Who is the best: Hussein Tuwa, Beka Mfaume na Shigongo

holygrail

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2012
Posts
1,303
Reaction score
597
hawa jamaa ni balaa sana. Wakati nakua nilikuwa napenda sana hadithi za shigongo.

Badae nikaja kuwajua waandishi wengi sana. Ila walionivutia zaidi ni hawa watatu,..tuwa,shigongo na mzee beka.

Wote ni watunzi mahiri sana ila binafsi namkubali sana tuwa. Wale wapenzi wa riwaya hebu tutiririke mnaowakubali kati ya hawa jamaa watatu.
 
Nampenda shigongo,japo hao wengine nawasoma pia
 
Wote wako poa kila mtu anaandika story za aina yake...
 
Tuwa is the best!!

story line za shigongo ni zilezile na binafsi naboreka sana na hadithi zake!

Beka ananikera na stori zake zinakua za kichawi chawi tu!

Tuwa anakaribia kufanana na waandishi wa zamani kidogo
 
Mi hadithi siku hizi sisomi kabisaa
 
Tuwa ni zaidi aisee.
Shigongo hapana, hadithi zake anazirefusha makusudi ili ziwe ndefu kama bongo muvi wanavyofanya.
 
hussein tuwa kwa sasa hana mpinzani walauvanatufanya tuenjoy japo tunawakosa watunzi kama akina msiba na mfululizo wake wa willy gamba, mfaume namkubari sana pia lakini shigongo story zake zinaboa ndefu na siku zote ziko vile vile, soma kitu mdunguaji, mtuhumiwa, mkimbizi acha ni balaa tupu, utata wa ..... yani Tuwa ni habari nyingine
 
Nimewasoma wote ingawa shigongo niliacha muda kidogo....
Tuwa ni mzuri na hadithi zake zina mwendelezo mzuri ila anakosa sustainabe sparkling storrytelling skills........
Hadithi zake nyingi zina wahusika wengi na majina yao hayana uhalisia......

Beka mfaume ni habari nyingine kabisa,
Yuko kwenye sayari ya peke yake kabisa.....
Labda angeweza kufanana kidogo na marehemu ben r mtobwa (joram kiango)
Hata wakina jackson kalidimya na aristablus elvis musiba hawaingiii

Hadithithi zake zinavutia na zina uhalisia wa ajabu unaweza hisi hichi kitu ni kweli lakini beka anaweza sana kubadilisha maudhui kwenye hadithi zake
Leo atakuja na story za kibabe za kina mzee beka na kesho atakuja na story za mapenzi za kina muhsin rejea kitabu cha mzee beka na pia kitabu chake cha dhihaka na bado ww msomaji ukasoma vyote na ukaridhika....kumbuka watu wengine hawawezi kusoma vitabu ambavyo maudhui yake hayapendi.
Ila kwa beka mfaume namvulia kofia.......
 
W.E MUSIBA mbunifu wa kijana mahiri kwa upepelezi WILLY GAMBA kwangu mimi he is the best.
 
Tuwa anytime.,shigongo wanamsoma watu wenye upeo mdogo wa mambo,hadithi zake haziingia akilini!
 
unamkumbuka UNONO wa kwenye ''Dae es salaam Usiku''!???...........utafikiri nimewahi kumuona picha niliochorewa!mwanamke mbaya kuiko neno lenyewe
Tutarudi na Roho Zetu? ndo mpango mzima...ni bonge la story idea!! Kwa hawa wa sasa, Hussein Tuwa ni habari nyingine...jamaa ni mkali katika plotting...hata story ideas zake si haba! Niliacha kumsoma Shigongo tangu alipotoa stori ya mtoto wa Kitanzania mwenye mtindio wa ubongo lakini ni genius hakuna tena duniani kiasi cha CIA kutuma timu kumteka...nikaona this's too much bhana...waliosoma story hii sijui wanaweza kunieleza hatima ya Mbongo yule mwenye mtindio wa ubongo lakini ni bonge la genius?
 
W.E MUSIBA mbunifu wa kijana mahiri kwa upepelezi WILLY GAMBA kwangu mimi he is the best.
Musiba ni mkali wa lugha...uandishi isn't all about putting words in paper but tasteful your words are...kwa hili Musiba hana mpinzani!!! Jamaa ana maneno matamu yenye kumfanya msomaji apende kuendelea kusoma zaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…