaani sisi bara ndio iwe kazi yetu kubeba wasiokubalika huko visiwani? Salim aende agombee urais wa visiwani alikotokea na kuzaliwa, huku Bara tunawafagilia kina Dr. slaa na Dr. Mwakyembe watoto wa nyumbani!

7.
Sema nachomkubali ni tabia yake akiwa kazini ya kutokubali upuuzi wa kujuana na ku favour mtu kwa sababu tu mnatoka nchi moja. Wapo Wadanganyika kibao wamefanya nae kazi na wamemshtumu sana na hata kumwita arrogant kwa sababu hakuwajali ama kuwapendelea wao kama Watanzania... Hii ndio hulka ya Mdanganyika yaani akisha kuwa ndugu yako anataka anina fulani ya attention na p[engione kujikosha kuwa mnafahamiana.. Salim ni mtu asiyependa uvivu ktk kazi, mpango wa kusukana nywele kazini na hadithi za saloon ama migahawani.

Mkuu wangu this is what you only know kuhusu Salim, one side of the story waliofanya kazi naye kule Adis wanasema vingine kabisa mkuu, na mpaka leo hajaweza ku-explain mlinzi wake yule mbongo alikufaje kule Adis, kama kuajiri aliajiri waarabu wengi sana wa Oman kule OAU, Watu wa West Afrika moja ya sifa yao kubwa ni kusaidia wananchi wa nchi zao wakipata nafasi huko nje, sasa kweli unasema kuwa Salim kutowasaidia wabongo huko nje ni sifa kubwa ya kumpa urais wa bongo?

8.
Hizi zote ni sifa ambazo kwa sababu sio reflection yetu sisi basi bila shaka naweza kukubali kuwa hafai kuwa kiongozi na wala hastahili sifa za Ushujaa wa mdanganyika mvuvi wa kufikiri. Kwani hata Kinjeketile anaweza kuitwa shujaa pamoja na kwamba matokeo ya mbinu zake zilitughalimu zaidi kimwili lakini pia zilitufumbua macho zaidi ya kuelewa kuwa wazungu walikuja kututawala na sio wapita njia ama wahamiaji (immigrant) ktk makazi yetu. Kifikra aliweza kutukomboa zaidi kama matunda ya vita ile ya Majimaji.

Hapana Kinjeketile ni kama Nyerere, waliyoyafanya wakati ule yanaweza kuonekana kuwa ni ujinga kwa wakati huu, lakini they did what they could, kutokana na mazingara na wakati, na kama Salim sio reflection yetu basi angepewa ukatibu wa UN na anowa-reflect, sasa na CV yote hiyo ilikuwaje wakamnyima ni kwa sababu hafafanani nao kabisa mkuu, na sisi bongo ndio kabisaaa labda huko visiwani ndio atafaaa kuwa rais!

Mengi zaidi siwezi kuyatoa, ila ninaaamini kwenye siasa ipo siku yatatoka tu yena wazi, otherwise darasa zito mkuu! Kesho mkuu!
 
Mkandara, FMES,
Good points all of you. This is what makes JF kijiwe kitamu. Mkandara, usiwe unapotea sana hivyo yakhe, some of us look forward to reading from you. Kwa sasa comments zangu juu ya Salim naziweka kiporo kwani you guys are doing such a great job.
 
very interesting debate, educational back and forth bila matusi wala nini...the way its supposed to be. Hasa kwa sisi wenye kuuliza tu maana wengi hatumfahamu Dr.Salim kwa undani, tunafahamu jina la kimataifa tu. Ni vizuri kusoma hapa from people who lived through his time when he was in office here in Tanzania and those who know him.

One thing is Clear, JK clearly was not the man for the Job...he will leave office with a legacy of shame if he doesnt get his act together and bring those people to justice.


