#COVID19 WHO yasema janga la Corona bado lipo na aina zaidi ya virusi vya Corona zitajitokeza

#COVID19 WHO yasema janga la Corona bado lipo na aina zaidi ya virusi vya Corona zitajitokeza

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwanasayansi mkuu wa Shirika la Afya Duniani,WHO Soumya Swaminathan, amesema ulimwengu bado haujafikia mwisho wa janga la COVID-19 kwani aina zaidi za virusi vya corona zitaendelea kujitokeza.

Swaminathan aliwaambia hayo waandishi wa habari nchini Afrika Kusini, ambako alikuwa ametembelea viwanda vya kutengeneza chanjo. Mwanasayansi huyo mkuu aliandamana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Wakati huo huo uamuzi wa Marekani kuhusu chanjo za Pfizer na BioNTech za COVID-19 kwa ajili ya watoto wadogo kuanzia miezi 6 hadi miaka 4 umeahirishwa kwa takriban miezi miwili baada ya idara inayosimamia Chakula na Dawa (FDA) nchini Marekani kusema inahitaji data zaidi.

Serikali ya nchi hiyo ilipanga kuzindua chanjo kwa watoto wadogo mnamo Februari 21 kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya omicron miongoni mwa watoto.

DW Swahili
 
Back
Top Bottom