Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO), kirusi hicho kinasambaa kwa kasi zaidi barani Afrika kuliko wakati wowote ukilinganisha na idadi ya wagonjwa waliobainika juma lililopita.
Mkurugezi wa WHO kanda ya Afrika, Dokta Matshidiso Moeti amesema, kuongezeka kwa kasi ya kusambaa kwa kirusi hicho kwenye wimbi la tatu la janga la COVID- 19 ni tishio kwa bara Afrika.
Visa vya wagojwa waliobainika kuwa na virusi vya Delta vimeogezeka zaidi karibu katika wiki sita mfululizo.
Kwa mujibu wa takwimu mpya, wimbi hilo la Delta limebainika kwa asilimia 97% na 79% katika nchi ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Wakati visa vya Delta vikiendelea kuongezeka na watu kulazwa, WHO inakadiria kwamba mahitaji ya oksijen barani Afrika sasa ni asilimia 50% zaidi kuliko ilivyokuwa waka jana lilipoibuka wimbi la kwanza.