Side historical note,
Just a side interesting note on who was in his cabinet in 1984

Tanzania: New Cabinet

SOURCE: (a) Dar es Salaam in English for abroad 1600 gmt 24 Apr 84

Text of report


SECTION: Part 4 The Middle East, Africa and Latin America; B. AFRICA ; ME/7627/B/1;

LENGTH: 343 words



Dar es Salaam: President Nyerere has announced a major Cabinet reshuffle appointing the Zanzibar President, Ndugu Ali Hassan Mwinyi, the new Vice-President of the United Republic of Tanzania, and Ndugu Salim Ahmed Salim the new Prime Minister.According to the reshuffle, the number of Cabinet ministries has been reduced from 21 to 14. The full Cabinet is as follows [all names apart from Nyerere's given the title Ndugu]😛resident - Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Vice-President - Ali Hassan Mwinyi Prime Minister - Salim Ahmed SalimMinisters of State in the President's Office - Amir Jamal, Samuel Sitta, Mustafa Nyang'anyi Minister of State in the Vice-President's Office - Ramadhani Abdallah Shaabani Ministers of State in the Prime Minister's Office - Getrude Mwongola, Anna Makinda, Kingunge Ngombale MwiruOthers are:Agriculture and Livestock Development - John Machunda Finance - Cleopa Msuya Economic Affairs and Planning - Kighoma Malima Foreign Affairs - Benjamin Mkapa Home Affairs - Salmin Amour Defence and National Service - Muhiddin Kimario Labour and Manpower Development - Daudi MwakawagoOthers are:Industries and Trade - Basil Mramba Lands, Natural Resources and Tourism - Paul Bomani Water, Energy and Minerals - Al-Noor Kassum Communications, Transport and Works - John Malecela Education - Jackson Makweta Health - Aaron Chiduo [Kiduo] Justice - Joseph WariobaMinister without portfolio - Rashidi Kawawa The President has also appointed [a] Minister of State in several ministries as follows:Agriculture and Livestock Development - Herman Kirigini Communications, Transport and Works - Guntram Itatiro Water, Energy and Minerals - Pius Pius Ng'wanduThe Deputy Ministers are as follows:Home Affairs - Rashid Mohammed Industries and Trade - Evarist Mwanansao Finance - Steven Kibona and Arcado Ntagazwa Defence and National Service - (?Esley Mwakiambiki)The President has also announced new principal secretaries and deputy principal secretaries in several ministries. The new Cabinet would be sworn in tomorrow morning.

SUBJECT: APPOINTMENTS (90%); POLITICS (78%);

PERSON: ALI HASSAN MWINYI (92%); JULIUS KAMBARAGE NYERERE (56%); JOHN S MALECELA (51%);

COUNTRY: TANZANIA (92%); AFRICA (92%);

CITY: DAR ES SALAAM, TANZANIA (76%);

LANGUAGE: ENGLISH

Copyri
 
Nje ya mada,
Hivi Tanzania hatuna watu wanaoweza kuwa mawaziri na wakafanya kazi kwa ufanisi maana naona tunarecycle tuu tangu watu wa awamu ya kwanza mpaka juzi walikuwa mawaziri na wengine bado wako kwenye serikali ya sasa....

Samuel Sitta
Anna Makinda
Kingunge Ngombale
Basil Mramba
 
Wakuu Mkandara na FMES,

Naona mmetupa maelezo mazuri na marefu lakini nafikiri ingekuwa vema tukaangalia ni kipi tunachohitaji na vipi tunaweza kukipata kwa kutumia wale tunaowaita mashujaa wetu;

Kwanza nafikiri ni mapema mno kuwaita Zitto na Slaa mashujaa wetu kwa vile hawajagusa madaraka yoyote ya nchi na tukaona jinsi wanavyoyatumia. Je wakipewa watakuwa kama Chissano au Chiluba? Kupiga kelele tu sio ushujaa, maana hata akina Marmo, Mzindakaya n.k., walipigia sana kelele hapo awali, lakini hivi sasa, wote ni mafisadi wazuri kabisa. Mtu ambaye aliwahi kushika madaraka, tunatakiwa tuangalie jinsi alivyoyatumia. Wapiga kelele kama akina Msekwa, Warioba, Butiku n.k., sidhani kama walikuwa viongozi bora.

La muhimu hivi sasa ni kujiuliza, je ni nani mwenye uwezo wa kuleta haya mabadiliko? Offcourse upinzani wanaweza kufanya mabadiliko makubwa kuliko CCM lakini je wanao uwezo wa kushinda 2010?

Kama nilivyoelezea katika hoja zangu zilizopita, bado ninaamini kuwa hawawezi. CCM bila shaka watashinda 2010, hata kama wakimsimamisha tena JK labda litokee lingine kubwa zaidi la kumhsusu JK mwenyewe. Huu ni mtazamo wangu na sio lazima kwa kila mtu kukubaliana nao.

