#COVID19 WHO: Walioambukizwa Uviko-19 Afrika ni mara 97 ya takwimu zilizopo

#COVID19 WHO: Walioambukizwa Uviko-19 Afrika ni mara 97 ya takwimu zilizopo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Inaelezwa kuwa mbili ya tatu ya watu waliopo Afrika wameambukizwa Ugonjwa wa Uviko-19 ndani ya miaka miwili, ikiwa ni mara 97 ya takwimu zilizoripotiwa na mamlaka husika. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Taarifa hiyo iliyotoka wiki hii inaonyesha kuwa maambukizi yaliyoandikishwa ni watu milioni 11.5 na watu 252,000 wamepoteza maisha kwa Afrika.

Kiongozi wa WHO Ukanda wa Afrika, Matshidiso Moeti amesema kwa Afrika Nchi iliyoripotiwa kuwa na maambukizi mengi ni Afrika (watu milioni 3.7) wakati takwimu za duniani kote kwa jumla ni mara 16 zaidi ya inavyoripotiwa.

Source: Aljazeera
 
Sasa hao WHO hizo takwimu za Afrika kuwa ina mambukzi mara16 zaidi ya takwimu tajwa ili hali walisema africa imekosa vipimo vya kolona mara haina uwezo wa kununua chanjo mbona idadi waliyo iweka ya vifo hata italy inazidi africa nzima, watuache Bana sisi corona ilikuwa mafua tu .
 
Waende huko na Corona yao,Sisi tushasahau.
 
Wajinga sana kule Ukraine hakuna cha BARAKOA wala Social DISTANCE. Njia ya muongo ni fupi
 
Tunamshukuru Putin, Kwa kuifuta Corona kwenye ramani ya ulimwengu wangu!

Siifikirii wala kuiwazia kwamba ni deadly disease! Watu waliokimbilia nchi za jirani na Ukraine wamepokelewa bila kuulizwa vyeti au kupimwa au majibu ya vipimo!?
 
Back
Top Bottom