Wakuu habarini.....toka kuumbwa kwa huu ulimwengu mtu mweusi amekua akibaguliwa na mtu mweupe!!hivi nini asili ya chuki hii...tukikumbuka slavery...apartheid!!nadhani kuna la zaidi kwa hawa wenzetu kuhusu blacks...asanteni
Mimi nina mtazamo mwengine.
Ubaguzi ni social dynamics zinazojitokeza katika maisha ya viumbe wote (binadamu na wanyama) ili kundi (mbari) moja lilishinde kundi (mbari) lingine katika kinyang'anyiro cha resources (suvival of the fittest). Ubaguzi kati ya weusi na weupe sio tofauti na baguzi katika sehemu nyingine lakini unaleta hisia kubwa kwa sababu ya rangi zetu. Tukiiondoa hii dhana - ubaguzi wa weupe na weusi (ambayo kwa maoni yangu ni inferiority complex tunayojijengea sisi wenyewe na vizazi vyetu), weusi na weupe wanaweza kushindana on an equal footing. Cha muhimu kwetu ni kupata elimu ya kujitegemea na SIO elimu tegemezi kama hii tunayopata sasa. Ukianza pambano wakati unafikiri kuwa yule adui simuwezi, basi utakuwa umekwishashindwa kabla hata hujaanza pambano. Lazima ugangamale from get go.
Mfano:
Si miaka mingi iliyopita marekani na ulaya walikuwa wanawadharau sana Wachina kuwa ni masikini kwa ukomunisti wao. Hivi sasa wanakwenda kwa magoti uchina kukopa.
Zifuatazo ni baguzi nyingine duniani:
- Waisraeli na Wapalestina
- Hitler (Aryan race) na wazungu wengine (ingawaje Hitler hakuwa aryan)
- Hitler na Waisraeli
- Hutu na Tutsi
- Indian brahimin na untouchables
- Rich Arabs na Indian/Pakistani servants
- Luo na Kikuyu (oversimplification lakini pana kwa ukweli)
- Wamerikani na rest of the world
- Suni na Shia
- Waislamu na Wakristu
- Wanawake na Wanaume
- Wacha Mungu na sisi tutakaokwenda chomwa (mimi na mkuu Kiranga )
- Waafrika waliopelekwa utumwani na sisi tuliobaki barani (kama alivyosema Nyani Ngabu )
- Wahindi E.Afrika na Wamatumbi (proof: rate of intermarriages)
- Simba na fisi au chui
- Paka na mbwa
Unajua, kama mwalimu Nyerere asingekemea ukabila hapa Tanzania basi tungekuwa tunabaguana sana. Tafakari ni kabila gani lingelibagua kabila lingine. Baada ya hii mizizi ya ubaguzi kuzimwa kilichobaki sasa ni yale makabila ambayo yangebaguana sasa wanakuwa WATANI. Naomba wale waliokubuhu katika anthropolojia na sosholojia wanikosoe au waendeleze mada.
MUHIMU
Ni muhimu tuwajengee vijana wetu hisia ya kuwa wana nafasi sawa na weupe. Tuwawezeshe!