Kwa hiyo kama ni mapinduzi ya 2010, inabidi yafanyike ndani ya CCM. Bunge wanaweza wakamuondoa JK kabla ya 2010, lakini hili kwa hivi sasa halielekei kuwa na pumzi maana hata hapa ukumbini ni wachache sana wanaoliona kama ufumbuzi wa haraka tulionao. Kwa hiyo tunabakia na njia moja tu 2010. Hapa swali linabaki kuwa, je ni ni nani ndani ya CCM mwenye sifa, umaarufu na uwezo wa kumuondoa JK madarakani 2010? Kwangu mimi naona SAS anao huo uwezo na sifa zote.

Ki ukweli ni kuwa SAS aliupigania sana uteuzi wa 2005 ila alishindwa kwa sababu ya majungu aliyowefanyiwa, kukataa kwake kutumia takrima na pia kampeni za wazi za mweyekiti wa wakati ule, Mkapa, wa kuwataka wana CCM wamchague JK. Hivyo ndivyo vilivyomwangusha bila hivyo angekuwa ndie raisi wetu hivi sasa. Tukumbuke kuwa hata baada ya hayo yote, JK alipata zaidi kidogo tu ya 60% kitu ambacho kinaweza kubadilika kirahisi hivi sasa.

SAS ameitumikia nchi, ndani na nje kwa ujasiri na uadilifu mkubwa.

Ameweza kufanya hivyo kwa miaka zaidi ya 40 bila ya kuhusishwa katika ubadhilifu wowote.

Kukaa kwake katika nchi mbalimbali zilizoendelea na zinazopigania kuendelea kumempa uona mbali mkubwa tofauti na Kikwete kwenye nini cha kufanya ili kuisukuma nchi mbele.

Hii kwangu ni sifa kubwa sana kwa yeyote anayetaka kuiongoza nchi yetu na sio kuwa na kiongozi anayetumia muda wake kutalii badala ya kusimamia maendeleo. JK kwenye safari yake ya kwanza US kama raisi alinukuliwa akisema kuwa TZ haina uwezo wa kujijengea barabara interchangers (flyovers) kama US, jambo ambalo linawezekana ingawa kwa viwango tofauti. Kwangu hili lilionyesha ukosefu wake wa kuona mbali (vision) kwa vile hajawahi kuishi nje ya Dar es salaam, Bagamoyo na Zanzibar.

SAS pia anao uelewa mkubwa zaidi wa suala la Muungano na kwa kumtumia yeye akiwa madarakani anaweza kuwashawishi wapemba wenzake wakafikia makubaliano na wazanzibara. Wazanzibari wengi wanajifanya kumuogopa SAS lakini ukiangalia kiundani, SAS hana sababu yeyote ya kujitengenezea historia mbaya kwa kuzua vurugu ZNZ/PBA. Kwangu mimi SAS ni mtatuzi zaidi ya kuwa mchochezi.

Kwahiyo kwa mawazo yangu, SAS anafaa sana kuwa mgombea ndani ya CCM mwaka 2010. Anachotakiwa kufanya tu ni kujitokeza mapema, say 2009, na kuashiria kuwa anataka kupambana na JK mwaka 2010.

Baada ya hapo aanze kuunganisha wale wote walio na uchungu na jinsi JK alivyoiendesha nchi, kama akina Mwakyembe, Seleli, Mrs. Malecela n.k. Hili ni gumu kufanywa na kiongozi mwenye sifa ndani na nje ya nchi kama SAS, lakini kama akitaka kujitengenezea historia ya kubwa zaidi na kuikoa nchi, hii ndio njia pekee ya kuchukua na sidhani kama JK atamshinda hivi sasa.

Tafadhali, mwenye namba ya simu ya SAS atupatie ili tuanze kumshawishi mzee wetu na kuanza kumpigia debe.
 
Mkandara na FMES,

Safi sana wakuu. Nimetulia na popcorn yangu hapa navinjari.

Hii ndo naita majadiliano!
 
mwanahabari thanks for the useful information...nimesoma nikakuta kumbe baraza la mwisho la mawaziri la mwalimu lilikuwa na wizara 14..mawaziri na manaibu jumla 21...safi sana!!

kikwete angetufurahisha kama angeweza kupunguza idadi ya mwawaziri na mnaibu 60..wabaki angalau 28!!!
 
