#COVID19 WHO: Nchi 16 Afrika zimekumbwa na kirusi kipya cha Delta

#COVID19 WHO: Nchi 16 Afrika zimekumbwa na kirusi kipya cha Delta

View attachment 1837855Wimbi la tatu la janga la COVID-19 kwa kirusi cha Delta linasambaa kwa kasi barani Afrika na mpaka sasa nchi 16 za bara hilo zimebainika kukumbwa na kirusi hicho.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO), kirusi hicho kinasambaa kwa kasi zaidi barani Afrika kuliko wakati wowote ukilinganisha na idadi ya wagonjwa waliobainika juma lililopita.

Mkurugezi wa WHO kanda ya Afrika, Dokta Matshidiso Moeti amesema, kuongezeka kwa kasi ya kusambaa kwa kirusi hicho kwenye wimbi la tatu la janga la COVID- 19 ni tishio kwa bara Afrika.

Visa vya wagojwa waliobainika kuwa na virusi vya Delta vimeogezeka zaidi karibu katika wiki sita mfululizo.

Kwa mujibu wa takwimu mpya, wimbi hilo la Delta limebainika kwa asilimia 97% na 79% katika nchi ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Wakati visa vya Delta vikiendelea kuongezeka na watu kulazwa, WHO inakadiria kwamba mahitaji ya oksijen barani Afrika sasa ni asilimia 50% zaidi kuliko ilivyokuwa waka jana lilipoibuka wimbi la kwanza.
Maelezo yote yaelekezwa african, ili mnunue chanjo.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Wanataka kuwaondoa wakongo wengi iwezekanavyo ili wachukue Mali ya kutosha bila kelele zozote
 
Tukisimama na Mungu tena tutashinda.

Ni jukumu letu sote kila mmoja kwa imani yake tumwombe Mungu atuepushe na janga hili.
Imeandikwa.
Kizazi hiki kinataka muujiza, nawaambieni hakika hamtapata muujiza tena zaidi ya ule wa Yona alivyomezwa na samaki"
,, Basi yule mtu akasema ,, Bwana wangu akitoka mtu huku akaenda kuwaonya ndugu zangu, basi wataacha uovu wao na kukwepa adhabu hii ninayoipata" jibu- ,,wanao Musa na manabii wawaamini wao"

Mungu amekupa akili ili kwenye jambo la akili yakupasa utumie akili yako. Sayansi uliyonayo unayotumia kutengeneza hizi dawa ni Mungu amekupa. Jichunguzeni binadamu ikiwa mnahitaji miujiza bila kuwajibika"
 
Back
Top Bottom