Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema WHO haijapokea taarifa yoyote kutoka Tanzania juu ya hatua zinazochukuliwa na serikali kuhusiana na janga la corona.
Tedros amesema kwenye taarifa yake kwamba hali hiyo inatia wasiwasi na ameitolea mwito serikali ya Tanzania kuanza kuratibu maambukizi ya corona na kutoa data kuhusiana na COVID-19 nchini humo.
Mkurugenzi mkuu huyo wa Shirika la Afya Ulimwenguni amesema, mwishoni mwa mwezi Januari alishirikiana na mkuu wa shirika la WHO barani Afrika Matshidiso Moeti, katika kuihimiza Tanzania kuongeza jitihada kwenye hatua za kiafya dhidi ya COVID-19 na kujiandaa na mikakati ya kutoa chanjo.
Ameitaka Tanzania kuchukua hatua za kuwalinda raia wake na watu wengine ndani na nje ya nchi hiyo.
DW swahili