The more I read of the ongoing debate the more confused I am. Are we dicussing the plus and minusses of SAS or are we debating who is best suited to deal with the leadership of Tz.Given the mess we are in;credit to BMW (who took full advantage of Mwalimus demise ),we need a President who would be strong, courages, bold, daring enough, to take to task the culprits (Mafisadis)that have swallowed the country.

To me it seems obvious he needs the backing of the Armed Forceis (Jeshi).Or am I totally wrong ?
 
Mkandara said:
Nitamalizia kwa kusema kwamba, Mheshimiwa Salim kwa yale aloweza kuyafanya chini ya Utawala wa mwalimu na wakati mfupi sana ndani ya serikali yetu chini ya Mwinyi unatosha kabisa kumpa sifa ya Ushujaa kwa sababu sii lazima mchezaji acheze dakika 90 kuipata sifa ya ufungaji goli..Machache aloweza kuyafanya ktk muda mfupi ndani yasiwe sababu kubwa ya kuondoa ushujaa wake ati kwa sababu tu alitumikia Taifa letu nje zaidi ya ndani. Yale Mapinduzi za Zanzibar tu kumwondoa Sultan yalitosha kumpa sifa ya Ushujaa na sio watu kama Karume waliodandia sifa hii waka hijack Utawala wa visiwani. Bila shaka kwa tendo hilo tu hawezi kupendwa na pande zote mbili iwe Hizbu ama ASP..kama alivyoondoka Abraham Babu bila kupatiwa heshima ya kitaifa.
Nitafurahi sana kuona kama ataweza kuandika kitabu kinachoeleza mchango wake ktk maisha yake alotumikia taifa na Ulimwengu kwa Ujumla.

Mkandara,

..Karume alikuwa ndiye father figure wa harakati za kuleta utawala wa mtu mweusi na walio wengi ZNZ.

..ASP walishiriki uchaguzi ZNZ zaidi ya mara 3 na kushinda kwa wingi wa kura. mara zote hizo Karume ndiyo alikuwa mwenyekiti wa ASP.

..Mapinduzi yalifanikishwa na vijana wa ASP na wale wa Umma Party.

..mchango wa Salim Salim hauwezi kulinganishwa na ule wa Kassim Hanga,Abdularahman Babu, Abdalah Natepe,Seif Bakari, Saidi Washoto etc etc. Hilo ndilo lilosababisha yeye akawa Balozi na wenzake wakapewa nafasi nyeti kama uwaziri na wengine kuwepo ktk baraza la Mapinduzi.

..Vilevile Karume alikuwa mtu mzito na mwenye heshima mbele ya Wazanzibari na ndiyo maana akapewa heshima ya Raisi wa Kwanza wa ZNZ.

..sidhani kama unaitendea haki historia unapodai mchango wa Salim Salim ktk harakati za kuleta Uhuru, Utawala wa mtu mweusi, na Mapinduzi ya ZNZ, ulikuwa mkubwa kuliko wa Sheikh Abeid Amaan Karume.
 
Tatizo la CCM si hiyo mitandao yao hata mtu akiwa mchovu lakini ana mtandao strong atapiga bao tu so Salim ku-survive CCM in ngumu but nakubali he can make changes in Tz...
 
Mkandara said:
Sasa mtu kama Salim, mheshimiwa Field Marshall ES hawezi kumweka ktk kundi la mashujaa kwa sababu hayupo kundi moja na kina Mandela, Slaa na Zitto na hakuna wakati wowote ktk Utawala wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa ama JK ameweza kusimama against the Government pale yeye FMES anaona haki ilikosekana.

Na ndio maana mimi muda wote nimemwambia kwamba Salim ktk wakati wote wa Matatizo Tanzania alitupwa nje na kafungwa kamba za miguu.. Hii ilikuwa ni jeuri ya mwalimu ambaye alifahamu uwezo wa Salim.

Ni pale tu alipotaka kujiuzuru ndipo alipomrudisha Salim nchini na kwa bahati mbaya kama inavyojulikana viongozi wa CCM Zainzibar(baraza la Mapinduzi) ambao wali hijack Mapinduzi kisiasa walikataa pendekezo la mwalimu ikiwa hana jinsi isipokuwa kumweka Mwinyi.

This guy hakuteteleka wala kuonyesha dalili ya kudhoofika na kukataa position ya Waziri mkuu ama wadhifa uliofuata.

Mkapa pia alihakikisha mtu huyu anatupwa nje tena kuondoa upinzani ndani hivyo bado sii rahisi kumshutumu Salim anapolitumikia taifa kama walivyofanywa kina Sarakikya na kundi kubwa la wafuasi wa mwalimu ambao walipingana sana na mfumo huu mpya wa kiutawala.

