Whozu asaini too much money zaidi ya milioni 60+

Whozu asaini too much money zaidi ya milioni 60+

Aseme kabisa gharama za kujitoa, ukiwa na matatizo TZS 60 million ni nyingi ila kwa uhalisia wa uchumi wa sasa kujikwamua lazma weledi wa kiwango cha juu utumike hasa kwa mtu mwenye umaarufu.
 
Msanii wa muziki wa bongo fleva Whozuamesaini mkataba na kampuni ya entertainment iitwayo Too Much Money inayoongozwa na kaka yake Frank pamoja na Fred yenye ofisi zake jijini Guangzhou, China.

Na mkataba huo unahusisha Kusimamia kazi za Muziki, vichekesho pamoja na biashara ambazo zitahusisha jina la msanii huyo, mkataba huo mrefu ambao kwa mujibu wake amelipwa Dola za kimarekani 30,000 kama Deposit ambazo ni zaidi ya Millioni 60 za kibongo

Pia, akiwa nchini China Whozu amefanya kazi mbalimbali ikiwa kurekodi nyimbo kadhaa na maproducer wa China wenye asili ya Nigeria pamoja na kufanya video tatu nchini nchini humo.

Msanii wa bongo Fleva Whozu asaini dili ambalo litamlipa Zaidi ya MILIONI 60+

View attachment 1255961

Chanzo: Hot News TZ
yeye na kaka ake wote wezi
 
Milioni 60 ni vocha ya Diamond kwa mwezi
Ndivyo mafukara mnavyowaza....
hiyo 60 m jamaa anaikatikia kiuno balaa ili walau aoene hata faida maana nyuma yake kuna watu wengi wanasubiri gawio kama kina babu tale and the like....
 
Tatizo la management na wasanii wa kibongo hawasemagi ukweli ila ngoja washindwane ndio utasikia wanasema mara hakuna kitu chochote mara msanii haingizii faida management na kwa msanii kama whozu mjanja mjanja hyo management ijue kabsa kurudisha hela ni ngumu sana sababu hana talent ya muziki na pia hata ukiangalia na kusikiliza nyimbo zake huoni kesho yake ataimba nin ni ujanja ujanja tu
Acha kumvunja moyo huyu MANGI mbona na bonge la FUTURE kimuziki labda wewe humpendi tuu
 
Acha kumvunja moyo huyu MANGI mbona na bonge la FUTURE kimuziki labda wewe humpendi tuu

Hamna kitu anabebwa tu huyu. Ukitaka kujua wasanii wa kweli njoo mtaani ndio utajua hiz mbiv au mbich. Hiv unamjua msanii anaitwa b2k? yupo kwenye maredio yao ? Ila njoo mtaani ndio utamjua
 
Ndivyo mafukara mnavyowaza....
hiyo 60 m jamaa anaikatikia kiuno balaa ili walau aoene hata faida maana nyuma yake kuna watu wengi wanasubiri gawio kama kina babu tale and the like....
Babu tale,sallam,mkubwa fela,madensa wake km 8,watu wa make up,DJs,n.k
 
Back
Top Bottom