Down To Earth
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 21,940
- 16,643
kariakoo kipleft hapa zinapaki daladala za mbagala na temeke....kuna book stands pale.Tuwa mwenyewe huwa anawaachia copy pale wanauza.
tatizo lenu wote ni kwamba hamjawasoma wote hao...mimi hakuna kitabu cha willy gamba sijakisoma na wala hakuna cha joram kiango sijakisoma wala cha kalidimya wala cha baba yake banana zorro maana najua hamjui ameshatunga vitabu vingi tu wala hakuna cha mtunzi yoyote mahiri hapa tanzania nimesoma hadithi zote za tuwa na beka mfaume....naendelea kusisitiza beka mfaume ni habari nyingine kabisa.....kabla hamjasifia msome hadithi za wote haoNadhani Tuwa anawazidi hao wote....
Tafuta Riwaya zake kama Mdunguaji , Mkimbizi na Miss Tanzania
Baadhi utazipata hapa, hasa hiyo Miss Tanzania https://www.facebook.com/pages/KONA-YA-Riwaya-Reloaded/162439457293280
Nimewasoma wote ingawa shigongo niliacha muda kidogo....
Tuwa ni mzuri na hadithi zake zina mwendelezo mzuri ila anakosa sustainabe sparkling storrytelling skills........
Hadithi zake nyingi zina wahusika wengi na majina yao hayana uhalisia......
Beka mfaume ni habari nyingine kabisa,
Yuko kwenye sayari ya peke yake kabisa.....
Labda angeweza kufanana kidogo na marehemu ben r mtobwa (joram kiango)
Hata wakina jackson kalidimya na aristablus elvis musiba hawaingiii
Hadithithi zake zinavutia na zina uhalisia wa ajabu unaweza hisi hichi kitu ni kweli lakini beka anaweza sana kubadilisha maudhui kwenye hadithi zake
Leo atakuja na story za kibabe za kina mzee beka na kesho atakuja na story za mapenzi za kina muhsin rejea kitabu cha mzee beka na pia kitabu chake cha dhihaka na bado ww msomaji ukasoma vyote na ukaridhika....kumbuka watu wengine hawawezi kusoma vitabu ambavyo maudhui yake hayapendi.
Ila kwa beka mfaume namvulia kofia.......