Mkandara,

..postings zako zinachangamsha sana, lakini wakati huohuo unatuburuza with some very serious factual errors.

..Ni wakati gani Salim Salim alitishia kujiuzulu? alikuwa akishika wadhifa gani wakati huo?

..Salim Salim alitolewa UN akaja kuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Wakati Dr.Kurt Waldheim alipoachia nafasi kule UN, Mwalimu akaamua kumpigia debe Salim Salim awe UN SG.

..Aliposhindwa uchaguzi UN, Salim Salim aliendelea na nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje. Marehemu Sokoine alipofariki Salim Salim akateuliwa Waziri Mkuu.

..Wakati Aboud Jumbe anajiuzulu Salim Salim alikuwa Waziri Mkuu. sasa ni ni kilimshinda Mwalimu kumpachika Uraisi wa ZNZ na moja kwa moja kuwa Makamu wa Raisi
? Kumbuka kwamba Salim Salim alikuwa ameshika madaraka makubwa na ana sifa za kimataifa kuliko Ally Mwinyi.

..pia Salim Salim alikuwa na nafasi ya kuwa Raisi wa ZNZ kumpokea Mzee Mwinyi. Je, ni kwanini hakupigania nafasi hiyo na Mzee Idris Abdul Wakil na Maalim Seif Sharriff?

..Katiba yetu ya mwaka 1985, wakati Mwalimu anaachia ngazi, ilikuwa inaelekeza kwamba ikiwa Raisi atatoka Zanzibar, basi Waziri Mkuu atatoka Tanzania Bara na ndiye atakuwa Makamu wa kwanza wa Raisi. Kwa msingi huo wa Kikatiba Salim Salim alikuwa hastahili nafasi ya Uwaziri Mkuu. Hili lilikuwa nje ya uwezo wake, tofauti na unavyoelekeza hapo juu.

..pia Mkapa had no role na Salim Salim kukaa huko OAU. Mwalimu alimuomba Salim Salim agombee Uraisi mwaka 1995 lakini mwenyewe akaamua kuendelea na ukatibu mkuu OAU.

..kuna habari kwamba Salim Salim aliombwa na Mkapa kuja kuwa Makamu wa Raisi baada ya Dr.Omari Juma kufariki. Inasemekana Salim Salim alikataa offer hiyo.

..Mwisho, Ben Mkapa alimteua Salim Salim kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM baada ya kurudi nyumbani toka OAU. Hivi mlitegemea Mkapa amsaidie nini zaidi?
 
Jokakuu,
Nakusikia mkuu ila naomba kidogo unisome kwa makini haya yafuatayo na ikiwezekana nipe hoja...
Ni wakati gani Salim Salim alitishia kujiuzulu? alikuwa akishika wadhifa gani wakati huo?
naomba nukuu ya pale niliposema hivyo..
Salim Salim alitolewa UN akaja kuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Wakati Dr.Kurt Waldheim alipoachia nafasi kule UN, Mwalimu akaamua kumpigia debe Salim Salim awe UN SG.

..Aliposhindwa uchaguzi UN, Salim Salim aliendelea na nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje. Marehemu Sokoine alipofariki Salim Salim akateuliwa Waziri Mkuu.
Hapa mkuu una maana sikuzungumzia wakati akiwa - Waziri wa mambo ya nje?... nadhani tulichokuwa tukizungumzia ni mchango wa Salim akiwa ndani haya maswala ya nje yote FMES kayakubali isipokuwa alitaka kujua alichokifanya akiwa ndani... Kwa mtaji huo sijui kama kuna mtu anaweza kutuambia waziri wetu gani ktk wizara hiyo amewahi kuyafanya la kusifiwa ndani ya nchi..
pia Salim Salim alikuwa na nafasi ya kuwa Raisi wa ZNZ kumpokea Mzee Mwinyi. Je, ni kwanini hakupigania nafasi hiyo na Mzee Idris Abdul Wakil na Maalim Seif Sharriff
Why apiganie wakati kisha ombwa kushika nafasi ya waziri mkuu toka Nyerere akiwa rais.. Kumbuka mkuu Salim aliendelea nafasi hiyo hadi November 1985, tayari Mwinyi kisha kamata Ikulu Jan 1985..
Halafu kama ulivyojua Makamu wa rais hakuchaguliwa na mtu toka bara hata kidogo.. Kifupi ukitazam wadhifa wote wa Salim nchini ni kama vile alikuwa mtu wa bara zaidi ya visiwani..Wewe nambie ni waziri gani wa mambo ya nje ametoka visiwani, waziri mkuu, waziri wa Ulinzi bado tu mjomba hujaelewa kuwa alikuwa hana nafasi ZNZ..mkuu Salim alifungwa kamba za miguu na malisho yake yalikuwa bara tu.

