Why Africa girls think all white men have money?

Sio wanawake Tu, kuna masela wanawinda wazungu ili watoboe...

Hatuna mapenzi, kunachotupeleka kwai ni visa ya kuingia nchini kwako ili tupambane na maisha yetu lakin sio cos ya hela zake
 
Kwasababu white man akija huku afrika na zile hela zao kidogo tu akizibadili anaweza kula bata la maana hapa bongo na kununua ardhi na kujenga nyumba hata kwa mwezi mmoja tu

Weupe wamejenga sana nyumba kwao na mademu zao tena kwa muda mfupi sana,yaan nyumba ya 30 mil inajengwa mchana na usiku

Ila kumbuka wengi wao nyumba hawana
 
Kwa nini uulize swali kwa lugha ya "mizungu" halafu utake majawabu kwa lugha "nyeusi"?Hapo na weye umeonesha jibu umelikalia.Acha ushamba.

Swali nimeulizwa kwa kizungu ndomana nimelileta kama lilivyo boss
 
Wakuu nimeulizwa swali hilo hapo juu. Karibu kwa majibu.
Sababu ni kwamba, zamani, kumuona mzungu huku Afrika, ni eidha;
1. Mtalii au
2. Padre
Watajwa hapo juu, wote walikuwa wanakuja na hela nyingi.

Kwa mapadre, walikuwa wanatoa misaada makanisani na maeneo mbalimbali ya vijijini na ha mijini. Mfano kule Peramiho kuliwa na Fr. Gothad na mapadre wengine wa kizungu, ambao kila mmoja kwa nafasi yake alitoa msaada. Na hii ilifanya iaminike kuwa kila penye kanisa pana misaada. Pale Songea enzi zetu tulikuwa tunatumwa na mama zetu tukiwa na kadi za kliniki za wadogo zetu na tulikuwa tunapewa maziwa kilo 5 na mitumba, bulga tena pale Jimbo kuu katoliki la Songea (nimekumbuka CALITUS) etc..

Kwa watalii, inajulikana kuwa anayekuja kufanya utalii ana hela. Imani hii ipo hadi leo.

Kwa bahati mbaya, siku za hivi karibuni wanakuja wazungu hata wasio na kitu, yaani sawa na sisi tu kiasi fulani. Lakini vichwani mwetu bado tunawawaza kuwa nao watakuwa na hela. Lakini hili huchochewa zaidi na viwango vya mishahara wanavyolipana wanapakuwa wanafanya kazi hapa nchini kwetu
 
All in All..a real Gentleman you should have a money.the reason is money is part of love which it take more than 70% of our daily life.
 
Sababu ni kwamba, zamani, kumuona mzungu huku Afrika, ni eidha;
1. Mtalii au
2. Padre
Watajwa hapo juu, wote walikuwa wanakuja na hela nyingi.

Kwa mapadre, walikuwa wanatoa misaada makanisani na maeneo mbalimbali ya vijijini na ha mijini. Mfano kule Peramiho kuliwa na Fr. Gothad na mapadre wengine wa kizungu, ambao kila mmoja kwa nafasi yake alitoa msaada. Na hii ilifanya iaminike kuwa kila penye kanisa pana misaada. Pale Songea enzi zetu tulikuwa tunatumwa na mama zetu tukiwa na kadi za kliniki za wadogo zetu na tulikuwa tunapewa maziwa kilo 5 na mitumba, bulga tena pale Jimbo kuu katoliki la Songea (nimekumbuka CALITUS) etc..

Kwa watalii, inajulikana kuwa anayekuja kufanya utalii ana hela. Imani hii ipo hadi leo.

Kwa bahati mbaya, siku za hivi karibuni wanakuja wazungu hata wasio na kitu, yaani sawa na sisi tu kiasi fulani. Lakini vichwani mwetu bado tunawawaza kuwa nao watakuwa na hela. Lakini hili huchochewa zaidi na viwango vya mishahara wanavyolipana wanapakuwa wanafanya kazi hapa nchini kwetu

[emoji736]
 
Back
Top Bottom