Mkuu Kiranga ninakuheshimu sana kwani nina imani kupata mengi toka kwako.....historia yangu haijakaa sawasawa lakini sikumbuki ni lini mtu mweusi amewahi pata heshima kwa mtu mweupe....nimeanzia kwenye era ya slavery kujustify thread yangu....karibu mkuu unijuze nisiyoyafahamu
Tatizo unaanzia kwenye era ya slavery, ungesema kwa nini mtu mweusi hapati heshima tangu slavery ungekuwa na hoja. Lakini huko nyuma mtu mweusi alifanya biashara na mtu mweupe on equal footing.
Karl Peters alivyokuja kuchukua nchi aliwekeana mikataba na masultani wa pwani ya Tanzania ya sasa. Hakuja na jeshi kuswaga watu tu. Admittedly mikataba ilikuwa ya treachery, lakini aliingia kwa heshima ya treaty.
Kabla ya hapo watu wa Azania walifanya biashara kama watu sawa na Wachina, Waliokaa Uingereza ya sasa walinunua chuma kutoka Afrika mashariki katika biashara iliyohusisha watu sawa, wao hawakujua kutengeneza chuma.
Hata hiyo biashara ya utumwa yenyewe mostly iliendeshwa na machifu wa Kiafrika waliokuwa wanawauza maadui zao na mateka wa vita. Wazungu waliokuja kununua watumwa walifanya biashara na hawa machifu kama watu sawa.
Mansa Musa alivyokwenda kuhiji Mecca mwaka 1324 alimwaga dhahabu hapo Cairo watu bado wanazungumzia habari zake mpaka leo, alifanya mpaka bei ya dhahabu ipungue. Huyu alikuwa mtu mweusi aliyeheshimika dunia nzima. Watu kutoka pande zote za dunia walikuwa wanakuja kwenye chuo kikuu cha Timbuktu kusoma na kukopi vitabu.
Contrary to popular belief, Waafrika wamefanya biashara kwa muda mrefu na sehemu nyingine za dunia kama watu sawa. Matatizo ya kudharauliwa mtu mweusi yameanza baada ya watu weusi kudharauliana wenyewe na kujifungia sana tusitoke huko Afrika.
Waafrika walikuwa majenerali walioheshimika katika majeshi ya Warumi. Wengine waliwapiga Warumi bado kidogo wauangushe ufalme huu mkubwa.
Someni kabla ya kutoa habari ambazo si timilifu.
Shukurani kwa kuanzisha uzi tuweke record straight.
I am not saying this out of racial pride or black supremacy - which I think is just as bad as white supremacy - but historically sound accounts.