Reason hasa haijulikani kwa sababu ikiwa watu kama Seif Sharrif wa Hizbu ameweza kuingia ktk mafia ya serikali ya ZNZ vipi mtu kama Salim?.. jer na yeye ni mmoja kati ya wakisiwa ktk hujuma za kumuua Karume?

Mkuu kama kiongozi wa Tanzania atapewa madhifa ndani ya serikali yetu ni vigumu kwa OAU kuweza kumchagua mtu huyo.

Inakuwaje unasema Nyerere alimpwndekeza Salim kugombea nafasi ya UN SG lakini unapofdika kwa Mkapa inakuwa hana mamlaka! By the wa, majina ya wale wanaoteuliwa hupendeklezwa na kina nani haswa! nipe darasa nipo kujifunza pia.

Binafsi sina jibu mkuu labda wewe unaweza kutusaidia..
 
Jokakuu,
Nakusikia mkuu ila naomba kidogo unisome kwa makini haya yafuatayo na ikiwezekana nipe hoja...

naomba nukuu ya pale niliposema hivyo..

Hapa mkuu una maana sikuzungumzia wakati akiwa - Waziri wa mambo ya nje?... nadhani tulichokuwa tukizungumzia ni mchango wa Salim akiwa ndani haya maswala ya nje yote FMES kayakubali isipokuwa alitaka kujua alichokifanya akiwa ndani... Kwa mtaji huo sijui kama kuna mtu anaweza kutuambia waziri wetu gani ktk wizara hiyo amewahi kuyafanya la kusifiwa ndani ya nchi..

Why apiganie wakati kisha ombwa kushika nafasi ya waziri mkuu toka Nyerere akiwa rais.. Kumbuka mkuu Salim aliendelea nafasi hiyo hadi November 1985, tayari Mwinyi kisha kamata Ikulu Jan 1985..
Halafu kama ulivyojua Makamu wa rais hakuchaguliwa na mtu toka bara hata kidogo.. Kifupi ukitazam wadhifa wote wa Salim nchini ni kama vile alikuwa mtu wa bara zaidi ya visiwani..Wewe nambie ni waziri gani wa mambo ya nje ametoka visiwani, waziri mkuu, waziri wa Ulinzi bado tu mjomba hujaelewa kuwa alikuwa hana nafasi ZNZ..mkuu Salim alifungwa kamba za miguu na malisho yake yalikuwa bara tu... Reason hasa haijulikani kwa sababu ikiwa watu kama Seif Sharrif wa Hizbu ameweza kuingia ktk mafia ya serikali ya ZNZ vipi mtu kama Salim?.. jer na yeye ni mmoja kati ya wakisiwa ktk hujuma za kumuua Karume?...
Mkuu kama kiongozi wa Tanzania atapewa madhifa ndani ya serikali yetu ni vigumu kwa OAU kuweza kumchagua mtu huyo.. Inakuwaje unasema Nyerere alimpwndekeza Salim kugombea nafasi ya UN SG lakini unapofdika kwa Mkapa inakuwa hana mamlaka!..
By the wa, majina ya wale wanaoteuliwa hupendeklezwa na kina nani haswa! nipe darasa nipo kujifunza pia.
Binafsi sina jibu mkuu labda wewe unaweza kutusaidia..

Mkandara, Marehemu Diria alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Zanzibar. Rekebisha kidogo hilo. Mengine yote nipo pamoja nawe

Zitto
 
Zitto,
Shukran, nachojaribu kusema hapa ni kumwonyesha tu ndugu yangu Jokakuu kuwa Salim hakuwa na nafasi yoyote ZNZ.. kila wadhifa alopata umetokana na Bara kama vile hakutoka ZNZ.

Sijui kama aliwahi kushika hata Ukatibu kata ktk kitongoji chochote ZNZ
 
Zaidi ya kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi Zanzibar chini ya chama cha UMMA, hakuwahi kuwa na nafasi nyingine yeyote tofauti na ubalozi.

