Who is the best: Hussein Tuwa, Beka Mfaume na Shigongo

Who is the best: Hussein Tuwa, Beka Mfaume na Shigongo

Nadhani Tuwa anawazidi hao wote....

Tafuta Riwaya zake kama Mdunguaji , Mkimbizi na Miss Tanzania

Baadhi utazipata hapa, hasa hiyo Miss Tanzania https://www.facebook.com/pages/KONA-YA-Riwaya-Reloaded/162439457293280
tatizo lenu wote ni kwamba hamjawasoma wote hao...mimi hakuna kitabu cha willy gamba sijakisoma na wala hakuna cha joram kiango sijakisoma wala cha kalidimya wala cha baba yake banana zorro maana najua hamjui ameshatunga vitabu vingi tu wala hakuna cha mtunzi yoyote mahiri hapa tanzania nimesoma hadithi zote za tuwa na beka mfaume....naendelea kusisitiza beka mfaume ni habari nyingine kabisa.....kabla hamjasifia msome hadithi za wote hao
 
dah hadithi ya mzee beka khatariiii jamaa namkubali sana kwa maoni yangu.
 
Kwangu mimi Hussen Tuwa ni habari nyingine, nimemsoma kwenye mkimbizi, mdunguaji na nyinginezo ukianza kumsoma hata muda wa kunywa maji hutakuanao.

Joramu Kiango kwa hadithi za kijasusi hakuna anaegusa, Lazima ufe, tutarudi na roho zetu, malaika mweusi......., ninavyomsoma kama naangalia filamu hivi.

Shigongo hadithi zake ni kama filamu za kibongo ni rahisi kutabiri kitakachotokea baadae, japo nimewai kuwa mlevi wa hadithi zake ila kwa sasa hanikamati.!
 
Wakuu mi nadhani mzee beka is one the best mi huwa namfananisha na Mario puzo kwa story za kimafia.....nilipata kuifuatilia hadithi yake ya mzee beka kipind hicho cha gazeti la lete raha cjajua km Kuna kitab chake mwenye details kinapouzwa anijuze
 
Nimewasoma wote ingawa shigongo niliacha muda kidogo....
Tuwa ni mzuri na hadithi zake zina mwendelezo mzuri ila anakosa sustainabe sparkling storrytelling skills........
Hadithi zake nyingi zina wahusika wengi na majina yao hayana uhalisia......

Beka mfaume ni habari nyingine kabisa,
Yuko kwenye sayari ya peke yake kabisa.....
Labda angeweza kufanana kidogo na marehemu ben r mtobwa (joram kiango)
Hata wakina jackson kalidimya na aristablus elvis musiba hawaingiii

Hadithithi zake zinavutia na zina uhalisia wa ajabu unaweza hisi hichi kitu ni kweli lakini beka anaweza sana kubadilisha maudhui kwenye hadithi zake
Leo atakuja na story za kibabe za kina mzee beka na kesho atakuja na story za mapenzi za kina muhsin rejea kitabu cha mzee beka na pia kitabu chake cha dhihaka na bado ww msomaji ukasoma vyote na ukaridhika....kumbuka watu wengine hawawezi kusoma vitabu ambavyo maudhui yake hayapendi.
Ila kwa beka mfaume namvulia kofia.......

kitabu cha hadithi bora zaidi kukisoma
1:TUFANI~beka mfaume
.....mama jeni..msalaba wa shetani...
...2.MKIMBIZI-tuwa
3. UTATA WA TISA DISEMBA~tuwa
......ben mtombwa's....elvis musiba's
 
Back
Top Bottom