ukweli mchungu ni kwamba, wayahudi asilia hawakuwa blonde, walikuwa na sura kama za watu wa iraq hivi. ila miaka ilivyoenda tangu enzi hizo, walichangamana na mataifa mengine, mfano, walioa waarabu, wakaoa wafilisti, wakaoa waashuru n.k. kwenye biblia unaona kuna mwanajeshi wa israel anaitwa "uria mhiti", hawa alikuwa sio wayahudi ila walijiunga upande wa wayahudi wakawa wanapigana jeshi la wayahudi, mkewe aliitwa bethsheba, ndio mama yake solomon. pia walioa mataifa mengi around that middle east, hivyo sura zao zikawa zimechangamana kidogo.
baada ya kuchukuliwa ukimbizini, huko walikoenda walioa mataifa ya huko, wengi walienda north africa, na hadi leo kuna wayahudi wa asili ya north africa ikiwa na maana wale waliokimbilia na kusettle kule north africa (aljeria, libya, morroco, misri n.k), kuan wayahudi wa ukiriki, italia, malta, cyprus wengi sana, Yemen, iran, iraq n.k. mataifa hayo ya kiarabu kulikuwa na wayahudi malaki na malaki ila uislam ulivyo pamba moto wakawa wanaenda nchi za kikristo. wengi toka mataifa ya kiarabu walikimbia baada ya Israel kutwaa tena ardhi mwaka 1948.
kuna wayahudi walienda kusettle Ulaya yote, kuanzia pale juu karibia na caspian sea, wakazaliana na wazungu, hao ndio ashkenaz jews. walikuwa wengi na walisambaa wakitokea maeneo ya iraq wakapanda uelekeo ule, na kote huko walikuwa wanajenga masinagogi, na wapo wazungu ambao waliconvert kwenye dini ya kiyahudi, hao nao wakajumuishwa humo, hao ndio ashkenaz jews wanaoonekana kama wazungu, hao kina netanyahu. vizazi vyao vimechuja, ukiwapima sasaivi DNA zao utakuta asilimia ndogo sana ya kiyahudi, na hii ndio sababu DNA imepigwa marufuku israel. ila hii haimaanishi kwamba hawakuwa wayahudi kabisa, jua wamekuwepo ukimbizini miaka 400, hapo kuna vizazi kama 4 au 5 wakizaliana na mataifa mengine, hapo tegemea tu kwamba mtoto atatoka wa rangi mbalimbali. ndio maana wale waliokuwa poland, austria, ujerumani na urusi ambako kuna blonde wengi, utakuta kwa mbali wanafanana na wazungu, na ni dhahidi, myahudi akizaa na mwafrica mtoto atatoka na sura ya kiafrika kidogo, akizaa na mzungu mweupe kabisa mtoto anaweza kufanana na either of his parents. na hatuwezi kusema sio wayahudi.
tunawaita wayahudi kwasababu tangu enzi, wamekuwa isolated, wanajitenga sana na kujuana wao kwa wao na ndio maana wana uhakika kwamba wao ni wayahudi. hadi leo kwenye masinagogi yao huwa sio tu wanaabudu ila wanapeana na dili za viashara na maendeleo ndio maana hakuna myahudi masikini.
kwa wasiojua, hadi india kuna wayahudi, ila ukiwaangalia utakuta ni mhindi ambaye ana mchanganyiko wa kihindi na kiyahudi, sio mhindi pure na sio myahudi pure, na tangu karne kuna masinagogi hadi india. na kati ya eneo ambalo wayahudi hawakunyanyaswa ni india. jaribu hata kugoogle tu wayahudi wa india utawaona.
hii inadhihirisha kwamba, kutokana na maeneo walikokuwa wametawanyika, wamekuwa na sura mbalimbali ila asili yao ile ile, na kwasababu wao ni matreleaneal, mtoto anahesabika wa mama, basi mama akizalishwa na mtu wa kabila/taifa lolote mtoto anakuwa myahudi. jumlisha na wayahudi wa ethiopia ambao hadi sasa wamefikia kama 160,000 pale israel, wayahudi weusi.
kipo hadi kizazi cha wayahudi japan, walienda huko kuhemea na wakazaliana huko na wana mchanganyiko wa kijapan na kiyahudi.