Kumbuka Ubalozi aliteuliwa na Karume ili kumtoa nje ya Zanzibar kama ilivyokuwa kwa wanachama wengi wa UMMA. Hat Uhizbu wa SAS kikweli haupo kwani alikuwa ZNP muda mfupi sana kabla hawajaanzisha chama chao kipya cha UMMA chini ya Babu
 
Zitto,
Shukran, nachojaribu kusema hapa ni kumwonyesha tu ndugu yangu Jokakuu kuwa Salim hakuwa na nafasi yoyote ZNZ.. kila wadhifa alopata umetokana na Bara kama vile hakutoka ZNZ....
Sijui kama aliwahi kushika hata Ukatibu kata ktk kitongoji chochote ZNZ...
SAS KAMWE HAWEZI KUISHI AU KUWA KIONGOZI ZENJ...YEYE NA MAREHEMU KASSIM HANGA WANAHUSISHWA NA MAUAJI YA KARUME MKUBWA,MPAKA SASA MKE WA KARUME MKUBWA NA SAS HAWASALIMIANI.JK NDIE ALIMUOKOA SAS HASIENDE KUUWAWA ZENJ KAMA AMBAVYO KASSIM HANGA ALIUWAWA BAADA YA KUFA KARUME.
 
sas Kamwe Hawezi Kuishi Au Kuwa Kiongozi Zenj...yeye Na Marehemu Kassim Hanga Wanahusishwa Na Mauaji Ya Karume Mkubwa,mpaka Sasa Mke Wa Karume Mkubwa Na Sas Hawasalimiani.jk Ndie Alimuokoa Sas Hasiende Kuuwawa Zenj Kama Ambavyo Kassim Hanga Aliuwawa Baada Ya Kufa Karume.

I Mean Jkn And Not Jk
 
SAS KAMWE HAWEZI KUISHI AU KUWA KIONGOZI ZENJ...YEYE NA MAREHEMU KASSIM HANGA WANAHUSISHWA NA MAUAJI YA KARUME MKUBWA,MPAKA SASA MKE WA KARUME MKUBWA NA SAS HAWASALIMIANI.JK NDIE ALIMUOKOA SAS HASIENDE KUUWAWA ZENJ KAMA AMBAVYO KASSIM HANGA ALIUWAWA BAADA YA KUFA KARUME.

Rekebisha historia yako. Kassim Hanga amekufa kabla ya Karume kufa. Inakuwaje marehemu amuue aliyemzima.
Kasim Hanga inasemekana ndie alieuwawa na Karume kwa kufungwa jiwe na kurushwa baharini na mpaka leo watoto wa Hanga hawajaona mwili wa baba yao ili kuzika kwa heshima. Wengi tu waliuwaw, wapi Twala nk.

Wakati Karume anauwawa na Humud, SAS wala hakuwapo nchini alikuwa ubalozini. UMMA walipewa tu kifo kile ili kuwafuta kabisa katika siasa za Zanzibar lakini ninaamini sio Babu wala SAS wala Sultan Ali waliohusika.

Uchunguzi huru ufanyike na Karume mtoto ili kujua ukweli wa kifo cha baba yake.
 
Rekebisha historia yako. Kassim Hanga amekufa kabla ya Karume kufa. Inakuwaje marehemu amuue aliyemzima.
Kasim Hanga inasemekana ndie alieuwawa na Karume kwa kufungwa jiwe na kurushwa baharini na mpaka leo watoto wa Hanga hawajaona mwili wa baba yao ili kuzika kwa heshima. Wengi tu waliuwaw, wapi Twala nk. Wakati Karume anauwawa na Humud, SAS wala hakuwapo nchini alikuwa ubalozini. UMMA walipewa tu kifo kile ili kuwafuta kabisa katika siasa za Zanzibar lakini ninaamini sio Babu wala SAS wala Sultan Ali waliohusika. Uchunguzi huru ufanyike na Karume mtoto ili kujua ukweli wa kifo cha baba yake.

kwani hadi leo hajachunguza pamoja na kuwa madarakani kwa miaka 8!!!???? Kama hajafanya uchunguzi inamaanisha anajua chanzo cha kifo cha baba yake, na kama sivyo atakuwa mjinga kwa kutokujari (taking it for granted)
 
Back
Top Bottom