Mkuu Mwanahabari,
Ni kweli Mwandosya alikuwa amefanikiwa kwa kiasi fulani lakini hakuwa tajiri wa kutanua. Matanuzi yameonekana kuongezeka alipokuwa PS ambapo u-consultant ulikuwa haupo tena. Huko wizarani ndio alipoona utamu wa siasa na kuamua kwenda kugombea ubunge ili asiwe tu PS bali awe ndio waziri kabisa. Na kati ya alivyotuletea pamoja na utaalamu wake wa electronics ni hiyo ndege na radar. Hivi vyote alivitetea bungeni.
Nijuavyo mimi ni kuwa ile ndege ni pre-owned, maana GS 550 bei yake ni zaidi ya $50million, ni ndege ya anasa. Boeng 737-600 mpya kutoka kwenye makaratasi, Boeng wenyewe wanaweza wakakupa kwa bei sawa na ya GS 550. Sasa kwa ukonsaltanti wa Mwandosya kwa nini hakuishauri serikali vizuri wakati national airline ilikuwa inarusha Boeng 737-200 ambazo hata uundwaji wake umesitishwa? Huyu bwana ana maswali mengi ya kutujibu.
_________________________
G550 ilikuwa Mpya Kabisa, na Tanzania Govenrment FLight Agency walikuepo Marekani wakisimamia na kuifanyia majaribio Savannah Georgia ambako they build the Gulfstream. Ilikuwa Custom Made to Tanzanian Specifications including APU design and other performance settings, na walikabidhiwa ndege na CEO wa Gulfstream kiwandani ----> Ongea na CEO TGFA/John Mkony Pilot wa Rais, Alikuwepo kule na atakupa uthibitisho zaidi.
Kuhusu Air Tanzania, ile ni Shirika la kibiashara ambalo management mbovu ya miaka mingi, hata wangepewa ndege mpya, ni shirika ambalo serikali ishauriwe itupiliwe mbali, uza kila kitu, hata wabunge wengi walisita kuongezea hela lile kampuni.
Yeye ni consultant wa mambo ya Engineering na mazingira, na kuhusu ndege mambo yote ya negotiations za bei, na mikataba yanashughulikiwa na Attourney General na Wizara ya Fedha. Wizara ya Mawasiliano inahusika na Certifying na registering the plane na uchunguzi wa kitaalamu kupitia TGFA (na rada kupitia watu wa CIvil aviation). Yeye kama waziri anawasilisha reports anazopewa na watu wake wizarani bungeni na kwenye baraza la mawaziri ili ipitishwe, hawezi tu kusimama na kusema nunueni 737-600 wakati wataalam wametoa recommendation ya G550 baada ya kupitia ndege nyingi tu ikiwemo Boeing BBJ, na baraza la mawaziri kupitia kabla haijawasilishwa bungeni , na wabunge kupitisha.
Kama vilikuwa havihitajiki, Bunge lisingepitisha. Kuhusu Rada, malipo yalikuwa yameshaanza kutolewa wakati yeye anaingia Uwaziri hata ukisoma Hansard za bunge anakupa timeline na kwanini Rada ilihitajika (sasa kama wakina CHenge walikula dili wakati wanagawa pesa, hiyo ni issue ya kuchunguza), kuhusu Gulfstream you have to look at the Cost of it spread over 50 yrs, thats 1 million US a yr, Ikulu ya JK tayari imetumia zaidi ya dola Millioni 54 (thats just for a quarter of 2006/2007 3 mnths!!!)kwa sababu tofauti zikiwemo safari zake ambazo hatumii hii ndege.
Tanzania Government Flight linaendesha ndege za Serikali mbili ambazo ni Fokker (the company doesnt even exist anymore) na ile anayotumia Rais F28 ilinunuliwa 1978! G550 imenunuliwa ili itumike sawa sawa for more than 50 years, ina moja performance na range kubwa kuliko ndege nyingi sasa, ikitumiwa sawasawa its cheaper to use over the years kuliko kutumia commercial. Sasa Kama raisi wa sasa hataki kuitumia na kusafiri na Emirates and the rest first class na team ya watu 50 ambayo gharama zake zinatisha, hilo ni chaguo lake. Ndege ilinunuliwa ili itumike. Ndege mpya was the right choice.
G550 can fly 18 (yetu nadhani up to 20 people) passengers up to 6,750 nautical miles (12501 kilometers) nonstop at a cruising speed of .885 Mach and at an altitude of up to 51,000 feet. uwezo wa kutua viwanja vidogo ambavyo 737 haiwezi, this means kwasababu za kiusalama kiongozi anaweza kutumia viwanja vidogo na rahisi kumsafirisha kiongozi kuliko kutumia commercial airport.
Mwisho I agree, Maswali mengi ya kujibu.