Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakuu habarini.....toka kuumbwa kwa huu ulimwengu mtu mweusi amekua akibaguliwa na mtu mweupe!!hivi nini asili ya chuki hii...tukikumbuka slavery...apartheid!!nadhani kuna la zaidi kwa hawa wenzetu kuhusu blacks...asanteni
Toka kuumbwa huu ulimwengu?
Una hakika?
Tangu nilipoulizwa kwa nini hakuna mitume weusi na sikuwa na jibu basi tena!!!!!
Mkuu Kiranga ninakuheshimu sana kwani nina imani kupata mengi toka kwako.....historia yangu haijakaa sawasawa lakini sikumbuki ni lini mtu mweusi amewahi pata heshima kwa mtu mweupe....nimeanzia kwenye era ya slavery kujustify thread yangu....karibu mkuu unijuze nisiyoyafahamu
Tatizo unaanzia kwenye era ya slavery, ungesema kwa nini mtu mweusi hapati heshima tangu slavery ungekuwa na hoja. Lakini huko nyuma mtu mweusi alifanya biashara na mtu mweupe on equal footing.
Karl Peters alivyokuja kuchukua nchi aliwekeana mikataba na masultani wa pwani ya Tanzania ya sasa. Hakuja na jeshi kuswaga watu tu. Admittedly mikataba ilikuwa ya treachery, lakini aliingia kwa heshima ya treaty.
Kabla ya hapo watu wa Azania walifanya biashara kama watu sawa na Wachina, Waliokaa Uingereza ya sasa walinunua chuma kutoka Afrika mashariki katika biashara iliyohusisha watu sawa, wao hawakujua kutengeneza chuma.
Hata hiyo biashara ya utumwa yenyewe mostly iliendeshwa na machifu wa Kiafrika waliokuwa wanawauza maadui zao na mateka wa vita. Wazungu waliokuja kununua watumwa walifanya biashara na hawa machifu kama watu sawa.
Mansa Musa alivyokwenda kuhiji Mecca mwaka 1324 alimwaga dhahabu hapo Cairo watu bado wanazungumzia habari zake mpaka leo, alifanya mpaka bei ya dhahabu ipungue. Huyu alikuwa mtu mweusi aliyeheshimika dunia nzima. Watu kutoka pande zote za dunia walikuwa wanakuja kwenye chuo kikuu cha Timbuktu kusoma na kukopi vitabu.
Contrary to popular belief, Waafrika wamefanya biashara kwa muda mrefu na sehemu nyingine za dunia kama watu sawa. Matatizo ya kudharauliwa mtu mweusi yameanza baada ya watu weusi kudharauliana wenyewe na kujifungia sana tusitoke huko Afrika.
Waafrika walikuwa majenerali walioheshimika katika majeshi ya Warumi. Wengine waliwapiga Warumi bado kidogo wauangushe ufalme huu mkubwa.
Someni kabla ya kutoa habari ambazo si timilifu.
Shukurani kwa kuanzisha uzi tuweke record straight.
I am not saying this out of racial pride or black supremacy - which I think is just as bad as white supremacy - but historically sound accounts.
Wakuu habarini.....toka kuumbwa kwa huu ulimwengu mtu mweusi amekua akibaguliwa na mtu mweupe!!hivi nini asili ya chuki hii...tukikumbuka slavery...apartheid!!nadhani kuna la zaidi kwa hawa wenzetu kuhusu blacks...asanteni
Wakuu habarini.....toka kuumbwa kwa huu ulimwengu mtu mweusi amekua akibaguliwa na mtu mweupe!!hivi nini asili ya chuki hii...tukikumbuka slavery...apartheid!!nadhani kuna la zaidi kwa hawa wenzetu kuhusu blacks...asanteni
Mkuu Kiranga,
Yaliyopita si ndwele, tungange yajayo!
Tunatakiwa kuwajengea uelewa watu wetu na hasa watoto wetu kuwa wanaweza kuwadhibiti watu wa rangi zote duniani na wasikubali kujishusha na kudharauliwa. Mtu yeyote yule akijifanya yuko juu yao, hasa mgeni wamshughulikie inavyostahili bila kujali sana madhara kwake bali wajali zaidi madhara kwetu! Kwa msingi huo jamii yetu itaanza kuinuka.
Pia waafrika walipata heshima kutoka kwa weupe hasa pale waethiopia walipompiga Ufaransa...